Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 2 uku. 10-uku. 11 fu. 1
  • Mungu Aliumba Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Aliumba Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Kwa Nini Tunazeeka na Kufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Adui wa Mwisho, Kifo, Aangamizwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Kifo na Ufufuo wa Yesu—Jinsi Unavyoweza Kufaidika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 2 uku. 10-uku. 11 fu. 1
Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni

SOMO LA 2

Mungu Alimuumba Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

Yehova alipanda bustani katika eneo lililoitwa Edeni. Bustani hiyo ilikuwa na maua, miti, na wanyama wengi. Kisha, Mungu akatumia mavumbi kumuumba mwanamume wa kwanza Adamu na kumpulizia pumzi puani mwake. Je, unajua ni nini kilichotokea? Mtu huyo akawa hai! Yehova alimpa Adamu kazi ya kuitunza bustani, na kuwapa wanyama wote majina.

Yehova alimpa Adamu agizo muhimu. Alimwambia hivi: ‘Unaweza kula matunda ya miti yote isipokuwa matunda ya mti mmoja. Ukila matunda ya mti huo utakufa.’

Baadaye, Yehova akasema: ‘Nitamfanyia Adamu msaidizi.’ Mungu akamfanya Adamu alale usingizi mzito, halafu akachukua ubavu mmoja na kumuumba mwanamke. Mwanamke huyo aliitwa Hawa. Adamu na Hawa wakawa familia ya kwanza. Adamu alihisije alipopata mke? Alifurahi sana na kusema: ‘Yehova ameumba mwanamke kutokana na ubavu wangu! Hatimaye! Huyu ni mwenzangu.’

Yehova akawaambia Adamu na Hawa wazae watoto na kuijaza dunia. Alitaka wafurahie kufanya kazi pamoja na kuifanya dunia yote kuwa paradiso, au bustani nzuri, kama bustani ya Edeni. Lakini hawakufanikiwa kuifanya dunia kuwa paradiso. Unajua ni kwa nini? Tutajifunza zaidi katika somo linalofuata.

“Yule aliyewaumba tangu mwanzo aliwaumba mwanamume na mwanamke.”​—Mathayo 19:4

Maswali: Yehova alimpa Adamu kazi gani? Adamu na Hawa wangepatwa na nini kwa kula matunda ya mti waliokatazwa?

Mwanzo 1:27-31; 2:7-9, 15-23; Zaburi 115:16; Mathayo 19:4-6

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki