Mafunzo Juu ya Maandiko Yenye Pumzi ya Mungu na Habari ya Msingi Yayo
Funzo Namba 10—Biblia Asilia na Kweli
Uzungumziaji wa Biblia wa historia, jiografia, na vyanzo vya kibinadamu; usahihi wayo kuhusu sayansi, utamaduni, na desturi; unyoofu, upatani, na uaminifu wa waandikaji wayo; na unabii wayo.
1. (a) Kwa ujumla Biblia hukubaliwa kuwa nini? (b) Ni nini sababu ya msingi ya umaarufu wa Biblia?
BIBLIA hukubaliwa kwa ujumla kuwa kitabu chenye utaalamu wa upendezi wa kishairi usio na kifani na ubuni wenye kutokeza wa wanaume waliokuwa waandikaji wayo. Lakini hiyo ni zaidi ya hayo. Waandikaji hao wenyewe walishuhudia kwamba yale waliyoandika yalitokana na Yehova, Mungu mwenye nguvu zote mwenyewe. Hiyo ndiyo sababu ya msingi ya upendezi wa maneno wa Biblia na, la maana zaidi, thamani yayo yenye kuzidi sana ikiwa kitabu cha maarifa na hekima yenye kutoa uhai. Yesu, Mwana wa Mungu, alishuhudia kwamba maneno aliyonena “ni roho, tena ni kweli,” naye alinukuu kwa utele kutokana na Maandiko ya Kiebrania ya kale. “Kila andiko, [ni] lenye pumzi ya Mungu,” akasema mtume Paulo, aliyenena juu ya Maandiko ya Kiebrania kuwa “mausia ya Mungu.”—Yn. 6:63; 2 Tim. 3:16; Rum. 3:1, 2.
2, 3. Waandikaji wa Biblia walishuhudiaje kupuliziwa kwayo na Mungu?
2 Mtume Petro alishuhudia kwamba manabii wa Mungu walichochewa na roho takatifu. Mfalme Daudi aliandika hivi: “Roho ya BWANA [Yehova, NW] ilinena ndani yangu, na neno lake likawa ulimini mwangu.” (2 Sam. 23:2) Manabii walihesabia sifa ya maneno yao Yehova. Musa alionya juu ya kuongeza au kuondoa maneno yoyote matakatifu aliyopewa na Yehova. Petro alihesabu maandishi ya Paulo kuwa yaliyopuliziwa na Mungu, na yaelekea Yuda alinukuu taarifa ya Petro kuwa mamlaka iliyopuliziwa na Mungu. Mwishowe, Yohana, mwandikaji wa Ufunuo, aliandika kama vile alivyoelekezwa na roho ya Mungu na akaonya kwamba yeyote mwenye kuongeza au kuondoa kutokana na ufunuo huo wa kimungu angetoa hesabu, si kwa binadamu, bali moja kwa moja kwa Mungu.—1 Pet. 1:10-12; 2 Pet. 1:19-21; Kum. 4:2; 2 Pet. 3:15, 16; Yuda 17, 18; Ufu. 1:1, 10; 21:5; 22:18, 19.
3 Watumwa hao wa Mungu wenye ujitoaji, wote walishuhudia kwamba Biblia imepuliziwa na Mungu na ni kweli. Kuna vithibitisho vingine vingi vya uasilia wa Maandiko Matakatifu, baadhi yavyo tutazungumza chini ya vichwa 12 vifuatavyo.
4. Vitabu vya Maandiko ya Kiebrania sikuzote vilionwaje na Wayahudi?
4 (1) Usahihi wa Kihistoria. Tangu nyakati za kale, vitabu vinavyokubalika vya Maandiko ya Kiebrania vimepokewa na Wayahudi kuwa vimepuliziwa na Mungu na ya kuwa ni hati zenye kutumainika kabisa. Kwa hiyo, katika wakati wa Daudi, matukio yaliyoandikwa kutoka Mwanzo mpaka Samweli wa kwanza yalikubaliwa kikamili kuwa historia ya kweli ya taifa hilo na shughuli za Mungu pamoja nao, na hilo latolewa kielezi na Zaburi ya 78, ambayo hurejezea kwenye habari ndogo-ndogo zaidi ya 35 kati yazo.
5. Waandikaji wa kale wameshuhudia nini kuhusu Musa na orodha ya Sheria ya Wayahudi?
5 Wapinzani wa Biblia wameshambulia vikali Pentateuki, hasa kuhusu uasilia na ubuni. Hata hivyo, kwenye kule kukubali kwa Wayahudi kuwa Musa ni mwandikaji wa Pentateuki kwaweza kuongezwa ushuhuda wa waandikaji wa kale, baadhi yao ambao walikuwa maadui wa Wayahudi. Hekateo wa Abdera, Mwanahistoria Mmisri Manetho, Lisimako wa Aleksandria, Eupolemo, Takito, na Juvenal wote humhesabia Musa uanzishaji wa fungu la sheria zilizotofautisha Wayahudi na mataifa yale mengine, na walio wengi huonyesha waziwazi kwamba yeye aliandika sheria zake. Numenio, mwanafalsfa wa Paithagorea, hata hutaja Yane na Yambre kuwa makuhani wa Kimisri waliompinga Musa. (2 Tim. 3:8) Watungaji hao ni wa kipindi cha kuanzia wakati wa Aleksanda (karne ya 4 K.W.K.), wakati ambapo kwa mara ya kwanza Wagiriki walidadisi historia ya Kiyahudi, mpaka kile cha Maliki Aurelio (karne ya tatu W.K.). Waandikaji wengine wengi wa kale hutaja Musa kuwa kiongozi, mtawala, au mtoa sheria.a Kama tulivyokwisha kuona katika funzo la hapo awali, magunduzi ya kiakiolojia mara nyingi huunga mkono usahihi wa kihistoria wa matukio yaliyoandikwa katika Biblia wakati ambao watu wa Mungu walijihusisha na mataifa yaliyozunguka.
6. Ni ushuhuda gani unaounga mkono usahihi wa kihistoria wa Maandiko ya Kigiriki?
6 Lakini vipi juu ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo? Si kwamba tu yanathibitisha Andiko la Kiebrania bali pia yao yenyewe yanatolewa uthibitisho kuwa ni sahihi kihistoria na pia ni asilia na yenye upulizio ule ule wa Mungu wa Maandiko ya Kiebrania. Waandikaji hutujulisha rasmi sisi yale waliyosikia na kuona, kwa maana wao walikuwa mashahidi waliojionea na mara nyingi washiriki katika matukio yale yale waliyoandika. Waliaminiwa na maelfu ya marika wao. Ushuhuda wao huthibitishwa kwa utele katika marejezo ya waandikaji wa kale, miongoni mwao wakiwamo Juvenal, Takito, Seneka, Suetonio, Plini Mchanga, Lusiani, Selso, na mwanahistoria wa Kiyahudi Yosefo.
7. (a) Ni hoja gani anayotoa S. A. Allibone juu ya madai makubwa ya Biblia kuwa ni asilia? (b) Anasema ni nini kasoro ya wale wanaokataa uthibitisho wayo?
7 Akiandika katika The Union Bible Companion, S. Austin Allibone asema: “Sir Isaac Newton . . . alikuwa maarufu pia akiwa mchambuzi wa maandishi ya kale, na alichunguza kwa uangalifu mkubwa Maandiko Matakatifu. Kauli yake ni nini juu ya jambo hilo? ‘Nakuta,’ yeye asema, ‘alama hakika zaidi za uasilia katika Agano Jipya kuliko ilivyo katika historia nyingineyo yote ya kilimwengu.’ Dakt. Johnson asema kwamba tuna uthibitisho zaidi kwamba Yesu Kristo alifia Kalvari, kama inavyoelezwa katika zile Gospeli, kuliko tulio nao kwamba Kaisari Julius alifia Capitol. Hakika, sisi tuna mwingi zaidi. Mwulize yeyote anayedai kuwa na shaka ya historia ya Gospeli ana sababu gani ya kuamini kwamba Kaisari Julius alifia Capitol, au kwamba Maliki Charlemagne alivikwa taji kuwa Maliki wa Magharibi na Papa Leo 3. katika 800 . . . Wajuaje mwanamume kama Charles I alipata kuishi, na alikatwa kichwa, na kwamba Oliver Cromwell akawa mtawala badala yake? . . . Sir Isaac Newton huhesabiwa sifa ya ugunduzi wa sheria ya nguvu za uvutano . . . Sisi huamini madai yote yanayofanywa tu kuhusu wanaume hao; na tunafanya hivyo kwa sababu tuna uthibitisho wa kihistoria wa ukweli wao. . . . Endapo, baada ya uthibitisho kama huo kutolewa, wowote wanakataa kuamini, tunawaachilia mbali kuwa ni wapumbavu waliopotoka au mabaradhuli wasiofaa kitu. Basi, tusemeje juu ya wale, ujapokuwapo uthibitisho tele uliotokezwa sasa wa uasilia wa Maandiko Matakatifu, wanadai hawajasadikishwa? . . . Hakika tuna sababu ya kukata maneno kwamba ni moyo wala si kichwa kilicho na kasoro;—kwamba hawataki kuamini kile kinachonyenyekeza kiburi chao, na ambacho kitawalazimisha waishi maisha tofauti.”b
8. Ni kwa njia gani Ukristo wa Biblia huonyeshwa kuwa tofauti na dini nyingine zote?
8 Ubora wa Ukristo ukiwa dini ambayo wafuasi wao huabudu kwa ukweli unakaziwa na George Rawlinson, ambaye aliandika hivi: “Ukristo—kutia ndani mfumo wa Agano la Kale, ambalo lilikuwa ndilo hatua yao ya kwanza—jambo linaloupambanua zaidi ya mengine yote kutoka kwa dini nyinginezo za ulimwengu ni lengo au unamna wa kihistoria. Dini za Ugiriki na Rumi, za Misri, India, Uajemi, na Mashariki kwa ujumla, zilikuwa mifumo ya udhanifu, ambayo haikutoa kwa uzito hata kidogo dhana ya msingi wa kihistoria. . . . Lakini ni tofauti na dini ya Biblia. Humo, kama tukitazama Agano la Kale au Jipya, mfumo wa Kiyahudi au wa Kikristo, tunaona mpango wa fundisho ambao umefungamanishwa na mambo ya hakika; ambao huyategemea kabisa; ambao hutanguliwa kabisa bila hayo; na ambao waweza kuonwa kwa makusudi yote yenye kutumika kuwa umethibitishwa endapo yaonyeshwa yastahili ukubali.”c
9. Toa kielezi cha usahihi wa marejezo ya kijiografia ya Biblia.
9 (2) Usahihi wa Kijiografia na Kijiolojia. Waandikaji wengi wameeleza juu ya usahihi wenye kutokeza wa habari ya Biblia juu ya Bara Lililoahidiwa na maeneo jirani. Kama kielelezo, msafiri mmoja wa Nchi za Mashariki, Dakt. A. P. Stanley, alisema hivi kuhusu kirago cha nyikani cha Waisraeli: “Hata kama njia iliyo barabara waliyopitia haingekuwa inajulikana, bado sehemu za kipekee za nchi hiyo zina mengi yanayofanana hivi kwamba historia ingali ingepokea vielezi vingi vya kutokeza. . . . Chemchemi za pindi kwa pindi, na visima, na vijito, vinapatana na taarifa za ‘maji’ ya Mara; ‘chemchemi’ za . . . Elimu; ‘kijito’ cha Horebu; ‘kisima’ cha mabinti wa Yethro, kikiwa na ‘mitaro’ au matangi yacho, katika Midiani. Majani yangali yale yale tunayowazia kutokana na historia ya Musa.”d Katika simulizi la Misri, usahihi unaonekana si katika maelezo ya ujumla ya eneo hilo tu—mabara yalo ya nafaka yenye rutuba, Mto Naili walo wenye kingo zenye matete (Mwa. 41:47-49; Kut. 2:3), maji yalo yenye kutoka kwa ‘mito, mifereji, vidimbwi vyenye kangaja, na maji ya boma’ (Kut. 7:19), ‘kitani, shayiri, ngano na kusemethu’ zalo (Kut. 9:31, 32)—bali pia katika majina na vituo vya miji.
10. Wanasayansi wa ki-siku-hizi wamethawabishwaje katika kufuata maandishi ya Biblia?
10 Huo ndio utegemeo unaowekwa juu ya maandishi ya kijiolojia na kijiografia katika Biblia na wanasayansi fulani wa ki-siku-hizi hivi kwamba wameifuata kuwa kiongozi na wamethawabishwa sana. Miaka kadhaa iliyopita, mtaalamu fulani wa jiolojia ajulikanaye, Dakt. Ben Tor, alifuata andiko hili: “Kwa kuwa BWANA [Yehova, NW], Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, . . . nchi ambayo mawe yake ni chuma.” (Kum. 8:7, 9) Kilometa chache kutoka Beer-sheba, alipata magenge makubwa sana yaliyojaa timbe nyekundu-nyeusi. Hapo palikuwako tani za metriki milioni 13.6 za timbe ya chuma cha hali ya chini. Baadaye, wahandisi waligundua mchomozo wa kilometa 1.5 wa timbe bora kabisa, asilimia 60 mpaka 65 ya chuma safi. Dakt. Joseph Weitz, wa Israeli ajulikanaye kuwa mwenye amri kuhusu upandaji wa misitu, alisema: “Mti wa kwanza ambao Abrahamu alipanda katika udongo wa Beersheba ulikuwa ni mkwaju.” “Tukifuata uongozi wake, miaka minne iliyopita tulipanda milioni mbili katika eneo lilo hilo. Abrahamu alisema kweli. Mkwaju ni mojawapo wa miti michache ambayo tumeona husitawi kusini ambako mvua ya kila mwaka ni chini ya inchi sita.”e Kitabu Tree and Shrub in Our Biblical Heritage, cha Nogah Hareuveni, huongezea hivi: “Yaonekana kwamba Mzee wa Ukoo Abrahamu hakupanda tu mti wowote alipowasili Beersheva. . . . Alichagua mti ambao uvuli wao ni wenye ubaridi zaidi ya ule wa miti mingineyo. Zaidi ya hayo, [mkwaju] waweza kustahimili joto na vipindi virefu vya ukame kwa kutia mizizi yao kina kirefu chini ili kupata maji ya chini ya ardhi. Haishangazi, [mkwaju] ungaliko mpaka leo hii katika ujirani wa Beersheva.”f—Mwa. 21:33.
11. Profesa Wilson anashuhudiaje usahihi wa Biblia?
11 Kuhusu habari ndogo ndogo kama taarifa za kronolojia na jiografia katika Biblia, Profesa R. D. Wilson aandika hivi katika A Scientific Investigation of the Old Testament, kurasa 213-14: “Taarifa za kronolojia na jiografia ni sahihi na zenye kutegemeka zaidi ya zile zinazotolewa na hati nyinginezo zozote za kale; na masimulizi ya kiwasifu na mengineyo ya kihistoria hupatana kiajabu na uthibitisho unaotolewa na hati nyinginezo zisizo za kibiblia.”
12. Mambo ya hakika yapatanaje na maandishi ya Biblia ya awali ya ainabinadamu?
12 (3) Makabila na Lugha Mbalimbali za Ainabindamu. Katika kitabu After Its Kind, Bryon C. Nelson husema hivi: “Binadamu ndiye aliyefanywa, wala si Mweusi, Mchina, Mzungu. Wale binadamu wawili ambao Biblia huwaita Adamu na Hawa waliumbwa, ambao kutoka kwao kupitia uzao wa asili na utofautiano zimekuja tofauti-tofauti zote za wanadamu walioko juu ya uso wa dunia. Makabila yote ya wanadamu, bila kujali rangi au ukubwa wao, ni jamii moja ya asili. Wote hufikiria mamoja, huhisi mamoja, ni mamoja katika muundo wa kimwili, huoana bila kusita, na wanaweza kuzaa wengine wa namna iyo hiyo. Mbari zote za watu zimetokana na wazazi wawili wale wale ambao walikuja kuwapo wakiwa wameumbika kikamili kwa mkono wa Muumba.”g Huo ndio ushuhuda wa Mwanzo 1:27, 28; 2:7, 20-23; 3:20; Matendo 17:26; na Warumi 5:12.
13. Mwakiolojia mmoja alisema nini juu ya chanzo ambacho kutoka kwacho lugha za kale zilienea?
13 Kwa habari ya simulizi la Biblia juu ya chanzo kile ambacho mweneo wa lugha za kale ulianzia, mwakiolojia Sir Henry Rawlinson alisema kwamba “endapo sisi tungeongozwa hivyo na makutano ya vijia vya kilugha tu, na bila kutegemea mrejezo wote kwenye maandishi ya kimaandiko, bado tungeweza kuongozwa tuthibitishe nyanda za Shinari, kuwa kitovu ambacho lugha mbalimbali zilitawanyikia.”h—Mwa. 11:1-9.
14. (a) Ni nini pekee kingetenga Biblia kuwa iliyopuliziwa na Mungu? (b) Ni maoni gani yenye usawaziko yanayotolewa na Biblia peke yayo, na utumikaji wayo huhusishaje kila sehemu ya maisha ya kila siku?
14 (4) Utumikaji. Kama kusingalikuwako vithibitisho vinginevyo vya uasilia, bado kanuni za uadilifu na viwango vya adili vya Biblia vingeitenga kuwa tokeo la akili ya kimungu. Kuongezea hayo, utumikaji wayo huhusisha kila sehemu ya maisha ya kila siku. Hakuna kitabu kinginecho chote kinachotoa maoni yenye usawaziko ya chanzo cha vitu vyote, kutia ndani ainabinadamu, na juu ya kusudi la Muumba kuelekea dunia na mwanadamu. (Mwa., sura 1; Isa. 45:18) Biblia hutuambia ni kwa nini mwanadamu hufa na ni kwa nini kuna uovu. (Mwa., sura 3; Rum. 5:12; Ayu. sura 1, 2; Kut. 9:16) Hiyo huonyesha kiwango cha juu zaidi cha haki. (Kut. 23:1, 2, 6, 7; Kum. 19:15-21) Hiyo hutoa shauri linalofaa juu ya shughuli za biashara (Law. 19:35, 36; Mit. 20:10; 22:22, 23; Mt. 7:12); mwenendo safi wa kiadili (Law. 20:10-16; Gal. 5:19-23; Ebr. 13:4); mahusiano pamoja na wengine (Law. 19:18; Mit. 12:15; 15:1; 27:1, 2, 5, 6; 29:11; Mt. 7:12; 1 Tim. 5:1, 2); ndoa (Mwa. 2:22-24; Mt. 19:4, 5, 9; 1 Kor. 7:2, 9, 10, 39); mahusiano ya familia na majukumu ya mume, mke, na watoto (Kum. 6:4-9; Mit. 13:24; Efe. 5:21-33; 6:1-4; Kol. 3:18-21; 1 Pet. 3:1-6); mtazamo unaofaa kuelekea watawala (Rum. 13:1-10; Tito 3:1; 1 Tim. 2:1, 2; 1 Pet. 2:13, 14); kazi ya ufuatiaji-haki na pia mahusiano ya bwana-mkubwa na mtumwa na ya mwajiri na mwajiriwa (Efe. 4:28; Kol. 3:22-24; 4:1; 1 Pet. 2:18-21); mashirika yanayofaa (Mit. 1:10-16; 5:3-11; 1 Kor. 15:33; 2 Tim. 2:22; Ebr. 10:24, 25); kutatua ugomvi (Mt. 18:15-17; Efe. 4:26); na mambo mengine mengi ambayo yanahusu sana maisha zetu za kila siku.
15. Ni ushauri gani wa Biblia juu ya afya ya kiakili na kimwili umeonyeshwa kuwa wenye kutumika?
15 Pia Biblia hutoa vielekezi vyenye thamani kuhusu afya ya kimwili na kiakili. (Mit. 15:17; 17:22) Katika miaka ya majuzi, utafiti wa kitiba umeonyesha kwamba afya ya kimwili ya mtu inahusiana kikweli na mtazamo wake wa kiakili. Kwa kielelezo, uchunguzi mbalimbali umeonyesha kwamba watu ambao wanaelekea kuonyesha kasirani ndio wenye viwango vya juu zaidi vya mpigo wa damu. Wengine waliripoti kwamba kasirani ilitokeza miguso ya moyo, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu puani, kisuunzi, au kushindwa kusema. Hata hivyo, zamani za kale Biblia ilieleza hivi: “Moyo mtulivu ndio uhai wa organi ya kimnofu.”—Mit. 14:30, NW; linganisha Mathayo 5:9.
16. Ni zipi baadhi ya taarifa za Biblia za kweli ambazo zilitangulia mno ugunduzi wazo na sayansi?
16 (5) Usahihi wa Kisayansi. Ingawa Biblia si maandishi ya sayansi, inapogusia mambo ya kisayansi, hupatikana kuwa sahihi na yenye kupatana na ugunduzi wa kweli wa kisayansi na maarifa. Maandishi yayo ya utaratibu wa uumbaji, kutia ndani uhai wa hayawani (Mwa., sura 1); kuwa kwa dunia mviringo, au duara (Isa. 40:22); na kuning’inia kwa dunia angani kwenye “nafasi isiyo na kitu” ni kweli zilizotangulia magunduzi ya kisayansi. (Ayu. 26:7) Elimu ya utaratibu wa mwili ya ki-siku-hizi imeonyesha ukweli wa taarifa ya Kimaandiko kwamba “mnofu wote si mnofu mmoja,” muundo wa chembe wa mnofu wa aina moja ni tofauti na ule wa mwingine, binadamu akiwa ana “mnofu” wake mwenyewe wa kipekee. (1 Kor. 15:39, NW)i Katika upande wa elimu ya wanyama, Walawi 11:6 hupanga sungura na wanyama wacheuaji. Hilo lilifanyiwa dhihaka wakati mmoja, lakini sasa sayansi imekuta kwamba sungura hula tena kinyesi chake.j
17. Biblia imeonyeshwaje kuwa timamu kitiba?
17 Taarifa ya kwamba ‘uhai wa mnofu umo ndani ya damu’ imekuja kutambuliwa katika nyakati za ki-siku-hizi kuwa ukweli wa msingi wa sayansi ya kitiba. (Law. 17:11-14, NW) Sheria ya Musa ilionyesha ni wanyama, nyuni, na samaki gani waliokuwa “safi” kuliwa na binadamu, na hiyo haikutia ndani vyakula vya kuhatarisha. (Law., sura 11) Sheria ilitaka kwamba kwenye kambi ya kijeshi, kinyesi kifunikwe, hivyo kutoa kinga kubwa kutokana na maradhi ya kuambukia yenye kusambazwa na nzi, kama vile kuhara damu na homa ya matumbo. (Kum. 23:9-14) Hata leo, katika mabara fulani matatizo makubwa ya afya yapo kwa sababu ya uondoaji usiofaa wa mavi ya binadamu. Watu katika mabara hayo wangalikuwa wenye afya zaidi kama wangalifuata shauri la Biblia juu ya usafi wa kiafya.
18. Ni kielezi gani kingine kilichotolewa cha usahihi wa kisayansi wa Biblia?
18 Biblia hupendekeza divai kidogo “kwa ajili ya tumbo lako” na kwa ajili ya “magonjwa.” (1 Tim. 5:23) Dakt. Salvatore P. Lucia, profesa wa tiba kwenye Chuo Kikuu cha California cha Shule ya Tiba, aandika hivi: “Divai ndicho kinywaji cha ulaji ufaao cha kale zaidi na kiwakili chenye maana zaidi cha kitiba chenye matumizi yenye kuendelea katika historia ya ainabinadamu.”k
19. Usahihi wa maandishi ya Luka ungeweza kutolewa kielezi gani?
19 (6) Utamaduni na Desturi. A. Rendle Short aandika hivi katika Modern Discovery and the Bible, juu ya kitabu cha Matendo: “Ilikuwa desturi ya Kirumi kutawala mikoa ya milki yao iliyosambaa sana kwa kuendeleza kwa kadiri ambayo wangeweza kwa usalama mfumo wa mahali wa usimamizi, na kwa hiyo mamlaka katika wilaya tofauti zilijulikana kwa majina tofauti. Hakuna mtu, isipokuwa yeye awe alikuwa ama msafiri aliye macho au mwanafunzi mwangalifu sana wa maandishi, angeweza kuwapa wakuu hao vyeo vilivyo sahihi. Huo ndio mojawapo wa mitihani mikubwa zaidi ya kihistoria ya kuelewa ambao Luka anaupita kwa usahihi kamili. Katika visa kadhaa ni ushuhuda wa sarafu moja tu, au maandishi fulani, ambayo yametupa habari iliyo ya lazima ili kumchunguza; wanahistoria wanaotambuliwa wa Kirumi hawathubutu kufafanua juu ya sehemu hiyo iliyo ngumu. Kwa hiyo Luka huwaita Herode na Lisania matetraki; ndivyo na Yosefo. Herode Agripa, aliyemchinja Yakobo kwa upanga na kumtupa Petro gerezani, huitwa mfalme; Yosefo hutuambia jinsi alivyokuwa rafiki wa Kaisari Gayo (Kaligula) kule Rumi na akathawabishwa na cheo cha kifalme wakati Kaligula alipokuja kuwa maliki. Liwali wa Saiprasi, Sergio Paulo, huitwa prokonso. . . . Muda usio mrefu kabla, Saiprasi ilikuwa imekuwa mkoa wa kimaliki, na kutawalwa na propraeta au jumbe, lakini katika wakati wa Paulo, kama inavyoonyeshwa na sarafu za Saiprasi, katika Kigiriki na Kilatini pia, cheo sahihi kilikuwa ni prokonso. Maandishi ya Kigiriki yaliyopatikana kule Soloi upande wa kaskazini wa pwani ya Saiprasi yana tarehe ya ‘wakati wa uprokonso wa Paulo’ . . . Katika Thesalonika makabaila wa jiji walitwaa cheo cha kiajabu sana cha mapolitaki [watawala wa jiji, Mdo. 17:6, NW, kielezi-chini], jina lisilojulikana katika fasihi ya maandishi yaliyo bora sana. Isipokuwa uhakika wa kwamba linaonekana katika maandishi; lingekuwa lisilofahamika kwetu kabisa, kama mwenye kulitumia angekuwa ni Luka tu. . . . Akaya chini ya Augusto ulikuwa mkoa wa kiseneti, chini ya Tiberia ulikuwa moja kwa moja chini ya maliki, lakini chini ya Klaudio, kama atuambiavyo Takito, ulirudia useneti, na kwa hiyo cheo sahihi cha Galio [Mdo. 18:12] kilikuwa ni prokonso. . . . Hali moja na hiyo Luka mjuzi, hali moja na hiyo ni msahihi, katika jiografia yake na maoni ya safari zake.”l
20. Maandishi ya Paulo huonyeshaje kwa usahihi nyakati ambazo yeye aliishi na kuandika?
20 Barua za Paulo huonyesha kwa usahihi habari inayohusu wakati wake na huonyesha kwamba yeye alikuwa shahidi aliyejionea mambo yaliyoandikwa. Kwa kielelezo, Filipi ilikuwa koloni ya kijeshi ambayo raia zayo walionea fahari hasa uraia wao wa Kirumi. Paulo aliwaonya Wakristo huko kwamba uraia wao ulikuwa katika mbingu. (Mdo. 16:12, 21, 37; Flp. 3:20) Efeso lilikuwa jiji lililojuliwa kwa ajili ya mambo ya kichawi na mazoea ya uasiliani-roho. Paulo aliagiza Wakristo huko juu ya jinsi ya kuvaa silaha ili wasidhuriwe na roho waovu, na wakati uo huo, akatoa maelezo sahihi ya silaha za askari Mrumi. (Mdo. 19:19; Efe. 6:13-17) Desturi ya washindi wa Kirumi ya kuongoza matembezi yenye shangwe ya ushindi ya mwandamano wa watekwa, wengine wao wakiwa uchi, yatumiwa katika kielezi. (2 Kor. 2:14; Kol. 2:15) Katika 1 Wakorintho 1:22, maoni yenye kutofautiana ya Wayahudi na Wagiriki yanatajwa. Katika mambo hayo waandikaji Wakristo waonyesha usahihi wa Musa, yule mwandikaji wa Pentateuki, ambayo juu yayo George Rawlinson asema: “Usahihi wa kitamaduni wa Pentateuki kwa habari ya adabu na desturi za Nchi za Mashariki kwa ujumla, haujapata kutiliwa shaka.”a
21. (a) Toa vielelezo vya kutoficha makosa kwa waandikaji wa Biblia. (b) Hilo lajengaje uhakika katika Biblia kuwa kweli?
21 (7) Kutoficha Makosa kwa Waandikaji wa Biblia. Katika Biblia yote, kutosita kuficha makosa kwa waandikaji wayo ni uthibitisho wenye nguvu wa utegemeko wayo. Kwa kielelezo, Musa asema kwa njia ya moja kwa moja juu ya dhambi yake mwenyewe na hukumu ya Mungu kwamba yeye na ndugu yake, Haruni, hawangeingia Bara Lililoahidiwa. (Hes. 20:7-13; Kum. 3:23-27) Dhambi za Daudi katika pindi mbili na pia uasi-imani wa mwanae Sulemani zafichuliwa waziwazi. (2 Sam., sura 11, 12, 24; 1 Fal. 11:1-13) Yona aandika juu ya kutokutii kwake mwenyewe na tokeo lako. Taifa lote la Israeli lililaaniwa na karibu waandikaji wote wa Maandiko ya Kiebrania, wote wakiwa walikuwa Wayahudi, kwa ajili ya kutokutii kwao Mungu, hayo yakiwa katika maandishi yale yale ambayo Wayahudi walitunza sana na kukubali kuwa matamko ya Mungu na historia ya kweli ya taifa lao. Waandikaji wa Kikristo waliandika vivyo hivyo bila kuficha makosa. Waandikaji wote wanne wa Gospeli walifunua juu kanusho la Petro kuelekea Kristo. Na Paulo alivuta uangalifu kwenye kosa zito la Petro juu ya jambo la imani la kufanya ubaguzi kwa Wayahudi na wasio Wayahudi katika kundi la Kikristo kule Antiokia. Inajenga uhakika katika Biblia kuwa hiyo ni kweli tunapotambua kwamba waandikaji wayo hawakuficha habari za yeyote, hata zao wenyewe, kusudi wafanyize maandishi yenye uaminifu.—Mt. 26:69-75; Mk. 14:66-72; Luka 22:54-62; Yn. 18:15-27; Gal. 2:11-14; Yn. 17:17.
22. Ni nini kingine kinachotoa uthibitisho kwamba Biblia ni Neno la Mungu kweli kweli, nayo iliandikwa kwa kusudi gani?
22 (8) Upatano wa Waandikaji. Biblia iliandikwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 1,600 na waandikaji karibu 40, bila ya kuwapo kutopatana kokote. Imetawanywa sana kwa hesabu kubwa sana ijapokuwa upinzani ulio mkali zaidi na jitihada zenye bidii nyingi za kuiangamiza. Mambo hayo ya hakika yasaidia kutoa uthibitisho kwamba iko kama inavyodai kuwa ni Neno la Mungu mweza yote, na kwamba kweli kweli hiyo ni ‘yafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.’—2 Tim. 3:16.b
23. Ni habari gani kuu yenye upatano ambayo huthibitisha pia kupuliziwa kwa Biblia na Mungu? Toa kielezi.
23 Kupuliziwa kwayo na Mungu kwaonyeshwa na upatano kamili ambao kwao inakazia habari kuu ya utakaso wa jina la Yehova kupitia Ufalme wake mikononi mwa Kristo. Vichache kati ya visa vyenye kutokeza ni:
Mwa. 3:15 Ahadi ya Mbegu ambayo
itaharibu Nyoka
Mwa. 22:15-18 Mataifa yote yatajibariki kupitia
mbegu ya Abrahamu
Kut. 3:15; 6:3 Mungu akazia jina lake la
ukumbusho, Yehova
Kut. 9:16; Rum. 9:17 Mungu aeleza kusudi la kujulishwa
rasmi kwa jina lake
Kut. 18:11; Yehova ni mkubwa zaidi ya
Isa. 36:18-20; 37:20, 36-38; miungu mingine yote
Kut. 20:3-7 Mungu huheshimu jina lake, hudai
ujitoaji kamili
Ayu., sura 1, 2 Enzi kuu ya Yehova ambayo ni haki yake
na mtazamo wa mwanadamu na
ukamilifu kuielekea
Ayu. 32:2; 35:2; 36:24; 40:8 Kutangulizwa kwa Mungu
kuondolewa malawama
Isa. 9:7 Mungu aunga mkono kwa bidii Ufalme wa
milele wa Mwanae
Dan. 2:44; 4:17, 34; Umaana wa Ufalme wa Mungu mikononi
7:13, 14 mwa “Mwana wa Adamu”
Eze. 6:10; 38:23, NW Watu ‘watapaswa kujua kwamba
mimi ni Yehova.’ Taarifa hiyo
huonekana zaidi ya mara
60 katika unabii wa Ezekieli
Mal. 1:11 Jina la Mungu litakuwa tukufu miongoni mwa
mataifa
Mt. 6:9, 10, 33 Utakaso wa jina la Mungu kupitia
Ufalme wake ni wenye umaana wa kwanza
Yn. 17:6, 26 Yesu alijulisha rasmi jina la Mungu
Mdo. 2:21; Rum. 10:13 Jina la Yehova lapasa kuitiwa
kwa ajili ya wokovu
Rum. 3:4 Kuthibitishwa kwa Mungu kuwa wa kweli,
ijapokuwa kila mwanadamu ni mwongo
1 Kor. 15:24-28 Ufalme kurudishiwa Mungu; Mungu kuwa
vitu vyote kwa kila mmoja
Ebr. 13:15 Lazima Wakristo wafanye julisho rasmi
la peupe la jina la Yehova
Ufu. 15:4 Jina la Yehova kutukuzwa
na mataifa yote
Ufu. 19:6 Jina la Yehova kusifiwa baada ya kufanywa
ukiwa kwa Babuloni Mkubwa
24. (a) Ukamilifu wa Wakristo wa mapema huthibitishaje ukweli wa “Hadithi ya Kikristo”? (b) Kuna uthibitisho gani mwingine kwamba waandikaji wa Biblia waliandika mambo ya hakika, wala si hekaya?
24 (9) Ukamilifu wa Mashahidi. Kuhusu uzito unaoweza kupewa ushuhuda wa Wakristo wa mapema—waandikaji wa Maandiko ya Kikristo na pia wengine—George Rawlinson asema hivi: “Waongofu wa mapema walijua kwamba wakati wowote wangeweza kutakwa wafie dini yao. . . . Kila mwandikaji wa mapema mwenye kutetea Ukristo, kwa kule kutetea kwake, alijasiri mamlaka ya kiserikali, na kujiweka katika hali ya kupatwa na mwisho kama huo. Imani inapokuwa jambo la uhai na kifo, wanadamu hawafuati kwa wepesi tu fundisho lolote linalotukia kuwavutia; wala hawajitambulishi waziwazi miongoni mwa dhehebu lenye kunyanyaswa, isipokuwa wawe wamepima vizuri madai ambayo dini hiyo hudai, na kujisadikisha kuwa hiyo ndiyo kweli. Ni wazi kwamba waongofu wa mapema walikuwa na njia za kupima usahihi wa kihistoria wa masimulizi ya Kikristo kwa kadiri kubwa zaidi yetu; wao wangeweza kuchunguza na kuuliza mashahidi kutoka pande zote—kulinganisha usimulizi wao kadha wa kadha—kuulizia jinsi taarifa zao zilivyokabiliwa na wakinzani wao—kuchunguza hati za wasiodai dini zozote za wakati huo—kuchuja kabisa kabisa na kikamili uthibitisho. . . . Kwa ujumla yote hayo—na lazima ikumbukwe kwamba uthibitisho hurundamana—hufanyiza jumla ya uthibitisho ambao ni haba kutokezwa kwa habari ya matukio yoyote ya nyakati za kale sana; na huimarisha pasipo shaka lolote ukweli wa Hadithi za Ukristo. Hata katika njia moja . . . hadithi hiyo haina namna ya hekaya. Ni hadithi moja, inayosimuliwa bila ya utofautiano, hali hekaya hubadilika-badilika na zina maumbo mengi; bila kuachana imechanganyika na historia ya serikali ya nyakati hizo, ambayo kila mahali huiwakilisha kwa usahihi usio wa kawaida, hali hekaya hupotosha au kutia chumvi historia ya serikali; imejawa na habari za kirefu za nathari, ambazo hekaya hufanya ujanja kuepuka; hujawa na maagizo yenye kutumika ya aina iliyo rahisi na sahili zaidi, hali hekaya hufundisha udhanifu. . . . Bidii sahili, uaminifu, usahihi mkubwa, upendo safi kwa ajili ya ukweli, ndizo sifa zenye kuambatana na waandikaji wa Agano Jipya, ambao kwa wazi hushughulika na mambo ya hakika, wala si ndoto . . . Wao huandika ‘ili kwamba tupate kujua uhakika wa mambo hayo’ ambayo ‘yaliaminiwa bila shaka’ katika siku yao.”c—Linganisha Luka 1:1, 4
25. Ni nini ambacho kwa kutokeza huonyesha uasilia wa Biblia?
25 Sehemu yenye kusisimua inayoshughulikiwa na Biblia ni ile ya unabii wa kimungu. Uasilia wa Biblia haujaonyeshwa kwa njia yenye kutazamisha zaidi kama vile katika utimizo wa unabii mwingi mbalimbali, wote ukiwa unaonyesha njozi ya kutokeza ya kimbele ya Yehova katika kutabiri wakati ujao. Hilo Neno la kiunabii kwa hakika ni “taa ing’aayo mahali penye giza,” na kulipa uangalifu kutatia nguvu imani ya wale wanaotamani kuokoka mpaka unabii wote wa Ufalme uwe umetimizwa katika ulimwengu mpya wa milele wenye Uadilifu wa Mungu. Majedwali matatu yafuatayo yaongezea uthibitisho wa uasilia wa Biblia katika kuonyesha mengi ya matimizo hayo ya kiunabii, na pia upatano wa Maandiko yote ya Kiebrania na Kigiriki. Kwa kadiri wakati upitavyo, Biblia hung’aa zaidi na zaidi kuwa ‘imepuliziwa na Mungu na yenye mafaa’ kweli kweli.—2 Pet. 1:19; 2 Tim. 3:16.
[Maelezo ya Chini]
a The Historical Evidences of the Truth of the Scripture Records, 1862, George Rawlinson, kurasa 54, 254-8.
b 1871, kurasa 29-31.
c The Historical Evidences of the Truth of the Scripture Records, kurasa 25-6.
d Sinai and Palestine, 1885, kurasa 82-3.
e Reader’s Digest, Machi 1954, kurasa 27, 30.
f 1984, ukurasa 24.
g 1968, kurasa 4-5.
h The Journal of the Royal Asiatic Society of Great Britain and Ireland, London, 1855, Buku 15, ukurasa 232.
i Insight on the Scriptures, Buku 2, ukurasa 246.
j Insight on the Scriptures, Buku 1, kurasa 555-6, 1035.
k Wine as Food and Medicine, 1954, ukurasa 5.
l 1955, kurasa 211-13.
a The Historical Evidences of the Truth of the Scripture Records, ukurasa 290.
b The Bible—God’s Word or Man’s?, kurasa 12-36.
c The Historical Evidences of the Truth of the Scripture Records, kurasa 225, 227-8.
(10) UNABII MBALIMBALI UNAOTOKEZA KUHUSU YESU NA UTIMIZO WAO
Unabii Tukio Utimizo
Mik. 5:2 Kazaliwa Bethlehemu Luka 2:4-11; Yn. 7:42
Isa. 7:14 Kazaliwa na bikira Mt. 1:18-23;
Yer. 31:15 Watoto kauawa baada ya Mt. 2:16-18
kuzaliwa kwake
Hos. 11:1 Kaitwa kutoka Misri Mt. 2:15
Mal. 3:1; 4:5; Njia katayarishwa mbele Mt. 3:1-3; 11:10-14;
7:27;
Dan. 9:25 Katokea akiwa Mesiya Kajitoa mwenyewe “majuma” 69
kwenye mwisho wa abatizwe na akapakwa mafuta kwa
wakati ulioratibiwa katika 29 W.K.
Isa. 61:1, 2 Kapewa utume Luka 4:18-21
Zab. 78:2 Kanena kwa vielezi Mt. 13:11-13, 31-35
Isa. 53:4 Kachukua magonjwa yetu Mt. 8:16, 17
Zab. 69:9 Mwenye bidii kwa ajili Mt. 21:12, 13;
ya nyumba ya Yehova Mk. 11:15-18;
Isa. 42:1-4 Akiwa mtumishi wa Yehova, Mt. 12:14-21
hangeshindana mabarabarani
Isa. 53:1 Hakuaminiwa Yn. 12:37, 38;
Zek. 9:9; Mwingio katika Yerusalemu Mt. 21:1-9;
Zab. 118:26 juu ya mwana-punda; Mk. 11:7-11;
katukuzwa kuwa mfalme na Luka 19:28-38;
mwenye kuja katika jina Yn. 12:12-15
la Yehova
Isa. 28:16; Kakataliwa, lakini Mt. 21:42, 45, 46;
53:3; akawa jiwe kuu Mdo. 3:14; 4:11;
Zab. 69:8; la pembeni 1 Pet. 2:7
Zab. 41:9; Mtume mmoja kutokuwa Mt. 26:47-50;
109:8 mwaminifu; asaliti Yesu Yn. 13:18, 26-30;
Zek. 11:12 Kasalitiwa kwa vipande Mt. 26:15; 27:3-10;
30 vya fedha Mk. 14:10, 11
Zek. 13:7 Wanafunzi watawanyika Mt. 26:31, 56;
Zab. 2:1, 2 Mamlaka za Kirumi na Mt. 27:1, 2;
viongozi wa Israeli Mk. 15:1, 15;
watenda pamoja kupinga Luka 23:10-12;
mpakwa mafuta wa Yehova Mdo. 4:25-28
Isa. 53:8 Kajaribiwa na kuhukumiwa Mt. 26:57-68;
27:1, 2, 11-26;
Zab. 27:12 Kutumiwa kwa mashahidi Mt. 26:59-61;
bandia Mk. 14:56-59
Isa. 50:6; Kapigwa, katemwa mate Mt. 26:67; 27:26, 30;
Zab. 22:18 Mavazi yake yapigiwa Mt. 27:35;
kura Yn. 19:23, 24
Isa. 53:12 Kahesabiwa pamoja na Mt. 26:55, 56; 27:38;
watenda dhambi Luka 22:37
Zab. 22:7, 8 Katukanwa alipokuwa Mt. 27:39-43;
juu ya mti Mk. 15:29-32
Zab. 69:21 Kapewa siki na nyongo Mt. 27:34, 48;
Zab. 34:20; Hakuna mifupa iliyovunjwa Yn. 19:33, 36
Isa. 53:5, 8, Kafa kifo cha kidhabihu Mt. 20:28;
11, 12 ili achukue dhambi na Yn. 1:29;
kufungua njia ya kuingia Rum. 3:24; 4:25;
kwenye msimamo wa uadilifu 1 Kor. 15:3;
pamoja na Mungu Ebr. 9:12-15;
Isa. 53:9 Kazikwa pamoja na matajiri Mt. 27:57-60;
Yona 1:17; Ndani ya kaburi kwa Mt. 12:39, 40; 16:21;
2:10 sehemu za siku tatu, 17:23; 20:19;
Zab. 16:8-11, Kafufuliwa kabla ya Mdo. 2:25-31;
NW, kielezi-chini uharibifu 13:34-37
Zab. 2:7 Yehova ajulisha rasmi kuwa Mt. 3:16, 17;
ni Mwana Wake kwa kumzaa Mk. 1:9-11;
kwa roho na kumfufua Luka 3:21, 22;
Maswali juu ya chati “Unabii Mbalimbali Unaotokeza Kuhusu Yesu na Utimizo Wao”:
(a) Ni unabii gani mbalimbali kuhusu kuzaliwa kwake humpa Yesu taraja la Umesiya?
(b) Ni unabii gani mbalimbali uliotimizwa mwanzoni mwa huduma ya Yesu?
(c) Yesu alitimizaje unabii kwa njia ambayo alitekeleza huduma yake?
(d) Ni unabii gani mbalimbali uliotimizwa wakati wa siku chache za mwisho kabla ya kujaribiwa kwa Yesu?
(e) Unabii ulitimizwaje wakati wa jaribio lake?
(f) Ni unabii gani mbalimbali uliotia alama kutundikwa kwake kwenyewe, kifo chake, na ufufuo wake?
[Chati katika ukurasa wa 344-346]
(11) VIELELEZO VYA UNABII MBALIMBALI MWINGINE WA BIBLIA ULIOTIMIZWA
Unabii Tukio Utimizo
Mwa. 9:25 Wakanaani kuwa Yos. 9:23, 27; Amu. 1:28;
watumwa wa Israeli 1 Fal. 9:20, 21
Mwa. 15:13, 14; Israeli wangetoka Misri Kut. 12:35, 36;
Kut. 3:21, 22 wakiwa na mali nyingi Zab. 105:37
wakati Mungu angehukumu
mataifa yenye
kuwatumikisha
Mwa. 17:20; Ishmaeli angezaa wakuu Mwa. 25:13-16; 21:13, 18
12 na kuwa taifa kubwa 1 Nya. 1:29-31
Mwa. 25:23; Waedomi wangekaa mbali Mwa. 36:8; 27:39, 40
na udongo wenye rutuba, Kum. 2:4, 5;
wangetumikia Waisraeli, 2 Sam. 8:14;
na nyakati nyingine 2 Fal. 8:20;
wangeasi 1 Nya. 18:13;
Mwa. 48:19, 22 Efraimu angeongezeka Hes. 1:33-35;
zaidi ya Manase, na Kum. 33:17;
kila kabila lingekuwa Yos. 16:4-9;
na urithi 17:1-4
Mwa. 49:7 Simeoni na Lawi wangetawa- Yos. 19:1-9;
nyika katika Israeli 21:41, 42
Mwa. 49:10 Uongozi wa kifalme 2 Sam. 2:4;
ungetoka Yuda 1 Nya. 5:2;
Kum. 17:14 Israeli wangeomba utawala 1 Sam. 8:4, 5, 19, 20
wa kifalme
Kum. 28:52, 53, Israeli wangeadhibiwa kwa Ulitimizwa juu ya
64-66, ajili ya ukosefu wa Samaria katika 740 K.W.K.
68 uaminifu; majiji (2 Fal. 17:5-23), juu ya Yerusalemu
yangezingirwa, wangepelekwa katika 607 K.W.K. (Yer. 52:1-27),
utumwani na juu ya Yerusalemu tena
katika 70 W.K.
Yos. 6:26 Adhabu ya kujenga upya Yeriko 1 Fal. 16:34
1 Fal. 9:7, 8; Hekalu lingeharibiwa endapo 2 Fal. 25:9;
2 Nya. 7:20, 21 Israeli wangeasi imani 2 Nya. 36:19;
1 Fal. 13:1-3 Madhahabu ya Yeroboamu 2 Fal. 23:16-18
ingechafuliwa
1 Fal. 14:15 Kupinduliwa kwa ufalme wa 2 Fal. 17:6-23;
makabila kumi ya Israeli 18:11, 12
Isa. 13:17-22; Uharibifu wa Babuloni; Dan. 5:22-31; historia ya
45:1, 2; malango ya Babuloni kilimwengu huunga mkono.
Yer. 50:35-46; yangeachwa wazi; Koreshi alitwaa Babuloni
51:37-43 Wamedi na Waajemi malango yalipoachwa
wangeshinda chini ya wazid
Koreshi
Isa. 23:1, 8, Jiji la Tiro kuharibiwa 2 Nya. 36:22, 23;
13, 14; na Wakaldayo chini ya Historia ya kilimwengu
Eze. 26:4, Nebukadreza huandika sehemu ya bara
7-12 ya jiji iliharibiwa na
sehemu ya kisiwa ikatiishwa
na Nebukadreza baada ya
mazingiwa ya miaka 13e
Isa. 44:26-28 Kujengwa upya kwa 2 Nya. 36:22, 23;
Yerusalemu na hekalu Ezra 1:1-4
na wahamishwa Wayahudi
wenye kurejea; fungu la
Koreshi katika hilo
Yer. 25:11; Kurudishwa kwa baki Dan. 9:1, 2;
29:10 kungekuwa baada ya miaka Zek. 7:5;
70 ya ukiwa 2 Nya. 36:21-23
Yer. 48:15-24; Moabu ingefanywa ukiwa Moabu sasa ni
Eze. 25:8-11; taifa ambalo
Sef. 2:8, 9 limekomeshwaf
Yer. 49:2; Majiji ya Amoni Amoni sasa ni taifa
Eze. 25: 1-7; kuwa marundo yaliyo ambalo limekomeshwag
Sef. 2:8, 9 ukiwa
Yer. 49:17, 18; Edomu ingekatiliwa mbali Edomu ilikomeshwa
Eze. 25:12-14; kama kwamba ilikuwa kama taifa baada
35:7, 15; haijapata kuwapo ya uharibifu wa
70 W.K.h
Dan. 2:31-40; Falme nne zaonyeshwa: Historia ya kilimwengu
7:2-7 Babuloni, Uajemi, yathibitisha utimizo
Ugiriki, na Rumi. mbalimbali wa kiunabii
Habari nyingi za katika kusimama na
kirefu za kiunabii kuanguka kwa mataifa
zilitabiriwa hayo yenye uwezo
zaidii
Dan. 8:1-8, Baada ya ufalme wa Aleksanda Mkuu
20-22; Uajemi, mmoja wenye alishinda Milki ya
11:1-19 nguvu, Ugiriki, ungetawala. Uajemi. Baada
Ufalme huo ungegawanywa ya kifo chake
kuwa sehemu nne, ambazo majemadari wanne
zingetoa mamlaka mbili, walichukua mamlaka.
mfalme wa kaskazini na Hatimaye Mamlaka ya
mfalme wa kusini Seleucus na ya
Ptolemy zilisitawi
na wakati wote zikawa
zapiganaj
Dan. 11:20-24 Mtawala kutoa amri ya Amri ya uandikishaji
kuandikishwa. Katika siku katika Palestina
za mwandamizi wake, “mkuu wakati wa utawala
wa agano” angevunjwa wa Kaisari Augusto;
Yesu kauawa wakati wa
utawala wa mwandamizi
wake, Kaisari Tiberiok
Sef. 2:13-15; Ninawi kuwa ukiwa Likawa rundo
Nah. 3:1-7 la takatakal
Zek. 9:3, 4 Jiji la kisiwani la Tiro Aleksanda alifanya hivyo
kuharibiwa katika 332 K.W.K.a
Mt. 24:2, Yerusalemu kuzingirwa kwa Ilitimizwa na
16-18; boma la miti iliyochongwa Warumi katika
Luka 19:41-44 na kuharibiwa 70 W.K.b
Mt. 24:7-14; Wakati mkubwa wa taabu Wakati usiopata kuwa
Mk. 13:8; watabiriwa kabla ya na kifani wa taabu
Luka 21:10, 11, mwisho kamili wa huu duniani tangu vita
25-28; mfumo wa mambo; ungetia ya ulimwengu ya
2 Tim. 3:1-5 vita, upungufu wa chakula, kwanza katika 1914.
matetemeko ya dunia, Sasa kuhubiriwa kwa
magonjwa ya kipuku, uvunjaji Ufalme kwafanywa
wa sheria, kuhubiriwa kwa katika mabara
habari njema za Ufalme kwa zaidi ya 200
mataifa yote
[Maelezo ya Chini]
d Herodotus I, 191, 192; Insight on the Scriptures, Buku 1, ukurasa 567.
e Cyclopedia ya McClintock na Strong, chapa-mrudio ya 1981, Buku X, ukurasa 617; Insight on the Scriptures, Buku 2, kurasa 531, 1136.
f Insight on the Scriptures, Buku 2, kurasa 421-2.
g Insight on the Scriptures, Buku 1, ukurasa 95.
h Insight on the Scriptures, Buku 1, kurasa 681-2.
i “Your Will Be Done on Earth,” kurasa 104-25, 166-77, 188-95, 220-9.
j “Your Will Be Done on Earth,” kurasa 121-2, 172-4, 194-5, 220-63; Insight on the Scriptures, Buku 1, kurasa 70-1.
k “Your Will Be Done on Earth,” kurasa 248-53; Insight on the Scriptures, Buku 1, ukurasa 220.
l Ona ukurasa 159, mafungu 5, 6.
a McClintock and Strong’s Cyclopedia, 1981 chapa-murido, Buku X, kurasa 618-19.
b Ona ukurasa 188, fungu 9.
(a) Ni matukio gani yaliyotabiriwa ambayo yalikuja kutokea baada ya taifa la Israeli kuingia bara la Kanaani?
(b) Ni unabii gani mbalimbali wa hukumu juu ya Israeli na Yuda uliokuja kutimia, na wakati gani?
(c) Ni nini kilichotabiriwa juu ya mrejesho? Je! hilo lilitimizwa?
(d) Ni mataifa gani yaliyoorodheshwa ambayo juu yao ujumbe mbalimbali wa moja kwa moja wa hukumu uliwapata, na hukumu hizo za kiunabii zilitimizwaje?
(e) Ni yapi baadhi ya matukio ya kihistoria yenye kutokeza yaliyotabiriwa na Danieli? na Yesu?
(12) BAADHI YA MANUKUU NA MATUMIZI YA MAANDIKO YA KIEBRANIA YANAYOFANYWA NA WAANDIKAJI WA MAANDIKO YA KIGIRIKI
(ANGALIA: Orodha hii haitii ndani marejezo yaliyoorodheshwa katika “Unabii Mbalimbali Unaotokeza Kuhusu Yesu,” kwenye kurasa zinazotangulia.)
Nukuu Taarifa Matumizi
Mwa. 1:3 Mungu aamuru nuru ing’ae 2 Kor. 4:6
Mwa. 1:26, 27 Binadamu afanywa katika mfano wa Mungu, Yak. 3:9;
wa kiume na kike Mk. 10:6
Mwa. 2:2 Mungu apumzika kutoka kazi ya uumbaji wa kidunia Ebr. 4:4
Mwa. 2:7 Adamu afanywa kuwa nafsi iliyo hai 1 Kor. 15:45
Mwa. 2:24 Mwanamume ataacha wazazi wake na kushikamana Mt. 19:5;
na mkeye; hao wawili huwa mnofu mmoja Mk. 10:7, 8;
Mwa. 15:5 Mbegu ya Abrahamu ingeongezeka Rum. 4:18
Mwa. 17:5 Abrahamu baba ya wale wenye imani kutoka Rum. 4:16, 17
“mataifa mengi”
Mwa. 18:10, 14 Sara aahidiwa mwana Rum. 9:9
Mwa. 18:12 Sara aita Abrahamu “bwana” 1 Pet. 3:6
Mwa. 21:10 Drama ya kimfano yenye kuhusisha Sara, Hagari, Gal. 4:30
Isaka, na Ishmaeli
Mwa. 21:12 Mbegu ya Abrahamu ingepitia Isaka Rum. 9:7;
Mwa. 22:16, 17 Mungu aapa kupitia yeye mwenyewe kumbariki Abrahamu Ebr. 6:13, 14
Mwa. 25:23 Kibali cha Mungu kwa Yakobo badala ya Esau
kilitabiriwa Rum. 9:12
Kut. 9:16 Sababu ya Mungu ya kuruhusu Farao aendelee Rum. 9:17
Kut. 13:2, 12 Mzaliwa wa kwanza awekwa wakfu kwa Yehova Luka 2:23
Kut. 16:18 Mungu asawazisha mambo katika ukusanyaji wa mana 2 Kor. 8:15
Kut. 19:5, 6 Israeli katika taraja la kuwa ufalme wa makuhani 1 Pet. 2:9
Kut. 19:12, 13 Ukuu wenye kutisha wa Yehova kwenye Mlima Sinai Ebr. 12:18-20
Kut. 20:12-17 Amri za tano, sita, saba, nane, tisa, na kumi Mt. 5:21, 27; 15:4;
Kut. 21:17 Adhabu ya kuvunja amri ya tano Mt. 15:4; Mk. 7:10
Kut. 21:24 Jicho kwa jicho na jino kwa jino Mt. 5:38
Kut. 22:28 “Usimlaani mkuu wa watu wako” Mdo. 23:5
Kut. 25:40 Musa aliagizwa juu ya kigezo cha tabenakulo Ebr. 8:5
na vifaa vyayo
Kut. 32:6 Waisraeli wajitokeza wafanye karamu ya ulevi 1 Kor. 10:7
na kujifurahisha
Kut. 33:19 Mungu yuna rehema juu ya yeyote apendezwaye naye Rum. 9:15
Law. 11:44 “Iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu” 1 Pet. 1:16
Law. 12:8 Utoaji wa maskini baada ya kuzaliwa kwa mwana Luka 2:24
Law. 18:5 Yeye atunzaye Sheria ataishi kwa kulingana nayo Gal. 3:12
Law. 19:18 Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe Mt. 19:19; 22:39;
Law. 26:12 Yehova alikuwa Mungu wa Israeli 2 Kor. 6:16
Hes. 16:5 Yehova ajua wale walio mali yake 2 Tim. 2:19
Kum. 6:16 “Msimjaribu BWANA [Yehova, NW], Mungu wenu” Mt. 4:7; Luka 4:12
Kum. 8:3 Mtu hataishi kwa mkate peke yake Mt. 4:4; Luka 4:4
Kum. 18:15-19 Mungu atainua nabii kama Musa Mdo. 3:22, 23
Kum. 19:15 Kila jambo litathibitishwa kwa Mashahidi Yn. 8:17;
wawili au watatu 2 Kor. 13:1
Kum. 23:21, NW ‘Usiwe mlegevu katika kuiondoa nadhiri yako Mt. 5:33, NW
kwa Yehova’
Kum. 24:1 Mpango wa Sheria ya Musa kwa ajili ya talaka Mt. 5:31
Kum. 25:4 “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa” 1 Kor. 9:9;
Kum. 27:26 Waisraeli ambao hawakuishi kulingana na Sheria Gal. 3:10
walikuwa wamelaaniwa
Kum. 29:4 Si Wayahudi wengi waliosikiliza habari njema Rum. 11:8
Kum. 30:11-14, Uhitaji wa mtu kuwa na “‘neno’ la imani” Rum. 10:6-8 NW
katika moyo na kulihubiri
Kum. 31:6, 8 Kwa vyovyote Mungu hataacha watu wake Ebr. 13:5
Kum. 32:17, 21 Mungu alichochea wivu wa Wayahudi kwa kuwaalika Rum. 10:19;
wasio Wayahudi. Waisraeli walichochea Yehova 1 Kor. 10: 20-22
kwenye wivu kupitia ibada ya sanamu
Kum. 32:35, 36 Kisasi ni cha Yehova Ebr. 10:30
Kum. 32:43 “Furahini, enyi mataifa” Rum. 15:10
1 Sam. 13:14; Daudi, mwanamume mwenye kukubalika kwa moyo Mdo. 13:22
16:1 wenyewe wa Mungu
1 Fal. 19:14, Ni baki tu la Wayahudi lililobaki Rum. 11:3, 4
18 jaminifu kwa Mungu
2 Nya. 20:7 Abrahamu kaitwa “rafiki” (mpenda) ya Mungu Yak. 2:23
Ayu. 41:11 “Ni nani aliyetangulia [kumpa Mungu]?” Rum. 11:35
Zab. 5:9 “Koo lao ni kaburi wazi” Rum. 3:13
Zab. 8:2 Mungu atokeza sifa “vinywani mwa watoto wachanga” Mt. 21:16
Zab. 8:4-6 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke?” Mungu alitiisha Ebr. 2:6, 7;
vitu vyote chini ya nyayo za Kristo 1 Kor. 15:27
Zab. 10:7 “Vinywa vyao vimejaa laana” Rum. 3:14
Zab. 14:1-3 “Hakuna atendaye mema” Rum. 3:10-12
Zab. 18:49 Watu wa mataifa kutukuza Mungu Rum. 15:9
Zab. 19:4, NW, Hakuna ukosefu wa nafasi ya kusikia ukweli Rum. 10:18
kielezi-chini wa kuwapo kwa Mungu kama inavyoshuhudiwa na
uumbaji wote
Zab. 22:22 “Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu” Ebr. 2:12
Zab. 24:1 Dunia ni mali ya Yehova 1 Kor. 10:26
Zab. 32:1, 2 “Heri mtu yule ambaye BWANA [Yehova, NW] Rum. 4:7, 8
hamhesabii dhambi”
Zab. 34:12-16 “Macho ya BWANA [Yehova, NW] huwaelekea wenye haki” 1 Pet. 3:10-12
Zab. 36:1 “Kumcha Mungu hakupo machoni pao” Rum. 3:18
Zab. 40:6-8 Mungu hakukubali tena dhabihu chini ya Sheria; Ebr. 10:6-10
utoaji mmoja wa mwili wa Yesu, kulingana na
mapenzi ya Mungu, huleta utakaso
Zab. 44:22 “Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa” Rum. 8:36
Zab. 45:6, 7, NW “Mungu ni kiti cha enzi [cha Kristo] milele” Ebr. 1:8, 9
Zab. 68:18 Kristo alipopaa juu, alitoa zawadi katika wanadamu Efe. 4:8
Zab. 69:22, 23 Meza ya amani ya Waisraeli yawa mtego Rum. 11:9, 10
Zab. 78:24 Mkate kutoka mbinguni Yn. 6:31-33
Zab. 82:6 “Ndinyi miungu” Yn. 10:34
Zab. 94:11 “Bwana [Yehova, NW] anayafahamu mawazo ya wenye 1 Kor. 3:20
hekima ya kwamba ni ya ubatili”
Zab. 95:7-11 Waisraeli wasiotii hawakuingia katika pumziko Ebr. 3:7-11;
Zab. 102:25-27 “Wewe, Bwana, . . . uliitia misingi ya nchi Ebr. 1:10-12
[dunia, NW]”
Zab. 104:4 “Afanyaye malaika zake kuwa pepo [roho, NW]” Ebr. 1:7
Zab. 110:1 Bwana angeketi kwenye mkono wa kuume wa Yehova Mt. 22:43-45;
Zab. 110:4 Kristo ni kuhani milele kwa kulingana na namna Ebr. 7:17
ya Melkizedeki
Zab. 112:9 “Ametapanya, . . . Haki yake yakaa milele” 2 Kor. 9:9
Zab. 116:10 “Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena” 2 Kor. 4:13
Zab. 117:1 “Enyi mataifa yote, msifuni BWANA [Yehova, NW]” Rum. 15:11
Zab. 118:6 “Bwana [Yehova, NW] ndiye anisaidiaye, sitaogopa” Ebr. 13:6
Zab. 140:3 “Sumu ya fira i chini ya midomo yao” Rum. 3:13
Mit. 26:11 “Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe” 2 Pet. 2:22
Isa. 1:9 Isipokuwa baki, Israeli wangalikuwa kama Sodoma Rum. 9:29
Isa. 6:9, 10 Waisraeli hawakutoa uangalifu kwa habari njema Mt. 13:13-15;
Isa. 8:17, 18 “Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Ebr. 2:13
Mungu [Yehova, NW]”
Isa. 10:22, 23 Ni baki tu la Israeli lingeokolewa Rum. 9:27, 28
Isa. 22:13 “Na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa” 1 Kor. 15:32
Isa. 25:8 “Mauti imemezwa kwa kushinda [milele, NW]” 1 Kor. 15:54
Isa. 28:11, 12 Watu hawakuamini hata ingawa walisemwa nao 1 Kor. 14:21
“kwa midomo ya wageni”
Isa. 28:16 Hakuna kukata tamaa kwa wale wanaoweka imani 1 Pet. 2:6;
yao juu ya Kristo, aliye msingi katika Sayuni Rum. 10:11
Isa. 29:13 Unafiki wa waandishi na Mafarisayo waelezwa Mt. 15:7-9; Mk. 7:6-8
Isa. 29:14 Mungu hufanya hekima ya wenye hekima ikwishe 1 Kor. 1:19
Isa. 40:6-8 Neno lililonenwa na Yehova huvumilia milele 1 Pet. 1:24, 25
Isa. 40:13, NW ‘Ni nani aliyekuwa mshauri wa Yehova?’ Rum. 11:34
Isa. 42:6; “Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa” Mdo. 13:47
Isa. 45:23 Kila goti litainamia Yehova Rum. 14:11
Isa. 49:8 Wakati wenye kukubalika wa kusikiwa, katika 2 Kor. 6:2
“siku ya wokovu”
Isa. 52:7 Nyayo za wachukuaji wa habari njema zapendeza Rum. 10:15
Isa. 52:11 “Tokeni kati yao, mkatengwe nao” 2 Kor. 6:17
Isa. 52:15 Habari njema zatangaziwa wasio Wayahudi Rum. 15:21
Isa. 54:1 “Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa” Gal. 4:27
Isa. 54:13 “Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu Yn. 6:45
[Yehova, NW]”
Isa. 56:7 Nyumba ya Yehova ingekuwa nyumba ya sala kwa Mt. 21:13;
ajili ya mataifa yote Mk. 11: 17;
Isa. 59:7, 8 Uovu wa binadamu kaelezwa Rum. 3:15-17
Isa. 65:1, 2 Yehova alidhihirishwa kwa mataifa yasiyo Wayahudi Rum. 10:20, 21
Isa. 66:1, 2 “Mbingu ni kiti changu cha enzi, na nchi ni pa Mdo. 7:49, 50
kuwekea miguu yangu”
Yer. 5:21 Kuwa na macho, lakini kutoona Mk. 8:18
Yer. 9:24 “Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana 1 Kor. 1:31;
[Yehova, NW]” 2 Kor. 10:17
Yer. 31:31-34 Mungu kuja kufanya agano jipya Ebr. 8:8-12;
Hos. 1:10; Wasio Wayahudi pia kuwa watu wa Mungu Rum. 9:24-26
Hos. 6:6 “Nataka rehema, wala si sadaka” Mt. 9:13; 12:7
Hos. 13:14 “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako?” 1 Kor. 15:54, 55
Yoe. 2:28-32 “Kila atakayeliitia jina la Bwana [Yehova, NW] Mdo. 2:17-21;
ataokolewa” Rum. 10:13
Amo. 9:11, 12 Mungu kuja kujenga upya banda la Daudi Mdo. 15:16-18
Hab. 1:5 “Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni” Mdo. 13:40, 41
Hab. 2:4 “Mwenye haki wangu ataishi kwa imani” Ebr. 10:38;
Hag. 2:6 Mbingu na dunia kuja kutikiswa Ebr. 12:26, 27
Mal. 1:2, 3 Yakobo kapendwa, Esau kachukiwa Rum. 9:13
Maswali juu ya chati “Baadhi ya Manukuu na Matumizi ya Maandiko ya Kiebrania Yanayofanywa na Waandikaji wa Maandiko ya Kigiriki”:
(a) Marejezo kwenye Mwanzo katika Maandiko ya Kigiriki huungaje mkono simulizi lacho la uumbaji?
(b) Ni matumizi gani yanayofanywa ya marejezeo katika Mwanzo kwa Abrahamu na kwa mbegu ya Abrahamu?
(c) Ni manukuu gani yanayofanywa kutoka kitabu cha Kutoka juu ya zile Amri Kumi na sehemu nyinginezo za Sheria?
(d) Tunapata wapi yale majulisho rasmi ya awali ya zile amri kubwa mbili, ile ya kupenda Yehova kwa moyo wote na nafsi na ile ya kupenda jirani kama mtu ajipendavyo mwenyewe?
(e) Taja baadhi ya kanuni za msingi zilizoelezwa katika Pentateuki ambazo zimenukuliwa katika Maandiko ya Kigiriki. Zinatumikaje?
(f) Ni vifungu vipi katika Zaburi, vilivyonukuliwa katika Maandiko ya Kigiriki, hutukuza Yehova (1) akiwa Muumba na Mwenyeji wa dunia? (2) akiwa Yeye aonyeshaye upendezi katika waadilifu na kuwatunza?
(g) Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo hutumiaje vifungu kutoka Isaya na manabii wale wengine kwa (1) kuhubiri habari njema? (2) wengine kukataa habari njema? (3) watu wa mataifa, kuongezea baki la Israeli, kuwa waamini? (4) mafaa za kuzoea imani katika habari njema?