Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 29 uku. 72-uku. 73 fu. 8
  • Je, Mtu Anaweza Kufanya Mambo Mema Siku ya Sabato?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Mtu Anaweza Kufanya Mambo Mema Siku ya Sabato?
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Aliwapenda Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • “Nenda Ukanawe Katika Dimbwi la Siloamu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 29 uku. 72-uku. 73 fu. 8
Yesu akizungumza na mgonjwa katika dimbwi la Bethzatha

SURA YA 29

Je, Mtu Anaweza Kufanya Mambo Mema Siku ya Sabato?

YOHANA 5:1-16

  • YESU AHUBIRI HUKO YUDEA

  • AMPONYA MTU MGONJWA KWENYE DIMBWI

Yesu amefanya mambo mengi wakati wa huduma yake kuu huko Galilaya. Hata hivyo, anaposema, “Ni lazima pia nitangaze habari njema ya Ufalme wa Mungu katika majiji mengine,” Yesu anafikiria maeneo mengine zaidi ya Galilaya. Hivyo, anaenda “kuhubiri katika masinagogi ya Yudea.” (Luka 4:43, 44) Hilo linapatana na akili kwa sababu ni majira ya kuchipua na hivi karibuni kutakuwa na sherehe huko Yerusalemu.

Katika Injili tunapata mambo machache sana kuhusu utendaji wa Yesu huko Yudea, kwa kulinganisha na mambo tunayosoma kuhusu huduma yake huko Galilaya. Hata kama watu hawapendezwi huko Yudea, hilo halimzuii Yesu kuhubiri kwa bidii na kufanya mambo mema popote alipo.

Baada ya muda mfupi Yesu anaelekea Yerusalemu, jiji kuu la Yudea, kwa ajili ya Pasaka ya mwaka 31 W.K. Katika eneo lenye shughuli nyingi lililo karibu na Lango la Kondoo, kuna dimbwi kubwa lenye safu ya nguzo liitwalo Bethzatha. Watu wengi wagonjwa, vipofu, na vilema wanakuja kwenye dimbwi hilo. Kwa nini? Kwa sababu inaaminiwa kwamba watu wanaweza kuponywa wakiingia kwenye dimbwi hilo maji yanapotibuliwa.

Ni siku ya Sabato, naye Yesu anamwona mwanamume fulani kando ya dimbwi hilo ambaye amekuwa mgonjwa kwa miaka 38. Yesu anamuuliza: “Je, unataka kupona?” Mtu huyo anajibu: “Bwana, sina mtu wa kuniweka ndani ya dimbwi maji yanapotibuliwa, lakini ninapotaka kuingia, mtu mwingine huingia kabla yangu.”—Yohana 5:6, 7.

Yesu anasema jambo ambalo lazima linamshangaza mwanamume huyo na wengine wanaosikia: “Simama! Chukua mkeka wako, utembee.” (Yohana 5:8) Na hivyo ndivyo anavyofanya. Papo hapo anapona, anachukua mkeka wake na kuanza kutembea!

Wayahudi wakizungumza na mtu aliyeponywa

Badala ya kushangilia kwa sababu ya jambo la kustaajabisha lililotokea, Wayahudi wanamwona mtu huyo na kumhukumu wakisema: “Ni Sabato, hupaswi kubeba mkeka.” Mtu huyo anawajibu: “Yule aliyeniponya aliniambia, ‘Beba mkeka wako utembee.’” (Yohana 5:10, 11) Wayahudi hao wanamshutumu mtu anayeponya siku ya Sabato.

“Ni nani huyo aliyekuambia, ‘Beba mkeka wako utembee’?” wanauliza. Kwa nini wanamuuliza mtu huyo hivyo? Kwa sababu Yesu “ameingia katika umati,” na mtu huyo aliyeponywa hajui jina la Yesu. (Yohana 5:12, 13) Lakini mtu huyo atakutana tena na Yesu. Baadaye, mtu huyo anakutana na Yesu hekaluni na kumtambua mtu aliyemponya kwenye dimbwi.

Mtu huyo aliyeponywa anawatafuta Wayahudi waliomuuliza kuhusu kuponywa kwake. Anawaambia kwamba Yesu ndiye aliyemponya. Wanapojua hivyo, Wayahudi hao wanamwendea Yesu. Je, wanamwendea ili kujua Yesu anafanya miujiza hiyo kwa uwezo wa nani? Hapana. Badala yake, wanaenda kumshutumu Yesu kwa kufanya mambo mema siku ya Sabato. Hata wanaanza kumtesa!

  • Kwa nini Yesu anaenda Yudea, na bado anaendelea kufanya nini?

  • Kwa nini watu wengi wanaenda kwenye dimbwi liitwalo Bethzatha?

  • Yesu anafanya muujiza gani kwenye dimbwi, na baadhi ya Wayahudi wanatendaje kuhusu jambo lililotokea?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki