Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • sp kur. 11-12
  • Mashetani ni Wauaji!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mashetani ni Wauaji!
  • Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je Ziko Kweli?
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Ana Nguvu Kuliko Roho Waovu
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Mawakili wa Uovu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Ukweli Kuhusu Malaika
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Je, Roho Waovu Ni Halisi?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je Ziko Kweli?
sp kur. 11-12

Mashetani ni Wauaji!

Sikuzote Shetani na roho waovu wamekuwa wakatili na hatari. Katika nyakati za kale Shetani aliua mifugo na watumishi wa Ayubu mwaminifu. Kisha, akaua watoto kumi wa Ayubu kwa kutokeza “upepo mkali” uharibu nyumba walimokuwa. Baada ya hapo Shetani akampiga Ayubu kwa “majipu yenye maumivu makali kuanzia wayo wa mguu mpaka utosini.”—Ayubu 1:7-19; 2:7.

Katika siku za Yesu, mashetani waliwafanya watu fulani kuwa bubu na vipofu. (Mathayo 9:32, 33; 12:22) Walimtesa mwanamume mmoja na kumfanya ajikatekate kwa mawe. (Marko 5:5) Walimfanya mvulana mmoja apige kelele, wakamwangusha chini, “na kumfanya agaegae sana.”—Luka 9:42.

Shetani na mashetani wanamfanya Ayubu augue majipu yenye maumivu makali, na wanamfanya mtu agaegae chini

Nyakati zilizopita, mashetani waliwafanya watu fulani wawe wagonjwa na kuwafanya wengine wagaegae

Leo, Shetani na roho wake waovu ni wauaji kama vile ambavyo wamekuwa sikuzote. Kwa kweli, utendaji wao mwovu umeongezeka tangu walipotupwa kutoka mbinguni. Ripoti kutoka kote ulimwenguni zinathibitisha jinsi walivyo wakatili. Wao huwatesa watu wengine kwa magonjwa. Huwasumbua wengine usiku, wakiwanyima usingizi au kuwafanya waote ndoto zenye kuogopesha. Huwatendea wengine vibaya kingono. Pia wao huwafanya watu wengine wawe vichaa, waue, au wajiue.

Mashetani yanafanya mtu fulani awe mkatili, na kumfanya mtu aote ndote yenye kuogopesha usiku

Leo Mashetani huwafanya watu fulani wawe wakatili; wao husumbua wengine usiku, wakiwafanya waote ndoto zenye kuogopesha

Lintina, anayeishi Suriname, alisema kwamba shetani, au roho mmoja mbaya, aliua washiriki 16 wa familia yake na kumtesa kimwili na kiakili kwa miaka 18. Kutokana na mambo ambayo amejionea yeye mwenyewe, anasema kwamba mashetani “hufurahia kuwatesa mateka wao, na hata kuwaua.”

Lakini Yehova anaweza kuwalinda watumishi wake dhidi ya mashambulio ya Shetani.—Methali 18:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki