Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 25
  • Huruma kwa Mwenye Ukoma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Huruma kwa Mwenye Ukoma
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Huruma kwa Mwenye Ukoma
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Amponya Mtu Mwenye Ukoma kwa Huruma
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mwenye Ukoma Mmoja Alimtukuza Mungu
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • “Kuujua Upendo wa Kristo”
    Mkaribie Yehova
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 25

Sura 25

Huruma kwa Mwenye Ukoma

YESU na wanafunzi wake watembeleapo miji ya Galilaya, habari juu ya maajabu anayofanya zaenea sehemu zote za wilaya. Habari za matendo yake zafikia mji mmoja ambako kuna mwanamume mwenye ugonjwa wa ukoma. Tabibu Luka aeleza kuwa mtu huyo alikuwa “amejaa ukoma.” Ugonjwa huo wa kuogopesha sana, ukiwa katika hatua zake za kukolea, unaumbua pole kwa pole sehemu mbalimbali za mwili. Kwa hivyo mwenye ukoma huyo yu katika hali ya kusikitikiwa.

Yesu afikapo mjini, mwenye ukoma amkaribia. Kulingana na Sheria ya Mungu, mwenye ukoma apaswa kupaaza sauti ya kuonya akisema, “Ni najisi, ni najisi!” ili alinde wengine wasimkaribie mno na kuwa katika hatari ya kuambukiwa. Sasa mwenye ukoma huyo aanguka kifudifudi, na kumwomba Yesu hivi: “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.”

Ni imani iliyoje mtu huyo aliyo nayo kwa Yesu! Hata hivyo, hakika ugonjwa wake wa kusikitisha wamfanya aonekane vibaya sana! Yesu atafanya nini? Wewe ungefanya nini? Kwa kuvutwa na huruma, Yesu anyoosha mkono na kumgusa mtu yule, akisema: “Nataka; takasika.” Halafu ukoma watoweka na kumwacha mara hiyo.

Je! wewe ungependa mtu mwenye huruma kama huyo awe mfalme wako? Njia ambayo Yesu amtendea mwenye ukoma huyo yatupa sisi uhakika kwamba wakati wa utawala wa Ufalme Wake, unabii huu wa Biblia utatimizwa: “Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, na nafsi za wahitaji ataziokoa.” Ndiyo, hapo ndipo Yesu atakapoitimiza tamaa ya moyo wake ya kusaidia wote wenye kutaabika.

Hata kabla ya kuponywa kwa mwenye ukoma huyo, huduma ya Yesu imekuwa ikitokeza msisimuko mkubwa kati ya watu. Kwa kutimiza unabii wa Isaya, sasa Yesu amwagiza hivi mtu huyo aliyeponywa: “Angalia, usimwambie mtu neno lolote.” Halafu amwagiza hivi: “Enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.”

Lakini mtu huyo afurahi sana hivi kwamba ashindwa kunyamaza asieleze wengine habari za muujiza huo. Aenda zake na kuanza kueneza habari hizo kila mahali, na yaonekana afanya watu wapendezwe sana na kuingiwa na hamu nyingi hivi kwamba Yesu awa hawezi kuingia mji kwa njia ya waziwazi. Hivyo, Yesu akaa mahali pa upweke-upweke ambako hakuna mtu anayeishi, na watu wa kutoka kila mahali waja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Luka 5:12-16; Marko 1:40-45; Mathayo 8:2-4; Walawi 13:45; 14:10-13; Zaburi 72:13; Isaya 42:1, 2.

▪ Ukoma waweza kuwa na matokeo gani, na mtu mwenye ukoma alipaswa kutoa onyo gani?

▪ Mwenye ukoma mmoja amsihije Yesu, nasi twaweza kujifunza nini kutokana na itikio la Yesu?

▪ Mtu huyo aliyeponywa akosaje kumtii Yesu, na matokeo yawa nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki