Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ll seh. ya 5 kur. 12-13
  • Gharika Kubwa​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gharika Kubwa​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?
  • Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Habari Zinazolingana
  • Safina ya Noa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Sehemu ya 5
    Msikilize Mungu
  • Nuhu Anajenga Safina
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • “Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Msikilize Mungu Uishi Milele
ll seh. ya 5 kur. 12-13

SEHEMU YA 5

Gharika Kubwa​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?

Watu wengi katika siku za Noa walitenda mabaya. Mwanzo 6:5

Malaika waovu walio na miili ya kibinadamu wanashirikiana na wanawake

Adamu na Hawa walipata watoto, na watu wakawa wengi duniani. Baada ya muda, malaika fulani walijiunga na Shetani katika uasi wake.

Wakaja duniani na wakajifanyia miili ya kibinadamu ili waweze kuoa wanawake. Wanawake hao wakazaa wana wenye kutisha na wenye nguvu waliokuwa na uwezo unaopita wa wanadamu.

Mwanamke anambeba mtoto huku mvulana akimpiga; Wanefili, yaani wana wa malaika waovu ni wakatili

Ulimwengu ukajaa watu waliofanya mambo mabaya. Biblia inasema: “Uovu wa mwanadamu ulikuwa mkubwa duniani na kwamba kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote.”

Noa alimsikiliza Mungu na akajenga safina. Mwanzo 6:13, 14, 18, 19, 22

Noa anamsikiliza Mungu

Noa alikuwa mtu mzuri. Yehova alimwambia Noa kwamba angewaharibu watu waovu kwa gharika kubwa.

Noa na familia yake wanajenga safina

Pia, Mungu akamwambia Noa ajenge meli kubwa, inayoitwa safina, na aingize humo familia yake pamoja na wanyama wa kila aina.

Noa anawaonya watu kuhusu Gharika inayokuja lakini wanamcheka

Noa aliwaonya watu kuhusu Gharika iliyokuwa inakaribia, lakini hawakumsikiliza. Baadhi yao walimcheka; wengine wakamchukia.

Noa na familia yake wanawakusanya wanyama na kuwaingiza ndani ya safina

Safina ilipokamilika, Noa aliwaingiza wanyama ndani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki