Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 4/1 kur. 151-157
  • Kuamua Ulizo la Uenyeji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuamua Ulizo la Uenyeji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ULIZO LATOKEZWA JUU YA UENYEJI
  • SULUHU YA ULIZO YAHAKIKISHWA
  • Wewe U wa Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Kusudi la Yehova Litatimizwa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya”
    “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya”
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 4/1 kur. 151-157

Kuamua Ulizo la Uenyeji

“Tazama, mbingu ni mali za [Yehova], Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.”​—Kum. 10:14.

1. Ni ushuhuda gani wa kwanza juu ya uenyeji wa Mungu wa mbingu na dunia, na Biblia yashuhudiaje hili?

“HAPO mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” (Mwa. 1:1) Maneno haya ya kwanza ya Biblia Takatifu yatoa ushuhuda wa wazi juu ya uenyeji wa Mungu wa mbingu na dunia. Yeye ndiye aliyeziumba, yaani, alizitokeza na kuzifanya ziwepo. Yeye ndiye Mfanyi. Zilikuwa mali yake nazo ni mali yake, naye anayo haki ya peke yake iliyo kamili juu ya uenyeji wazo. Mungu ndiye mwenye haki ya mali zote hizi, nayo Biblia Takatifu yatoa ushuhuda ufaao juu yake. Ndiyo hati yake ya kuhakikisha haki yake ya uenyeji. Hii yasemwa mara nyingi katika Neno la Mungu lote mpaka kitabu chake cha mwisho, Ufunuo.​—Ufu. 4:11; 10:6; 14:7.

2. Biblia yatoaje ushuhuda zaidi kwa habari ya uenyeji wa Mungu?

2 Sura ya kwanza ya Mwanzo yaendelea kuunga mkono yaliyotangulia kwa maneno hakika kabisa. Katika kila hatua ya uumbaji Mungu ndiye aliyetoa agizo la lipaswalo kufanywa. Mara nyingi twasoma kwamba Mungu “akafanya” hiki na kile, mbinguni na duniani, viishivyo na visivyoishi. Yeye alivipa majina pia. “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita, Usiku.” Mwishowe, “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.” Kilikuwa na kibali yake. Vitu vyote vilikuwa vyake yeye, Mungu wa pekee wa kweli, “mbingu na nchi zilipoumbwa.” (Mwa. 1:5, 31; 2:4) Baadaye, Musa aliongozwa na Mungu ahakikishe hili, alipowaambia Israeli: “Tazama, mbingu ni mali za [Yehova], Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo. Kwa maana [Yehova], Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya.”​—Kum. 10:14, 17.

3. Kwa habari hii, sababu gani kuumbwa kwa mwanadamu kwahitaji fikira za pekee?

3 Kuumbwa kwa mwanadamu ndiko kulikokamilisha uzuri wa uumbaji wa kidunia, nalo hili lastahili tulikazie fikira za pekee. Kusimulia hili mara moja kwaonyesha maendeleo, kupanuka kwa habari ya uenyeji. Hali mbalimbali zatajwa, kama vile utii, ukionyesha uenyeji mdogo wa kadiri na madaraka mbalimbali. Angalia yasemwayo katika habari hii.

4. (a) Twajifunza nini kutokana na usemi: “Na tufanye mtu kwa mfano wetu”? (b) Neno la Mungu lamjulishaje wakili wa uumbaji aliyetumiwa?

4 Kwa mara ya kwanza katika maandishi, mtu fulani akaribishwa ashirikiane katika uumbaji. “Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Je! ushirikiano huu wamaanisha kuachishwa kwa uenyeji wa Mungu kwa kadiri yo yote, au uenyeji wa ushirikiano? Sivyo. Hatua ya kwanza ya kufanya mambo, daraka na uongozi vilikuwa mikononi mwa Mungu vyote, kwa maana twasoma baada ya hapo: “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwa. 1:26, 27) Kutokana na maandiko mengine twajifunza kwamba yeye aitwaye Yesu Kristo sasa ndiye aliyetumiwa na Yehova kama wakili wake wa pekee wa uumbaji, alipokuwa hajakuwa mwanadamu. Yeye, kama Hekima ikisemwa kama mtu, alikuwa “kabla ya matendo yake [Yehova] ya kale,” “stadi wa kazi” wa Yehova. Alikuwa ndiye “Neno,” ambaye kupitia kwake “vitu vyote [vingine] viliumbwa”. Yeye ndiye “mfano wa Mungu asiyeonekana mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote,” kwa hiyo kwa kufaa alihusika wakati kuumbwa kwa mwanadamu, kwa maana mwanadamu pia aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Kweli, Yesu Kristo asemekana kuwa “aliye peke yake Mola, [au, Bwana], na Bwana,” lakini, kama tutakavyozungumza baadaye, cheo hiki alipewa kwa sababu ya ununuzi alioufanya, si kwa sababu ya daraka lake kama wakili wa Mungu wa uumbaji.​—Mit. 8:22, 30; Yohana 1:1-3; Kol. 1:15, 16; Yuda 4.

5. Ni maandiko gani yawezayo kutajwa yanayoonyesha kadiri fulani ya uenyeji wa mwanadamu?

5 Walakini, ulizo latokea juu ya mwanadamu alipokea kadiri kubwa ya uenyeji alipoumbwa na kupewa agizo hili, “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi kuitiisha; mkatawale samaki wa bahari na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” (Mwa. 1:28) Kutokana na hili yaweza kuhakikishwa kwamba ndivyo ilivyokuwa. Je! kuumbwa kwa mwanadamu kwa mfano wa Mungu hakukutia na uwezo wa kutumia uenyeji? Maandiko mengine yaungayo mkono hili yaweza kukumbukwa. Baada ya gharika, Mungu alimwambia Nuhu hivi, juu ya ‘kila kilicho hai’: “Vimetiwa mikononi mwenu.” Halafu, tena, twayakumbuka maneno ya Daudi alipomwambia Yehova hivi: “Umemtawaza [mwanadamu mwenye kufa] juu ya kazi za mikono yako umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.” Tena, usemi ujulikanao sana wa mtunga zaburi utakumbukwa: “Mbingu ni mbingu za [Yehova], bali nchi amewapa wanadamu.”​—Mwa. 9:2; Zab. 8:6; 115:16.

6. Kwa sababu gani ni jambo la maana kuangalia maneno yanayozunguka andiko lo lote?

6 Ndiyo, yakubaliwa kwamba maandiko yaliyotangulia yazungumza juu ya uenyezi, lakini hasa ni kwa kadiri ndogo. Hii ni wazi kila wakati tutazamapo maneno yanayozunguka mistari hiyo, ambayo ni ya lazima sikuzote katika kutafuta ufahamu ufaao wa Neno la Mungu juu ya habari yo yote.

7. Kwa habari ya cheo cha mwanadamu kama mwenyeji twajifunza nini kutokana na (a) Mwanzo 2:15-17, (b) Mwanzo 9:3-6, (c) Zaburi 8, na (d) Zaburi 115?

7 Kwa habari ya cheo cha kwanza cha mwanadamu, hakuna shaka Mwenyeji hasa alikuwa nani tusomapo kwamba “[Yehova] Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.” Halafu twasoma: “[Yehova] Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” (Mwa. 2:15-17) Kwa kweli mtu huyo hakuwa na sababu wala udhuru wa kusahau yeye alikuwa mali ya nani, wakati ambapo uhai wake wenyewe ulitegemea utii wake kwa Muumba na Mwenyeji wake. Katika maana iyo hiyo, Mungu alipoviweka viumbe vyote vilivyo hai mikononi mwa Nuhu, mara hiyo twasoma katazo kali juu ya kula damu na kumwaga damu ya mwanadamu. Tena hii yakazia aliyekuwa Mwenyeji wa asili wa uhai kama unavyofananishwa katika damu ya viumbe vyote vilivyo hai. (Mwa. 9:3-6) Tukifungua Zaburi 8, twaona kwamba, badala ya kuonyesha mwanadamu akipewa uenyeji wa dunia, kichwa chote chaonyesha ustahili na sifa ya Yeye ambaye ndiye mwenye vitu vyote na aviongozaye: “Wewe, [Yehova], Bwana wetu [Mwenyeji], jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!” (Mist. 1, 9) Twaona kichwa kinachofanana na hiki tutazamapo Zaburi 115, NW. Yaangalie hasa maneno ya mwanzo: “Sisi hatuna cho chote chetu, Ee Yehova, sisi hatuna cho chote chetu, lakini ulitukuze jina lako kulingana na fadhili zako za upendo, kulingana na ukweli wako.” Hii haikazii kwamba Yehova ndiye Mwenyeji wa pekee tu kwa kweli, bali pia ni Mwenyeji mwema astahiliye. Hakuwezi kuwako mwingine aliye bora.

8. (a) Mwanadamu aliwekwa katika cheo gani na Muumba wake? (b) Je! hii yakubaliwa kwa ujumla, na ni maulizo gani yanayotokezwa?

8 Kutokana na maandiko yaliyokwisha kuangaliwa, twaweza kufahamu kwamba mwanadamu alipewa cheo cha agizo na daraka kubwa hapo kwanza. Kwa kuwa aliumbwa kwa mfano wa Mungu kama kiumbe chenye uhuru wa hiari, yeye alikuwa na uwezo wote uliokuwa wa lazima kutimiza kila takwa. Yehova alikuwa ndiye Mwenye shamba. Mwanadamu alikuwa ndiye mkulima mwenye kupanga, aliyeagizwa awe mwangalizi wa dunia nzima. Alipewa agizo na uwakili mtakatifu. Hiyo ni wazi. Lakini ni wazi pia kwamba mwanadamu leo, kwa ujumla, hakubali wajibu wo wote katika habari hiyo. Mambo yako tofauti kabisa. Hii ilitukiaje? Ulizo la uenyeji lilitokeaje, nalo litaamuliwaje? Zaidi ya hayo, sisi twahusikaje kama watu mmoja mmoja, na kwa matokeo gani kwetu wenyewe? Twapendezwa kweli kupata majibu yafaayo kwa maulizo haya.

ULIZO LATOKEZWA JUU YA UENYEJI

9. Kula tunda lililokatazwa kulionyesha nini?

9 Shetani Ibilisi alipomshawishi Hawa alile tunda lililokatazwa, hakuna mtajo wa moja kwa moja uliofanywa juu ya uenyeji wake. Lakini fikiri kidogo juu ya litukialo ulapo kitu fulani. Kiwapo mkononi mwako au sahanini mwako, umekichukua kiwe chako, kama una haki ya kuwa nacho au sivyo. Walakini, baada ya kukila kwa kweli umekifanya sehemu yako mwenyewe. Umekifanya chako mwenyewe, si kitu usemeje kwa kutoa udhuru au kuungama. Ndivyo ilivyokuwa kwa Hawa. Ingawa yeye alikuwa amerudia kuitaja amri ya Mungu mara hiyo tu: “Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa,” twasoma baada ya hapo kwamba “alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.” (Mwa. 3:1-6) Sababu ya Shetani iliyoongoza tendo lao ilionyesha kwamba wao walikuwa na haki ya kula katika tunda hilo. Hivyo kwa tendo la makusudi na la uasi lenye nguvu zaidi kuliko maneno, Adamu na Hawa pia aliutia mti huo uliokatazwa katika fungu moja na miti mingine yote waliyokuwa wamepewa haki ya kuila. Lakini mara tu walipokwisha wote wawili kulila tunda lililokatazwa, je! walijiona wenye haki katika uamuzi wao wa kupanga miti katika mafungu? Kusumbuliwa kwao na dhamiri kwasema Hapana! Kweli, wasingeweza kuvirudisha vipande vya tunda walivyokuwa wamevila mtini, lakini kutumia kwao tunda walilolila miilini mwao hakukuwaletea maono ya uenyeji ya haki ya kulila tunda lililokatazwa. Majani ambayo kwayo walitengeneza mavazi ya kiunoni wafiche uchi waliouona sasa hayakutolewa katika mti uliokatazwa, bali yalitolewa katika mtini. Matokeo ya shauri lote yalikuwa kana kwamba walikuwa wamekula zabibu mbichi.​—Eze. 18:2.

10. Ni kwa njia gani ambavyo ulizo lililotokezwa halikuwa kitu cha kimwili tu, na ni maulizo gani zaidi yanayotokezwa?

10 Hata hivyo, ulizo lilitokezwa juu ya uenyeji ufaao wa Mungu. Tafadhali angalia kwamba kwa vyo vyote ulizo hilo halikuwa kitu cha kimwili tu, tunda la mti fulani. Namna gani mwanadamu mwenyewe, si maisha yake mwenyewe tu, bali pia sifa zile njema za adili za uaminifu na kujitoa na shukrani? Je! sifa hizi zote zisitumiwe nyakati zote kwa sifa ya Yehova, zikihakikishwa na mwendo wa utii wenye nia na unyenyekevu kwake? Je! mwanadamu hamtegemei Mungu kabisa kwa uhai na yote yawezayo kupatikana kutokana nao na baraka? Je! Mungu hapaswi kushukuriwa kwa haki sikuzote juu ya kutegemewa hivyo?

11. (a) Paulo alitumiaje kuwaza kwa namna hiyo alipokuwa akiwaandikia Wakorintho? (b) Ni ukamatano gani unaoonyeshwa kwa njia hiyo kati ya uhusiano na uenyeji?

11 Paulo alitumia kuwaza kwa namna hiyo alipowaandikia Wakristo katika Korintho: “Nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.” Mwendo huo wa unyofu na usafi kwa upande wa Wakristo hawa ulikuwa wa Kristo kwa haki, kwa maana, kama Paulo alivyoeleza, “naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” Ufahamu ufaao wa Maandiko juu ya shauri la uhusiano utatusaidia tupate maoni yafaayo juu ya uenyeji, ili tusidanganywe kwa maneno ya hila.​—2 Kor. 11 2, 3.

12. Mungu alitendaje uasi ulipofanywa Edeni?

12 Wazazi wetu wa kwanza walichagua mwendo wa kutokutii na wa kujitegemea wenyewe kwa makusudi, mwendo wa upotovu. Kwa sababu hiyo, waliukataa uenyeji wa Mungu juu yao. Walifuata maoni ya kwamba wao walikuwa mali yao wenyewe na ya mmoja na mwenzake, lakini si mali ya Mungu. Walivunja uhusiano wao mwema naye. Itikio la Mungu lilikuwa nini kwa mwito huu wa kushindana? Je! yeye aliacha uenyeji wake juu yao na makao yao ya Edeni? Hata kidogo. Yeye alikuwa ndiye Mpaji wao wa Sheria na Hakimu, naye sasa alitenda katika cheo hiki. Baada ya kutangaza hukumu, aliilinda mali yake kwa kumfukuza mwanadamu atoke katika bustani ya Edeni na kufanya isiwezekane airudie, zaidi akiilinda “njia ya mti wa uzima.”​—Mwa. 3:24.

13. Ni kwa faida ya nani unabii uliomo katika Mwanzo 3:15 ulitolewa, nao ulitoa uhakikisho gani?

13 Ingawa twaweza kusema kwamba baada ya hapo Mungu aliwaacha Adamu na Hawa kabisa wategemee njia zao wenyewe, yeye hakuwatendea wazao wao namna hiyo. Alipokuwa akitangaza hukumu juu ya nyoka, Mungu alieleza kwa unabii juu ya “uzao” unaokuja wa mwanamke ambao ungemponda nyoka kichwani. (Mwa. 3:15) Maelezo marefu juu ya wakati na namna ambavyo hili lingefanywa hayakutolewa, lakini ilitoa ahadi ya wazi kwamba Mungu angetoa jibu la kutosheleza kwa mwito wa kushindana uliotokezwa na uasi wa mwanadamu. Kwa hiyo, ilielekeza pia kwenye uenyeji wenye kuendelea wa Mungu juu ya dunia na mbingu pia, pamoja na wakaaji wake wote, kujapokuwa kuruhusiwa kwa muda kwa uovu na waovu.

14. Habili, Henoko na Nuhu waliukubalije uenyeji wa Mungu juu yao?

14 Kwa kuunga hili mkono, angalia lisemwalo juu ya wanaume watatu wenye imani aliowataja Paulo, Habili, Henoko na Nuhu. Wao ‘walitembea na Mungu wa kweli,’ na Paulo alihakikisha hili katika Waebrania 11:1-7. (Mwa. 5:24; 6:9, NW) Waliukubali uenyeji wa Mungu juu yao, wakahakikisha hivyo kwa kuendeleza mwendo wa utii mwaminifu kwa roho ya kujitoa kuaminifu na unyenyekevu. Ujapokuwa mkazo mwingi wa uadui wao walimpa Mungu alichokistahili kwa unyofu na usafi kabisa.

15. (a) Ni mwendo gani ambao umefuatwa na wanadamu kwa ujumla, ukitia ndani maulizo gani? (b) Nia ya Yehova na kusudi lake ni nini juu ya maulizo haya? (c) Yesu aliwekaje mfano juu ya nia ifaayo?

15 Mbali na wachache waliokwisha kutajwa, walio wengi wa jamaa ya kibinadamu walifuata njia yao wenyewe. Ulizo la uenyeji lilikuwa mbali na kuamuliwa kwake. Wachache hao, tangu Habili na kuendelea, walionyesha kwa mwendo wao wa maisha kanuni zifaazo zilizohusika, lakini, kama maandishi yaonyeshavyo, wingi mkubwa wa watu waliupuza au wakauonea uchungu na kuupinga vikali mfano mwema huo. (Ebr. 11:36-38) Hata gharika ya siku za Nuhu, ambayo ni ukumbusho wenye nguvu juu ya aliyekuwa mwenyeji wa dunia kweli na wakaaji wake, ilikomesha mwendo wa uasi wa makusudi na wa kichoyo kwa muda tu. Hii ilimhuzunisha Mwenyeji mkuu, Yehova, lakini haikumshangaza. Maulizo mengine yanayohusiana sana yalitiwa ndani: enzi kuu au utawala, na ibada. Maulizo ya kushindana yalikuwa yametokezwa na Shetani na Yehova alikuwa akilitimiza kusudi lake, alilolijua mapema tangu uasi ulipoanza. Kutimizwa kabisa kwa kusudi hili kutaonyesha kwa wakati wote, si uhakika tu wa uenyeji mkuu zaidi wa Mungu, bali pia ustahili wake kamili kuchukua cheo hicho na wajibu wa mwanadamu kuukubali. Ukubali huu waonyeshwa na utaonyeshwa mpaka jaribu la mwisho na wale wanaoendeleza uhusiano ufaao kwa njia ile ile Yesu aliyojibu kishawishi cha mwisho jangwani: “Msujudie [Yehova] Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”​—Mt. 4:10; Ayubu 1:7-12; 2:2-5; Isa. 46:9-11; Ufu. 20:7-9.

16. Ni wakati gani na namna gani ulizo la uenyeji lilipotokezwa kuhusu mataifa, likatokeza nini?

16 Upesi baada ya Gharika, ulizo la uenyeji lilitokea tena. Nimrodi, kitukuu cha Nuhu, alijaribu kwa nguvu kuwa kiongozi wa wanadamu wote. Alijenga na kusimamia miji katika nchi yake mwenyewe, “mwanzo wa ufalme wake.” Kisha “akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru” akishinda na kujenga miji mingine. Kwa kuambukizwa na roho hiyo, alianza mpango wa kushindanisha. Wanadamu wakafanya shauri pamoja wakasema: “Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.” Yehova alipambana na mwito huo wa kushindana kwa kuchafua lugha yao, “akawatawanya kutoka huko [Babeli] waende usoni pa nchi yote.” Walakini, walikwenda wakiwa na nia ile ile na roho ile ile. Vikundi vya mataifa vilitokea, nalo ulizo la uenyeji na utawala sasa lilihusu mataifa, likatokeza matendo ya kipumbavu ya kukuza hali ya nchi zao, ushindani na vita ambazo zimeleta huzuni na uchungu usioelezeka mpaka siku zetu wenyewe.​—Mwa. 10:8-12; 11:1-9.

17. (a) Yehova alichukuliaje mataifa hatua? (b) Ni kwa njia gani Israeli walivyoonekana kuwa wasioaminika na wasiostahili, wakafikia upeo gani?

17 Katika wakati wake Yehova alichukulia mataifa hatua pia. Kutokana na wana kumi na wawili wa Yakobo, ambaye jina lake lilibadilishwa likawa Israeli, Yehova alifanyiza taifa la Israeli. Katika Mlima wa Sinai, aliwaambia hivi: “Ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu.” (Kut.19:5) Maneno “watu wake hasa” yanatumiwa katika Kumbukumbu la Torati, na habari zinazotangulia na kufuata mistari zinatilia mkazo kwa nguvu maoni na mwendo wa tendo ufaao kwa habari ya ibada na uenyeji. (Kum. 7:6; 14:2; 26:18) Walakini, taifa la Israeli lilishindwa mara nyingi kuitikia au kutii matendo ya Mungu kwao au kuwatii manabii wake. Waliukataa uenyeji wake juu yao ama kama Mfalme au kama Mpaji wa Sheria. (1 Sam. 8:7; Isa. 33:22; Eze. 20:13, 30-32) Upeo ulikuja Mungu alipowatumia Mwanawe mwenyewe aliye mpendwa. Walikuwa na kila sababu ya kumkubali kama Masihi wao. Badala yake, wakiwa chini ya uongozi wa viongozi wao, walimkataa na kumwua. Yesu mwenyewe alieleza hili kwa usahihi katika mfano wake juu ya Yehova kama “bwana wa shamba la mizabibu” ‘aliyelipangisha kwa wakulima.’​—Luka 20:9-16.

SULUHU YA ULIZO YAHAKIKISHWA

18. (a) Ni tukio gani jipya lililotukia katika Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E.? (b) Ni kweli gani za maana ambazo Petro aliwafahamisha wasikiaji wake wakati huo?

18 Viongozi hao wa kidini walidhani sasa wangeweza kuendelea kuwa mabwana wasiopingwa wa cheo hicho na wa watu wa kawaida. Walakini, haikuwa hivyo. Penye sikukuu ya Pentekoste, siku ya 52 tangu kutundikwa mtini kwa Yesu, roho takatifu, pamoja na karama ya mwujiza ya kusema kwa lugha nyingi, ilimiminwa juu ya wanafunzi wake Yerusalemu. Kundi kubwa la watu lilikusanyika upesi. Akiwahutubia, mtume Petro aliwaambia waziwazi laumu lao kwa kumwondolea mbali Yesu, lakini akaongeza kwamba hii ilikuwa imetukia “kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani.” Ilikuwa sehemu ya lazima ya kutimia kwa kusudi la Yehova. Petro aliendelea kusema kwamba Mungu alikuwa amemfufua Yesu na kumtukuza kwenye mkono wake mwenyewe wa kuume ‘akamfanya kuwa Bwana na Kristo.’​—Matendo 2:22-24, 32-36.

19. Petro na Yuda walifanya mitajo gani juu ya cheo cha Yesu cha haki, naye Paulo alihakikishaje hili?

19 Nyakati nyingine tatu, Petro alikazia kweli izi hizi waziwazi na mbele ya Baraza Kuu, akiongeza kwamba Yesu alikuwa ndiye “Mkuu wa uzima,” na alikuwa amekuwa “jiwe kuu la pembeni,” na kwamba “hakuna wokovu katika mwingine awaye yote.” (Matendo 3:15-18; 4:10-12; 5:30-32) Miaka mingi baadaye, Petro na Yuda pia walionya juu ya waalimu wa uongo katika barua zao ambao ‘watamkana hata Bwana aliyewanunua,’ “aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.” (2 Pet. 2:1; Yuda 4) Kwa hiyo, inakuwa wazi kwamba lilikuwa kusudi la Mungu lililojulikana zamani kwamba suluhu ya ulizo la uenyeji ingewekwa juu ya Yesu, na kwamba kwa kifo chake na ufufuo wake hatua ya kwanza ya maana, msingi, ilihakikishwa kabisa. Kama vile Paulo alivyowaambia watu wa Athene: “[Mungu] ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.”​—Matendo 17:31.

20. Yesu alipataje kuwa mwenyeji wa wanadamu, kupatana na upendo na haki ya Mungu?

20 Maandiko mengine yanatoa maelezo zaidi juu ya namna Yesu alivyopata kuwa mwenyeji wa wanadamu wote. Tunapoyatazama haya kwa ufupi, twaona kwamba Paulo aeleza katika Warumi 5:12-21 namna Adamu alivyojiuza mwenyewe na wazao wake (wasiozaliwa bado katika viuno vya Adamu) utumwani kwa uasi wake, wakawa raia za Wafalme Dhambi na Mauti. Walakini, kwa upendo wake mkuu na rehema, lakini kwa kupatana kabisa na haki, Mungu alifanyiza njia ya upatanisho. Hii ilihitaji mpango na malipo ya bei ya kutosha ambayo kwayo mwanadamu angeweza kufidiwa na kukombolewa na laana. Lazima bei ilingane kabisa na mwanadamu mkamilifu Adamu. Kwa mwujiza, Mungu alipanga Mwanawe wa kimbinguni aje duniani, azaliwe na kukua afikie utu mzima mkamilifu. Yesu aliufuata mwendo huu kwa nia na, kama alivyosema, yeye ‘alitoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.’ Kama vile Paulo alivyoandika: “Kuna Mungu mmoja, na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, mwanadamu Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi unaolingana kwa ajili ya wote.” Mungu alikuwa ndiye Mwenyeji-Muumba na Mwanzilishi pia wa mpango huo; kwa hiyo, twaweza kusema sasa ni shauri la uenyeji wa ushirika.​—Mt. 20:28; 1 Tim. 2:5, 6, NW; Matendo 20:28.

21. Ni namna gani na wakati gani faida za ukombozi zitakapopatikana kwa wanadamu kwa ujumla?

21 Haki ambayo Mungu amhesabia mtu aaminipo na kuikubali dhabihu ya ukombozi ya Kristo yasemekana kuwa “kipawa cha bure.” (Rum. 5:15-17, NW; 6:23) Faida za ukombozi zitapatikana kwa wanadamu kwa ujumla wakati wa ufalme wa Mungu wa miaka elfu. Mpaka sasa, watu walio wengi wameishi na kufa bila kuujua kabisa mpango huu. Lakini chini ya utawala wa ufalme wa Mungu kutakuwako ufufuo wa “wote wale waliomo katika makaburi ya ukumbusho,” na hukumu yenye haki kwa wote ikisimamiwa na Mfalme, yaani, Kristo Yesu.​—Yohana 5:28, NW; Ufu. 20:11-21:4.

22. Yesu alionyeshaje mwendo ulio tofauti na ule wa uenyeji, akitokeza maulizo gani?

22 Walakini, kabla ya siku hiyo ya kuhukumiwa wanadamu, kuanza, sehemu nyingine ya kusudi la Mungu itatimia. Inahusu pia kuukubali uenyeji wa Mungu. Wakati mmoja Yesu alisema hivi: “Ikiwa ye yote anataka anifuate mimi, mwacheni ajikane mwenyewe na kuchukua mti wake wa mateso na kunifuata sikuzote.” (Mt. 16:24, NW) Alikuwa na maana gani? Je! alituwekea mfano kwa njia yo yote tuufuate katika habari hii wakati wa taratibu hii ya mambo? Hii ina maana gani kwetu leo kama watu mmoja mmoja? Maulizo haya yatokea kwa vyepesi nasi twatazamia kuyazungumza katika makala ifuatayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki