Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 53 uku. 128
  • Ujasiri wa Yehoyada

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ujasiri wa Yehoyada
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mfalme Aliyesahau Shukrani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Yehoashi Alimwacha Yehova kwa Sababu ya Marafiki Wabaya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Kwa Nini Tunapaswa Kumwogopa Yehova?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Yehova Huwathawabisha Watu Wanaotenda kwa Ujasiri
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 53 uku. 128
Kuhani Mkuu Yehoyada akimtambulisha Mfalme Yehoashi mbele ya watu

SOMO LA 53

Ujasiri wa Yehoyada

Yezebeli alikuwa na binti anayeitwa Athalia, ambaye alikuwa mwovu kama mama yake tu. Athalia alikuwa mke wa mfalme wa Yuda. Mume wake alipokufa, mwana wake akaanza kutawala. Lakini mwana wake alipokufa, Athalia akajiweka kuwa malkia wa Yuda. Kisha akajaribu kuangamiza ukoo wote wa kifalme, kwa kuua kila mtu ambaye angeweza kuwa mfalme, kutia ndani wajukuu wake mwenyewe. Kila mtu alimwogopa.

Kuhani Mkuu Yehoyada na mke wake, Yehosheba, walijua kwamba jambo ambalo Athalia alikuwa akifanya lilikuwa baya sana. Kwa hiyo, wakahatarisha uhai wao ili kumficha mjukuu wa Athalia, mtoto mchanga aliyeitwa Yehoashi. Wakamlea hekaluni.

Yehoashi alipokuwa na umri wa miaka saba, Yehoyada aliwakusanya wakuu wote na Walawi na kuwaambia hivi: ‘Yalindeni malango ya hekalu na msimruhusu mtu yeyote aingie ndani.’ Kisha Yehoyada akamfanya Yehoashi kuwa mfalme wa Yuda na kumvika taji kichwani. Watu wa Yuda wakapaza sauti hivi: ‘Mfalme na aishi muda mrefu!’

Malkia Athalia akipaaza sauti

Malkia Athalia aliposikia sauti za umati akakimbia kwenda hekaluni. Alipomwona mfalme mpya, akalia kwa sauti: “Ni njama! Ni njama!” Wakuu wakamkamata malkia huyo mwovu, wakamwondoa hekaluni, na kumuua. Lakini, namna gani kuhusu uvutano wake mbaya juu ya taifa hilo?

Yehoyada alilisaidia taifa lifanye agano na Yehova, nao wakaahidi kumwabudu Yehova peke yake. Yehoyada aliwaagiza wabomoe hekalu la Baali na kuvunja sanamu zote. Kisha, akawaweka rasmi makuhani na Walawi wafanye kazi hekaluni ili watu waabudu huko tena. Akawaweka watunza-malango walinde hekalu ili mtu yeyote asiye safi asiingie. Kisha Yehoyada na wakuu wakampeleka Yehoashi kwenye nyumba ya mfalme na kumweka juu ya kiti cha ufalme. Watu wa Yuda wakashangilia. Hatimaye wangeweza kumtumikia Yehova bila uvutano mbaya wa Athalia mwovu na ibada ya Baali. Je, umeona jinsi ujasiri wa Yehoyada ulivyowasaidia watu wengi?

“Msiwaogope wale wanaoua mwili lakini hawawezi kuua nafsi; badala yake, mwogopeni yule anayeweza kuangamiza nafsi na mwili katika Gehena.”​—Mathayo 10:28

Maswali: Yehoyada alionyeshaje ujasiri? Unafikiri Yehova anaweza kukusaidia uwe jasiri?

2 Wafalme 11:1–12:12; 2 Mambo ya Nyakati 21:1-6; 22:10-12; 23:1–24:16

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki