Sura 9
Maisha ya Mapema ya Jamaa ya Yesu
YESU anapokuwa akikua katika Nazareti, ni mji mdogo, usio wa maana sana. Uko katika nchi ya vilima-vilima katika eneo liitwalo Galilaya, si mbali na Bonde zuri la Yezreeli.
Wakati Yesu, labda akiwa na umri wa miaka miwili anapoletwa hapa na Yusufu na Mariamu kutoka Misri, kwa wazi ndiye mtoto wa pekee wa Mariamu. Lakini si kwa muda mrefu. Baada ya wakati, Yakobo, Yusufu, Simoni, na Yuda wazaliwa, na Mariamu na Yusufu wazaa wasichana pia. Hatimaye Yesu awa na angalau ndugu na dada sita wachanga zaidi yake.
Yesu ana watu wa ukoo wengine pia. Tayari sisi tunajua habari za Yohana binamu yake mwenye umri mkubwa kuliko wake, ambaye aishi umbali wa maili nyingi katika Yudea. Lakini Salome ambaye yaonekana ni dada ya Mariamu, aishi karibu zaidi katika Galilaya. Salome ameolewa na Zebedayo, kwa hiyo, wale wana wao wawili, Yakobo na Yohana, wangekuwa ni binamu za Yesu. Hatujui kama, walipokuwa wakikua, Yesu atumia wakati mwingi akiwa pamoja na wavulana hao, lakini baadaye wawa waandamani wa karibu.
Yusufu hana budi kufanya kazi kwa bidii ili kuruzuku familia yake inayoongezeka. Yeye ni seremala. Yusufu amlea Yesu kama mwana wake mwenyewe, kwa hiyo Yesu aitwa “mwana wa seremala.” Yusufu amfundisha Yesu awe seremala pia, naye ajifunza vizuri sana. Ndiyo sababu baadaye watu wasema kwa habari za Yesu, “Huyu si yule seremala”?
Maisha ya familia ya Yusufu yategemea sana ibada ya Yehova Mungu. Kupatana na Sheria ya Mungu, Yusufu na Mariamu huwapa watoto wao mafundisho ya kiroho ‘waketipo nyumbani mwao, watembeapo njiani, walalapo, na waamkapo.’ Kuna sinagogi katika Nazareti, nasi twaweza kuwa na hakika kwamba Yusufu huipeleka pia kwa ukawaida familia yake wakaabudu humo. Lakini bila shaka wapata shangwe yao kuu zaidi katika safari za ukawaida za kwenda kwenye hekalu la Yehova katika Yerusalemu. Mathayo 13:55, 56; 27:56; Marko 15:40; 6:3; Kumbukumbu 6:6-9.
▪ Yesu ana angalau ndugu na dada wangapi wachanga zaidi yake, na ni yapi majina ya baadhi yao?
▪ Binamu watatu wa Yesu wanaojulikana vizuri zaidi ni akina nani?
▪ Hatimaye Yesu afanya kazi gani ya kimwili, na kwa nini?
▪ Ni mafundisho gani ya muhimu ambayo Yusufu aipa familia yake?