KRONOLOJIA
Njia Inayotumiwa Katika Biblia Kuhesabu Wakati. Lazima maandishi yote ya kilimwengu ya kale yatumiwe kwa uangalifu unaofaa. Yanajulikana kuwa si sahihi katika mambo mengi, na haina budi kwamba kwa namna fulani kronolojia zao zingekuwa na makosa. Tofauti na hilo, Biblia imethibitika kuwa ya kweli katika nyanja zote zinazoshughulikiwa, ikiwa inatoa picha iliyo sahihi zaidi sana ya nyakati za kale inazozishughulikia. Kronolojia yake inategemeka pia.—Ona BIBLE (Authenticity).
Wakati vipindi vya Biblia vinapopimwa kulingana na mbinu za kisasa za kutathmini tarehe, inapasa kukumbukwa kwamba namba kamili (au kiasi, Kiingereza ni cardinal) na namba mpango (au pahali, Kiingereza ni ordinal) hutofautiana. Namba kamili, kama vile 1, 2, 3, 10, 100, na kadhalika, zina thamani iliyo kamili. Lakini namba mpango, kama vile -a tatu, -a tano, na -a ishirini na mbili, ni muhimu kuondoa moja ili kuipata namba kamili. Kwa hivyo, katika rejeleo “mwaka wa 18 wa Nebukadreza,” neno “wa 18” ni namba mpango na yawakilisha miaka 17 kamili kuongezea siku kadhaa, majuma, au miezi (wakati wowote ule uliokuwa umepita kuanzia mwisho wa mwaka wa 17).—Yer 52:29.
Wakati wa kuhesabu hesabu fulani ya miaka katika tarehe ya kalenda katika kipindi cha “K.W.K.” hadi tarehe katika kipindi cha “W.K.,” inapasa kukumbukwa kwamba kuanzia tarehe fulani kama vile Oktoba 1 ya mwaka 1 K.W.K. hadi Oktoba 1 ya mwaka 1 W.K. ni mwaka mmoja tu, wala si miwili, kama inavyoonyeshwa katika jedwali hili:
K.W.K
W.K.
2
1
1
2
Okt. 1
Okt. 1
Hii ni kwa sababu tarehe hizo za miaka ni namba mpango. Kwa hiyo, kuanzia karibu Oktoba 1 ya mwaka 2 K.W.K. (wakati unaokadiriwa wa kuzaliwa kwa Yesu) hadi Oktoba 1 ya mwaka 29 W.K. (wakati unaokadiriwa wa kubatizwa kwa Yesu) ni jumla ya miaka 30, yaani, mwaka mmoja kamili kuongezea miezi 3 katika kipindi cha K.W.K. na miaka 28 kamili kuongezea miezi 9 katika kipindi cha W.K.—Lu 3:21-23.
Tangu Kuumbwa kwa Binadamu Hadi Wakati Huu. Wanahistoria wa kisasa hawawezi kujua tarehe yoyote hakika ya mwanzo wa “kipindi kilichosajiliwa kimaandishi” cha jamii ya wanadamu. Iwe wanageukia historia ya Ashuru, Babiloni, au Misri, kronolojia hiyo inazidi kuwa isiyo hakika na yenye kigeugeu wanapofuatisha kurudi nyuma hadi milenia ya pili K.W.K., na katika milenia ya tatu K.W.K. wanakabiliwa na vurugu na utata. Kinyume na hilo, Biblia huandaa historia inayofululiza, inayowezesha hesabu yenye utaratibu kurudi nyuma hadi mwanzo wa historia ya kibinadamu, hesabu ambayo inawezeshwa na marejeleo ya Biblia kwenye vipindi fulani virefu vya wakati, kama vile kile kipindi cha miaka 479 kamili tangu ile harakati ya Kutoka hadi mwanzo wa ujenzi wa hekalu wakati wa utawala wa Sulemani.—1Fa 6:1.
Ili kuhesabu kulingana na kutathmini tarehe za kisasa za kalenda, ni lazima tutumie kituo fulani mathubuti au tarehe ya msingi ya kuanzia, yaani, tarehe fulani katika historia iliyo na msingi imara wenye kukubalika na inayolingana na tukio fulani hususa katika Biblia. Kuanza na tarehe hiyo ikiwa msingi wa kiegemezo tunaweza kufuatisha kwenda nyuma au mbele na kutathmini tarehe za kalenda za matukio mengi yanayorejelewa katika Biblia.
Tarehe moja kama hiyo, inayopatana na historia ya Biblia na pia ya kilimwengu, ni mwaka 29 W.K., ambayo miezi yake ya mapema ilikuwa katika mwaka wa 15 wa Kaisari Tiberio, aliyetangazwa kuwa maliki na Seneti ya Roma katika Septemba 15, 14 W.K. (Kalenda ya Gregory). Ni katika mwaka wa 29 W.K. Yohana Mbatizaji alipoanza mahubiri yake na pia wakati, pengine miezi sita hivi baadaye, alipombatiza Yesu.—Lu 3:1-3, 21, 23; 1:36.
Tarehe nyingine inayoweza kutumiwa kuwa msingi muhimu ni mwaka 539 K.W.K., unaoungwa mkono na vyanzo mbalimbali vya kihistoria kuwa mwaka wa kupinduliwa kwa Babiloni na Koreshi Mwajemi. (Vyanzo vya kilimwengu juu ya utawala wa Koreshi vinatia ndani Diodoro, Africano, Eusebio, and Ptolemy, vilevile mabamba ya Babiloni.) Wakati wa mwaka wa kwanza wa Koreshi amri yake ya kuwaachilia Wayahudi watoke uhamishoni ilitolewa. Na, kama ilivyozungumziwa katika makala juu ya CYRUS, inawezekana kwamba amri hiyo ilitolewa kufikia majira ya baridi kali ya 538 K.W.K. au kuelekea masika ya 537 K.W.K. Jambo hilo lingewapa Wayahudi nafasi ya kufanya matayarisho ya lazima, wafunge safari hiyo ya miezi minne kwenda Yerusalemu, na bado wafike huko kufikia mwezi wa saba (Tishri, au karibu na Oktoba 1) wa mwaka 537 K.W.K.—Ezr 1:1-11; 2:64-70; 3:1.
Tukitumia tarehe hizo za msingi, ndipo tunapoweza kuhusianisha idadi muhimu ya matukio mengi sana ya Biblia na tarehe hususa za kalenda. Muundo wa kimsingi unaohusisha kronolojia hiyo ni kama ifuatavyo:
Tukio Tarehe ya Kalenda Kipindi cha Wakati Baina ya Matukio Tangu kuumbwa kwa Adamu 4026 K.W.K. Hadi mwanzo wa Gharika 2370 K.W.K. miaka 1,656 Hadi kuhalalishwa kwa Agano la Abrahamu 1943 K.W.K. miaka 427 Hadi ile harakati ya Kutoka Misri 1513 K.W.K. miaka 430 Hadi mwanzo wa Ujenzi wa hekalu 1034 B.C.E. miaka 479 Hadi kugawanywa kwa ufalme 997 K.W.K. miaka 37 Hadi kufanywa ukiwa kwa Yuda 607 K.W.K. miaka 390 Hadi kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni 537 K.W.K. miaka 70 Hadi kujengwa upya kwa Kuta za Yerusalemu 455 K.W.K. miaka 82 Hadi kubatizwa kwa Yesu 29 W.K. miaka 483 Hadi wakati huu 1987 W.K. miaka 1,958 Jumla ya kipindi cha wakati tangu kuumbwa kwa Adamu hadi 1987 W.K. miaka 6,012
[it-1 pp. 463-467 Chronology]Yesu alitokea akiwa Masihi hususan katika mwaka uliotabiriwa, pengine miezi sita hivi baada ya Yohana Mbatizaji kuanza mahubiri yake katika “mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwa Kaisari Tiberio.” (Lu 1:36; 3:1, 2, 21-23) Tangu Seneti ya Roma ilipomtangaza Tiberio kuwa maliki katika Septemba 15 wa 14 W.K., mwaka wake wa 15 ulianza katika sehemu ya mwisho ya 28 W.K. hadi baadaye sana katika mwaka 29 W.K. (Ona TIBERIUS.) Kwa hiyo, uthibitisho ni kwamba kubatizwa na kutiwa mafuta kwa Yesu kulitokea katika vuli ya mwaka 29 W.K.
Kwa kuwa Yesu alikuwa “na umri wa karibu miaka 30” wakati wa kubatizwa kwake mwaka 29 W.K. (Lu 3:23), alizaliwa miaka 30 kabla ya hapo, au karibu na vuli ya mwaka 2 K.W.K. Alizaliwa wakati wa utawala wa Kaisari Augusto na wakati wa ugavana wa Siria wa Kirenio. (Lu 2:1, 2) Utawala wa Augusto ulianzia 27 K.W.K. hadi 14 W.K. Seneta Mroma P. Sulpicio Kirenio alikuwa gavana wa Siria mara mbili, ni wazi mara ya kwanza ilikuwa baada ya P. Kintilio Varo, ambaye muhula wake akiwa mjumbe wa Siria ulimalizika mwaka 4 K.W.K. Wasomi fulani hukadiria ugavana wa kwanza wa Kirenio ulikuwa mwaka 3-2 K.W.K. (Ona REGISTRATION.) Wakati huo Herode Mkuu alikuwa mfalme wa Yudea, na tumeona kwamba kuna uthibitisho unaoelekeza kwenye mwaka 1 K.W.K. kuelekea kuwa ndio wakati wa kifo chake. Kwa hiyo, uthibitisho wote uliopo, na hasa marejeleo ya Kimaandiko, yanaonyesha vuli ya 2 K.W.K. kuwa wakati wa Mwana wa Mungu kuzaliwa akiwa binadamu.
Kipindi cha baadaye cha mitume. Inawezekana kukadiria tarehe za baadhi ya matukio yaliyotokea wakati wa kipindi hicho. Unabii wa njaa kubwa uliosemwa na nabii Mkristo Agabo, na mateso yaliyofuata ambayo yalichochewa na Herode Agripa wa 1, yaliyosababisha kifo cha mtume Yakobo na kufungwa gerezani kwa Petro, kwa wazi yalitokea karibu na mwaka 44 W.K. (Mdo 11:27-30; 12:1-4) Herode Agripa alikufa mwaka huo, na pana uthibitisho kwamba njaa iliyotabiriwa ilitokea mwaka 46 W.K. Yawezekana kuwa tarehe hiyo ya mwisho yaonyesha kuwa huo ndio wakati wa huduma ya usaidizi iliyoanzishwa na Paulo na Barnaba.—Mdo 12:25.
Ziara ya kwanza ya Paulo huko Korintho yaweza kukadiriwa tarehe yake kupitia uliwali wa Galio. (Mdo 18:1, 11-18) Kama ilivyoelezwa katika makala inayohusu GALLIO, inaelekea uliwali huo ulianzia kiangazi cha 51 W.K. hadi kiangazi cha 52 W.K., ijapokuwa baadhi ya wasomi hupendelea mwaka 52/53 W.K. Kwa hiyo, inaelekea utendaji wa Paulo wa miezi 18 katika Korintho ulianzia vuli ya mwaka 50 W.K., na kwisha katika masika ya mwaka 52 W.K. Jambo hilo linathibitishwa zaidi na uhakika wa kwamba wawili kati ya washiriki wa Paulo katika Korintho, Akila na Prisila, walikuwa ndipo tu wamewasili kutoka Italia kwa sababu ya amri ya Maliki Klaudio iliyowataka Wayahudi wote waondoke Roma. (Mdo 18:2) Paulo Oroso, mwanahistoria wa karne ya tano, anasema kwamba agizo hilo lilitolewa katika mwaka wa tisa wa Klaudio, yaani, mwaka 49 au mapema mwaka 50 W.K.
Ile miaka miwili ambayo Paulo alitumia gerezani huko Kaisaria ilikuwa kwenye miaka miwili ya mwisho ya ugavana wa Feliki, kisha Paulo alipelekwa hadi Roma na Porkio Festo, mwandamizi wa Feliki. (Mdo 21:33; 23:23-35; 24:27) Tarehe ya Festo kupanda kwenye cheo si hakika kabisa, kwa kuwa uthibitisho wote wa kihistoria hauelekezi kwenye mkataa ule mmoja. Hata hivyo, inaelekea sana ni mwaka 58 W.K. Kuwasili kwa Paulo katika Roma hatimaye kwaweza kukadiriwa kuwa kati ya 59 na 61 W.K.
Ule moto mkubwa ulioteketeza Roma ulifanyika Julai mwaka 64 W.K. na kufuatwa na mateso makali ya Wakristo, yenye kuchochewa na Nero. Yaelekea kwamba kufungwa kwa Paulo gerezani mara ya pili na kuuawa kwake kulitokea muda mfupi baada ya hapo. (2Ti 1:16; 4:6, 7) Kuhamishwa kwa Yohana hadi kisiwa cha Patmo hufikiriwa na wote kuwa kulitokea wakati wa utawala wa Maliki Domitiani. (Ufu 1:9) Mateso ya Wakristo yalifikia kilele wakati wa utawala wake (81-96 W.K.), hasa katika miaka mitatu ya mwisho. Maoni ya kimapokeo ni kwamba Yohana alifunguliwa kutoka uhamishoni baada ya kifo cha Domitiani, naye akafa katika Efeso karibu na mwisho wa karne ya kwanza W.K. Kwa hiyo, baada ya Yohana kuandika nyaraka zake karibu na wakati huo, vitabu vinavyokubalika vya Biblia vilikamilika na kipindi cha mitume kikamalizika.