Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 3
  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Yule Atakayetayarisha Njia Azaliwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Elisabeti Apata Mtoto
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Walithawabishwa kwa Kutembea Bila Lawama
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 3

Sura 3

Mtayarishaji wa Njia Azaliwa

ELISABETI yuko karibu sana kupata mtoto wake. Kwa miezi mitatu iliyopita Mariamu amekuwa akiishi pamoja naye. Lakini sasa umefika wakati wa Mariamu kusema kwa heri na kufanga safari ndefu ya kurudi nyumbani Nazareti. Baada ya miezi sita hivi yeye pia atazaa mtoto.

Upesi baada ya Mariamu kuondoka, Elisabeti azaa. Kuna shangwe kama nini anapozaa bila matatizo, na Elisabeti na mtoto wake ni wazima! Elisabeti awaonyeshapo majirani wake na watu wa ukoo mtoto, wote washangilia pamoja naye.

Siku nane baada ya kuzaliwa kwake, kulingana na Sheria ya Mungu, mtoto mvulana katika Israeli ni lazima atahiriwe. Marafiki na watu wa ukoo waja kuwatembelea kwa ajili ya pindi hiyo. Wasema kwamba mvulana huyo apasa kuitwa jina la baba yake, Zakaria. Lakini Elisabeti ajibu kwa sauti kubwa. ‘Hapana!’ asema, ‘ataitwa Yohana.’ Kumbuka hilo ndilo jina ambalo malaika Gabrieli alisema apasa kupewa mtoto huyo.

Lakini, marafiki wao wapinga: ‘Hakuna yeyote kati ya watu wenu wa ukoo mwenye jina hilo.’ Kisha, wakitumia ishara, wamuuliza baba yake jina atakalo kumpa mvulana huyo. Anapoomba ubao wa kuandikia, kwa kustaajabisha wote, Zakaria aandika: ‘Jina lake ni Yohana.’

Baada ya hilo uwezo wa kusema wa Zakaria warudishwa kimuujiza. Wakumbuka kwamba alipoteza uwezo wake wa kusema alipokosa kusadiki tangazo la malaika kwamba Elisabeti angezaa mtoto. Basi, Zakaria azungumzapo, wote wanaoishi katika ujirani wastaajabu na kujiambia: ‘Kwa kweli mtoto huyo atakuwa nani?’

Sasa Zakaria ajazwa roho takatifu, naye ajawa na shangwe na kusema: “Atukuzwe Bwana [Yehova, NW], Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.” Hii “pembe ya wokovu,” bila shaka, ni Bwana Yesu, ambaye angali atazaliwa. Kupitia yeye, asema Zakaria, Mungu “atatujalia sisi, tuokoke mikononi mwa adui zetu, na kumwabudu pasipo hofu, kwa utakatifu na kwa haki [uadilifu, NW] mbele zake siku zetu zote.”

Kisha Zakaria atabiri hivi kwa habari za mwana wake, Yohana: “Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana [Yehova, NW] umtengenezee njia zake; uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao. Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia, kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”

Kufikia wakati huu Mariamu, ambaye kwa wazi angali mwanamke ambaye hajaolewa, amefika nyumbani Nazareti. Itakuwaje kwake inapojulikana wazi kwamba ana mimba? Luka 1:56-80; Walawi 12:2, 3.

▪ Yohana ana umri mkubwa kadiri gani kuliko Yesu?

▪ Ni mambo gani yatukia wakati Yohana anapokuwa mwenye umri wa siku nane?

▪ Mungu amewageuziaje watu wake fikira?

▪ Ilitabiriwa Yohana angefanya kazi gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki