Wayahudi Waathiriwa Na Utawala Wa Wagiriki Na Waroma
UPANUZI wa Milki ya Ugiriki ulianzia milima ya Makedonia. Akiwa huko, Aleksanda mwenye umri wa miaka 20 hivi alianza kufikiria jinsi atakavyoteka maeneo yaliyokuwa upande wa mashariki. Katika mwaka wa 334 K.W.K., aliongoza jeshi lake kuvuka eneo la Hellespont (Dardanelles), linalotenganisha Ulaya na Asia. Likiwa kama “chui” mwenye mbio, jeshi la Ugiriki chini ya Aleksanda lilianza kuteka maeneo mengi haraka. (Da 7:6) Aleksanda aliwashinda Waajemi karibu na jiji la Troyi, kwenye nchi tambarare za Mto Granicus, kisha akawashinda kabisa huko Iso.
Wagiriki walishambulia Siria na Foinike, na kuliharibu jiji la Tiro baada ya kulizingira kwa miezi saba. (Eze 26:4, 12) Aleksanda aliteka Gaza lakini hakushambulia Yerusalemu. (Zek 9:5) Alipofika Misri, alijenga jiji la Aleksandria ambalo hatimaye lilikuwa kituo cha biashara na elimu. Baada ya kuvuka tena Nchi ya Ahadi, aliwashinda kabisa Waajemi tena huko Gaugamela, karibu na magofu ya jiji la Ninawi.
Aleksanda alielekea upande wa kusini na kuteka Babiloni, Shushani (Susa), na Persepoli—vituo vya kuendesha shughuli za serikali ya Uajemi. Kisha aliteka haraka maeneo ya Uajemi, na kufika Mto Indus, eneo ambalo ni Pakistan ya sasa. Kwa muda wa miaka minane tu, Aleksanda aliteka maeneo mengi yaliyojulikana wakati huo. Lakini katika mwaka wa 323 K.W.K., akiwa na umri wa miaka 32, Aleksanda aliugua malaria na kufa huko Babiloni.—Da 8:8.
Uvutano wa Wagiriki ulionekana wazi katika Nchi ya Ahadi. Baadhi ya wanajeshi waliostaafu wa Aleksanda waliishi katika eneo hilo. Kufikia karne ya kwanza kulikuwa na muungano wa majiji (Dekapoli) ya watu waliozungumza Kigiriki. (Mt 4:25; Mk 7:31) Maandiko ya Kiebrania yalikuwa yametafsiriwa katika Kigiriki. Koine (Kigiriki cha kawaida) ambayo ilikuwa lugha ya kimataifa ilitumiwa kusambaza mafundisho ya Kikristo.
Milki ya Roma
Ni nini kilichokuwa kikiendelea upande wa magharibi? Roma ambayo hapo awali ilifanyizwa na vijiji vingi vilivyokuwa kando ya Mto Tiber iliibuka kuwa milki mashuhuri. Kwa kuwa Roma ilikuwa na serikali moja kuu na majeshi yake yalikuwa yamepangwa vizuri, hatimaye jambo hilo liliiwezesha kuteka haraka maeneo yaliyotawaliwa na wale majenerali wanne wa Aleksanda. Kufikia mwaka wa 30 K.W.K., Milki ya Roma ndiyo iliyokuwa serikali kuu na hivyo kujionyesha yenyewe kuwa ‘mnyama mwenye kutisha’ ambaye Danieli aliona katika maono.—Da 7:7.
Milki ya Roma ilianzia Uingereza hadi Afrika Kaskazini, Bahari ya Atlantiki hadi Ghuba ya Uajemi. Kwa sababu milki hiyo ilizunguka Bahari ya Mediterania, Waroma waliiita bahari hiyo Mare Nostrum (Bahari Yetu).
Roma pia ilikuwa na uvutano kwa Wayahudi kwa sababu nchi yao ilikuwa sehemu ya Milki ya Roma. (Mt 8:5-13; Mdo 10:1, 2) Yesu alibatizwa na kufa wakati wa utawala wa Maliki Tiberio. Baadhi ya watawala Waroma waliwanyanyasa kinyama Wakristo lakini hawangeweza kukomesha ibada ya kweli. Baada ya karne 13, milki hiyo ilishambuliwa na kushindwa na makabila ya Ujerumani kutoka upande wa kaskazini na makabila yenye kuhama-hama kutoka upande wa mashariki.
[Ramani katika ukurasa wa 26]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Milki ya Ugiriki
Baada ya utawala wa Aleksanda, majenerali wake wanne walitawala milki hiyo kubwa
▪ Kasanda
▫ Lisimako
○ Ptolemy wa Kwanza
• Seleuko wa Kwanza
A2 ▪ UGIRIKI
A2 ▪ Athene
A2 ▪ AKAYA
A3 ○ Kirene
A3 ○ LIBYA
B2 ▫ Byzantiumu
B3 ○ SAIPRASI
B4 ○ No-amoni (Thebesi)
C3 Palmira (Tadmori)
C3 ○ Gerasa
C3 ○ Filadelfia
C3 ○ Yerusalemu
C5 ○ Sewene
G2 • Aleksandria Margiana
Njia ya Aleksanda
A2 ▪ MAKEDONIA
A2 ▪ Pella
A2 ▫ THRACE
B2 ▫ Troy
B2 ▫ Sardi
B2 ▫ Efeso
B2 ▫ Gordium
C2 ▫ Ankara
C3 • Tarso
C3 • Iso
C3 • Antiokia (ya Siria)
C3 ○ Tiro
C4 ○ Gaza
B4 ○ MISRI
B4 ○ Memfisi
B4 ○ Aleksandria
A4 ○ Chemchemi cha Siwa
B4 ○ Memfisi
C4 ○ Gaza
C3 ○ Tiro
C3 ○ Damasko
C3 • Aleppo
D3 • Nisibis
D3 • Gaugamela
D3 • Babiloni
E3 • Shushani
E4 • UAJEMI
E4 • Persepoli
E4 • Pasargadae
E3 • UMEDI
E3 • Ekibatana
E3 • Rhagae
E3 • Hekatompylo
F3 • PARITHIA
G3 • ARIA
G3 • Aleksandria Areioni
G3 • Aleksandria Prophthasia
F4 • DRANGIANA
G4 • ARIACHOSIA
G4 • Aleksandria Ariachosiorum
H3 • Kabul
G3 • Drapsaca
H3 • Aleksandria Oxiana
G3 • Drapsaca
G3 • BACTRIA
G3 • Bactra
G2 • Derbent
G2 • SOGDIANA
G2 • Maracanda
G2 • Bukhara
G2 • Marakanda
H2 • Aleksandria Eschate
G2 • Marakanda
G2 • Derbent
G3 • Baktra
G3 • BAKTRIA
G3 • Drapsaka
H3 • Kabul
H3 • Taxila
H5 • INDIA
H4 • Aleksandria
G4 • GEDROSIA
F4 • Pura
E4 • UAJEMI
F4 • Aleksandria
F4 • CARIMANIA
E4 • Pasargadae
E4 • Persepoli
E3 • Shushani
D3 • Babiloni
[Mahali pengine]
A3 KRETE
D4 ARABIA
[Bahari na Ziwa]
B3 Bahari ya Mediterania
C5 Bahari Nyekundu
E4 Ghuba ya Uajemi
G5 Bahari ya Arabia
[Mito]
B4 Nile
D3 Efrati
D3 Tigri
G4 Indus
[Ramani katika ukurasa wa 27]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Milki ya Roma
A1 UINGEREZA
A3 UHISPANIA
B1 UJERUMANI
B2 GAUL
B2 ITALIA
B2 Roma
B3 Carthage
C2 ILIRIKAMU
C3 UGIRIKI
C3 Actiumu
C3 Kirene
D2 Byzantiumu (Konstantinopo)
D3 ASIA NDOGO
D3 Efeso
D3 Alepo
D3 Antiokia (ya Siria)
D3 Damasko
D3 Gerasa (Yarashi)
D3 Yerusalemu
D3 Aleksandria
D4 MISRI
[Bahari na Ziwa]
A2 Bahari ya Atlantiki
C3 Bahari ya Mediterania
D2 Bahari Nyeusi
D4 Bahari Nyekundu
[Picha katika ukurasa wa 26]
Baada ya kujenga upya jiji la Raba, Ptolemy wa Pili aliliita Filadelfia. Magofu ya jumba la maonyesho la Waroma
[Picha katika ukurasa wa 27]
Jiji la Dekapoli la Gerasa (Yarashi)
[Picha katika ukurasa wa 27]
Barabara za Waroma, kama barabara hii karibu na Alepo, zilipitia Ulaya, Afrika Kaskazini, na Mashariki ya Kati. Wakristo walipitia barabara hizi ili kueneza kweli za Biblia