Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 51 uku. 124-uku. 125 fu. 2
  • Shujaa na Msichana Mdogo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Shujaa na Msichana Mdogo
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Alitaka Kusaidia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Alikuwa Mkaidi Lakini Mwishowe Alitii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Msichana Anamsaidia Mwanamume Mwenye Nguvu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • “Jifungeni Unyenyekevu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 51 uku. 124-uku. 125 fu. 2
Naamani akimtembelea Elisha ili aponywe

SOMO LA 51

Shujaa na Msichana Mdogo

Kulikuwa na msichana mdogo Mwisraeli katika nchi ya Siria aliyekuwa amepelekwa mbali na kwao. Jeshi la Siria lilikuwa limemchukua kutoka kwa familia yao, na sasa alikuwa mtumishi wa mke wa mkuu wa jeshi aliyeitwa Naamani. Msichana huyo mdogo alimwabudu Yehova hata ingawa watu alioishi nao hawakufanya hivyo.

Naamani alikuwa na ugonjwa mbaya wa ngozi, na kila wakati alikuwa na maumivu. Msichana huyo alitamani sana kumsaidia. Alimwambia mke wa Naamani hivi: ‘Ninajua mtu ambaye anaweza kumsaidia mume wako. Kule Israeli, kuna nabii wa Yehova anayeitwa Elisha. Anaweza kumponya mume wako.’

Mke wa Naamani akamwambia mume wake maneno ya yule msichana mdogo. Naamani alikuwa tayari kufanya lolote, kwa hiyo akaenda kwenye nyumba ya Elisha nchini Israeli. Naamani alitazamia kwamba Elisha angempokea kama mtu wa pekee. Lakini badala ya kuzungumza naye moja kwa moja, Elisha akamtuma mtumishi wake ampe Naamani ujumbe huu: ‘Nenda ukaoge mara saba katika Mto Yordani. Kisha utaponywa.’

Naamani akaudhika sana. Akasema hivi: ‘Nilifikiri nabii huyu angeniponya kwa kumwomba Mungu wake na kutikisa mkono wake kwenda mbele na nyuma juu yangu. Badala yake, ananiambia niende kwenye mto huu wa Israeli. Kule Siria tuna mito bora kuliko huu. Kwa nini nisiende kuoga huko?’ Naamani akakasirika sana, na kuondoka katika nyumba ya Elisha.

Naamani akioga kwenye Mto Yordani na kuponywa

Watumishi wa Naamani wakamsaidia kufikiri vizuri. Wakamwambia hivi: ‘Je, si uko tayari kufanya jambo lolote ili uponywe? Jambo ambalo nabii huyu anakuambia ufanye ni rahisi sana. Kwa nini usilifanye tu?’ Naamani akawasikiliza. Akaenda kwenye Mto Yordani na kujitumbukiza mara saba. Baada ya kujitumbukiza mara ya saba, Naamani akatoka kwenye maji akiwa ameponywa kabisa. Alifurahi sana, na akarudi kwa Elisha kumshukuru. Naamani akasema: ‘Sasa ninajua kwamba Yehova ndiye Mungu wa kweli.’ Unafikiri yule msichana Mwisraeli alihisije Naamani aliporudi akiwa ameponywa?

“Kutoka katika vinywa vya watoto wadogo na wanaonyonya, umetoa sifa?”​—Mathayo 21:16

Maswali: Je, unafikiri ilikuwa rahisi kwa msichana huyo mdogo Mwisraeli kuzungumza na mke wa Naamani? Unafikiri ni nini kilichomsaidia awe jasiri hivyo?

2 Wafalme 5:1-19; Luka 4:27

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki