Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 12/15 kur. 5-6
  • Mfalme Aliyesahau Shukrani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfalme Aliyesahau Shukrani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ATAWALA VEMA CHINI YA UONGOZI WA YEHOYADA
  • AWA MKOSA-SHUKRANI
  • Yehoashi Alimwacha Yehova kwa Sababu ya Marafiki Wabaya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Ujasiri wa Yehoyada
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Kwa Nini Tunapaswa Kumwogopa Yehova?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Yehova Huwathawabisha Watu Wanaotenda kwa Ujasiri
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 12/15 kur. 5-6

Mfalme Aliyesahau Shukrani

YEHOASHI alikuwa kitoto kidogo kisichojiweza wakati Athalia bibi yake (nyanya) alipochukua hatua ya kukinyakua kiti cha ufalme wa Yuda. Bibi huyo hakuwa na shauku ya kumpenda. Mwanamke huyu mwenye kujitakia makuu alitaka kuagiza wajukuu wake wote wa kiume wauawe, kwa maana wakiwako wangemzuia asitawale akiwa malkia. Kama Yehoshabeathi asingalichukua hatua ya haraka, yaani yule mke wa Yehoyada kuhani mkuu, Yehoashi angaliuawa pamoja na wale watoto wengine wa kiume wa ukoo wa kifalme.

Yehoshabeathi alikiondosha kitoto hicho kiwe mbali na wavulana ambao wangeuawa. Kwa miaka sita, mwanamke huyo na mumewe walimficha Yehoashi katika nyua za hekalu. Wakati wote huo Athalia alitawala akiwa malkia. Halafu, katika mwaka wa saba, Yehoyada akamtia mafuta huyu mrithi kijana mwenye haki ya kutawala, akamweka juu ya kiti awe mfalme na kufanya Athalia mnyakua-mamlaka auawe. Kwa uhakika Yehoashi alikuwa na sababu iliyompasa awashukuru shangazi na mjomba wake. Wao walikuwa wameshiriki kumhifadhi hai na kumtengenezea njia ya kujipatia mamlaka ya kifalme.​—2 Nya. 22:10-12; 23:11-15.

ATAWALA VEMA CHINI YA UONGOZI WA YEHOYADA

Kijana huyo mfalme alifanikiwa akiwa chini ya uongozi wa Yehoyada. Moja ya shughuli kubwa sana zilizofanywa wakati wa utawala wake ni kutengeneza sehemu zilizoharibika za hekalu la Yehova. Wakati huo jengo hilo lilikuwa na miaka zaidi ya 150 nalo lilikuwa limekosa sana kutunzwa wakati wa Yehoramu mume wa Athalia na wa mwanawe Ahazia, na vilevile wakati wa mwanamke huyo mwenyewe. Ni wazi kwamba uovu wa mwanamke huyo uliwaongoza sana wanawe hata wakafikia hatua ya kuvunja hekalu na kuliingia, bila shaka wakiwa na kusudi la kuchukua vitu vilivyokuwamo.​—2 Nya. 24:7.

Kwa sababu ya hali mbaya iliyokuwa imelipata hekalu, pesa nyingi sana zilihitajiwa ili kutengeneza sehemu zilizoharibika. Mara ya kwanza, jitihada za kukusanya pesa hazikufaulu. Walawi waliokabidhiwa daraka la kuzikusanya hawakuitikia kwa moyo kamili. Walakini, badiliko lilipofanywa katika mpango wa kukusanya pesa na kusimamia matumizi yazo, watu walishirikiana kwa umoja nayo kazi ikafanikiwa.​—2 Fal. 12:4-6; 2 Nya. 24:5, 6, 8-14.

AWA MKOSA-SHUKRANI

Baada ya kifo cha Yehoyada, Yehoashi hakuendelea kuwa mtumishi mwaminifu wa Yehova Mungu. Alijiruhusu aongozwe na wana wa kifalme wenye kuabudu sanamu. Kwa hiyo, ibada ya Baali iliyokuwa imesimamishwa kwa uongozi wa Yehoyada ilirudishwa. Yehova akawa akizidi kutuma manabii wakawafanye watu warudiwe na fahamu zao, wakiwatia moyo watubu. Lakini wala mfalme mwenyewe wala wana wa kifalme hawakusikiliza.​—2 Nya. 24:17-19.

Zekaria, mwana wa Yehoyada, aliongozwa na Mungu kuhubiri hivi: “Hivi ndivyo yule Mungu wa kweli amesema, ‘Kwa nini ninyi mnaziruka amri za Yehova, hivi kwamba hamwezi kufaulu? Kwa sababu ninyi mmemwacha Yehova, yeye, naye, atawaacha ninyi.’”​—2 Nya. 24:20, NW.

Je! Yehoashi alilithamini neno hilo la Yehova alilompelekea kupitia binamu yake? Wapi, hata hakuzifikiria fadhili alizokuwa ameonyeshwa na Yehoyada baba ya binamu yake. Yehoashi alitoa amri kwamba Zekaria apigwe kwa mawe afe katika ua wa hekalu. Alipokuwa akifa, Zekaria alipaza sauti akasema: “[Yehova] na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.” —2 Nya. 24:21, 22.

Karne nyingi baadaye ni wazi Yesu Kristo alikitaja kisa hicho, akisema: “Na kwa sababu hiyo hekima ya Mungu ilisema, Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na kuwafukuza, ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu; tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu.”​—Luka 11:49-51.

Malipo ya kisasi yalimfikia Yehoashi na ivyo hivyo yakakifikia baadaye kizazi kisicho na uaminifu cha Wayahudi katika karne ya kwanza W. K. Yehova Mungu alimwondolea baraka na ulinzi wake mfalme huyu asiyethamini mambo. Kikosi kidogo cha jeshi la Shamu kilifaulu kushambulia Yuda kikiwa chini ya amri ya Hazaeli, kikamlazimisha Yehoashi awape hazina za mahali patakatifu. Jeshi hilo la Shamu lilipoondoka, mfalme alikuwa mwanamume mgonjwa aliyekwisha kazi. Mwishowe, wawili wa watumishi wake mwenyewe walimwua.​—2 Fal. 12:17-21; 2 Nya. 24:23-27.

Looo, jinsi maisha yangaliweza kuwa tofauti kwa Yehoashi kama angaliendelea kuwa mtumishi mwenye kuthamini mambo wa Yehova na kuendelea kupata upendeleo na ulinzi wa kimungu! Maisha yanaweza kuwa tofauti kwetu pia, maadamu tunaendelea kuthamini matakwa yenye haki ya Mungu. Roho ya kukosa shukrani inaweza kuleta uangamivu tu, kama ilivyomfanyia Yehoashi. Basi, sisi na tujitahidi kuendelea kuuthamini sana uongozi wa kimungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki