Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 53 uku. 130-uku. 131 fu. 7
  • Mtawala Anayeweza Kudhibiti Nguvu za Asili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtawala Anayeweza Kudhibiti Nguvu za Asili
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Mtawala Anayetamaniwa Mwenye Nguvu Zipitazo za Kibinadamu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mtawala Anayetamaniwa Mwenye Nguvu Zaidi ya Wanadamu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Yesu Anaweza Kutulinda
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Nguvu Juu ya Upepo na Mawimbi
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 53 uku. 130-uku. 131 fu. 7
Petro anapotembea juu ya maji, anaanza kuzama; Yesu ananyoosha mkono wake na kumshika

SURA YA 53

Mtawala Anayeweza Kudhibiti Nguvu za Asili

MATHAYO 14:22-36 MARKO 6:45-56 YOHANA 6:14-25

  • WATU WANATAKA KUMFANYA YESU AWE MFALME

  • YESU ATEMBEA JUU YA MAJI, ATULIZA UPEPO

Watu wanachochewa sana na uwezo wa Yesu wa kulisha maelfu ya watu kimuujiza. Wanafikia mkataa kwamba “kwa kweli huyu ndiye Nabii aliyepaswa kuja ulimwenguni,” yule Masihi, na kwamba kwa hakika atakuwa mtawala anayefaa. (Yohana 6:14; Kumbukumbu la Torati 18:18) Basi watu wanapanga kumkamata Yesu ili wamfanye kuwa mfalme.

Hata hivyo, Yesu anatambua jambo ambalo watu wanapanga. Anauaga umati na kuwaagiza wanafunzi wake warudi kwenye mashua. Wanaelekea wapi? Wataelekea Bethsaida kisha waende Kapernaumu. Lakini Yesu anaenda mlimani ili kusali akiwa peke yake usiku huo.

Muda mfupi kabla ya mapambazuko, kupitia mwangaza wa mwezi, Yesu anaiona ile mashua kwa mbali. Mawimbi ya bahari yanapigwa na upepo wenye nguvu, nao mitume ‘wanataabika kupiga makasia kwa kuwa upepo unavuma kinyume chao.’ (Marko 6:48) Yesu anashuka kutoka mlimani na kuanza kutembea juu ya mawimbi kuwaelekea wanafunzi. Kufikia sasa ‘wamepiga makasia umbali wa karibu kilomita tano au sita.’ (Yohana 6:19) Wanafunzi wanaona kwamba Yesu anataka kuwapita, basi wanapaza sauti kwa woga: “Ni mzuka!”—Marko 6:49.

Yesu anawafariji kwa kuwaambia: “Jipeni moyo! Ni mimi; msiogope.” Lakini Petro anasema: “Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako nikitembea juu ya maji.” Yesu anajibu: “Njoo!” Papo hapo Petro anatoka kwenye mashua na kwa kweli anatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. Lakini Petro anapoitazama ile dhoruba ya upepo, anaogopa na kuanza kuzama. Anapaza sauti: “Bwana, niokoe!” Yesu anaunyoosha mkono wake na kumshika Petro kisha anasema: “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini umekuwa na shaka?”—Mathayo 14:27-31.

Petro na Yesu wanapanda kwenye mashua, na ule upepo unatulia. Wanafunzi wanashangaa, lakini je, wanapaswa kushangaa? Kama wangeelewa “maana ya ule muujiza wa mikate,” ambao Yesu alifanya saa kadhaa mapema alipolisha maelfu, hawangeshangaa kwamba anaweza kutembea juu ya maji na kuutuliza upepo. Sasa wanamsujudia wakisema: “Kwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”—Marko 6:52; Mathayo 14:33.

Baada ya muda mfupi wanafika kwenye eneo maridadi, tambarare, na lenye rutuba la Genesareti, upande wa kusini wa Kapernaumu. Wanaegesha mashua na kwenda ufuoni. Watu wanamtambua Yesu, na pamoja na watu wengine kutoka maeneo jirani, wanamletea wagonjwa. Watu hao wanapogusa tu pindo za mavazi ya nje ya Yesu, wanapona kabisa.

Wakati huohuo, umati uliomwona Yesu akilisha maelfu ya watu kimuujiza unatambua kwamba Yesu ameondoka. Basi mashua ndogo kutoka Tiberia zinapofika, watu wanapanda na kuelekea Kapernaumu ili kumtafuta Yesu. Wanapompata, wanamuuliza: “Rabi, ulifika hapa wakati gani?” (Yohana 6:25) Akiwa na sababu nzuri, Yesu anawakemea, kama tutakavyoona.

  • Baada ya Yesu kulisha maelfu ya watu, watu wanataka kumfanyia nini?

  • Kwa nini wanafunzi hawapaswi kushangaa kwamba Yesu anaweza kutembea juu ya maji na kutuliza upepo?

  • Ni nini kinachotokea Yesu anapofika kwenye ufuo karibu na Kapernaumu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki