Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 10/15 kur. 23-24
  • Maisha ya Yesu ya Kijamaa Hapo Mwanzoni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maisha ya Yesu ya Kijamaa Hapo Mwanzoni
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Maisha ya Mapema ya Jamaa ya Yesu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Maisha ya Utotoni Huko Nazareti
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Alikuwa Baba na Mume Aliyemwogopa Mungu
    Igeni Imani Yao
  • Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na Akavumilia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 10/15 kur. 23-24

Maisha na Huduma ya Yesu

Maisha ya Yesu ya Kijamaa Hapo Mwanzoni

YESU anapokua katika Nazareti, huo ni mji mdogo, usio na maana. Uko kwenye nchi ya kilimani ya sehemu inayoitwa Galilaya, si mbali kutoka Bonde la Yezreeli lenye kuvutia.

Wakati Yesu, labda akiwa na miaka miwili hivi, anapoletwa hapa kutoka Misri na Yusufu na Mariamu, kwa wazi yeye ndiye mtoto pekee wa Mariamu. Lakini haendelei kuwa mtoto pekee kwa muda mrefu. Punde si punde, Yakobo, Yusufu, Simoni, na Yuda wanazaliwa, na Mariamu na Yusufu wanakuwa wazazi wa wasichana pia. Mwishowe Yesu anakuwa, angalau, na ndugu na dada sita.

Yesu pia ana watu wengine wa ukoo. Tayari tunajua juu ya Yohana, binamu yake, anayeishi maili nyingi kutoka hapo, huko Yudea. Lakini anayeishi karibu zaidi katika Galilaya ni Salome, ambaye inaelekea ni dada yake Mariamu. Salome ameolewa na Zebedayo, kwa hiyo wavulana wao wawili, Yakobo na Yohana, wangekuwa binamu zake Yesu. Hatujui kama, alipokuwa akikua, Yesu alitumia wakati mwingi akiwa na wavulana hao, lakini baadaye walikuja kuwa wenzi wa karibu, kama tutakavyoona.

Inakuwa lazima Yusufu afanye kazi kwa bidii sana ili aruzuku jamaa yake inayoongezeka. Yeye ni seremala. Yusufu anamlea Yesu kama mtoto wake mwenyewe, na kwa hiyo Yesu anaitwa ‘mwana wa seremala.’ Yusufu anamfunza Yesu awe seremala pia, naye anajifunza vizuri. Ndiyo sababu baadaye watu wanasema hivi juu ya Yesu, ‘Huyu ndiye seremala.’

Maisha ya jamaa ya Yusufu yamekazwa juu ya ibada ya Yehova Mungu. Kwa kulingana na sheria ya Mungu, Yusufu na Mariamu wanawapa watoto wao maagizo ya kiroho ‘wanapoketi katika nyumba yao, wanapotembea barabarani, wanapolala na wanapoamka.’ Kuna sinagogi katika Nazareti, na tunaweza kuwa na uhakika kwamba Yusufu pia anapeleka jamaa yake kwa ukawaida wakaabudu huko. Lakini bila shaka wanapata furaha kubwa zaidi katika safari za ukawaida za kwenda kwenye hekalu la Yehova katika Yerusalemu, kama tutakavyochunguza katika makala yetu inayofuata. Mathayo 13:55, 56; 27:56; Marko 15:40; 6:3; Kumbukumbu la Torati 6:6-9.

◆ Yesu alikuwa na ndugu na dada wadogo wangapi, na baadhi yao waliitwa nani?

◆ Binamu ya Yesu watatu wenye kujulikana sana nani?

◆ Kazi ya kimwili ya Yesu ilikuwa kazi gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki