Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 11/15 kur. 10-15
  • Kuuthamini Utakatifu wa Uhai na Damu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuuthamini Utakatifu wa Uhai na Damu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ANAYOSEMA MUNGU JUU YA UHAI NA DAMU
  • TATIZO (GUMU) LETU​—UVUMBUZI WA MUNGU​—UHAI NA DAMU
  • Thamini Ifaavyo Zawadi Yako ya Uhai
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Damu Ambayo Huokoa Uhai Kikweli
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
  • Damu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Heshima ya Kimungu kwa Uhai na Damu
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 11/15 kur. 10-15

Kuuthamini Utakatifu wa Uhai na Damu

“Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai.”​—Ufu. 7:17.

1, 2. Watu wanaonyeshaje kwamba hawaoni thamani ya uhai? (Zab. 115:17)

NI KITU gani chenye dhamani kuliko uhai? Pasipo kuwa nao huwezi kujifurahisha cho chote kinginecho. Hata hivyo, tunazungukwa na ushuhuda unaoonyesha kwamba wengi leo wanathamini kidogo sana thamani (ubora) ya uhai​—ama wao wenyewe au wa wengine.

2 Je! hatuuoni ushuhuda huo katika njia ambayo watu wengi wanaendesha magari yao? Au namna gani wale wanaoendesha magari wakiwa wamelewa na kuwaua watu elfu nyingi kila mwaka? Tena kunao wale wanaotaka kujifurahisha kwa kushiriki katika michezo yenye hatari ambayo inasemekana kwamba inawaua watu wengi kila mwaka. Vilevile, namna gani watu milioni nyingi wanaojua kwamba wanahatarisha afya yao na kufupiza maisha zao kwa kutumia tumbako au kula kupita kiasi?

3. Kwa sababu gani tutafute maoni ya Mungu juu ya uhai? (Zab. 25:4, 5)

3 Lakini tunapoelekeana na maoni ya namna hiyo, kila mmoja wetu anaweza kujiuliza, ‘Je! kweli mimi ninauthamini uhai? Jambo la maana la kumwezesha mtu kuuthamini uhai kweli kweli na ambalo linaongoza fikira na matendo ya mtu ni kukubali kwamba uhai ni zawadi kutoka kwa Yehova. Ndiye “Mungu aliye hai,” na katika yeye “iko chemchemi ya [uhai wetu].” (Yer. 10:10; Zab. 36:9) Alipokuwa akizungumza na wanafilosofia Wagiriki, mtume Paulo alitoa ushuhuda juu ya Aliye Mkuu Zaidi: “Ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. . . . Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai.” (Matendo 17:25, 28) Kulingana na akili nzuri, maoni yetu juu ya uhai yanapaswa yapatane na yale ya Mungu. Je! ndivyo yalivyo? Ili tuweze kujibu hilo, tunahitaji kujua namna anavyouona uhai. Ndipo tunapoweza kulinganisha maoni yetu na yake.

4. Ni ushuhuda gani unaoonyesha kwamba Yehova anauona uhai kuwa mtakatifu?

4 Yehova anauona uhai kuwa mtakatifu, si kitu cha kutumiwa vibaya. Tunajua hivyo kwa kuwa tunaona mara nyingi akilaumu mauaji na chuki ambayo mara nyingi inaongoza kwenye uuaji. (Kut. 20:13; 1 Yohana 3:11-15; Ufu. 21:8) Tena, katika Israeli wa kale, Yehova aliweka mpango wa miji ya makimbilio ambayo katika hiyo mtu angekimbilia apate usalama ikiwa angeua mwingine pasipo kukusudia. Sababu gani mwuaji asiyekusudia alilazimika kuchukua hatua hiyo kubwa ya kuacha nyumba yake akakae, katika mji wa makimbilio, labda kwa muda wa miaka mingi? Kwa kuwa alikuwa amemfanya mwingine apoteze uhai wake, uhai mtakatifu. Unaweza kuona kwamba mpango huu wa kimungu wa miji ya makimbilio ungesitawisha zaidi kuheshimu utakatifu wa uhai.​—Hes. 35:9-29.

5, 6. Sababu gani kwa kufaa damu inafunganishwa na uhai?

5 Baada ya kuueleza mpango huo, Mungu aliwaambia Israeli hivi: “Hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi.” (Hes. 35:33) Sababu gani ilikuwa hivyo? “Damu” inayotajwa hapa ilisimamia uhai wa aliyeuawa. Kwa hiyo Mungu akaonyesha kwa nguvu sana ukamatano wa maana sana ulioko kati ya uhai wetu na damu.

6 Hata ingawa damu si jambo linalozungumzwa sana, ni nani kati yetu asiyejua kwamba tunahitaji damu ili tuendelee kuishi? Inahusiana sana na kila utendaji mkubwa wa miili yetu. Damu inaipeleka hewa inayoendeleza uhai wetu kwenye chembe zetu, inaondoa uchafu kutoka chembe hizi, inatuwezesha tujipatanishe na hali zenye kubadilika za hewa na vilevile ni sehemu yenye maana ya kutusaidia tujikinge na magonjwa. Walakini watu wengi wanaiona damu kama kitu tu chenye umajimaji kinachohitajiwa. Kwa wengine, ni kitu cha kufanyia biashara. Inanunuliwa kutoka kwa watu ovyo ovyo au maskini na kuuzwa kwenye benki za kuhifadhi damu au kwa hospitali. Nayo damu nyingi ya wanyama inatengenezwa kuwa chakula, mbolea pamoja na vitu vingine vya biashara. Kwa wazi kuna watu wengi wasiouona uhai kuwa mtakatifu.

7, 8. (a) Sababu gani inatupasa tuangalie yale yanayosemwa na Neno la Mungu juu ya uhai na damu? (b) Ni maulizo gani yanayozuka juu ya Waefeso 1:7 na juu ya ukombozi?

7 Walakini, Neno la Mungu linatusaidia kujua kwamba damu ni zaidi ya umajimaji tu wa asili unaohitajiwa. Yale anayosema Muumba wetu juu ya uhai na damu yanapaswa yaongoze maoni na matendo yetu ya sasa. Vilevile yaweza kuwa na matokeo juu ya wakati wetu ujao wa milele. Namna gani hivyo? Kama msaada wa kuona jibu, linganisha mitajo hii ya Waefeso 1:7 kutoka kwa tafsiri mbili za Biblia za kisasa, sana sana ukiangalia maneno ambayo tumelaza:

“Katika yeye huyo [Kristo], kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.”

“Kwa kuwa kwa kifo cha Kristo tunawekwa huru, yaani, tunasamehewa dhambi zetu. Jinsi ilivyo kuu neema ya Mungu.”​—Today’s English Versiona

8 Kutokana na yo yote ya tafsiri hizi mbili tunaweza kujifunza kwamba Mungu anapendezwa nasi, na uhai wetu. Kwa sababu hiyo alimtuma Mwanawe wa pekee Yesu awe dhabihu ya ukombozi ambayo ingeweza kuweka watu huru na dhambi, ikiwakomboa wanadamu kutokana na laana. (1 Tim. 2:5, 6; Yohana 3:16, 17) Yesu mwenyewe alisema: “Mimi nalikuja ili [mwe] na uzima.” (Yohana 10:10) Lakini je! kuna tofauti yo yote kwamba tafsiri nyingine zasema kwamba hii ni kwa sababu ya kifo cha Kristo mahali pa kuwa kwa sababu ya damu ya Kristo? Nayo tofauti hiyo inaweza kuwa na uhusiano (ukamatano) gani na uhai wetu​—kufikiri kwetu, matendo yetu na wakati wetu ujao? Na tuone.

ANAYOSEMA MUNGU JUU YA UHAI NA DAMU

9. Tunajuaje kwamba Yehova anaiona damu kuwa inasimamia uhai?

9 Yehova alipowapa wanadamu ruhusa ya kwanza wale nyama ya wanyama, yeye alitoa jambo linalopaswa kuangaliwa linalotuonyesha anavyofikiri Mungu juu ya uhai na damu. Mungu alimwambia Nuhu na jamaa yake, ambao sisi sote tumetoka kwao hivi:

“Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai [“nafsi,” NW], yaani, damu yake, msile. Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka. . . . Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu; maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.”​—Mwa. 9:3-6.

Basi wanadamu wote waliokuwa wakiishi wakati huo walijulishwa kwamba, katika maoni ya Mungu, damu iliwakilisha uhai. Damu ya mwanadamu ingesimamia “nafsi,” yake, au, kama tafsiri nyingi za Biblia zinavyoutaja, “uhai” wake. (Union Version; Jerusalem Bible ya Kikatoliki; tafsiri ya Rabi Isaac Leeser) Baadaye Mungu Mpaji-Uzima aliongezea hayo, akatoa mambo mengi zaidi yanayotusaidia tuione maana inayokamatana na mema na mabaya ambayo yeye anakamatanisha na uhai kama unavyosimamiwa na damu.

10, 11. Makuhani Waisraeli walifanya nini na damu ya wanyama waliotolewa dhabihu, ikiongoza kwenye ulizo gani?

10 Sana sana hii ilikuwa hivyo katika agano ambalo Mungu alifanya na Israeli, agano la Torati. Wakati wa kuanzishwa kwalo, wanyama walichinjwa na damu yao ilitumiwa katika kuhalalisha agano hilo. (Kut. 24:3-8; Ebr. 9:17-21) Kati ya mipango ya agano hilo kulikuwako na sheria zilizohusu kutoa sadaka za dhambi; katika sadaka hizo, damu ilimwagwa ikisimamia uhai unaotolewa kwa Mungu kufunika dhambi. (Law. 4:4-7, 13-18, 22-30) Kwa sababu ya uwezo wake wa kufunika dhambi machoni pa Mungu, damu ya sadaka za wanyama ilitumiwa katika Siku ya Upatanisho ya kila mwaka. Kwanza ng’ombe kisha mbuzi walichinjwa wakiwa toleo la dhambi. Ndipo kuhani mkuu alipopeleka sehemu ya damu ya kila mnyama katika Patakatifu Zaidi pa hema (baadaye, hekalu) akainyunyizia juu ya sanduku, lililosimamia kuwapo kwa Mungu. (Hes. 7:89; Kut. 25:22; Law. 16:2) Baadaye vilevile aliweka sehemu ya damu hiyo juu ya madhabahu ya sadaka.​—Law. 16:11-19.

11 ‘Yote haya yananipasaje?’ wengine waweza kuuliza. Huenda yakaonekana kama kwamba yanaeleza kawaida za kale ambazo hata Wayahudi hawazifuati tena. Yana ukamatano gani na tumaini letu la wakati ujao na kuthamini kwetu uhai na damu?

12. Yehova alionyesha matumizi gani ya pekee ya damu? Kwa sababu gani? (Kum. 12:20-27)

12 Katika Mambo ya Walawi sura ya 17, Yehova Mungu mwenyewe anaeleza kanuni inayohusika katika matakwa hayo ya kutoa sadaka; yale aliyoyasema hapo yana maana kwetu sisi. Mungu alisema hivi: “Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu.” (Law. 17:11, 12) Ndiyo, Muumba wetu na Mpaji-Uzima wetu alieleza waziwazi uamuzi wake: Damu (inayosimamia uhai kutoka kwake) ilipaswa kutumiwa katika njia moja tu​—katika kutoa sadaka. Hivyo Mungu aliipa damu thamani, akaitenga iwe takatifu. Chini ya Torati, haingeliwa au kunywewa, au kutumiwa katika njia nyingine yo yote inayobuniwa na wanadamu. Mnyama alipouawa kwa chakula wala si kwa sababu ya sadaka, damu ilipaswa imwagwe chini; katika njia hiyo uhai wa mnyama huyo ulikuwa kama kwamba unarudishiwa Mungu, mwindaji Mwisraeli akijiwekea nyama yake peke yake. (Law. 17:13, 14) Lakini je! haya yanatupasaje kwa kuwa wala Wayahudi wala Wakristo sasa hawana hekalu linalokubaliwa na Mungu ambamo wanyama waweza kutolewa?

TATIZO (GUMU) LETU​—UVUMBUZI WA MUNGU​—UHAI NA DAMU

13. Tunajuaje kwamba tunalemewa na dhambi?

13 Sisi sote lazima tukubali kwamba tu wenye makosa na wenye dhambi. Mtume Paulo alihakikisha hilo akaeleza namna ilivyopata kuwa hivyo. “Kwa mtu mmoja [Adamu] dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti na kwa hivyo mauti ikawafikia watu wote [kutia na sisi] kwa sababu wote wamefanya dhaukamatano wa moja kwa moja na kuthambi.” (Rum. 5:12) Uhakika huu una mini kwetu uhai na damu.

14. Dhabihu zilizotolewa katika Siku ya Upatanisho zilifananisha nini?

14 Kama vile mtume Paulo alivyoongozwa aeleze katika kitabu cha Waebrania, dhabihu za wanyama katika agano la Torati hazingeweza kufunika dhambi kabisa, kama sivyo hazingetolewa kila mwaka. Dhabihu hizo, sana sana zile zilizotolewa katika Siku ya Upatanisho, zilikuwa tu “kivuli cha mema yatakayokuwa.” (Ebr. 10:1-4; 8:5, 6; 9:9, 10) Sura yenyewe iliyofananishwa ilikuwa dhabihu ya ukombozi ya Kristo ambayo ingeweza kufunika kabisa dhambi zetu zote. Akieleza hili, Paulo alisema hivi:

“Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, . . . wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu [mbinguni kwenyewe], akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali . . . hutakasa hata kusafisha mwili; basi si zaidi damu ya Kristo, ambaye kwamba kwa [roho ya] milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itakayowasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. . . . Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”​—Ebr. 9:11-15, 22.

15. Maoni yetu juu ya damu yanakamatanaje na tumaini letu la uzima wa milele?

15 Je! hili halitusaidii tufahamu zaidi sababu lilivyo jambo la maana sana kuwa na maoni ya Mungu juu ya damu, inayosimamia uhai? Mojawapo wa vichwa vikubwa vya Biblia ni kwamba Yesu alikuja duniani atoe uhai wake uwe dhabihu ya ukombozi. Ni kwa njia ya ukombozi huo tu tunapoweza kuwa na taraja la kusamehewa dhambi zetu na tumaini la “uzima wa milele.” (Mt. 20:28; Rum. 3:23, 24; 6:22, 23; 1 Tim. 1:15, 16) Ili tupokee baraka hizo, lazima tuonyeshe imani katika ukombozi wa Yesu, ambao unakamatana na kuwa na maarifa yaliyo sahihi na kuthamini namna alivyotoa uhai wake unaosimamiwa na damu yake.​—1 Tim. 2:3, 4; Gal. 3:22.

16, 17. Ni katika njia gani wafasiri wa Biblia wamegeuza mistari inayotaja damu? (Rum. 5:9 Kol. 1:20)

16 Tukiwa na msingi wa mambo haya yanayohusu dhabihu, upatanisho, damu pamoja na ukombozi wa Yesu, na tugeuze mawazo yetu tena kwenye andiko la Waefeso 1:7. Tafsiri za Kiswahili za mstari huu zaonyesha kwamba unasema, “kwa damu yake [Kristo] tunao ukombozi, wetu, masamaha ya dhambi.” Hata hivyo, tafsiri fulani za kisasa zinatumia mahali pake neno “kifo cha Kristo.” Je! kuna tofauti kubwa?

17 Katika Kigiriki cha asili, Waefeso 1:7 linatumia neno haima, linalomaanisha “damu.” Kwa sababu gani, basi, tafsiri fulani zatumia neno “kifo” hapa na kwingineko? Wafasiri walifahamu kwamba katika maandiko fulani yaliyotaja “damu,” kifo au daraka la uuaji wa mtu fulani ndio uliokuwa unamaanishwa. (Luka 11:50, 51; Matendo 5:20; Ufu. 6:10) Kwa mfano, Pilato alifanya tendo la kunawa mikono yake mbele ya Wayahudi waliokuwa na ghasia wakitaka Yesu auawe, akasema: “Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu.” Wayahudi walijibu: “Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.” (Mt. 27:24, 25; linganisha Ufunuo 7:14.) Walakini, tafsiri fulani zimejitanguliza zikatafsiri mistari hii hivi: “Mimi sina daraka juu ya kifo cha mtu huyu,” na “Adhabu ya kifo chake na ituangukie sisi na watoto wetu.” (TEV) Hata hivyo, je! matokeo yanakuwa nini wakati “kifo” kinatumiwa mahali pa “damu” katika mistari ambayo dhabihu ya Yesu inahusika? Je! inawezekana tukakosa jambo fulani ambalo Mungu alitaka kutujulisha?

18. Sababu gani kifo cha Kristo ni chenye maana? (1 Kor. 11:26; Ebr. 2:14)

18 Hatuwezi kukana kwamba Biblia inatia mkazo sana juu ya kifo cha Yesu. Paulo aliandika hivi: “Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu.” Tena: “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko.” (Rum. 5:8; 1 Kor. 15:3) Kufa kwake, kutoa uhai wake mkamilifu wa kibinadamu kwa nia, alilipia au akasawazisha kile ambacho Adamu alitupotezea na ambacho kilituingiza kwenye hali yetu ya dhambi.

19, 20. Ni mambo gani zaidi ya kifo cha Yesu tu, yanayotiwa ndani ya mitajo inayotaja damu yake Kristo? (Ebr. 4:14-16)

19 Walakini, mitajo ya Biblia juu ya “damu yake Kristo” inapaswa itufahamishe mambo ya maana ambayo huenda yasithaminiwe inaposemwa tu juu ya kifo chake. (Efe. 2:13) Kristo hakufa tu, wala haingewezekana afe tu, na aendelee kuwa mfu.b Katika utimizo wa Siku ya Upatanisho ambayo Yehova alianzisha, Yesu alipaswa aingie mbinguni, mbele za Mungu. Huko Kristo angetoa thamani (ubora) ya damu yake uhai wake, kama vile katika Siku ya Upatanisho kuhani mkuu alivyopeleka damu ya dhabihu katika Patakatifu Zaidi. Paulo anaonyesha waziwazi ulinganifu huu: “Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.”​—Ebr. 9:24, 11, 12; 13:11.

20 Zaidi ya hayo, huko mbinguni Yesu Kristo yu hai na anaweza kuwaombea wote wanaoonyesha imani katika ukombozi wake awasaidie wafikie wokovu. Kupatana na hayo, Paulo aliandika: “Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika [uhai] wake.”​—Rum. 5:10.

21, 22. Uhai wetu unapaswaje na usemi “damu yake Kristo”?

21 Hivyo, kikiwa na sababu nzuri, kitabu kiitwacho “Religion in History and in the Present” chasema kwamba katika sehemu nyingi “[mtu] hawezi kutumia kifo cha Kristo mahali pa Damu. Damu yake Kristo inamaanisha zaidi. Inatilia mkazo ukamatano mkubwa ulioko kati ya kifo cha Yesu pamoja na uhai wake na ushindi wake katika kufufuka kwake na kutukuzwa.” Kitabu hicho kinaongeza kwamba usemi “Damu yake Kristo”

“Unachukua maoni ya Kiyahudi katika Agano la Kale ya uwezo wenye kufunika [dhambi] wa damu, ambao ndio msingi wa Njia ambayo dhabihu zinaonwa na wazo la kwamba kifo cha mwenye haki kina uwezo wa kufunika [dhambi]. . . . Kwa upande mmoja usemi huu unatukumbusha uhakika wa kwamba tumenunuliwa kwa bei kubwa, ya yule aliyeutoa ukombozi na ulikuwa nini. Kwa upande mwingine, tumewekwa huru na dhambi na mauti milele kwa imani katika agano lililofanywa juu ya [msingi wa] damu yake. Damu yake Kristo inatia ndani matokeo ya kifo chake na kufufuka [kwake].”c

22 Hivyo, basi, namna sehemu za Biblia zinazotaja damu yake Yesu zilivyo na maana kubwa na yenye baraka kwetu sisi! Katika hiyo tunaweza kusamehewa dhambi zetu. (Ufu. 1:5; Ebr. 10:29) Kuna uwezekana wa kukombolewa kutokana na mwenendo usiofaa. (1 Pet. 1:18, 19) Tunaweza kuwa kati ya kundi la watu linalokubaliwa na Mungu na kuongozwa naye. (Matendo 20:28) Vilevile kuna tumaini la kuwa mkamilifu na uzima wa milele chini ya utawala wa ufalme ukiunganisha watu walionunuliwa na damu hiyo.​—Ufu. 5:9, 10; 12:10, 11; Kol. 1:20.

23. Maoni yetu juu ya damu yanapaswa kuwa nini?

23 Kwa hiyo, wote wanaothamini ubora wa uhai wanahitaji kuthamini yale yanayosemwa na Mungu juu ya damu. Yeye anaiona kuwa takatifu. Yeye alionyesha matumizi yake ya pekee na kukubaliwa kwake katika kutoa dhabihu madhabahuni. Naye alionyesha waziwazi katika Neno lake kwamba matumaini yetu yote ya wakati ujao wa milele yanategemea damu ya dhabihu ya Mwana wake. Lakini sisi wenyewe tunaweza kuonyeshaje kuthamini na kukubali kwetu utakatifu wa damu? Haya ni mambo ya maana yatakayozungumzwa katika makala (tungo) inayofuata.

[Maelezo ya Chini]

a Ufasiri unaofanana na huo unaonekana katika tafsiri zinazolingana katika Kispania (Version Popular, 1966) na katika Kijeremani (Des Neue Testament in heutigem Deutsch, 1967).

b Tazama The Harp of God (1921), kur. 138-142.

c Die Religion in Geschichte und Gegenwart, chapa wa 3, Kitabu cha 1, kur. 1329-1331.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki