Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 9/1 kur. 8-9
  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Mtayarishaji wa Njia Azaliwa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Yule Atakayetayarisha Njia Azaliwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Elisabeti Apata Mtoto
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Walithawabishwa kwa Kutembea Bila Lawama
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 9/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Mtayarishaji wa Njia Azaliwa

ELISABETI yuko karibu kuzaa mtoto wake. Kwa miezi mitatu iliyopita Mariamu amekuwa akiishi naye. Lakini sasa umefika wakati wa Mariamu kusema kwaheri na kufunga safari ndefu ya kurudi nyumbani Nazareti. Baada ya miezi sita hivi yeye, pia, atazaa mtoto.

Upesi Mariamu akiisha kuondoka, Elisabeti anazaa. Kuna furaha kama nini anapozaa bila matatizo, na Elisabeti na mtoto ni wazima! Elisabeti anapowaonyesha jirani zake na watu wa ukoo mtoto, wote wanafurahi pamoja na yeye.

Siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake, kulingana na sheria ya Mungu, mtoto mvulana katika Israeli ni lazima atahiriwe. Marafiki na watu wa ukoo wanakuja kutembelea kwa ajili ya pindi hiyo. Wanasema kwamba mvulana huyo anapaswa kuitwa jina la babaye, Zekaria. Lakini Elisabeti anajibu kwa sauti kubwa. ‘Hapana!’ anasema. ‘Ataitwa Yohana.’ Kumbuka, hilo ndilo jina malaika Gabrieli alisema lapasa kupewa mtoto huyo.

Lakini, marafiki wao wanapinga: ‘Hakuna ye yote kati ya watu wenu wa ukoo mwenye jina hilo.’ Kisha, wakitumia ishara, wanamuuliza baba yake jina analotaka kumpa mvulana huyo. Anapoomba ubao wa kuandikia, kwa kustaajabisha wote, Zekaria anaandika: ‘Jina lake ni Yohana.’

Baada ya hilo uwezo wa kusema wa Zekaria unarudishwa kimuujiza. Unakumbuka kwamba alipoteza uwezo wake wa kusema alipokosa kusadiki tangazo la malaika kwamba Elisabeti angezaa mtoto. Zekaria anapozungumza, wote wanaoishi katika ujirani wanastaajabu na kujiambia: ‘Kwa kweli mtoto huyu atakuwa nini?’

Sasa Zekaria ajazwa kwa roho takatifu, na atabiri hivi kuhusu mwanaye: ‘Ataitwa nabii wa Aliye Juu Zaidi, naye ataenda mbele ya Yehova kumtayarishia njia. Atawaambia watu kwamba wanapaswa kuokolewa kwa kusamehewa dhambi zao.’

Kufikia wakati huo Mariamu, ambaye kwa wazi angali mwanamke ambaye hajaolewa, amefika nyumbani Nazareti. Atapatwa na nini itakapojulikana wazi kwamba ana mimba? Luka 1:56-80; Mambo ya Walawi 12:2, 3.

◆ Yohana alimzidi Yesu umri kwa miaka mingapi?

◆ Ni mambo gani yaliyotokea wakati Yohana alipokuwa mwenye umri wa siku nane?

◆ Yohana alitabiriwa angefanya kazi gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki