Makao Makuu ya Ulimwengu na Ofisi ya Tawi Makuu ya Mashahidi wa Yehova
MAKAO MAKUU YA ULIMWENGU YA MASHAHIDI WA YEHOVA
[Picha katika ukurasa wa 352, 353]
Utendaji wa duniani pote wa Mashahidi wa Yehova umeelekezwa kutoka Brooklyn, New York, Marekani, tangu 1909. Majengo haya yamekuwa ofisi za makao makuu tangu 1980
[Picha katika ukurasa wa 352]
Kitovu cha Elimu cha Watchtower, katika Patterson, New York (kilikuwa kikijengwa katika 1992)
[Picha katika ukurasa wa 353]
Baadhi ya majengo ya makao ya maelfu wanaotumikia kwenye makao makuu ya ulimwengu
[Picha katika ukurasa wa 354]
Zile zilizokuwa hoteli katika Brooklyn zimerekebishwa ili kuandaa nafasi kwa ajili ya wafanyakazi wa kujitolea 1,476 zaidi
[Picha katika ukurasa wa 354]
Makao ya familia ya Betheli katika Wallkill, New York
[Picha katika ukurasa wa 354, 355]
Katika majengo haya ya viwanda (katika Brooklyn, New York), Biblia, vitabu, na broshua katika lugha 180 hutokezwa ili zigawanywe duniani pote
[Picha katika ukurasa wa 356]
Mamilioni ya kaseti za habari ya Biblia hutokezwa katika kiwanda hiki katika Brooklyn kila mwaka. Kutoka hapa, usafirishaji hufanywa pia. Kila mwaka fasihi za Biblia na vifaa vinginevyo zaidi ya tani 15,000 husafirishwa hadi kwenye sehemu zote za ulimwengu
[Picha katika ukurasa wa 356]
Katika kiwanda hiki kwenye Watchtower Farms, karibu na Wallkill, New York, mamia ya mamilioni ya nakala za “Mnara wa Mlinzi” na “Amkeni!,” katika lugha 14, huchapwa kila mwaka
Mashahidi wa Yehova na mashirika ya kisheria wanayotumia wana ofisi na viwanda vya kuchapia katika sehemu nyingi za ulimwengu. Picha zilizoko kwenye kurasa zinazofuata zinaonyesha majengo mengi, ingawa si yote. Mahali ambapo majengo mapya yalikuwa yakijengwa katika 1992, michoro yayo imeonyeshwa. Tarakimu zilizotolewa ni za kufikia 1992.
AMERIKA KASKAZINI NA WEST INDIES
ALASKA
[Picha katika ukurasa wa 357]
Wanaozuru ofisi ya tawi ya Sosaiti hukaribishwa kwa uchangamfu. Huku nchini Alaska, kama kwingineko, Mashahidi wa Yehova huhubiri nyumba kwa nyumba, ingawa nyakati nyingine hali-joto hushuka kufikia Sentigredi 50 chini ya sifuri.
[Picha katika ukurasa wa 357]
Ndege inayotumiwa kusafirisha wapiga-mbiu wa Ufalme kwenye sehemu za mbali za eneo
BAHAMAS
[Picha katika ukurasa wa 357]
Vichapo vya Watch Tower vilifika Bahamas kufikia 1901. Kutolewa kwa ushahidi kwa njia ya kawaida kulifanywa huku kwanza katika 1926. Tangu wakati huo fasihi za Biblia zipatazo kuwa zaidi ya 4,600,000 zimegawanywa katika visiwa vinavyosimamiwa sasa na ofisi hii.
BARBADOS
[Picha katika ukurasa wa 358]
Vikundi vya kidini zaidi ya 140 katika Barbados hudai kuwa vya Kikristo. Tangu 1905, Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakiwasaidia watu huku wajionee wenyewe yale ambayo Biblia husema.
BELIZE
[Picha katika ukurasa wa 358]
Karibu nusu ya idadi ya watu katika Belize huishi mashambani. Ili kufikia vijiji fulani vya ndanindani, Mashahidi wa Yehova husafiri kila mwaka kwa miguu wakiwa na mifuko na mikoba.
KOSTA RIKA
[Picha katika ukurasa wa 358]
Sosaiti ilifungua ofisi ya tawi katika Kosta Rika kwanza mwaka 1944. Tangu miaka ya 1950, Wakosta Rika wanaoshiriki katika ibada ya kweli wamefikia idadi ya maelfu.
JAMHURI YA DOMINIKA
[Picha katika ukurasa wa 359]
Fasihi za Watch Tower ziligawanywa huku mapema kama 1932. Lakini mafunzo ya binafsi ya watu wanaopendezwa yalianza mwaka 1945, wakati wamishonari wanaoonyeshwa upande wa kushoto walipowasili. Katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu makumi ya maelfu ya watu wamekuwa na hamu ya kujifunza Biblia pamoja na Mashahidi, majengo haya ya tawi yamehitajiwa.
EL SALVADOR
[Picha katika ukurasa wa 359]
Ushahidi fulani ulitolewa huku katika 1916. Hata hivyo, ilikuwa kwanza katika 1945 kwamba angalau mtu mmoja katika El Salvador alikuwa tayari kupata ubatizo wa maji wa Kikristo (kama inavyoonyeshwa hapa). Tangu wakati huo, maelfu zaidi wamekuwa watumishi wa Yehova.
GUADELOUPE
[Picha katika ukurasa wa 359]
Uwiano wa mhubiri na idadi ya watu wote katika eneo linalotumikiwa na ofisi hii ya tawi ni mmojawapo ulio bora sana ulimwenguni. Watu wengi katika Guade- loupe hupokea habari njema kwa uthamini.
KANADA
[Picha katika ukurasa wa 360, 361]
Ofisi ya Sosaiti katika Kanada husimamia kuhubiriwa kwa habari njema katika nchi ya pili kwa ukubwa duniani. Wapiga-mbiu wa Ufalme zaidi ya 100,000 wana shughuli nyingi katika nchi hii.
Jengo la usimamizi (picha iliyo juu ya ile ya jengo la tawi la sasa)
[Picha katika ukurasa wa 360]
Maeneo ya Kaskazini-Magharibi
[Picha katika ukurasa wa 360]
Kambi za ukataji-miti za British Columbia
[Picha katika ukurasa wa 360]
Malisho ya ng’ombe ya Alberta
[Picha katika ukurasa wa 361]
Quebec ya Kifaransa
[Picha katika ukurasa wa 361]
Mikoa ya Pwani
GUATEMALA
[Picha katika ukurasa wa 360]
Ingawa Kihispania ndiyo lugha ya taifa ya Guatemala, namna mbalimbali za lugha ngumu za Kihindi husemwa huku. Ofisi ya Sosaiti hujaribu kuona kwamba kila mtu ana fursa ya kusikia kuhusu Ufalme wa Mungu.
HAITI
[Picha katika ukurasa wa 361]
Kumtumikia Yehova huletea Mashahidi wa Yehova shangwe nyingi katika Haiti, kujapokuwa hali zinazowazunguka ambazo mara nyingi huwa ngumu.
HONDURAS
[Picha katika ukurasa wa 362]
Tangu 1916, muda wa saa zaidi ya 23,000,000 zimetolewa katika kufundisha wenyeji wa nchi hii Biblia. Nyakati nyingine, Mashahidi wa Yehova wamelazimika kufundisha watu jinsi ya kusoma na kuandika (kama uonavyo hapa) ili kuwawezesha wajifunze Neno la Mungu wao wenyewe.
JAMAIKA
[Picha katika ukurasa wa 362]
Mamia katika Jamaika walikuja kuwa watumishi wa Yehova waliojitoa wakati ambapo wale waliotazamia kuwa warithi wa Ufalme wa kimbingu walipokuwa wakikusanywa. Tangu 1935, maelfu zaidi wamejiunga katika kuhubiri ujumbe wa Ufalme. Ofisi hii ya tawi inajengwa ili kusaidia kushughulikia mahitaji yao ya kiroho.
VISIWA VYA LEEWARD (ANTIGUA)
[Picha katika ukurasa wa 362]
Mapema kama 1914, habari njema zilikuwa zikihubiriwa katika visiwa vinavyoshughulikiwa sasa na ofisi hii. Tangu wakati huo, watu katika sehemu hii ya dunia wamealikwa tena na tena ‘wayatwae maji ya uzima bure.’—Ufu. 22:17.
MEXICO
[Picha katika ukurasa wa 363]
Kituo kipya cha kutoa elimu ya Biblia kikijengwa na Mashahidi wa Yehova nchini Mexico
[Picha katika ukurasa wa 363]
Ofisi zikitumiwa katika 1992
[Picha katika ukurasa wa 363]
Fasihi za Biblia zinazochapwa hapa huandalia ugavi Mashahidi zaidi ya 410,000 wenye bidii katika Mexico na nchi nyinginezo za karibu zenye kusema Kihispania
[Picha katika ukurasa wa 363]
Kuanzia 1986 hadi 1992, mafunzo ya Biblia nyumbani zaidi ya asilimia 10 yaliyoongozwa na Mashahidi ulimwenguni pote yalikuwa katika Mexico, mengi yayo yakifanywa kwa vikundi vya familia
[Grafu katika ukurasa wa 363]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Mafunzo ya Biblia Katika Mexico
500,000
250,000
1950 1960 1970 1980 1992
MARTINIQUE
[Picha katika ukurasa wa 364]
Mbegu za ukweli zilipandwa huku mapema kama 1946. Lakini wakati Xavier na Sara Noll (wanaoonyeshwa hapa) walipokuja kutoka Ufaransa katika 1954, walibaki na kusitawisha kupendezwa kulikopatikana. Kufikia 1992, watu zaidi ya 3,200 walikuwa wakishiriki pamoja nao katika kupiga mbiu ya ujumbe wa Ufalme.
ANTILLES YA UHOLANZI (KURASAO)
[Picha katika ukurasa wa 364]
Wamishonari 23 wametumikia katika eneo la ofisi hii ya tawi. Wawili kati ya kikundi cha awali (wanaoonyeshwa hapa) waliowasili mwaka 1946 walikuwa wangali wakifanya kazi katika 1992.
NIKARAGUA
[Picha katika ukurasa wa 364]
Kuanzia 1945, wakati wamishonari walipowasili, Mashahidi wa Yehova katika Nikaragua walianza kuongezeka. Kufikia 1992, idadi yao ilikuwa zaidi ya 9,700. Sasa watu wanaotaka Mashahidi wawafunze Biblia wanapita kwa mbali idadi ya Mashahidi wenyeji.
PANAMA
[Picha katika ukurasa wa 365]
Tangu mwisho wa karne ya 19, watu katika Panama wamekuwa wakipokea msaada wa kujifunza matakwa ya Mungu kwa ajili ya uhai wa milele.
PUERTO RIKO
[Picha katika ukurasa wa 365]
Tangu 1930, fasihi za Biblia zaidi ya 83,000,000 zimegawanywa nchini Puerto Riko, na ziara za kurudia 25,000,000 zimefanywa ili kuandaa msaada zaidi kwa watu wanaopendezwa. Kazi ya kutafsiri inayofanywa huku husaidia kufanya fasihi za Biblia zipatikane kwa watu wapatao 350,000,000 ulimwenguni pote wanaosema Kihispania.
TRINIDAD
[Picha katika ukurasa wa 365]
Kazi ya kupiga mbiu ya habari njema ilikuwa tayari ikifanywa kwa bidii katika Trinidad mapema kama 1912. Mashahidi wengi, kutia hawa watatu waliozoezwa kwenye Shule ya Gileadi, wametoa wakati wao wote kwa kazi hii.
AMERIKA KUSINI
ARGENTINA
[Picha katika ukurasa wa 366]
Mpiga-mbiu wa Ufalme alitumwa kwanza kwa nchi hii katika 1924. Msaada mwingi ulitolewa baadaye na wamishonari waliozoezwa Gileadi, kutia ndani Charles Eisenhower (anayeonyeshwa hapa), aliyewasili na mke wake katika 1948. Kufikia 1992, usimamizi wa ujumla, pamoja na fasihi za Biblia, ulikuwa ukiandaliwa kutoka vifaa hivi kwa ajili ya Mashahidi wa Yehova zaidi ya 96,000 katika Argentina. Fasihi zilikuwa pia zikipelekwa kutoka huku ili kutolea ugavi Mashahidi zaidi ya 44,000 katika Chile.
BOLIVIA
[Picha katika ukurasa wa 367]
Wabolivia wamekuwa wakisikia ujumbe wa Ufalme tangu 1924. Maelfu hupokea fasihi za Biblia kwa uthamini na kunufaika na mafunzo ya Biblia nyumbani yaliyo ya kawaida.
CHILE
[Picha katika ukurasa wa 367]
Kufikia 1919, fasihi za Watch Tower zilikuwa zimefika Chile. Mahubiri yanayosimamiwa na ofisi hii yaenea sasa kutoka malisho ya kondoo yenye upepo mwingi yaliyo kusini hadi kambi za migodi za mbali zilizo kaskazini, kutoka Milima Andes hadi baharini.
EKUADO
[Picha katika ukurasa wa 367]
Mashahidi zaidi ya 870 walioacha nchi zao ili kutumika mahali penye uhitaji zaidi, walifanya sehemu kubwa katika kuhubiri habari njema katika Ekuado (kama hawa wawili wanaoonyeshwa hapa). Tawi hili sasa huandalia msaada wasifaji wa Yehova zaidi ya 22,000 wenye bidii.
BRAZILI
[Picha katika ukurasa wa 368, 369]
Katika 1992, wakati ofisi ya tawi ya Sosaiti, kiwanda cha kuchapia, na Kao la Betheli lilipokuwa likipanuliwa kufikia kiasi hiki, idadi ya Mashahidi wa Yehova katika Brazili ilikuwa zaidi ya 335,000 na walikuwa wakibatiza wanafunzi zaidi ya 27,000 kila mwaka. Kiwanda hapa pia huandaa fasihi za kugawanywa katika Bolivia, Paraguai, na Uruguai.
[Picha katika ukurasa wa 369]
Stediamu mbili kubwa zilizotumiwa kwa ajili ya mkusanyiko wa kimataifa wa Mashahidi wa Yehova katika São Paulo katika 1990; mikusanyiko mingine zaidi ya 100 ilipangwa kufanywa
[Grafu katika ukurasa wa 369]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Wapiga-Mbiu wa Ufalme Katika Brazili
300,000
200,000
100,000
1950 1960 1970 1980 1992
GUYANA
[Picha katika ukurasa wa 368, 369]
Sosaiti imekuwa na ofisi ya tawi katika Guyana tangu 1914. Mashahidi wamefikia ndani sana mashambani na kujitahidi kumtolea kila mtu fursa ya kusikia habari njema. Ingawa hata sasa idadi ya watu wa nchi hiyo ni chini ya milioni moja, Mashahidi wametoa muda wa saa zaidi ya 10,000,000 zimetolewa katika kuhubiri na kufundisha katika nchi hii.
PARAGUAI
[Picha katika ukurasa wa 369]
Kuhubiri habari njema kulianza katika Paraguai katika miaka ya katikati ya 1920. Tangu 1946, wamishonari 112 waliozoezwa Gileadi wamesaidia kutoa ushahidi. Ili kufikia vikundi vya lugha mbali na Kihispania na Kiguarani zinazosemwa huku, Mashahidi wengine wamejitolea pia kuhamia kutoka nchi mbalimbali.
Kutoka Ujerumani
Kutoka Korea
Kutoka Japani
KOLOMBIA
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 370, 371]
Mapema kama 1915, kichapo cha Watch Tower kilipelekwa kwa mtu aliyependezwa nchini Kolombia. Kufikia 1992, fasihi za Biblia zilizochapwa katika majengo haya zilikuwa zikisafirishwa ili kushughulikia mahitaji ya waeneza-evanjeli zaidi ya 184,000 katika Kolombia, Ekuado, Panama, Peru, na Venezuela.
[Ramani]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
KOLOMBIA
PERU
EKUADOR
PANAMA
VENEZUELA
PERU
[Picha katika ukurasa wa 370]
Mapema katika 1924, fasihi za Biblia ziligawanywa katika Peru na Mwanafunzi wa Biblia aliyekuwa akizuru. Kutaniko la kwanza lilifanyizwa huku miaka 21 baadaye. Sasa kuna wapiga-mbiu wa Ufalme wa Mungu zaidi ya 43,000 wanaotenda katika Peru.
[Picha katika ukurasa wa 370]
Mapainia wakihubiri katika sehemu za juu za Andes
SURINAME
[Picha katika ukurasa wa 371]
Katika 1903 hivi, kikundi cha kwanza cha funzo kilifanyizwa huku. Leo majengo haya ya tawi yanahitajiwa ili kusimamia makutaniko yaliyotawanyika kotekote nchini—katika maeneo yasiyo na maendeleo sana, wilaya, na jijini.
URUGUAI
[Picha katika ukurasa wa 372]
Tangu 1945, wamishonari zaidi ya 80 wamekuwa na sehemu katika kupiga mbiu ya Ufalme katika Uruguai. Wale wanaoonyeshwa hapa wamekuwa wakitumikia katika Uruguai tangu miaka ya 1950. Kufikia 1992, Mashahidi wenyeji zaidi ya 8,600 walikuwa wakitumikia pamoja nao.
VENEZUELA
[Picha katika ukurasa wa 372]
Baadhi ya vichapo vya Watch Tower viligawanywa katika Venezuela katika miaka ya katikati ya 1920. Mwongo mmoja baadaye mama na binti walio mapainia kutoka Marekani pamoja walianza kipindi cha kuhubiri huku kwa bidii, wakieneza jiji kuu tena na tena, pia wakizuru miji kotekote nchini. Sasa kuna Mashahidi zaidi ya 60,000 wenye bidii katika Venezuela.
[Picha katika ukurasa wa 372]
Uwanja wa mchezo wa fahali katika Valencia ukiwa na umati wa 74,600 kwa ajili ya kusanyiko la pekee katika 1988
ULAYA NA NCHI ZA MEDITERANIA
AUSTRIA
[Picha katika ukurasa wa 373]
Mapema kama miaka ya 1890, baadhi ya watu katika Austria walikuwa wakipewa fursa ya kunufaika na habari njema. Tangu miaka ya 1920, kumekuwa na ukuzi wa kiasi lakini wenye kuendelea wa idadi ya wanaosifu Yehova katika nchi hii.
[Picha katika ukurasa wa 373]
Zaidi ya makutaniko 270 hukutana katika Majumba ya Ufalme kotekote Austria
UBELGIJI
[Picha katika ukurasa wa 373]
Ubelgiji imekuja kuwa mojawapo vitovu muhimu ulimwenguni. Ili kushughulikia idadi ya watu wa namna mbalimbali wanaopatikana huku, tawi hili hugawanya fasihi za Biblia katika lugha zaidi ya 100.
UINGEREZA
[Picha katika ukurasa wa 374]
Utendaji wa Mashahidi wa Yehova zaidi ya 125,000 katika Uingereza husimamiwa kutoka ofisi hii ya tawi. Mashahidi kutoka Uingereza wamechukua migawo pia ili kueneza ujumbe wa Ufalme katika nchi nyinginezo za Ulaya pamoja na barani Afrika, Amerika Kusini, Australia, nchi za Mashariki, na visiwa vya bahari.
IBSA House
Watch Tower House
[Picha katika ukurasa wa 374]
Fasihi za Biblia huchapwa huku katika Kiingereza, Kimalta, Kigujarati, na Kiswahili
[Picha katika ukurasa wa 374]
Idara ya Utumishi hushughulikia makutaniko zaidi ya 1,300 katika Uingereza
[Picha katika ukurasa wa 374]
Ugavi wa fasihi hupelekwa kwenye sehemu zote za Uingereza, Scotland, Wales, Ireland, na Malta, kutia na nchi za Afrika na Karibea
UFARANSA
[Picha katika ukurasa wa 375]
Vichapo vyote vya Watch Tower vinavyochapwa ulimwenguni pote kwa ajili ya watu wanaosema Kifaransa, hutafsiriwa na kupangwa chapa kwa picha kwenye tawi katika Ufaransa. (Watu zaidi ya 120,000,000 husema Kifaransa.) Fasihi huchapwa huku kwa ukawaida katika lugha mbalimbali na husafirishwa kwa nchi za Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, Bahari ya Hindi, na Bahari ya Pasifiki.
Kiwanda cha kuchapia/ofisi katika Louviers
Kutafsiri
Kupanga chapa kwa picha
[Picha katika ukurasa wa 375]
Ofisi/makao katika Boulogne-Billancourt
[Picha katika ukurasa wa 375]
Makao katika Incarville kwa ajili ya familia ya Betheli
UJERUMANI
[Picha katika ukurasa wa 376, 377]
Kujapokuwa jitihada za ukatili ili kuwaangamiza katika Ujerumani wakati wa enzi ya Nazi, Mashahidi wa Yehova hawakuacha imani yao. Tangu 1946, wametumia muda wa saa zaidi ya 646,000,000 katika kueneza kweli ya Biblia kotekote nchini.
Vifaa vilivyopanuliwa katika Selters/Taunus
[Picha katika ukurasa wa 376]
Zaidi ya kutafsiri fasihi za Biblia katika Kijerumani, tawi hili katika Selters/Taunus huchapa katika lugha zaidi ya 40
[Picha katika ukurasa wa 377]
Kiasi kikubwa cha fasihi kinachotokezwa hapa husafirishwa kwa ukawaida kwenye nchi zaidi ya 20; magazeti huchapwa katika lugha nyingi na kupelekwa kwenye nchi zaidi ya 30
[Picha katika ukurasa wa 377]
Malori ya Sosaiti hutumiwa kusafirisha fasihi kotekote katika Ujerumani
SAIPRASI
[Picha katika ukurasa wa 376]
Muda mfupi baada ya kifo cha Yesu Kristo, habari njema zilikuwa zikihubiriwa kwa watu wa Saiprasi. (Mdo. 4:32-37; 11:19; 13:1-12) Katika siku za kisasa, mahubiri hayo yameanzishwa tena, na ushahidi kamili huendelea kutolewa chini ya mwelekezo wa ofisi ya tawi.
DENMARK
[Picha katika ukurasa wa 377]
Tangu miaka ya 1890, ushahidi umetolewa kwa kadiri kubwa katika Denmark. Fasihi za Biblia zimechapiwa huku si katika Kidenmark tu bali pia katika Kifaeroese, Kigreenland, na Kiiceland.
Tawi linavyoonekana kutoka juu (kiingilio kinaonyeshwa katika picha ya ndani)
ITALIA
[Picha katika ukurasa wa 378, 379]
Fasihi ya Biblia ya Kiitalia hutafsiriwa na kuchapwa huku pia. Tawi hili huchapa na kujalidi vitabu viweze kutumiwa hasa katika Italia na nchi nyinginezo jirani.
Sura mbalimbali za majengo ya tawi yaliyo karibu na Roma
[Picha katika ukurasa wa 379]
Makumi ya maelfu ya watu wameanza kukusanyika pamoja na Mashahidi wa Yehova baada ya kuona yale ambayo Biblia husema hasa
[Picha katika ukurasa wa 379]
Wajapokabiliwa na uhasama mwingi kutoka kwa Kanisa la Katoliki ya Roma, Mashahidi wa Yehova katika Italia wametumia muda wa saa zaidi ya 550,000,000 tangu 1946 katika ziara za kibinafsi kwa majirani wao ili kuzungumza nao juu ya Biblia. Kama tokeo, watu 194,000 katika Italia ni waabudu walio watendaji wa Yehova
FINLAND
[Picha katika ukurasa wa 378]
Kweli ya Biblia ilifika Finland kutoka Sweden katika 1906. Tangu wakati huo, imepelekwa kotekote nchini, hata mbali katika Mzingo Aktiki. Wengi kutoka huku wamehudhuria Shule ya Gileadi ili kuzoezwa kwa ajili ya utumishi mahali popote walipohitajiwa katika shamba la ulimwengu. Wengine walihama wao wenyewe ili kutumikia katika nchi ambako uhitaji ulikuwa mkubwa zaidi.
ICELAND
[Picha katika ukurasa wa 379]
Katika Iceland, ambayo ina idadi ya watu karibu 260,000 tu, fasihi za Biblia zaidi ya 1,620,000 zimegawanywa ili kusaidia watu kuchagua uhai. Sasa watu zaidi ya 260 huku humtumikia Yehova, Mungu wa kweli.
[Picha katika ukurasa wa 379]
Georg Lindal, aliyepainia huku kutoka 1929 hadi 1953; kwa muda mrefu wakati huo, yeye alikuwa ndiye Shahidi pekee nchini
UGIRIKI
[Picha katika ukurasa wa 380]
Mtume Paulo alikuwa mmojawapo watu wa kwanza kutangaza habari njema katika Ugiriki. (Mdo. 16:9-14; 17:15; 18:1; 20:2) Ijapokuwa Kanisa Othodoksi la Kigiriki limewanyanyasa sana Mashahidi wa Yehova kwa miaka mingi, sasa kuna watumishi waaminifu wa Yehova zaidi ya 24,000 katika nchi hii. Tawi linaloonyeshwa hapa liko umbali wa karibu kilometa 65 kaskazini mwa Athene.
[Picha katika ukurasa wa 380]
Kutoa ushahidi katika Athene
[Picha katika ukurasa wa 380]
Picha ilipigwa katika 1990 wakati wa maandamano yaliyoongozwa na makasisi dhidi ya Mashahidi
IRELAND
[Picha katika ukurasa wa 380]
Katika Ireland, itikio kwa ujumbe wa Biblia lilikuwa la polepole kwa miaka mingi. Walipata upinzani mwingi wa makasisi. Lakini baada ya miaka 100 ya kufuliza kutoa ushahidi, sasa kuna mavuno mengi ya kiroho.
Ofisi ya tawi katika Dublin
[Picha katika ukurasa wa 380]
Mapainia wawili wa muda mrefu katika utumishi wa shambani
POLAND
[Picha katika ukurasa wa 381]
Vifaa hivi vinatumiwa ili kuandaa msaada kwa Mashahidi zaidi ya 100,000 nchini Poland. Ibada yao ilipigwa marufuku kuanzia 1939 hadi 1945, lakini idadi yao iliongezeka kuanzia 1,039 katika 1939 hadi 6,994 katika 1946. Walipopigwa marufuku tena katika 1950, idadi yao ilikuwa 18,116; lakini muda mfupi baada ya marufuku hiyo kuondolewa katika 1989, ripoti zilionyesha kwamba walikuwa zaidi ya 91,000.
[Picha katika ukurasa wa 381]
Kwa miaka mingi walifanya makusanyiko madogo vichakani; sasa mikusanyiko yao hujaza stediamu kubwa zaidi nchini—na zaidi ya stediamu moja kwa wakati mmoja
Poznan (1985)
LUXEMBOURG
[Picha katika ukurasa wa 382]
Luxembourg ni mojawapo ya nchi ndogo sana za Ulaya. Lakini ujumbe wa Ufalme umehubiriwa huku pia, kwa miaka 70. Hasa kabla ya Vita ya Ulimwengu 2, msaada ulitolewa na Mashahidi waliokuja kutoka Ufaransa, Ujerumani, na Uswisi.
UHOLANZI
[Picha katika ukurasa wa 382]
Kutoka kwa tawi hili katika Emmen, usimamizi huandaliwa kwa ajili ya utendaji wa Mashahidi 32,000 wenye bidii katika Uholanzi. Kazi ya kutafsiri fasihi zote katika Kiholanzi hufanywa katika vifaa hivi. Kazi nyingi ya kutokeza kaseti za vidio za Kibiblia katika lugha za Ulaya hushughulikiwa huku pia.
NORWAY
[Picha katika ukurasa wa 383]
Miaka mia moja iliyopita, Mnorway aliyehamia Marekani na kujifunza kweli za Biblia huko alileta hizo habari njema katika mji alimozaliwa. Tangu wakati huo, Mashahidi wa Yehova wamezuru kila sehemu ya Norway tena na tena ili kuzungumza na watu kuhusu Ufalme wa Mungu.
URENO
[Picha katika ukurasa wa 383]
Kwa miongo ya miaka baada ya serikali kutia sahihi mkataba pamoja na Vatikani, polisi walikamata Mashahidi na kuwafukuza wamishonari wao. Lakini Mashahidi waliobaki waliendelea kukutana kwa ajili ya ibada, kuhubiri wengine, na kuongezeka. Mwishowe, katika 1974 walitambuliwa kisheria.
Ofisi hii husimamia utendaji wa Mashahidi zaidi ya 40,000 katika Ureno. Pia imetoa msaada mwingi kwa nchi za Afrika zilizokuwa na uhusiano wa karibu na Ureno
[Picha katika ukurasa wa 383]
Mkusanyiko wa kimataifa uliofanywa jijini Lisbon mwaka 1978
SWEDEN
[Picha katika ukurasa wa 383]
Kwa miaka zaidi ya 100, Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakihubiri nchini Sweden. Katika muda wa miaka kumi iliyopita, wametumia muda wa saa zaidi ya 38,000,000 katika utendaji huu. Makutaniko mengi nchini Sweden sasa husema lugha nyingine nyingi mbali na Kisweden.
[Picha katika ukurasa wa 383]
Ili kusaidia watu wa kila aina nchini Sweden, vichapo hupatikana hapa katika lugha 70
HISPANIA
[Picha katika ukurasa wa 384]
Tawi hili hushughulikia Mashahidi zaidi ya 92,000 katika Hispania. Hilo huchapa “Mnara wa Mlinzi” na “Amkeni!” kwa ajili ya Hispania na Ureno pia. Kujapokuwa jitihada nyingi za makasisi Wakatoliki za kutumia Serikali ili kukomesha Mashahidi wa Yehova, Mashahidi wameshiriki kweli za Biblia na Wahispania tangu 1916. Hatimaye, katika 1970, wakati Mashahidi wa Yehova nchini Hispania walipokuwa zaidi ya 11,000, wao walitambuliwa kisheria. Tangu wakati huo, idadi yao imeongezeka mara nane.
[Picha katika ukurasa wa 384]
Makutaniko zaidi ya 1,100 sasa hukutana kwa uhuru katika Majumba ya Ufalme yanayopatikana kotekote nchini
USWISI
[Picha katika ukurasa wa 384]
Tangu 1903 Watch Tower Society imekuwa na ofisi katika Uswisi. Kimojawapo viwanda vya uchapaji vya Sosaiti vya mapema sana katika Ulaya kilikuwa katika nchi hii. Kwa miaka mingi tawi hapa katika Thun lilichapa magazeti ili yatumiwe katika nchi nyinginezo nyingi.
AFRIKA
BENIN
[Picha katika ukurasa wa 385]
Nchini Benin kuna vikundi vya kikabila vipatavyo 60 vinavyosema lahaja 50. Wakati maelfu ya watu hao walipojiweka huru kutoka kwa dini zao za awa- li, hilo liliwaghadhibisha makuhani wa makago na makasisi wa Jumuiya ya Wakristo pia. Lakini mawi- mbi ya mnyanyaso yenye kurudia-rudia hayaku- komesha ukuzi wa ibada ya kweli katika nchi hii.
[Picha katika ukurasa wa 385]
Mkusanyiko uliofanywa katika 1990
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI
[Picha katika ukurasa wa 385]
Mapema kama 1947, ujumbe wa Ufalme ulianza kufikia watu huku. Mwanamume aliyekuwa amehudhuria mikutano fulani ya Mashahidi kwingineko alishiriki na wengine yale aliyokuwa amejifunza. Upesi kukawa na kikundi cha funzo, wale waliohudhuria wakaanza upesi kutoa ushahidi, na wale walioabudu Yehova wakaongezeka idadi.
CÔTE D’IVOIRE
[Picha katika ukurasa wa 386]
Wamishonari waliozoezwa Gileadi walisaidia kuanzisha ibada ya kweli katika nchi hii ya Afrika Magharibi katika 1949. Wamishonari zaidi ya mia moja wametumika huku. Kila mwaka, muda wa saa zaidi za milioni moja unatumiwa sasa katika kuwatafuta watu wenye njaa ya kiroho katika eneo linaloshughulikiwa na ofisi hii ya tawi.
GHANA
[Picha katika ukurasa wa 386, 387]
Kuhubiriwa kwa habari njema katika Ghana kulianza katika 1924. Sasa ofisi hii katika Accra husimamia makutaniko zaidi ya 640 katika Ghana. Pia imeshughulikia kazi ya kutafsiri fasihi za Biblia katika Kiewe, Kiga, na Kitwi na kuichapa katika lugha hizo.
[Picha katika ukurasa wa 387]
Kukutana katika Jumba la Ufalme linalopakana na ofisi ya tawi
KENYA
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 387]
Katika 1931, Mashahidi wa Yehova wawili walisafiri kutoka Afrika Kusini ili kuhubiri katika Kenya. Tangu 1963 katika nyakati mbalimbali, ofisi ya Sosaiti nchini Kenya imeandaa usimamizi wa kazi ya kueneza evanjeli katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashariki (kama inavyoonyeshwa chini). Mikusanyiko ya kimataifa nchini Kenya katika 1973, 1978, na 1985 imechangia kwenye ushahidi uliotolewa.
[Ramani]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
KENYA
UGANDA
SUDAN
ETHIOPIA
JIBUTI
SOMALIA
YEMENI
SHELISHELI
TANZANIA
BURUNDI
RWANDA
[Picha katika ukurasa wa 387]
Mkusanyiko wa Nairobi (1978)
NIGERIA
[Picha katika ukurasa wa 388, 389]
Habari njema zimehubiriwa katika nchi hii tangu mapema katika miaka ya 1920. Pia waeneza-evanjeli wametumwa kutoka Nigeria hadi kwenye sehemu nyingine za Afrika Magharibi, na fasihi za Biblia zinazochapwa hapa huendelea kujazia mahitaji ya nchi za karibu. Katika Nigeria yenyewe, Mashahidi wa Yehova wamewakabidhi watu fasihi zaidi ya 28,000,000 ili kuwasaidia waelewe Neno la Mungu.
[Picha katika ukurasa wa 388]
Kutoka Idara ya Utumishi, usimamizi huandaliwa kwa ajili ya wapiga-mbiu wa Ufalme zaidi ya 160,000 katika Nigeria
[Picha katika ukurasa wa 389]
Mkusanyiko katika Calabar, Nigeria (1990)
LIBERIA
[Picha katika ukurasa wa 388]
Wale ambao wamekuwa Mashahidi wa Yehova huku wamekabili mitihani mingi ya imani yao—wanapoacha mambo mbalimbali ya ushirikina, wanapoacha kuwa na wake zaidi ya mmoja, wanaponyanyaswa na maofisa walioarifiwa vibaya kuwahusu, na wanapozungukwa na vikundi vya kisiasa na kikabila vinavyopigana. Na bado, ibada ya kweli yaendelea kuunganisha watu wa aina zote katika nchi hii.
MAURITIUS
[Picha katika ukurasa wa 389]
Mapema kama 1933, Mashahidi wenye bidii kutoka Afrika Kusini walizuru kisiwa hiki cha Bahari ya Hindi. Sasa kunao Mashahidi zaidi ya elfu moja katika Mauritius wanaohimiza majirani zao kumtafuta Yehova ili waweze kuonwa naye kwa upendeleo wakati anapoharibu mfumo mwovu wa sasa.—Sef. 2:3.
AFRIKA KUSINI
[Picha katika ukurasa wa 390]
Kwa zaidi ya miaka 80, Watch Tower Society imekuwa na ofisi ya tawi katika Afrika Kusini. Waeneza-evanjeli wenye bidii kutoka huku wamefanya mengi katika kueneza ujumbe wa Ufalme katika nchi nyinginezo za kusini na mashariki mwa Afrika. Katika eneo lililokuwa chini ya tawi hili (ambako kulikuwa na wapiga-mbiu wa Ufalme 14,674 katika 1945), sasa kuna Mashahidi wa Yehova watendaji zaidi ya 300,000.
[Picha katika ukurasa wa 391]
Watafsiri zaidi ya 110 hufanya kazi chini ya mwelekezo wa tawi hili katika kutayarisha fasihi za Biblia katika lugha 16 za Afrika
[Picha katika ukurasa wa 391]
Kazi ya kuchapa hufanyiwa hapa katika lugha zaidi ya 40
SENEGAL
[Picha katika ukurasa wa 390]
Ingawa idadi ya Mashahidi huku ni ndogo, ofisi ya tawi imejaribu kuhakikisha kwamba kila jiji, kila kikundi cha kabila, na watu wa kila dini, si katika Senegal tu bali pia katika nchi zinazozunguka, wana fursa ya kusikia ujumbe wa Biblia wenye kuchangamsha moyo.
SIERRA LEONE
[Picha katika ukurasa wa 391]
Kuhubiriwa kwa habari njema kulianza katika Sierra Leone katika mwaka 1915. Nyakati nyingine ukuzi umekuwa wa polepole. Lakini wakati wale ambao hawakushikilia viwango vya juu vya Yehova walipoondolewa na wale ambao hawakutumikia kwa makusudi mazuri wakaondoka, wale walio waaminifu-washikamanifu kwa Yehova walisitawi kiroho.
ZAMBIA
[Picha katika ukurasa wa 392]
Ofisi hii ya tawi husimamia utendaji wa Mashahidi zaidi ya 110,000 katika Afrika ya kusini na kati. Ofisi ya kwanza ya Sosaiti huku ilifunguliwa katika 1936. Tangu wakati huo, Mashahidi wa Yehova katika Zambia wamefanya ziara za kurudia zaidi ya 186,000,000 ili kutoa msaada zaidi kwa wanaopendezwa. Pia wamefundisha wengi kusoma ili waweze kujifunza Biblia binafsi na kuishiriki na wengine.
[Picha katika ukurasa wa 392]
Mfululizo wa mikusanyiko nchini Zambia katika 1992 ulihudhuriwa na 289,643
ZIMBABWE
[Picha katika ukurasa wa 392]
Mashahidi wa Yehova wamekuwa watendaji katika Zimbabwe tangu miaka ya 1920. Wakati wa miaka iliyofuata, fasihi zao zilipigwa marufuku, wakakatazwa kufanya makusanyiko, na kunyimwa idhini ya wamishonari kuweza kuhubiri wenyeji Waafrika. Hatua kwa hatua, vikwazo vilishindwa, na sasa ofisi hii huwatunza Mashahidi zaidi ya 20,000.
NCHI ZA MASHARIKI
HONG KONG
[Picha katika ukurasa wa 393]
Vichapo vya Watch Tower hutafsiriwa huku katika Kichina, ambacho husemwa na watu zaidi ya bilioni moja katika lahaja zacho nyingi. Katika Hong Kong yenyewe, kazi ya kuhubiri habari njema ilianza wakati C. T. Russell alipohutubu kwenye jumba kuu la jiji katika 1912.
INDIA
[Picha katika ukurasa wa 393]
Tawi hili husimamia kazi ya kupiga mbiu ya ujumbe wa Ufalme kwa zaidi ya moja kwa sita ya idadi ya watu duniani. Wakati huu, ofisi hii huelekeza kazi ya kutafsiri katika lugha 18 na ya kuchapa katika 19. Miongoni mwa hizo ni Kihindi (kinachosemwa na watu milioni 367) pia Kiassami, Kibengali, Kigujarati, Kikanada, Kimaleya, Kimarathi, Kinepali, Kioriya, Kipunjabi, Kitamili, Kitelugu, na Kiurdu (kila moja ikisemwa na makumi ya mamilioni).
[Picha katika ukurasa wa 393]
Mashahidi wanaohubiri katika Kimaleya
. . . katika Kinepali
. . . katika Kigujarati
JAPANI
[Picha katika ukurasa wa 394]
Mashahidi wa Yehova katika Japani, kama kwingineko, ni wapiga-mbiu wa Ufalme wa Mungu wenye bidii. Katika 1992 pekee, walitumia zaidi ya saa 85,000,000 kuhubiri habari njema. Kwa wastani, karibu asilimia 45 ya Mashahidi Wajapani hushiriki katika utumishi wa upainia kila mwezi.
[Picha katika ukurasa wa 394]
Fasihi za Biblia huchapwa huku katika lugha nyingi, kutia na Kijapani, Kichina, na lugha za Filipino
[Picha katika ukurasa wa 394]
Ofisi ya Uhandisi ya Kimkoa husaidia kazi kwenye vifaa vya tawi katika nchi mbalimbali
[Grafu katika ukurasa wa 394]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Mapainia Katika Japani
75,000
50,000
25,000
1975 1980 1985 1992
JAMHURI YA KOREA
[Picha katika ukurasa wa 395]
Fasihi za Biblia zipatazo milioni 16, kuongezea trakti, hutokezwa huku kila mwaka ili kutoa ugavi kwa Mashahidi zaidi ya 70,000 katika Jamhuri ya Korea. Karibu asilimia 40 ya Mashahidi Wakorea wako katika utumishi wa painia.
MYANMAR
[Picha katika ukurasa wa 395]
Wakati Watch Tower Society ilipofungua ofisi ya tawi huku katika 1947, kulikuwa Mashahidi wa Yehova 24 pekee nchini. Mashahidi watendaji zaidi ya 2,000 sasa katika Myanmar hujaribu kufikia si wenyeji tu wa majijini, bali pia idadi kubwa ya watu wa mashambani.
FILIPINO
[Picha katika ukurasa wa 396]
Katika 1912, C. T. Russell alihutubu katika Grand Opera House la Manila juu ya kichwa “Wafu Wako Wapi?” Tangu wakati huo Mashahidi wa Yehova huku wametumia muda wa saa zaidi ya 483,000,000 katika kutoa ushahidi kwa watu wanaopatikana katika visiwa vinavyokadiriwa kuwa 900 vya Filipino. Usimamizi wa ujumla wa Mashahidi zaidi ya 110,000 katika makutaniko 3,200 huandaliwa kutoka tawi hili. Uchapaji hufanywa hapa katika lugha nane ili kujazia mahitaji ya wenyeji.
[Picha katika ukurasa wa 396]
Mashahidi kutoka kwa baadhi ya vikundi vya lugha kuu katika Filipino
SRI LANKA
[Picha katika ukurasa wa 397]
Kabla ya Vita ya Ulimwengu 1, habari njema ilikuwa ikihubiriwa katika Ceylon (sasa Sri Lanka), kusini mwa India. Kikundi cha funzo kilipangwa upesi. Tangu 1953 Sosaiti imekuwa na ofisi ya tawi katika jiji kuu, ili kuwapa Wasinhalisi, Watamili, na vikundi vinginevyo vya kikabila nchini fursa ya kusikia ujumbe wa Ufalme.
TAIWAN
[Picha katika ukurasa wa 397]
Ushahidi fulani ulitolewa huku katika miaka ya 1920. Lakini ulitolewa kwa kuendelea zaidi katika miaka ya 1950. Sasa vifaa hivi vipya vya tawi vinajengwa ili kuandaa kitovu cha utendaji ulioongezeka katika sehemu hii ya dunia.
[Picha katika ukurasa wa 397]
Kutaniko katika Taipei
THAILAND
[Picha katika ukurasa wa 397]
Wakati wa miaka ya 1930, Mashahidi mapainia walikuja kutoka Uingereza, Ujerumani, Australia, na New Zealand ili kushiriki kweli ya Biblia na Wathailand (wakati huo ikiitwa Siam). Wajumbe kutoka nchi nyingi walihudhuria mikusanyiko ya kimataifa huku katika 1963, 1978, 1985, na 1991 ili kuwatia moyo Mashahidi wenyeji na kuchochea kuenezwa kwa ujumbe wa Ufalme.
[Picha katika ukurasa wa 397]
Mkusanyiko wa 1963
[Picha katika ukurasa wa 397]
Wajumbe kutoka ng’ambo katika 1991
VISIWA VYA PASIFIKI
FIJI
[Picha katika ukurasa wa 398]
Ofisi katika Fiji ilifunguliwa katika 1958. Kwa muda fulani ilisimamia kazi ya kupiga mbiu ya Ufalme katika nchi 12 na lugha 13. Sasa tawi la Fiji hukazia fikira visiwa karibu mia moja vinavyokaliwa vya kikundi cha Fiji.
[Picha katika ukurasa wa 398]
Mikusanyiko ya kimataifa hapa katika 1963, 1969, 1973, na 1978 ilisaidia kuwaleta Mashahidi wenyeji karibu zaidi na wale wa nchi nyinginezo
GUAM
[Picha katika ukurasa wa 398]
Ofisi katika Guam huelekeza kuhubiriwa kwa habari njema katika visiwa vilivyoenea kilometa 7,770,000 za mraba katika Bahari ya Pasifiki. Kazi ya kutafsiri fasihi za Biblia katika lugha tisa imo chini ya usimamizi wayo.
[Picha katika ukurasa wa 398]
Mara nyingi mwangalizi wa mzunguko husafiri kwa ndege kati ya visiwa
[Picha katika ukurasa wa 398]
Mashahidi wenyeji (kama wanavyoonyeshwa hapa katika Maikronesia) waweza kutumia mashua ili kufikia eneo lao
HAWAII
[Picha katika ukurasa wa 399]
Watch Tower Society imekuwa na ofisi ya tawi katika Honolulu tangu 1934. Wengine kutoka Hawaii wameshiriki kazi ya kueneza evanjeli si katika visiwa vya Hawaii tu bali pia katika Japani, Taiwan, Guam, na visiwa vya Maikronesia.
NEW CALEDONIA
[Picha katika ukurasa wa 399]
Kujapokuwa vizuizi kutoka kwa wapinzani wa kidini, Mashahidi wa Yehova walileta ujumbe wa Ufalme wa Mungu katika New Caledonia. Watu wengi walisikiliza kwa uthamini. Katika 1956 kutaniko la kwanza lilifanyizwa. Sasa huku kuna wasifaji wa Yehova zaidi ya 1,300.
NEW ZEALAND
[Picha katika ukurasa wa 399]
Katika 1947 Watch Tower Society ilifungua ofisi ya tawi katika New Zealand ili kuandaa usimamizi wa karibu zaidi wa kazi ya kuhubiri habari njema huku.
[Picha katika ukurasa wa 399]
Kazi ya kutafsiri inayofanywa katika tawi hili huwezesha wenyeji wa Samoa, Rarotonga, na Niue kupokea ujenzi wa kiroho kwa kawaida.
[Picha katika ukurasa wa 399]
Watafsiri na wasahihishaji hushirikiana ili kuandaa vichapo vya hali ya juu
AUSTRALIA
[Picha katika ukurasa wa 400]
Watch Tower Society imekuwa na ofisi ya tawi katika Australia tangu 1904. Zamani tawi hili lilisimamia kazi ya kupiga mbiu ya Ufalme kwa karibu robo ya dunia yote, kutia na China, Kusini-Mashariki mwa Asia, na visiwa vya Pasifiki Kusini.
[Picha katika ukurasa wa 400]
Ofisi ya Uhandisi ya Kimkoa husaidia katika ujenzi wa tawi katika Pasifiki Kusini na Kusini-Mashariki mwa Asia
[Picha katika ukurasa wa 400]
Wakati huu, tawi hili huchapa fasihi za Biblia katika lugha zaidi ya 25. Kiwanda cha uchapaji huku husaidia kutoa ugavi wa fasihi zinazohitajiwa na Mashahidi wapatao 78,000 walio katika sehemu zinazosimamiwa na matawi manane katika Pasifiki Kusini.
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 400]
Nchi zinazopewa ugavi wa fasihi kutoka tawi la Australia
[Ramani]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
AUSTRALIA
PAPUA NEW GUINEA
NEW CALEDONIA
VISIWI VYA SOLOMON
FIJI
WESTERN SAMOA
TAHITI
NEW ZEALAND
PAPUA NEW GUINEA
[Picha katika ukurasa wa 400]
Magumu ya pekee hukabili Mashahidi wa Yehova katika nchi hii—watu husema lugha mbalimbali zipatazo 700. Mashahidi kutoka angalau nchi kumi nyingine wamehamia huku ili kushiriki kazi. Wamejitahidi kujifunza lugha za wenyeji. Wenye kupendezwa hutafsiria wale wanaosema lugha nyingine. Picha pia hutumiwa kwa matokeo zikiwa misaada katika kufundisha.
VISIWA VYA SOLOMON
[Picha katika ukurasa wa 401]
Funzo la Biblia lililoongozwa kimataifa kwa posta lilileta ujumbe wa Ufalme kwenye Visiwa vya Solomon kufikia mapema miaka ya 1950. Kujapokuwa vizuizi vikubwa, kweli ya Biblia ilienea. Ofisi hii ya tawi na Jumba la Kusanyiko lenye nafasi kubwa ni tokeo la ustadi mwingi wa wenyeji, ushirikiano wa kimataifa, na utele wa roho ya Yehova.
TAHITI
[Picha katika ukurasa wa 401]
Kufikia miaka ya 1930, Mashahidi wa Yehova walikuwa wamefika Tahiti na ujumbe wa Ufalme. Huku, katika Bahari ya Pasifiki, ushahidi mwingi unatolewa. Wakati wa miaka minne tu iliyopita, ushahidi uliofanywa unajumlika kuwa wastani wa muda wa saa zaidi ya tano za kusema, kwa kila mwanamume, mwanamke, na mtoto katika kisiwa hicho.
SAMOA MAGHARIBI
[Picha katika ukurasa wa 401]
Samoa Magharibi ni mojawapo mataifa yaliyo madogo zaidi ulimwenguni, lakini Mashahidi wa Yehova wana ofisi ya tawi huku pia. Jengo hili lilikuwa likijengwa katika 1992 ili kushughulikia utendaji katika kisiwa hiki na vinginevyo vilivyoko karibu, kutia na Samoa ya Amerika.