Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 9/1 kur. 387-388
  • Je! Unaona Udhaifu wa Wengine Tu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Unaona Udhaifu wa Wengine Tu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Habari Zinazolingana
  • Ungamo Liletalo Ponyo la Kiroho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Je, Mungu Hupuuza Udhaifu Wetu?
    Amkeni!—2002
  • Mwenye Nguvu Ingawa Dhaifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Sababu Inayofanya Watu Watende Mabaya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 9/1 kur. 387-388

Je! Unaona Udhaifu wa Wengine Tu?

MHUDUMU wa Kikristo mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 alisema hivi wakati mmoja: “Mimi nafanya iwe kawaida kuachilia walau makosa mawili ya rafiki zangu.” Kwa hekima alijua kwamba sote tuna udhaifu, na kwa hiyo hakutazamia rafiki zake wawe wakamilifu. Yeye hakufanya kosa la kuacha udhaifu wa watu wengine umpofushe asiyaone mambo yao mema.

Lakini kawaida ya wanadamu wasiokamilika ni kuona udhaifu tu wa wengine au kuacha udhaifu wao uyafunike mambo yao yaliyo bora. Inakumbusha wakati mmoja ambapo msemaji wa watu wote aliweka doa la wino katika kipande cha karatasi nyeupe, akaiinua juu na kuuliza wasikilizaji walichokiona. Walichoweza kuona ni lile doa la wino peke yake, si kipande cheupe cha karatasi.

Je! wewe umepata kuhukumu kwa ukali mwanamke ajifanyaye kuwa “bwana mkubwa,” ambaye alielekea sikuzote kutaka kumshauri au kumwamuru mumewe? Hii ni tabia ambayo yampasa Mkristo ajaribu kuishinda. Lakini ikiwa wewe uliuona udhaifu huo peke yake, huenda ikawa kwamba hukuyaona mambo mengi mema anayoyafanya. Mwanamke mmoja kama huyo, ajapokuwa sikuzote hakuwa mwenye busara kwa ambavyo alivyoyasema mambo aliyoyataka, kwa kweli alikuwa mwaminifu, mfanya kazi mwenye bidii, asiye na choyo, na anayefanya kazi sawasawa kusimamia mambo ya nyumba yake. Na, linalopendeza ni kwamba, ule ulioelekea kuwa ubwana haukuelekea kumwudhi mumewe kama ulivyoelekea kuwafanyia wengine. Wao waliuona udhaifu wake tu; lakini mumewe alijua na akashukuru kwamba alikuwa na sifa njema vile vile.

Si watu wachache wanaoacha makosa ya wengine yafunike mambo mema wanayoyafanya kwa habari ya Daudi anayetajwa na Biblia, mfalme wa kale wa Israeli. Wengi wanalishirikisha jina lake na uzinzi wake tu na Bath-sheba, mke wa Uria, mwanamume katika jeshi la Israeli. (2 Sam. 11:1-27; 1 Nya. (Sik.) 11:26, 41) Kama vile kinavyosema Jewish Encyclopedia: “Tabia ya Daudi mara nyingi imelaumiwa isivyofaa,” lakini kinaendelea kusema, “ni maoni mabaya yasiyo na msingi wala ufahamu yatakayokana kwamba hali yake, katika asili yake, haikuwa ya tabia nzuri.”​—Kit. cha 4, uk. 458.

Ndiyo, Daudi alikuwa na sifa njema nyingi, nalo kumbukumbu lake ni zuri sana. Lo! ni imani ya namna gani aliyoionyesha Daudi kwa kujitokeza na kuliua jitu Goliathi, aliyemfanyia Yehova mzaha na majeshi yote ya Israeli! (1 Sam. 17:4-54) Lo! ni huruma ya namna gani aliyoionyesha Daudi alipouachilia mara mbili uhai wa Mfalme Sauli, aliyekuwa amejishupaza amwangamize! (1 Sam. 24:4-22; 26:1-25) Lo! yeye aliithamini ibada ya Yehova kama nini kwa kutaka amjengee Yehova hekalu imara linalofaa, na, alipokatazwa pendeleo hilo, yeye, hata hivyo, alichanga hesabu kubwa ya fedha na kutia wengine moyo watoe michango mingi lipate kujengwa! (1 Nya. (Sik.) 28:1–29:19) Na lo! ni upendo mkuu namna gani na shukrani kwa wema wa Yehova vinavyoonyeshwa wazi katika zile zaburi zaidi ya 75 alizoziandika!

Kwa habari ya dhambi ya Daudi na Bath-sheba, na tuangalie kwamba kama mwanamuziki hodari inaelekea sana yeye alikuwa mwanamume mwenye maono ya ndani. Na kama mtunga mashairi alizidi katika ufasaha wa maneno kwa sababu ya maajabu na uzuri wa uumbaji. Kwa hiyo ilikuwa kawaida tu kwamba vile vile yeye alichochewa na uzuri wa mwanamke. Kama wazao wengine wote wa Adamu, Daudi alichukuliwa mimba katika dhambi. (Zab. 51:5) Alipokwisha kukosa na kufanya dhambi ya kwanza, kwa wepesi aliangukia nyingine katika jitihada ya ubatili ya kuyaepuka matokeo ya dhambi yake ya kwanza. Wakati mke wa Uria alipomwambia kwamba alikuwa na mimba, Daudi alijaribu kuficha mambo kwa werevu. Lakini hili liliposhindwa aliogopa Bath-sheba angepatwa na nini akishtakiwa na mumewe juu ya kufanya uzinzi. (Mit. 6:32-35) Lakini, alipokaripiwa alitubu, naye hakufanya uzinzi tena. Daudi alitaabika sana kwa ajili ya dhambi yake, sawa na Mungu alivyosema, lakini Yehova hakumtupilia mbali.​—2 Sam. 12:1-12.

Tukija kwenye wakati uliopo, si vigumu kwa mtu kuona mifano ya kisasa. Kuna mfanya kazi wa afisi anayelaumu-laumu sana, anayeelekea kusema anayoyataka kwa sauti kubwa na anayefadhaika upesi. Bila shaka anakuudhi. Halafu kuna mtu anayeelekea kuonyesha nia ya kiburi, nalo hili lakuchukiza. Kuliko kutetea tabia hizi, yawapasa watu hao wawili wajitahidi kufanya maendeleo. Hata hivyo, kila mmoja wa watu hawa ana mambo yake anayoyafanya vema. Huenda wakawa ni wafanya kazi waaminifu. Kwa kweli ukifahamiana nao au kuwaona wakiwa chini ya hali nyingine huenda ukawaona kuwa watu tofauti kabisa na vile ulivyowaza.

Zaidi katika jamaa kuna uhitaji wa kujihadhari waume na wake, wazazi na watoto wasiache udhaifu wa wengine uwafanye wayasahau mambo mema wanayoyafanya. Itasaidia tukiangalia kwamba mara nyingi udhaifu unatokana tu na tendo jema lililofanywa kupita kiasi au lililoponyoka, hata kama vile tuwezavyo kuona katika habari ya mtume Petro. Lo! ni bidii na imani ya namna gani aliyoionyesha! Yeye alitumiwa na Mungu kwa njia kubwa namna gani! Hata hivyo hali yake ya uchangamfu, ya shauku na ya kuona furaha kwa wepesi mara kwa mara ilimfanyizisha makosa ambayo wengine wasio na juhudi na shauku kama yeye hawakufanya. Lakini ingekuwa kosa kama nini kuyaacha makosa yake yatupofushe tusiyaone mambo mema aliyoyafanya!

Msaada mkubwa katika kuona ubora wa sifa njema walizo nazo wengine ni kufikiria hali zao na namna ambavyo ingekuwa kama wewe mwenyewe ungalikuwa katika hali hizo. Kumbuka kwamba udhaifu wa wengine huenda ukawa ni kwa sababu ya afya mbaya, walivyolelewa au hali nyingine ambazo huenda huzifahamu.

Nia isiyofaa ingekudhuru wewe na mtu yule mwingine vile vile. Ingeleta mtengano mahali pa umoja. Kwa njia hiyo ungezuia urafiki na kuwa kwenu wenye kusaidiana.

Ikumbuke “sheria ya kifalme.” Hata nawe una udhaifu. Hutaki wengine wajipofushe wasiyaone mema unayoyafanya, sivyo? Kwa hiyo jaribu kuyaona mambo mema na yanayostahili sifa yaliyomo katika wengine. Huenda kwanza yasionekane wazi sana kama udhaifu wao, lakini utakapoyaona, yaelekea sana yatakuwa yenye kupendeza zaidi kuyatazama.​—Luka 6:31.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki