Falme Zashambulia Nchi Ya Ahadi
SAMARIA, jiji kuu la ufalme wa kaskazini wa Israeli, lilitekwa na Waashuru mwaka wa 740 K.W.K. Hivyo Waisraeli wakawa chini ya utawala mkatili. Ashuru ilikuwa kaskazini ya nchi tambarare za Mesopotamia, karibu na Tigri, mojawapo ya mito mikubwa zaidi katika Eneo Lenye Rutuba. Nimrodi alijenga Ninawi na Kala, majiji makuu ya Ashuru. (Mwa 10:8-12) Katika siku za Shalmanesa wa Tatu, milki ya Ashuru ilienea upande wa magharibi, hadi maeneo ya Siria na Israeli kaskazini yaliyokuwa na rutuba na maji mengi.
Wakati wa utawala wa Mfalme Tiglath-pileseri wa Tatu (Pul), anayetajwa katika Biblia, Ashuru ilianza kukandamiza Israeli. Harakati zake za kivita ziliathiri Yuda iliyokuwa upande wa kusini wa Israeli. (2Fa 15:19; 16:5-18) Hatimaye, “maji” ya Ashuru yalifurika hadi Yuda na kufikia jiji lake kuu, Yerusalemu.—Isa 8:5-8.
Mfalme Senakeribu wa Ashuru alivamia Yuda mwaka wa 732 K.W.K. (2Fa 18:13, 14) Alishambulia na kupora majiji 46 ya Yuda kutia ndani Lakishi, jiji lililokuwa katika eneo muhimu kivita la Shefela. Kama ramani inavyoonyesha, majeshi yake yalikuwa yamezunguka Yerusalemu, jiji la Yuda, hadi eneo la kusini-magharibi ambapo jiji la Lakishi lilikuwa. Katika maandishi yake ya kihistoria, Senakeribu alijigamba kwamba alimweka Hezekia “kizimbani kama ndege,” lakini maandishi ya kale ya Waashuru hayataji kuangamizwa kwa majeshi ya Senakeribu na malaika wa Mungu.—2Fa 18:17-36; 19:35-37.
Milki ya Ashuru ilikuwa inakaribia kuporomoka. Wamedi ambao waliishi hasa kwenye uwanda wa milimani ambao ni Irani ya sasa, walianza kupigana na mabaki ya jeshi la Ashuru. Jambo hilo lilifanya Waashuru wasijishughulishe na mikoa yao ya magharibi ambayo pia ilianza kuasi. Wakati huohuo, jeshi la Babiloni lilikuwa likiimarika na hata liliteka jiji la Asihuru. Mnamo mwaka wa 632 K.W.K., Ninawi—“jiji la umwagaji wa damu”—lilitekwa na kuharibiwa na muungano wa majeshi ya Wababiloni, Wamedi, na Wasikithe ambao walikuwa watu wenye kupenda vita walioishi kaskazini ya Bahari Nyeusi. Kuanguka kwa jiji la Ninawi kulitimiza unabii uliotolewa na Nahumu na Sefania.—Nah 3:1; Sef 2:13.
Ashuru iliporomoka huko Harani. Jeshi la Babiloni lililokuwa limeazimia kupata ushindi liliwashambulia Waashuru ambao waliendelea kupigana huku wakisubiri msaada kutoka Misri. Lakini Farao Neko alipokuwa akielekea upande wa kaskazini, alizuiwa na Mfalme Yosia wa Yuda huko Megido. (2Fa 23:29) Hatimaye Neko alipowasili Harani, ilikuwa kuchelewa mno kwani Milki ya Ashuru ilikuwa imeporomoka.
Milki ya Babiloni
Usemi “bustani zenye kuning’inia” unakukumbusha jiji gani? Jiji kuu la serikali kubwa ya ulimwengu, Babiloni, ambayo katika unabii inafananishwa na simba mwenye mabawa. (Da 7:4) Babiloni lilikuwa jiji la kibiashara, lenye utajiri mwingi, na lilikuwa limesitawi kidini na katika ubashiri wa kutumia nyota. Eneo la katikati la milki hiyo lilikuwa katika nchi tambarare zenye majimaji kusini mwa Mesopotamia, katikati ya mito ya Tigri na Efrati. Jiji lake lilikuwa limetagaa juu ya Mto Efrati na lilionekana kana kwamba haliwezi kushambuliwa kwa sababu ya kuta zake.
Wababiloni walianzisha njia za kibiashara katika jangwa lenye miamba la Arabia kaskazini. Wakati mmoja, Mfalme Nabonido aliishi Tema, naye Belshaza alitawala Babiloni.
Babiloni lilishambulia Kanaani mara tatu. Baada ya Nebukadneza kuwashinda Wamisri huko Karkemishi mwaka wa 625 K.W.K., Wababiloni walielekea kusini hadi Hamathi, ambapo waliwashinda tena Wamisri waliokuwa wakikimbia. Kisha Wababiloni wakaelekea kwenye pwani ya bonde la mto la Misri, na kuharibu jiji la Ashkeloni lililokuwa njiani. (2Fa 24:7; Yer 47:5-7) Wakati wa harakati hiyo, Yuda ikawa chini ya utawala wa Babiloni.—2Fa 24:1.
Mfalme Yehoyakimu wa Yuda aliasi mwaka wa 618 K.W.K. Wababiloni walituma majeshi ya mataifa jirani yakapigane na Yuda, kisha majeshi ya Babiloni yakazingira na kushinda Yerusalemu. Muda mfupi baada ya hapo, Mfalme Sedekia wa Yuda alifanya mapatano na Misri, jambo ambalo liliwakasirisha sana Wababiloni. Walishambulia tena Yuda na kuanza kuharibu majiji yake. (Yer 34:7) Hatimaye, majeshi ya Nebukadneza yalishambulia jiji la Yerusalemu na kuliteka mwaka wa 607 K.W.K.—2Nya 36:17-21; Yer 39:10.
[Sanduku katika ukurasa wa 23]
VITABU VYA BIBLIA TANGU WAKATI HUO:
Hosea
Isaya
Mika
Methali (sehemu)
Sefania
Nahumu
Habakuki
Maombolezo
Obadia
Ezekieli
Wafalme wa 1 na 2
Yeremia
[Ramani katika ukurasa wa 23]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Milki za Babiloni na Ashuru
Milki ya Ashuru
B4 Memfisi (Nofu)
B4 Soani
B5 MISRI
C2 SAIPRASI (KITIMU)
C3 Sidoni
C3 Tiro
C3 Megido
C3 Samaria
C4 Yerusalemu
C4 Ashkeloni
C4 Lakishi
D2 Harani
D2 Karkemishi
D2 Aripad
D2 Hamathi
D3 Ribla
D3 SIRIA
D3 Damasko
E2 Gozani
E2 MESOPOTAMIA
F2 MINI
F2 ASSIRIA
F2 Khorsabad
F2 Ninawi
F2 Kala
F2 Asshur
F3 BABILONIIA
F3 Babiloni
F4 UKALDAYO
F4 Ereki
F4 Uru
G3 Shushani
G4 ELAMU
Milki ya Babiloni
C3 Sidoni
C3 Tiro
C3 Megido
C3 Samaria
C4 Yerusalemu
C4 Ashkeloni
C4 Lakishi
D2 Harani
D2 Karkemishi
D2 Aripad
D2 Hamathi
D3 Ribla
D3 SIRIA
D3 Damasko
D5 Tema
E2 Gozani
E2 MESOPOTAMIA
E4 ARIABIA
F2 MINI
F2 ASSIRIA
F2 Khorsabad
F2 Ninawi
F2 Kala
F2 Asshur
F3 BABILONIIA
F3 Babiloni
F4 UKALDAYO
F4 Ereki
F4 Uru
G3 Shushani
G4 ELAMU
[Mahali Pengine]
G2 UMEDI
Barabara Kuu (See publication)
[Bahari na Ziwa]
B3 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
C5 Bahari Nyekundu
H1 Bahari ya Kaspian
H5 Ghuba ya Uajemi
[Mitos]
B5 Nile
E2 Efrati
F3 Tigris
[Picha katika ukurasa wa 22]
Kilima cha Lakishi
[Picha katika ukurasa wa 22]
Mfano wa jiji la kale la Megido
[Picha katika ukurasa wa 23]
Mchoro wa bustani zenye kuning’inia za Babiloni