Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 12 uku. 34
  • Yakobo Alipewa Urithi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yakobo Alipewa Urithi
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mapacha Waliokuwa Tofauti
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Je! Unautazamia Urithi kwa Bidii?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Linda Urithi Wako kwa Kufanya Maamuzi ya Hekima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Yakobo na Esau Wafanya Amani
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 12 uku. 34
Yakobo akimpa Esau bakuli la mchuzi ili apewe haki ya kuwa mzaliwa wa kwanza

SOMO LA 12

Yakobo Alipewa Urithi

Isaka na Rebeka wakiwa na watoto wao mapacha Yakobo na Esau

Isaka alikuwa na umri wa miaka 40 alipomwoa Rebeka. Alimpenda sana. Baada ya muda walipata watoto wawili mapacha.

Mtoto wa kwanza aliitwa Esau, na mdogo wake aliitwa Yakobo. Esau alipenda kuwinda, naye alikuwa mwindaji hodari. Lakini, Yakobo alipenda kazi za nyumbani.

Wakati huo, mtoto wa kwanza alipewa vitu vingi vya baba yake, yaani, mali na shamba baba yake alipokufa. Vitu hivyo viliitwa urithi. Katika familia ya Isaka, urithi ulitia ndani kuwa sehemu ya ahadi ambazo Mungu alimwahidi Abrahamu. Esau hakuthamini ahadi hizo, lakini Yakobo alizithamini sana.

Yakobo na Esau

Siku moja, Esau alirudi kutoka mawindoni akiwa amechoka sana. Yakobo alikuwa akipika chakula kizuri, Esau akamwambia: ‘Nina njaa sana! Tafadhali, nipe mchuzi huo mwekundu!’ Yakobo akamjibu: ‘Nitakupa, lakini niapie kwanza kwamba utanipa urithi wako!’ Esau akamwambia: ‘Urithi hauna maana kwangu! Uchukue. Nipe chakula nile.’ Je, unafikiri Esau alifanya jambo la hekima? Hapana. Esau alimpa Yakobo kitu chenye thamani sana ili apewe tu mchuzi wa dengu.

Isaka alipozeeka, wakati wa kumbariki mtoto wake wa kwanza ulifika. Hata hivyo, Rebeka alimsaidia Yakobo, mtoto wake wa pili kupata baraka. Esau alipojua jambo hilo, alikasirika sana na akapanga kumuua ndugu yake. Isaka na Rebeka walitaka kumlinda Yakobo, hivyo wakamwambia hivi: ‘Ondoka, nenda ukaishi na Labani, mjomba wako, mpaka ghadhabu ya Esau itulie.’ Yakobo alisikiliza ushauri wa wazazi wake, naye akakimbia ili aokoe uhai wake.

“Mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote kisha apoteze uhai wake? Kwa kweli, mtu anaweza kutoa nini ili abadilishane na uhai wake?”​—Marko 8:36, 37

Maswali: Esau alipenda kufanya nini? Yakobo alipenda kufanya nini? Kwa nini Yakobo alibarikiwa badala ya Esau?

Mwanzo 25:20-34; 27:1–28:5; Waebrania 12:16, 17

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki