Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 29
  • Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Je, Mtu Anaweza Kufanya Mambo Mema Siku ya Sabato?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Kwa Sababu Gani Watu Wanakuwa Wagonjwa na Kufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 29

Sura 29

Kufanya Kazi Njema Siku ya Sabato

NI MASIKA ya mwaka 31 W.K. Miezi michache imepita tangu Yesu aliposema na mwanamke kwenye kisima katika Samaria akiwa njiani kutoka Yudea kwenda Galilaya.

Sasa, Baada ya kufundisha sana katika sehemu zote za Galilaya, Yesu aondoka tena kuelekea Yudea, ambako ahubiri katika masinagogi. Yakilinganishwa na yale ambayo Biblia hutuambia juu ya huduma yake ya Galilaya, Biblia haituambii mengi juu ya utendaji wa Yesu katika Yudea wakati wa ziara hii na wakati wa miezi aliyotumia hapa baada ya Sikukuu ya Kupitwa iliyopita. Ni wazi kwamba huduma yake haikupokewa vizuri katika Yudea kama ilivyopokewa katika Galilaya.

Upesi Yesu aelekea kwenye jiji kuu la Yudea, Yerusalemu, kwa ajili ya Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka 31 W.K. Hapa, karibu na Lango la Kondoo la jiji hili, ndipo kilipo kile kidimbwi kinachoitwa Bethzatha, ambapo wagonjwa wengi, vipofu, na viwete wanakuja. Wao wanaamini kwamba watu waweza kuponywa kwa kuingia ndani ya maji ya kidimbwi wakati yanapotibuliwa.

Ni siku ya Sabato, naye Yesu amwona mtu mmoja kwenye kidimbwi ambaye amekuwa mgonjwa kwa miaka 38. Kwa kujua kwamba mtu huyo amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu, Yesu auliza: “Wataka kuwa mzima?”

Yeye ajibu Yesu: “Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.”

Yesu amwambia: “Simama, jitwike godoro lako, uende.” Hapo mtu yule awa na afya nzuri mara hiyo, achukua godoro lake, na kuanza kutembea!

Lakini Wayahudi wanapomwona mtu yule, wanasema: “Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.”

Mtu yule awajibu: “Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.”

“Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?” wauliza. Yesu alikuwa amegeukia kando kwa sababu ya umati wa watu, na mwenye kuponywa hakujua jina la Yesu. Lakini, baadaye Yesu na mtu yule wanakutana hekaluni, naye mtu yule amjua yeye aliyemponya.

Kwa hiyo mtu huyo aliyeponywa awatafuta Wayahudi kuwaambia kwamba Yesu ndiye amemfanya awe na afya nzuri. Wanapojua hivyo, Wayahudi wamwendea Yesu. Kwa nini? Je! ni ili wajifunze njia anayotumia kufanya maajabu hayo? Hapana. Bali ni ili wamweleze makosa anayofanya kwa sababu ya kufanya mema siku ya Sabato. Na hata waanza kumnyanyasa! Luka 4:44; Yohana 5:1-16.

▪ Ni karibu muda gani umepita tangu ziara ya mwisho aliyofanya Yesu Yudea?

▪ Kwa nini watu wengi walikuwa wanakiendea kidimbwi cha Bethzatha?

▪ Yesu afanya muujiza gani kwenye kidimbwi hicho, na Wayahudi waitikiaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki