Kutoka Misri Hadi Nchi Ya Ahadi
KILA mahali watu wanajua kuhusu safari ya Waisraeli ya kutoka Misri. Lakini Musa na watu wa Mungu wangetazamia nini baada ya kuvuka Bahari Nyekundu? Walielekea wapi, nao walifikaje kwenye Mto Yordani na kuingia Nchi ya Ahadi?
Lengo lao lilikuwa kufika nchi ya Kanaani. Hata hivyo, Musa hakufuata njia fupi zaidi, yaani umbali wa kilometa 400 hivi kupitia pwani yenye mchanga, njia ambayo ingewaelekeza moja kwa moja hadi Ufilisti, eneo la adui. Wala hawakuvuka eneo kubwa la Rasi ya Sinai lililokuwa uwanda wenye changarawe na mawe ya chokaa, na uliokuwa pia na ukame na joto kali. Badala yake, Musa aliwaongoza watu kuelekea kusini hadi kwenye pwani tambarare. Kwanza walipiga kambi huko Mara ambapo Yehova alifanya maji machungu yawe matamu.a Baada ya kuondoka Elimu, watu walilalamika kuhusu chakula; Mungu akawapa kware, kisha mana. Walipofika Refidimu, watu walilalamika tena kuhusu maji, wakawashinda Waamaleki waliowashambulia, naye baba-mkwe wa Musa akamhimiza atafute msaada kutoka kwa wanaume wanaostahili.—Kut, sura 15-18.
Kisha Musa akawaongoza Waisraeli hadi milima iliyokuwa kusini kabisa, na wakapiga kambi kwenye Mlima Sinai. Wakiwa huko, watu wa Mungu walipewa Sheria, wakajenga tabenakulo, na kutoa dhabihu. Katika mwaka wa pili, walielekea kaskazini kupitia ‘nyika kuu na yenye kutia woga’ hadi Kadeshi (Kadesh-barnea), safari ambayo huenda ilichukua muda wa siku 11. (Kum 1:1, 2, 19; 8:15) Watu hao walitangatanga nyikani kwa miaka 38 kwa sababu ya woga uliowapata baada ya kupokea habari mbaya zilizoletwa na wale wapelelezi kumi. (Hes 13:1–14:34) Walipiga kambi katika sehemu mbalimbali kama vile Abrona na Esion-geberi, kisha wakarudi tena Kadeshi.—Hes 33:33-36.
Walipokaribia Nchi ya Ahadi, Waisraeli hawakuelekea moja kwa moja kaskazini. Walizunguka kandokando ya eneo la kati la Edomu na kupanda juu kupitia “barabara ya mfalme,” au Barabara Kuu ya Mfalme. (Hes 21:22; Kum 2:1-8) Haikuwa rahisi kwa taifa zima lenye watoto, wanyama, na mahema kupitia njia hiyo. Iliwabidi kuteremka kwa kufuata njia iliyojipinda-pinda na kupanda tena makorongo yenye miinuko mikali, yaani, Zeredi na Arnoni (yenye kina cha meta 520 hivi).—Kum 2:13, 14, 24.
Hatimaye, Waisraeli walifika Mlima Nebo. Miriamu alikufa huko Kadeshi, naye Haruni akafa kwenye Mlima Hori. Musa naye alikufa mahali ambapo angeweza kuona nchi aliyotamani kuingia. (Kum 32:48-52; 34:1-5) Yoshua alipewa jukumu la kuwaongoza Waisraeli hadi nchi hiyo, na hivyo kumaliza safari iliyoanza miaka 40 mapema.—Yos 1:1-4.
[Maelezo ya Chini]
a Haijulikani kambi nyingi zilikuwa mahali gani hususa.
[Sanduku katika ukurasa wa 8]
VITABU VYA BIBLIA TANGU WAKATI HUO:
Mwanzo
Kutoka
Mambo ya Walawi
Hesabu
Kumbukumbu la Torati
Ayubu
Zaburi (sehemu)
[Ramani katika ukurasa wa 9]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Njia Ambayo Waisraeli Walipitia
Njia ya Wafanyabiashara
A7 MISRI
A5 Ramesesi?
B5 Sukothi?
C5 Ethamu?
C5 Pihahirothi
D6 Mara
D6 Elimu
E6 NYIKA YA SINI
E7 Dofka
F8 Refidimu
F8 Ml. Sinai (Horebu)
F8 NYIKA YA SINAI
F7 Kibroth-hataava
G7 Haserothi
G6 Rimon-peresi
G5 Risa
G3 Kadeshi
G3 Bene-yaakani
G5 Hor-hagidgadi
H5 Yotbata
H5 Abrona
H6 Esion-geberi
G3 Kadeshi
G3 NYIKA YA ZINI
H3 Ml. Hori
H3 Salmona
I3 Punoni
I3 Iye-abarimu
I2 MOABU
I1 Diboni
I1 Almon-diblathaimu
H1 Yeriko
[Mahali pengine]
A3 GOSHENI
A4 Oni
A5 Memfisi (Nofu)
B3 Soani
B3 Tahpanhesi
C5 Migdoli
D3 SHURI
D5 NYIKA YA ETHAMU
F5 NYIKA YA PARANI
G1 UFILISTI
G1 Ashdodi
G2 Gaza
G2 Beer-sheba
G3 Asimoni
G3 NEGEBU
H1 Yerusalemu
H1 Hebroni (Kiriath-arba)
H2 Aradi (Mkanaani)
H4 SEIRI
H4 EDOMU
I7 MIDIANI
Barabara Kuu
Njia ya kuelekea Nchi ya Wafilisti
Njia ya kuelekea Shuri
I4 Barabara ya Mfalme
Njia ya Wafanyabiashara
Njia ya El Haji
[Milima]
F8 Ml. Sinai (Horebu)
H3 Ml. Hori
I1 Ml. Nebo
[Bahari]
E2 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
D7/G7 Bahari Nyekundu
I1 Bahari ya Chumvi
[Mito na Kijito]
A6 Mto Nile
F3 B.M. la Misri
I2 Arnoni
I3 Seredi
[Picha katika ukurasa wa 8]
Misafara ya wafanyabiashara walivuka Rasi ya Sinai
[Picha katika ukurasa wa 8]
Waisraeli walipiga kambi mbele ya Mlima Sinai
[Picha katika ukurasa wa 9]
Maji yalipatikana kwenye chemchemi zilizokuwa Kadeshi au karibu na eneo hilo
[Picha katika ukurasa wa 9]
Iliwabidi Waisraeli wote wavuke bonde la mto la Arnoni