Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gl kur. 4-5
  • Nchi Zinazotajwa Katika Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nchi Zinazotajwa Katika Biblia
  • ‘Ona Nchi Nzuri’
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Wa Mungu Warudi Nchini Kwao
    ‘Ona Nchi Nzuri’
  • Wayahudi Waathiriwa Na Utawala Wa Wagiriki Na Waroma
    ‘Ona Nchi Nzuri’
  • Ukristo Waenea Katika Nchi Nyingine
    ‘Ona Nchi Nzuri’
  • Falme Zashambulia Nchi Ya Ahadi
    ‘Ona Nchi Nzuri’
Pata Habari Zaidi
‘Ona Nchi Nzuri’
gl kur. 4-5

Nchi Zinazotajwa Katika Biblia

TAIFA la Israeli lilipokuwa likijitayarisha kuingia katika Nchi ya Ahadi, Musa alimweleza Mungu tamaa yake kubwa kwa kusema: “Acha nivuke, tafadhali, niione hiyo nchi nzuri iliyo ng’ambo ya Yordani.”—Kum 3:25.

Musa hakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi, lakini alipanda mlima ulioelekeana na Yeriko na kuiona nchi hiyo—‘Gileadi mpaka Dani na nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi na Negebu na uwanja wa bonde la Yordani.’ (Kum 3:27; 34:1-4) Je, umewahi kusikia majina hayo? Je, unajua maeneo hayo yako wapi?

Leo, ni watu wachache sana miongoni mwa watu wa Yehova wanaoweza kutembelea maeneo yanayotajwa katika Biblia. Hawawezi kufanya jambo ambalo Mungu alisema Abrahamu angefanya, yaani kusafiri kwa mapana na marefu katika Nchi ya Ahadi. (Mwa 13:14-17) Hata hivyo, Wakristo wa kweli wanatamani kujua maeneo yanayotajwa katika Biblia na kuona jinsi kila eneo linavyohusiana na lingine.

Broshua hii, ‘Ona Nchi Nzuri,’ inaweza kukusaidia kuyaelewa Maandiko vizuri zaidi. Ina picha za maeneo halisi, kama vile eneo la Gileadi ambalo limeonyeshwa kwenye jalada. Pia ramani zilizopo zinaweza kukusaidia sana kuelewa vizuri maeneo yanayotajwa katika Biblia.

Ramani iliyo kwenye ukurasa wa 2 na 3 inaonyesha maeneo au nchi kubwa-kubwa. Kwa mfano, ukijua Ashuru na Misri zilikuwa umbali gani kutoka Nchi ya Ahadi, utaweza kuelewa vizuri zaidi unabii unaotaja nchi hizo. (Isa 7:18; 27:13; Ho 11:11; Mik 7:12) Ukanda mdogo wa ardhi ambao uliitwa Nchi ya Ahadi ulikuwa kwenye makutano ya njia mbalimbali zilizotumiwa na wafanyabiashara, na mataifa mengine yalitaka kumiliki mashamba yake yenye rutuba ambapo nafaka, mizabibu, na mizeituni ilikuzwa.—Kum 8:8; Amu 15:5.

Nchi za Biblia na Miji Mikuu

Huenda nyakati nyingine ukataka kulinganisha ramani mbalimbali. Kwa mfano, Yona alipewa mgawo wa kwenda jiji kuu la Ashuru, lakini akasafiri kwa meli hadi Tarshishi. (Yon 1:1-3) Je, unaona maeneo hayo kwenye ramani ya kwanza? Hata hivyo, usidhani kwamba Tarshishi ni Tarso, mahali alipozaliwa mtume Paulo. Utaona Tarso na majiji mengine mashuhuri kwenye ramani unayoona hapa.

Fikiria umbali na pia njia ambayo Abrahamu alifuata unapotafuta majiji ya Uru, Harani, na Yerusalemu. Baada ya Yehova kumwita kutoka Uru, Abrahamu aliishi Harani kisha akahamia Nchi ya Ahadi. (Mwa 11:28–12:1; Mdo 7:2-5) Utafahamu vizuri zaidi safari ya Abrahamu unapochunguza “Maeneo Walikoishi Wazee wa Ukoo,” kwenye ukurasa wa 6-7.

Ramani ya kwanza na ile unayoona hapa hazihusu kipindi fulani hususa. Baada ya ramani hizo mbili, ramani nyinginezo zinafuata mpangilio wa matukio katika historia. Majiji au habari nyinginezo katika ramani zinaonyesha matukio ya wakati hususa. Ingawa Faharisi (ukurasa wa 34-35) haitaji kila eneo lililo katika ramani, inaweza kukusaidia kupata ramani zenye habari unayotafuta.

Ramani iliyo kwenye kurasa za katikati (ukurasa wa 18-19) ndiyo yenye miji na majiji mengi zaidi katika Nchi ya Ahadi. Ufunguo wa Ramani utakusaidia kupata miji ya Walawi na ile miji sita ya makimbilio, na vilevile kujua iwapo eneo fulani lilitajwa katika Maandiko ya Kiebrania, ya Kigiriki, au katika Maandiko yote mawili.

Leo, maeneo fulani yanayotajwa katika Biblia hayajulikani yalikuwa wapi, kwa hiyo mengi ya majina hayo hayako katika ramani iliyo kwenye kurasa za katikati. Pia, haingewezekana kuonyesha kila mji na jiji. Kwa mfano, haingewezekana kuonyesha miji yote inayotajwa katika orodha ya mipaka ya makabila. (Yos, sura ya 15-19) Hata hivyo, ramani hiyo inaonyesha majiji yaliyokuwa karibu na mipaka hiyo, na hivyo inakuwezesha kukisia mahali miji hiyo ilipokuwa. Kuna alama zinazoonyesha sura ya nchi (milima, mito, na mabonde ya mto), na rangi mbalimbali zimetumiwa kuonyesha sehemu tambarare na zilizoinuka. Habari hizo zinaweza kukusaidia upige picha akilini kuhusu matukio yanayotajwa katika Biblia.

Unaweza kupata habari zaidi kuhusu maeneo yanayotajwa katika Biblia katika kitabu Insight on the Scriptures, ambacho kimechapishwa katika lugha nyingi.a Unapotumia kitabu hicho pamoja na vitabu vingine vya kukusaidia kujifunza Biblia, iweke karibu broshua ‘Ona Nchi Nzuri.’ Tumia broshua hiyo unaposoma Maandiko yote, na hayo yananufaisha sana maishani.—2Ti 3:16, 17.

[Maelezo ya Chini]

a Kimechapishwa na Mashahidi wa Yehova.

[Sanduku katika ukurasa wa 5]

VITABU VYA BIBLIA VILIANDIKWA HUKO

Babiloni

Efeso

Kaisaria

Korintho

Makedonia

Misri

Moabu

Nchi ya Ahadi

Patmo

Roma

Shushani

Yerusalemu

[Ramani katika ukurasa wa 4, 5]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Nchi za Biblia na Miji Mikuu

A1 ITALIA

A2 ROMA

A3 SISILI

A3 MALTA

C2 MAKEDONIA

C2 Filipi

C2 UGIRIKI

C3 ATHENE

C3 Korintho

C3 KRETE

C4 LIBYA

D3 Antiokia (ya Pisidia)

D3 Efeso

D3 PATMO

D3 RODE

D4 MEMFISI

D5 MISRI

E2 ASIA NDOGO

E3 Tarso

E3 Antiokia (ya Siria)

E3 KIPRO

E4 Sidoni

E4 Damasko

E4 Tiro

E4 Kaisaria

E4 NCHI YA AHADI

E4 YERUSALEMU

E4 MOABU

E4 Kadeshi

E4 EDOMU

F3 Bustani ya Edeni?

F3 ASHURU

F3 Harani

F3 SIRIA

F5 ARABIA

G3 NINAWI

G4 BABILONI

G4 UKALDAYO

G4 Shushani

G4 Uru

H3 UMEDI

[Milima]

E5 Ml. Sinai

G2 MIL. YA ARARATI

[Bahari]

C3 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)

E1 Bahari Nyeusi

E5 Bahari Nyekundu

H2 Bahari ya Kaspian

H5 Ghuba ya Uajemi

[Mito]

D5 Mto  Nile

F3 Mto  Efrati

G3 Mto   Tigri

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki