Wimbo Na. 66
Kumtumikia Yehova kwa Nafsi Yote
Makala Iliyochapishwa
1. Ee Yehova, Baba yangu,
Ninakupenda wewe sana.
Unastahili ibada;
Sitakuacha wewe kamwe.
Nitafuata maagizo;
Kufanya mapenzi yako.
(KORASI)
Ee Yehova, wastahili,
Utumishi wa nafsi yote.
2. Kazi zako zakukweza,
Ukuu wako zatangaza.
Na kwa nguvu zangu zote;
Nitatangaza Jina Lako.
Ninajiweka wakfu kwako,
Ili nikutumikie.
(KORASI)
Ee Yehova, wastahili,
Utumishi wa nafsi yote.
(Ona pia Kum. 6:15; Zab. 40:8; 113:1-3; Mhu. 5:4; Yoh. 4:34.)