Wimbo Na. 141
Kutafuta Marafiki wa Amani
Makala Iliyochapishwa
Yesu asema: ‘Tukahubiri.’
Neno la Mungu tangaza.
Mfano aliuweka.
Kondoo wote alitafuta.
Hakuchoka, kwa upendo
alitafuta.
Milangoni na njiani,
Twasema habari njema
Matatizo karibu yatakwisha.
(KORASI)
Twatafuta
Kote rafiki wa amani,
Twatafuta
Mtu atakaye wokovu,
Kwa bidii
Hatuchoki.
Muda ni mfupi wa kutafuta.
Tuokoe mtu mmoja,
Kati ya mamilioni.
Upendo wetu hutuchochea.
Kuboresha maisha,
na kuponya moyo.
Kwenye miji na majiji,
Akistahili mmoja,
Sote pamoja tunashangilia.
(KORASI)
Twatafuta
Kote rafiki wa amani,
Twatafuta
Mtu atakaye wokovu,
Kwa bidii
Hatuchoki.
(Ona pia Isa. 52:7; Mt. 28:19, 20; Luka 8:1; Rom. 10:10.)