Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 90 uku. 210
  • Yesu Afa Huko Golgotha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Afa Huko Golgotha
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Pilato na Herode Wakosa Kumpata na Hatia
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Pontio Pilato Alikuwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 90 uku. 210
Yesu ametundikwa mtini huku ofisa wa jeshi na baadhi ya wanafunzi wa Yesu kutia ndani Maria na Yohana, wakiwa wamesimama kando yake

SOMO LA 90

Yesu Afa Huko Golgotha

Wakuu wa makuhani wakamchukua Yesu na kumpeleka kwenye jumba la gavana. Pilato akawauliza hivi: ‘Mna mashtaka gani dhidi ya mwanamume huyu?’ Wakasema hivi: ‘Anadai kwamba yeye ni mfalme!’ Pilato akamuuliza Yesu, “Je, wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.”

Kisha Pilato akamtuma Yesu kwa Herode, mtawala wa Galilaya, aone ikiwa angepata kosa lolote juu yake. Herode hakuweza kupata jambo lolote la kumshtaki Yesu na hivyo akamtuma tena kwa Pilato. Kisha Pilato akawaambia watu hivi: ‘Mimi wala Herode hatujapata kosa lolote dhidi ya mwanamume huyu. Nitamwachilia huru.’ Umati ukapiga kelele na kusema: ‘Muue! Muue!’ Askari wakampiga Yesu kwa mjeledi, wakamtemea mate, na kumpiga ngumi. Wakamvisha taji la miiba juu ya kichwa chake na kumdhihaki wakisema: ‘Siku njema, ewe Mfalme wa Wayahudi.’ Kwa mara nyingine Pilato akawaambia watu: ‘Sijaona kosa lolote juu ya mtu huyu.’ Lakini wakapiga kelele na kusema: “Atundikwe mtini!” Hivyo, Pilato akamtoa ili akauawe.

Wakampeleka Yesu mahali panapoitwa Golgotha, wakampigilia misumari kwenye mti na kisha wakainua mti huo. Yesu akasali hivi: ‘Baba, wasamehe kwa kuwa hawajui wanachokifanya.’ Watu wakamdhihaki Yesu wakisema: ‘Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka kwenye mti! Jiokoe.’

Mhalifu mmoja aliyekuwa ametundikwa kando yake akasema hivi: “Unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” Yesu akamwahidi hivi: “Utakuwa pamoja nami katika Paradiso.” Ilipofika mchana, kukawa na giza juu ya nchi kwa saa tatu. Baadhi ya wanafunzi walisimama karibu na mti huo, kutia ndani Maria, mama ya Yesu. Yesu akamwambia Yohana amtunze Maria kama ambavyo angemtunza mama yake mzazi.

Mwishowe, Yesu akasema: “Imetimizwa!” Akainamisha kichwa chake na kukata pumzi. Wakati huohuo, tetemeko kubwa la ardhi likatokea. Ndani ya hekalu, lile pazia zito lililotenganisha Patakatifu na Patakatifu Zaidi likararuka katikati. Ofisa mmoja wa jeshi akasema: “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

“Hata ahadi za Mungu ziwe nyingi kadiri gani, zimekuwa ‘ndiyo’ kupitia yeye.”​—2 Wakorintho 1:20

Maswali: Kwa nini Pilato aliruhusu Yesu auawe? Yesu alionyeshaje kwamba aliwajali wengine zaidi kuliko alivyojihangaikia?

Mathayo 27:11-14, 22-31, 38-56; Marko 15:2-5, 12-18, 25, 29-33, 37-39; Luka 23:1-25, 32-49; Yohana 18:28–19:30

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki