Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • it uku. 85
  • Yoeli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yoeli
  • Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Kitabu Cha Biblia Namba 29—Yoeli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Kuvumilia Majaribu Kulitusaidia Kumtegemea Yehova Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Wachukueni Manabii Kuwa Kielelezo—Yoeli
    Huduma ya Ufalme—2013
  • Yoeli Atoa Unabii juu ya Kisasi cha Yehova na Upendo Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Pata Habari Zaidi
Ufahamu wa Kina wa Maandiko
it uku. 85

YOELI

(Yoeli) [Yehova Ni Mungu].

1. Mzao wa Isakari na kichwa cha familia katika kabila lake.​—1Nya 7:1-4.

2. Mzao wa mwana wa Lawi aliyeitwa Kohathi; “mwana wa Azaria” na babu ya mwanamume anayetajwa kwenye Na. 5.​—1Nya 6:36-38.

3. Mrubeni ambaye mzao wake aliyeitwa Beera alichukuliwa na kupelekwa uhamishoni na Mfalme wa Ashuru, Tilgath-pilneseri (Tiglath-pileseri III).​—1Nya 5:3-10.

4. Kiongozi wa Wagadi aliyeishi Bashani.​—1Nya 5:11, 12.

5. Mwana wa kwanza wa nabii Samweli; mzao wa mwanamume anayetajwa kwenye Na. 2 na baba ya Hemani, mwimbaji wa kabila la Lawi. (1Nya 6:28, 33, 36; 15:17) Yoeli na mdogo wake Abiya, waliwekwa rasmi na baba yao kuwa waamuzi, lakini walikosa unyoofu na hivyo watu wakapata sababu ya kuomba wapewa mfalme wa kibinadamu.​—1Sa 8:1-5.

Kwenye 1 Mambo ya Nyakati 6:28 maandishi ya Wamasora (na baadhi ya tafsiri) husema kwamba “Vashni” alikuwa mwana wa kwanza wa Samweli. Hata hivyo, kwa ujumla wasomi wanakubaliana kwamba jina “Yoeli” lilikuwa kwenye maandishi ya awali ya Kiebrania, na lilipatikana pia kwenye Peshitta ya Kisiria na toleo la Lagardian la Septuajinti ya Kigiriki. (Linganisha 1Sa 8:2.) Kufanana kwa jina “Yoeli” na herufi za mwisho za jina linalotangulia katika maandishi hayo (“Samweli”) huenda kulimfanya mwandishi aondoe jina “Yoeli” bila kukusudia. Inaonekana alikosea kwa kufikiri neno la Kiebrania wehash·she·niʹ (linalomaanisha, “na [mwana] wa pili”) lilikuwa jina la mtu “Vashni” na hivyo akaweka neno waw (na) kabla ya jina Abiya.

6. Mmoja kati ya mashujaa hodari wa Daudi; ndugu ya Nathani.​—1Nya 11:26, 38.

7. Mlawi kutoka Gershoni wa nyumba ya Ladani; mwana wa Yehieli. (1Nya 23:7, 8) Yoeli aliyekuwa mkuu na ndugu zake 130 walijitakasa na walisaidia kupeleka sanduku la Yehova huko Yerusalemu. (1Nya 15:4, 7, 11-14) Yoeli na Zethamu ndugu yake, baadaye waliwekwa rasmi kuwa waangalizi wa hazina ya nyumba ya Yehova.​—1Nya 26:21, 22.

8. Wakati wa utawala wa Daudi, alikuwa mkuu wa nusu ya kabila la Manase lililokuwa upande wa Magharibi mwa Yordani; mwana wa Pedaya.​—1Nya 27:20-22.

9. Nabii wa Yehova na mwandishi wa kitabu cha Biblia chenye jina lake. Alikuwa mwana wa Pethueli.​—Yoe 1:1; ona YOELI, KITABU CHA.

10. Mlawi wa wana wa Kohathi; mwana wa Azaria. Katika mwaka wa kwanza wa Hezekia, Yoeli alisaidia kutupa vitu vichafu vilivyokuwa vimetolewa hekaluni na makuhani kwa kuvipeleka kwenye Bonde la Kidroni.​—2Nya 29:1, 3, 12, 15, 16.

11. Mmoja wa wakuu wa kabila la Simeoni, ambao katika siku za Hezekia, walichukua kwa nguvu eneo fulani lililokuwa la Wahamu na Wameunimu ili wapanue eneo lao la malisho.​—1Nya 4:24, 35, 38-41.

12. Mmoja wa wana wa Nebo ambaye aliwafukuza wake zake wa nchi za kigeni pamoja na wana wao katika siku za Ezra.​—Ezr 10:43, 44.

13. Msimamizi wa Wabenjamini walioishi Yerusalemu Nehemia alipokuwa gavana; mwana wa Zikri.​—Ne 11:4, 7-9.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki