Yerusalemu Na Hekalu La Sulemani
LILIITWA “ukamilifu wa uzuri” na “mji wa Mfalme Mkuu.” (Zb 48:2; 50:2; Omb 2:15) Yerusalemu lilikuwa jiji kuu la taifa la Mungu. (Zb 76:2) Baada ya Daudi kuteka jiji hilo kutoka kwa Wayebusi na kulifanya kuwa jiji lake kuu, liliitwa “Jiji la Daudi,” au “Sayuni.”—2Sa 5:7.
Ingawa Yerusalemu halikuwa mahali muhimu kivita, lilikuwa mashuhuri kwa sababu Mungu aliweka jina lake hapo. (Kum 26:2) Lilikuwa kituo cha kidini na cha kuendesha shughuli za serikali.
Yerusalemu liko katika mwinuko wa meta 750 juu ya usawa wa bahari katika safu ya milima iliyo katikati mwa Yudea. Biblia inataja kwamba jiji hilo lilikuwa ‘limeinuka’ na waabudu ‘walipanda’ kuelekea huko. (Zb 48:2, Union Version; 122:3, 4) Jiji hilo la kale lilizungukwa na mabonde: Bonde la Hinomu upande wa magharibi na kusini, na bonde la mto la Kidroni upande wa mashariki. (2Fa 23:10; Yer 31:40) Bubujiko la maji la Gihonia katika Bonde la Kidroni na En-rogeli lililokuwa upande wa kusini, lilikuwa chemchemi muhimu ya maji safi kwa jiji hilo hasa wakati maadui waliposhambulia.—2Sa 17:17.
Kwenye mchoro ulio katika ukurasa wa 21, Jiji la Daudi limeonyeshwa kwa rangi nyekundu. Wakati wa utawala wa Daudi na Sulemani, upande wa kaskazini wa jiji hilo ulifikia Ofeli (rangi ya kijani-kibichi) na Mlima Moria (rangi ya buluu). (2Sa 5:7-9; 24:16-25) Sulemani alimjengea Yehova hekalu lenye fahari kwenye mlima huo. Hebu wazia umati wa waabudu wakielekea “mlima wa Yehova” kwa ajili ya sherehe za kila mwaka! (Zek 8:3) Barabara zinazoonyeshwa kwenye ukurasa wa 17 zilifanya iwe rahisi kwa watu kusafiri.
Hekalu la Sulemani lililopambwa kwa dhahabu na mawe yenye thamani lilikuwa mojawapo ya majengo yaliyogharimu pesa nyingi zaidi. Jambo la kutokeza ni kwamba Yehova ndiye aliyetoa ramani ya ujenzi wa hekalu hilo. Kama unavyoona katika picha, kulikuwa na nyua kubwa na majengo ya usimamizi karibu na hekalu hilo. Utanufaika sana kujifunza kindani sehemu mbalimbali za hekalu hilo.—1Fa 6:1–7:51; 1Nya 28:11-19; Ebr 9:23, 24.
[Maelezo ya Chini]
a Mfalme Hezekia aliziba bubujiko hilo la maji na kujenga mtaro hadi kwenye kidimbwi kilichokuwa upande wa magharibi.—2Nya 32:4, 30.
[Sanduku katika ukurasa wa 21]
Baada ya muda, mipaka ya Yerusalemu ilipanuka upande wa magharibi na kaskazini. Wafalme wa Yuda waliotawala baada ya Sulemani walijenga kuta na malango zaidi. Utafiti wa kiakiolojia unaoendelea huenda ukaonyesha waziwazi ukubwa wa baadhi ya kuta hizo na mahali hususa zilipokuwa. Jiji hilo liliharibiwa mwaka wa 607 K.W.K. na likabaki ukiwa kwa miaka 70. Miaka 80 hivi baada ya Wayahudi kurudi, Nehemia alianza kazi kubwa sana ya kujenga upya kuta za Yerusalemu.
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 21]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Yerusalemu/Wakati wa Sulimani
ENEO LA HEKALU KATIKA SIKU ZA SULEMANI
Sehemu za Hekalu
1. Patakatifu Zaidi
2. Patakatifu
3. Ukumbi
4. Boazi
5. Yakini
6. Madhabahu ya Shaba
7. Bahari ya Kuyeyushwa
8. Mabehewa
9. Vyumba vya Kando
10. Vyumba vya Kulia Chakula
11. Ua wa Ndani
ENEO LA HEKALU
Ml. Moria
Vyumba vya
Mabehewa Kulia Chakula
Vyumba vya Kando
Patakatifu Boazi
Zaidi Patakatifu Ukumbi Madhabahu Ua wa
Yakini ya Shaba Ndani
Mabehewa Bahari ya
Kuyeyushwa
Ofeli
Kiwanja cha Watu Wote?
Lango la Maji?
JIJI LA DAUDI
Ml. Sayuni
Jumba la Mfalme Daudi
Lango la Chemchemi
Ukuta wa Manase?
Mnara wa Hananeli
Mnara wa Mea
Lango la Kondoo
Lango la Mlinzi
Lango la Ukaguzi
Lango la Farasi
KIDRONI VALLEY
Ukuta wa Chini?
Gihoni
Mfereji wa maji uliojengwa baadaye
TYROPOEON VALLEY
Lango la Marundo ya Majivu (Potsherds) (Dung)
En-rogeli
Lango la Bonde
VALLEY OF HINOMU
Lango la Pembeni
Mnara wa Jiko la Kuokea
Ukuta Mpana
Lango la Efraimu
Kiwanja cha Watu Wote
Lango la Jiji la Kale
Ukuta wa Kaskazini Uliotangulia Kujengwa
ENEO LA PILI
Lango la Samaki
[Picha]
Ofeli
Nyumba ya Binti ya Farao
Jumba la Mfalme Sulemani
Nyumba ya Msitu wa Lebanoni
Ukumbi wa Nguzo
Ukumbi wa Kiti cha Ufalme
Ml. Moria
Ua Mkuu
Hekalu
[Picha katika ukurasa wa 20]
Sehemu ya mbele ya picha hii inaonyesha mahali “Jiji la Daudi” lilipokuwa. Hekalu lilikuwa katika eneo tambarare (nyuma)
[Picha katika ukurasa wa 20]
Mchoro wa kompyuta unaoonyesha “Jiji la Daudi” la kale na hekalu la Sulemani