Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 127
  • Azikwa Ijumaa—Ziara Tupu Jumapili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Azikwa Ijumaa—Ziara Tupu Jumapili
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Azikwa Ijumaa—Ziara Tupu Jumapili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Mwili wa Yesu Watayarishwa na Kuzikwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kushika Sabato?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Siku ya Mwisho ya Maisha ya Yesu ya Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 127

Sura 127

Azikwa Ijumaa—Ziara Tupu Jumapili

KUFIKIA sasa inakaribia jioni ya Ijumaa, na Sabato ya Nisani 15 itaanza wakati wa jua kutua. Maiti ya Yesu yanyong’onyea juu ya mti, lakini wale wezi wawili walio kando zake bado wako hai. Alasiri ya Ijumaa yaitwa Maandalio kwa sababu huu ndio wakati ambao watu hutayarisha vyakula na kumaliza kazi nyingine yoyote inayopasa kufanywa ambayo haiwezi kungoja mpaka baada ya Sabato.

Sabato ambayo iko karibu kuanza si kwamba tu ni Sabato ya kawaida (ile siku ya saba ya juma) bali pia ni Sabato mara mbili, au Sabato “kubwa.” Inaitwa hivyo kwa sababu Nisani 15, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya ile Sikukuu ya siku saba ya Mikate Isiyotiwa Chachu (na sikuzote hiyo huwa sabato bila kujali inakuwa siku gani ya juma), imekuwa siku ile ile ya Sabato ya kawaida.

Kulingana na Sheria ya Mungu, miili haipasi kuachwa juu ya mti usiku kucha. Kwa hiyo Wayahudi wamwomba Pilato kwamba vifo vya hao wanaouawa viharakishwe kwa kuivunja miguu yao. Kwa hiyo, askari wavunja miguu ya wale wezi wawili. Lakini kwa kuwa Yesu aonekana kuwa amekufa, miguu yake haivunjwi. Hilo latimiza andiko hili: “Hapana mfupa wake utakaovunjwa.”

Hata hivyo, ili kuondoa shaka lolote kwamba kwa kweli Yesu amekufa, askari mmoja adunga upande wake kwa mkuki. Mkuki huo wachoma sehemu iliyo karibu na moyo wake, na mara hiyo damu na maji vyatoka. Mtume Yohana ambaye ni shahidi anayeyaona hayo, aripoti kwamba hilo latimiza andiko jingine: “Watamtazama yeye waliyemchoma.”

Yusufu wa kutoka jiji la Arimathea, ambaye ni mshiriki wa Sanhedrini mwenye sifa njema, yupo pia mahali pale pa mauaji hayo. Yeye alikataa kupiga kura ya kuunga mkono kitendo kisicho cha haki cha mahakama kuu dhidi ya Yesu. Kwa kweli Yusufu ni mwanafunzi wa Yesu, ingawa amekuwa na woga kujitambulisha kuwa mmoja wao. Hata hivyo, sasa, yeye aonyesha ujasiri kwa kumwendea Pilato kumwomba mwili wa Yesu. Pilato amwita ofisa mkuu wa jeshi, na baada ya ofisa huyo kuthibitisha kwamba Yesu amekufa, Pilato aagiza Yusufu apewe maiti hiyo.

Yusufu autwaa mwili na kuufunga kwa nguo nzuri ya kitani kuutayarisha kwa ajili ya maziko. Asaidiwa na Nikodemo, mshiriki mwingine wa Sanhedrini. Nikodemo pia ameshindwa kuungama imani yake katika Yesu kwa sababu ahofia kupoteza cheo chake. Lakini sasa yeye aleta furushi ambalo lina kilo 33 za manemane na uudi ambavyo ni vya bei kubwa. Wafunga mwili wa Yesu kwa vitambaa ambavyo vina viungo hivyo, kama vile Wayahudi walivyo na desturi ya kutayarisha miili kwa ajili ya maziko.

Halafu mwili huo walazwa katika ziara (kaburi) jipya la ukumbusho la Yusufu ambalo limechongwa katika mwamba kwenye bustani iliyo karibu. Mwishowe, jiwe kubwa lavingirishwa penye mlango wa ziara. Ili kumaliza mazishi kabla ya Sabato, mwili watayarishwa kwa haraka. Kwa hiyo, Mariamu Magdalene na Mariamu mama wa Yakobo Mdogo, ambao labda wamekuwa wakisaidia katika matayarisho, warudi nyumbani haraka ili watayarishe viungo zaidi pamoja na mafuta yenye manukato. Baada ya Sabato, wao wanapanga kuutia mwili wa Yesu viungo zaidi ili kuuhifadhi kwa muda mrefu zaidi.

Siku ifuatayo, ambayo ni Jumamosi (Sabato), makuhani wakuu na Mafarisayo wamwendea Pilato na kusema: “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.”

“Mna askari,” Pilato ajibu. “Nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.” Kwa hiyo wakaenda na kufanya kaburi liwe salama kwa kulitia lile jiwe kalafati na kuweka askari Waroma kuwa walinzi.

Mapema asubuhi ya Jumapili Mariamu Magdalene, Mariamu mama yake Yakobo, pamoja na Salome, Yoana, na wanawake wengine, waja na viungo kwenye ziara ili wautie viungo mwili wa Yesu. Wakiwa njiani wanaambiana: “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?” Lakini wafikapo, wakuta kwamba tetemeko la dunia limetokea na malaika wa Yehova amevingirisha mbali lile jiwe. Walinzi wameondoka, na ziara liko tupu! Mathayo 27:57–28:2; Marko 15:42–16:4; Luka 23:50–24:3, 10; Yohana 19:14, 31–20:1; 12:42; Walawi 23:5-7; Kumbukumbu 21:22, 23; Zaburi 34:20; Zekaria 12:10.

▪ Kwa nini Ijumaa yaitwa Maandalio, na Sabato “kubwa” ni nini?

▪ Ni maandiko gani yatimizwa kuhusiana na mwili wa Yesu?

▪ Yusufu na Nikodemo wahusikaje na mazishi ya Yesu, nao wana uhusiano gani na Yesu?

▪ Makuhani wamwomba Pilato nini, naye aitikiaje?

▪ Ni jambo gani latokea mapema asubuhi ya Jumapili?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki