Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • hb kur. 22-26
  • Damu Ambayo Huokoa Uhai Kikweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Damu Ambayo Huokoa Uhai Kikweli
  • Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • DAMU PEKEE AMBAYO HUOKOA UHAI
  • ONEA SHANGWE UHAI ULIOOKOLEWA KWA DAMU
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Thamini Ifaavyo Zawadi Yako ya Uhai
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kuuthamini Utakatifu wa Uhai na Damu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
Pata Habari Zaidi
Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
hb kur. 22-26

Damu Ambayo Huokoa Uhai Kikweli

Mambo fulani ni wazi kutokana na habari iliyotangulia. Ingawa watu wengi huona utiwaji-damu mishipani kuwa wenye kuokoa uhai, unajaa hatari. Kila mwaka maelfu hufa likiwa tokeo la kutiwa damu mishipani; watu wengine wengi zaidi huwa wagonjwa sana na hukabili matokeo ya muda mrefu. Hivyo, hata kutokana na maoni ya kimwili, kuna hekima sasa hivi ya kutii ile amri ya Biblia ya ‘kujiepusha na damu.’—Matendo 15:28, 29.

Wagonjwa hulindwa na hatari nyingi wakiomba utibabu wa kitiba bila damu. Matabibu stadi ambao wamekubali takwa la kutumia hilo juu ya Mashahidi wa Yehova wamesitawisha utaratibu wa kutumia ambao ni salama na wenye mafanikio, kama ilivyothibitishwa na ripoti nyingi za kitiba. Matabibu ambao huandaa utunzaji bora bila damu hawaridhiani na kanuni zenye kuthaminiwa za kitiba. Badala ya hivyo, wao huonyesha staha kwa haki ya mgonjwa ya kujua hatari na manufaa ili kwamba yeye aweze kufanya uchaguzi baada ya kuaarifiwa kwa habari ya jambo litakalofanywa kwa mwili na uhai wake.

Sisi hatuwi wajinga katika jambo hili, kwa maana twang’amua kwamba si wote wataafikiana na njia hiyo. Watu hutofautiana katika habari ya dhamiri, maadili, na maoni ya kitiba. Kwa sababu hiyo, wengine, kutia na madaktari, huenda wakaona ugumu wa kukubali uamuzi wa mgonjwa kujiepusha na damu. Daktari mpasuaji mmoja wa New York aliandika: “Mimi sitasahau kamwe miaka 15 iliyopita, nikiwa daktari kijana anayejizoeza ujuzi niliposimama kando ya kitanda cha Shahidi wa Yehova mmoja aliyekuwa anatokwa damu karibu kufa kutokana na donda la utumbo mdogo. Matakwa ya mgonjwa yalistahiwa naye hakupewa damu, lakini ningali naweza kukumbuka mtamauko mkubwa mno niliohisi nikiwa tabibu.”

Bila shaka yeye alihisi kwamba damu ingalikuwa yenye kuokoa uhai. Hata hivyo, mwaka uliofuata baada ya kuandika hivyo, jarida The British Journal of Surgery (Oktoba 1986) liliripoti kwamba kabla ya kuanza kutumia utiaji-damu mishipani, uvujaji-damu ndani ya tumbo na matumbo ulikuwa na “kima cha vifo asilimia 2.5 tu.” Tangu utiaji-damu uwe wa kidesturi, ‘uchunguzi mkubwa ulio mwingi huripoti vifo vya asilimia 10.’ Kwa nini kima cha vifo kiwe juu mara nne? Watafiti walidokeza hivi: “Utiaji-damu wa mapema huonekana ukizuia ugandaji-damu wenye kupita kiasi usiitikie uvujaji-damu na kwa njia hiyo ukitia moyo uvujaji-damu upya.” Wakati yule Shahidi mwenye donda lenye kutoka damu alipokataa damu, huenda uchaguzi wake ukawa ulizidisha sana matarajio yake ya kuendelea kuishi.

Daktari mpasuaji uyo huyo aliongeza: “Upitaji wa wakati na kutibu wagonjwa wengi kuna elekeo la kubadili maoni ya mtu, na leo mimi naona ule muamana kati ya mgonjwa na tabibu wake, na wajibu wa kustahi matakwa ya mgonjwa kuwa wenye umaana sana kuliko ile tekinolojia mpya ya kitiba inayotuzunguka. . . . Inapendeza kwamba ule mtamauko mkubwa mno sasa umetoa nafasi ya kuhisi hofu yenye staha na kuheshimu sana imani mathubuti ya mgonjwa huyo hasa.” Tabibu huyo alimalizia: ‘Hunikumbusha kwamba sikuzote napaswa kustahi matakwa ya mgonjwa ya kibinafsi na ya kidini bila kujali hisia zangu au matokeo.’

Wewe huenda ukawa tayari unang’amua jambo ambalo matabibu wengi wanakuja kuthamini kwa “upitaji wa wakati na kutibu wagonjwa wengi.” Hata kukiwa na utunzaji bora zaidi wa kitiba katika mahospitali yaliyo mazuri zaidi, ufikapo wakati fulani watu hufa. Watiwe au wasitiwe damu, wao hufa. Sisi sote tunazeeka, na ukomo wa uhai unakaribia. Hayo si maoni ya kutazamia ajali. Ni kuona mambo kama yalivyo. Kufa ni uhakika wa maisha.

Uthibitisho waonyesha kwamba watu wasiojali sheria ya Mungu juu ya damu mara nyingi hupata dhara la mara hiyo au lililokawizwa; baadhi yao hata hufa kutokana na damu. Wale ambao huendelea kuishi hawakupata uhai usiokoma. Kwa hiyo utiaji-damu mishipani hauokoi uhai kwa njia yenye kudumu.

Watu walio wengi ambao, kwa sababu za kidini na/au za kitiba, hukataa damu lakini huruhusu utibabu mwingine wa kitiba wafanya vizuri sana. Huenda wakarefusha hivyo uhai wao kwa miaka kadhaa. Lakini si bila ukomo.

Kwamba binadamu wote ni wasiokamilika na hufa kidato kwa kidato hutuongoza kwenye ule ukweli mkuu wa yale ambayo Biblia husema juu ya damu. Tukiuelewa na kuuthamini ukweli huu, tutaona jinsi damu yaweza kwa kweli kuokoa uhai—uhai wetu—daima.

DAMU PEKEE AMBAYO HUOKOA UHAI

Kama ilivyoonyeshwa mapema kidogo, Mungu aliambia ainabinadamu wote kwamba ni lazima wasile damu. Kwa nini? Kwa sababu damu huwakilisha uhai. (Mwanzo 9:3-6) Yeye alifafanua zaidi hili katika lile fungu la sheria alilowapa Israeli. Wakati fungu hilo la sheria lilipoimarishwa, damu ya wanyama waliodhabihiwa ilitumiwa juu ya madhabahu. (Kutoka 24:3-8) Sheria zilizokuwa katika fungu hilo la sheria zilizungumzia uhakika wa kwamba binadamu wote ni wasiokamilika; ni wenye dhambi, kama Biblia ionyeshavyo jambo hilo. Mungu aliambia Israeli kwamba kwa njia ya dhabihu za wanyama zilizotolewa kwake, wangeweza kukiri uhitaji wa kufunikiwa dhambi zao. (Walawi 4:4-7, 13-18, 22-30) Ni kweli, hilo ndilo Mungu aliwataka wafanye huko nyuma, silo analowataka waabudu wa kweli wafanye leo. Hata hivyo hilo lina maana muhimu kwetu sasa.

Mungu mwenyewe alifafanua kanuni iliyo msingi wa dhabihu hizo: “Kwa kuwa uhai [au, nafsi] wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa ya kula damu.”—Walawi 17:11, 12.

Katika sherehe ya kale iliyoitwa Siku ya Upatanisho, kuhani wa juu wa Israeli alipeleka damu ya wanyama waliodhabihiwa ndani ya sehemu takatifu zaidi ya hekalu, kitovu cha ibada ya Mungu. Kufanya hivyo kulikuwa njia ya ufananisho ya kumwomba Mungu afunike dhambi za watu. (Walawi 16:3-6, 11-16) Dhabihu hizo hazikuondolea mbali hasa dhambi zote, kwa hiyo ilikuwa lazima kuzirudia kila mwaka. Hata hivyo, utumizi huu wa damu uliweka kigezo chenye umaana.

Fundisho kubwa la Biblia ni kwamba hatimaye Mungu angeandaa dhabihu moja kamilifu ambayo ingeweza kufunika kabisa dhambi za waamini wote. Hiyo huitwa ukombozi, nayo huvuta fikira kwenye dhabihu ya Mesiya, au Kristo aliyetabiriwa.

Biblia hulinganisha jukumu la Mesiya na jambo lililofanywa katika Siku ya Upatanisho: “Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa [hekalu lililo] kubwa na kamilifu zaidi, [lisilofanyika] kwa mikono, . . . wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, [mbinguni], akiisha kupata ukombozi wa milele. Na katika Torati, karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”—Waebrania 9:11, 12, 22.

Hivyo inakuwa wazi kwa nini tunahitaji kuwa na maoni ya Mungu juu ya damu. Kupatana na haki yake akiwa Muumba, yeye ameamua utumizi wayo wenye mafaa usiotia ndani matumizi mengine. Huenda Waisraeli wa kale wakawa walipata manufaa za afya kwa kutotumia damu ya wanyama au ya kibinadamu, lakini hilo silo lililokuwa jambo la maana. (Isaya 48:17) Ilikuwa lazima waepuke kuendeleza uhai wao kwa damu, sana-sana si kwa sababu kufanya jambo jingine kulikuwa kinyume cha afya, bali kwa sababu lilikuwa jambo lisilo takatifu kwa Mungu. Walipaswa washike mwiko wa kula damu, si kwa sababu ilikuwa imechafuliwa, bali kwa sababu ilikuwa yenye thamani sana katika kupata msamaha.

Mtume Paulo alifafanua juu ya ukombozi: “Katika yeye huyo [Kristo], kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” (Waefeso 1:7) Neno la awali la Kigiriki linalopatikana hapo linatafsiriwa kwa kufaa “damu,” lakini tafsiri fulani fulani za Biblia hukosea kwa kulibadilisha na neno “kifo.” Kwa sababu hiyo, wasomaji huenda wakakosa mkazo juu ya maoni ya Muumba wetu juu ya damu na ile thamani ya kidhabihu ambayo ameifungamanisha nayo.

Kichwa cha Biblia hutegemea uhakika wa kwamba Kristo alikufa akiwa dhabihu ya ukombozi kamilifu lakini hakubaki akiwa mfu. Kufuata kigezo alichoweka Mungu katika siku ya upatanisho, Yesu aliinuliwa akaenda mbinguni “aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.” Alitoa huko thamani ya damu yake ya dhabihu. (Waebrania 9:24) Biblia inakazia kwamba lazima sisi tuepuke mwendo wowote ambao ungekuwa kama ‘kumkanyagia chini Mwana wa Mungu na kuihesabu damu yake kuwa ni kitu ovyo.’ Ni hivyo tu tunavyoweza kuendeleza uhusiano mwema na amani pamoja na Mungu.—Waebrania 10:29; Wakolosai 1:20.

ONEA SHANGWE UHAI ULIOOKOLEWA KWA DAMU

Tunapoelewa yale ambayo Mungu husema juu ya damu, tunakuja kuwa na staha kubwa zaidi kwa thamani yayo ya kuokoa uhai. Maandiko huaridhia juu ya Kristo kuwa yeye ambaye ‘hutupenda na ambaye alitufungua kutoka dhambi zetu kwa njia ya damu yake.’ (Ufunuo 1:5; Yohana 3:16) Ndiyo, kwa njia ya damu ya Yesu, sisi twaweza kupata msamaha kamili na wenye kudumu wa dhambi zetu. Mtume Paulo aliandika: “Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.” Hivyo ndivyo uhai wenye kudumu unavyoweza kuokolewa kwa damu.—Warumi 5:9; Waebrania 9:14.

Muda mrefu uliopita Yehova Mungu alitoa uhakikisho kwamba kwa njia ya Kristo ‘familia zote za dunia zitajibarikia.’ (Mwanzo 22:18, NW) Baraka hiyo hutia ndani kurudisha dunia kuwa paradiso. Hapo ndipo ainabinadamu wenye kuamini hawatasumbuliwa tena na magonjwa, kuzeeka, au hata kifo; wataonea shangwe baraka zinazozidi sana ule msaada wa kitambo kidogo ambao wafanya kazi wa kitiba waweza kututolea sasa. Tuna ahadi hii nzuri ajabu: “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”—Ufunuo 21:4.

Basi, ni jambo la hekima kama nini tuzingatie matakwa yote ya Mungu! Hiyo inatia ndani kutii amri zake juu ya damu, bila kuitumia vibaya hata katika hali za kitiba. Hivyo sisi hatutakuwa tukiishi kwa ajili ya sasa tu. Bali, tutadhihirisha ujali wetu juu ya uhai, kutia na tazamio letu la wakati ujao la uhai wa milele katika ukamilifu wa kibinadamu.

[Sanduku katika ukurasa wa 25]

Watu wa Mungu walikataa kuendeleza uhai wao kwa damu, si kwa sababu ilikuwa kinyume cha afya, bali kwa sababu lilikuwa jambo lisilo takatifu, si kwa sababu damu ilikuwa imechafuliwa, bali kwa sababu ilikuwa yenye thamani sana.

[Picha katika ukurasa wa 24]

“Katika yeye huyo [Yesu], kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi.”—Waefeso 1:7

[Picha katika ukurasa wa 26]

Kuokoa uhai kwa damu ya Yesu hufungua njia ya uhai wenye afya, usiokoma katika paradiso ya kidunia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki