Watu Wa Mungu Warudi Nchini Kwao
SAFU mbili za milima mirefu—Elburzi (kusini ya Bahari ya Kaspian) na Zagro (kusini-mashariki ya Ghuba ya Uajemi) zinazunguka uwanda wa juu ulio katika eneo lililo katika Irani ya sasa. Mabonde ya milima hiyo yana udongo wenye rutuba na miteremko yake ina miti mingi. Mabonde hayo yana tabia ya nchi yenye kupendeza, lakini maeneo tambarare ya milima hiyo ni makame na huwa baridi sana wakati wa majira ya baridi kali. Karibu na maeneo hayo tambarare kuna jangwa linalokaliwa na watu wachache. Milki ya Umedi na Uajemi ambayo iliibuka kuwa serikali kubwa ya ulimwengu ilikuwa katika eneo hilo lililo mashariki ya Mesopotamia.
Wamedi waliishi hasa kwenye eneo lililo kaskazini mwa uwanda huo wa juu, ijapokuwa baadaye walisambaa hadi Armenia na Kilikia. Hata hivyo, Waajemi waliishi kusini-magharibi mwa uwanda huo wa juu, mashariki ya Bonde la Tigri. Katikati ya karne ya sita K.W.K., wakati wa utawala wa Koreshi, falme hizo mbili ziliungana na kuwa Serikali Kubwa ya Ulimwengu ya Umedi na Uajemi.
Koreshi aliteka Babiloni mwaka wa 539 K.W.K. Milki yake ilienea upande wa mashariki hadi India na upande wa magharibi hadi Misri na eneo ambalo ni Uturuki ya sasa. Kwa kufaa, Danieli alifafanua Milki ya Umedi na Uajemi kuwa kama “dubu” mwenye tamaa ‘aliyekula nyama nyingi.’ (Da 7:5) Koreshi aliwavumilia na kuwahurumia watu aliowatawala. Aligawanya milki hiyo katika mikoa mbalimbali. Kila mkoa ulitawaliwa na liwali ambaye kwa kawaida alikuwa Mwajemi, lakini chini yake kulikuwa na mtawala mwenyeji aliyekuwa na mamlaka fulani. Raia wa miliki hiyo ambao walitoka mataifa na makabila mbalimbali walitiwa moyo waendelee na dini na desturi zao.
Kupatana na sera hiyo, Koreshi aliwaruhusu Wayahudi warudi kwao na kuanzisha tena ibada ya kweli na kujenga Yerusalemu, kama inavyoelezwa na Ezra na Nehemia. Unafikiri kundi hilo kubwa la watu walipitia wapi walipokuwa wakirudi kwao? Je, walitumia njia aliyotumia Abrahamu kwa kupitia upande wa juu wa Mto Efrati hadi Karkemishi au labda walitumia njia fupi zaidi kupitia Tadmori na Damasko? Biblia haielezi jambo hilo. (Ona ukurasa wa 6-7.) Baada ya muda, Wayahudi walianza kuishi sehemu nyingine za milki hiyo, kama vile kwenye Delta ya Nile na sehemu zilizo upande wa kusini kabisa. Wayahudi kadhaa waliendelea kuishi Babiloni, na yaelekea hiyo ndiyo sababu iliyofanya mtume Petro atembelee jiji hilo karne nyingi baadaye. (1Pe 5:13) Kwa kweli, Milki ya Umedi na Uajemi ilichangia sana kuwepo kwa Wayahudi katika sehemu nyingi wakati wa utawala uliofuata wa Wagiriki na Waroma.
Baada ya kuteka jiji la Babiloni, serikali ya Umedi na Uajemi ilitumia jiji hilo lenye majira yenye joto jingi kuwa kituo cha shughuli za serikali. Shushani, lililokuwa jiji kuu la Elamu hapo awali, lilikuwa mojawapo ya majiji ya kifalme. Baadaye, huko Shushani, Mfalme Ahasuero wa Uajemi (yaelekea ni Artashasta wa Kwanza) alimchagua Esta kuwa malkia wake na kuzuia njama ya kuangamiza watu wa Mungu katika milki hiyo kubwa. Majiji mengine mawili makuu ya milki ya Umedi na Uajemi yalikuwa Ekibatana (jiji lenye majira ya joto yenye kupendeza, lililokuwa zaidi ya meta 1,900 juu ya usawa wa bahari) na Pasargadae (lililokuwa zaidi ya meta 1,900 juu ya usawa wa bahari, karibu kilometa 650 kusini-mashariki ya Ekibatana).
Serikali hiyo kubwa ya ulimwengu iliporomokaje? Wakati serikali ya Umedi na Uajemi ilipokuwa imefikia upeo wa utawala wake, ilichukua hatua kumaliza uasi uliochochewa na Wagiriki kutoka mpaka wake wa kaskazini-magharibi. Wakati huo, nchi ya Ugiriki ilikuwa imegawanywa katika majiji yenye kujitawala yaliyokuwa yakipigana. Lakini majiji hayo yaliungana na kushinda majeshi ya Waajemi katika vita vya kufa na kupona huko Marathoni na Salami. Baada ya vita hivyo, Ugiriki iliyoungana iliibuka kuwa serikali kubwa ya ulimwengu.
[Sanduku katika ukurasa wa 25]
Chini ya utawala wa Zerubabeli, wanaume Waisraeli wapatao 50,000 walisafiri umbali wa kati ya kilometa 800 hadi 1,600 (ikitegemea njia waliyopitia) kurudi Yerusalemu. Walikabili hali ngumu sana ya kiuchumi. Nchi yao ilikuwa imeachwa ukiwa kwa miaka 70. Waisraeli waliorudi walianza kurudisha ibada ya kweli kwa kujenga madhabahu na kumtolea Yehova dhabihu. Katika mwezi wa Oktoba, mwaka wa 537 K.W.K., walisherehekea Sikukuu ya Vibanda. (Yer 25:11; 29:10) Kisha Waisraeli hao wakaweka msingi wa nyumba ya Yehova.
[Sanduku katika ukurasa wa 25]
VITABU VYA BIBLIA TANGU WAKATI HUO:
Danieli
Hagai
Zekaria
Esta
Zaburi (sehemu)
Mambo ya Nyakati 1 na 2
Ezra
Nehemia
Malaki
[Ramani katika ukurasa wa 24]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Milki ya Umedi na Uajemi
A2 MAKEDONIA
A2 THRACE
A4 Kirene
A4 LIBYA
B2 Byzantiumu
B2 LIDIA
B3 Sardi
B4 Memfisi (Nofu)
B4 MISRI
B5 No-amoni (Thebesi)
B5 Sewene
C3 KILIKIA
C3 Tarso
C3 Iso
C3 Karkemishi
C3 Tadmori
C3 SIRIA
C3 Sidoni
C3 Damasko
C3 Tiro
C4 Yerusalemu
D2 Phasis
D2 ARMENIA
D3 ASSIRIA
D3 Ninawi
D4 Babiloni
E3 UMEDI
E3 Ekibatana (Akmetha)
E3 HYRCANIA
E4 Shushani (Susa)
E4 ELAMU
E4 Pasargadae
E4 Persepoli
E4 UAJEMI
F3 PARTHIA
F4 DRANGIANA
G2 Marakanda (Samarkandi)
G3 SOGDIANA
G3 BAKTRIA
G3 ARIA
G4 ARIACHOSIA
G4 GEDROSIA
H5 INDIA
[Mahali Pengine]
A2 UGIRIKI
A3 Marathoni
A3 Athene
A3 Salamisi
C1 SCYTHIA
C4 Elathi (Elothi)
C4 Tema
D4 ARABIA
[Milima]
E3 MIL. ELBURUSI
E4 MIL. ZAGROS
[Bahari na Ziwa]
B3 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
C2 Bahari Nyeusi
C5 Bahari Nyekundu
E2 Bahari ya Kaspian
E4 Ghuba ya Uajemin
[Mito]
B4 Nile
C3 Efrati
D3 Tigri
H4 Indus
[Picha katika ukurasa wa 24]
Majeshi ya Koreshi yalilazimika kuvuka Milima ya Zagro ili kufika Babiloni
[Picha katika ukurasa wa 25]
Juu: Lango la Mataifa Yote huko Persepoli
[Picha katika ukurasa wa 25]
Picha ndogo: Kaburi la Koreshi huko Pasargadae