Wewe U wa Nani?
1. (a) “Yerusalemu mpya” unatumiwaje kama mfano katika Biblia? (b) Maandiko mengine yahakikishaje hili?
INGAWA suluhu ya ulizo la uenyeji imewekwa juu ya Yesu, Neno la Mungu laonyesha kwamba wengine watashirikiana sana na mkuu huyo. Katika njozi ya unabii ya “mbingu mpya na nchi mpya,” Yohana asema: “Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, . . . umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” Mji huu wa kimbinguni umefanyizwa na washiriki wa kundi la Kikristo. Kwa ujumla, wao wanafanyiza “Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo,” yaani, bibi-arusi wa Kristo Yesu. (Ufu. 21:1, 2, 9) Wao ni mali yake. Paulo alizungumza juu ya hili, akiufananisha ukichwa wa mume juu ya mke wake na ukichwa wa Kristo kama “kichwa cha [kundi].” Vile vile aliandika hivi: “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda [kundi], akajitoa kwa ajili yake.” Maandiko haya yaonyesha wazi Yerusalemu Mpya ni nani, nayo yazungumza juu ya uenyeji unaotumiwa kwa njia yenye upendo.—Efe. 5:22-25; tazama pia 2 Wakorintho 11:2.
2. (a) Kwa kuitikia tangazo la Petro juu ya Yesu ni nani, Yesu alisema nini? (b) Petro aliusema “mwamba” kuwa nani?
2 Yesu, alipokuwa duniani alizungumza juu ya kundi hili na juu yake mwenyewe kama mjenzi wake. Wakati mmoja, baada ya kuwauliza wanafunzi wake wengine walimnena yeye kuwa nani, ndipo yeye alipouliza: “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” Kwa kuitikia, Petro akajibu: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Baada ya kusema kwamba hili lilikuwa limefunuliwa kwa Petro na Mungu kwa njia ya pekee, Yesu aliongeza kwamba “juu ya mwamba huu nitalijenga [kundi] langu.” (Mt. 16:13-18) Petro uyu huyu ndiye aliyehakikisha katika barua yake ya kwanza kwamba Kristo Yesu ndiye msingi-mwamba ambao juu yake Wakristo wamejengwa kama “mawe yaliyo hai” aliposema kwamba Yesu Kristo ni “jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,” alipokuwa akitaja maneno ya Isaya.—1 Pet. 2:5, 6.
3. Petro alionyesha ni nani waliopata kuwa “watu wa milki” ya Mungu mwishowe?
3 Akiendelea, Petro alieleza kwamba nyumba ya kimwili ya Israeli, mali ya pekee ya Mungu ilimkataa Yesu Kristo kama Masihi wao ikiongozwa na viongozi wao wa kidini au wajenzi. Kama ilivyokuwa imetangulia kusemwa kwa unabii: “Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni.” Kwa sababu hiyo, Mungu aliikataa nyumba hiyo ya kimwili. Badala yake, aliliweka kundi la Kikristo kama nyumba ya kiroho ya Israeli liwe mali yake teule, “watu wa milki.” Kwa hiyo, twapendezwa na namna washiriki wa nyumba hii ya kiroho au kundi wanavyochaguliwa. Ni nini mambo ya lazima ya uanafunzi, na je! mambo haya yatumika kwa wote leo wanaotafuta kuwa wafuasi wanyofu wa Yesu?—1 Pet. 2:7-10; Gal. 6:16.
MAMBO YA LAZIMA YA UANAFUNZI
4. Yesu alitia nini katika mambo ya lazima ya uanafunzi?
4 Yesu alitaja mambo ya lazima yanayokamatana na uanafunzi kwa kuwafikiria washiriki wa kundi hili. Lazima mambo matatu yafanywe, kama Yesu alivyosema: “Mwacheni [1] ajikane mwenyewe na [2] kuchukua mti wake wa mateso na [3] kunifuata sikuzote.” Aliongeza maelezo haya kwa uongozi wetu: “Kwa maana ye yote atakaye kuiokoa nafsi yake ataipoteza; lakini ye yote apotezaye nafsi yake kwa ajili yangu mimi ataiona.”—Mt. 16:24, 25, NW.
5. Kujikana mwenyewe kuna maana gani yenye nguvu?
5 Kujikana kuna maana yenye nguvu. Kwamaanisha mengi zaidi kuliko kukosa tu kujidai kuwa mali yako mwenyewe na kudai haki zako, kuchukua maisha kama yalivyo tu. Yamaanisha mengi zaidi kuliko kujinyima vitu fulani tu, kwa mfano jamii za kidini zishauripo kuwa na juma ya kujinyima. Kukana maana yake ni kukataa uenyeji. Hapa kwamaanisha kukataa uenyeji wako mwenyewe kwa kupendelea uenyeji wa Yehova Mungu.
6. Ni nini linalomaanishwa na kuchukua mti wa mateso?
6 Kuchukua mti wako wa mateso kuna maana yenye nguvu pia. Ingawa wanafunzi walipokuwa wakimfuata Yesu hii haikuchukuliwa kwa maana ya halisi, ilionyesha wazi mwendo uliofuatwa kwa kujitolea ambao ungeleta mateso makali, fedheha, aibu na kifo. Tutafahamu hili zaidi tunapolifikiria kukamatana na yale mambo mengine ya lazima ya uanafunzi.
7, 8. Maana yake nini kumfuata Yesu sikuzote, naye alituwekea kielelezo gani, ikitokeza maulizo gani?
7 Jambo la mwisho la lazima alilolitaja Yesu lilikuwa kumfuata yeye sikuzote. Mwanafunzi ni mfunzwa. Walakini, ni wazi kutokana na maneno ya Yesu kwamba yeye alitaka, si kukubali na kuamini aliyofundisha tu, bali pia maisha yote ya mtu yafuate kielelezo kile kile kilichowekwa na Yesu, kwa kuendelea na bila kuacha. Kama alivyosema katika agizo lake la mwisho kwa wafuasi wake: “Kwa hiyo nendeni mkafanye wanafunzi . . . kuwafundisha kushika mambo yote ambayo nimewaamuru ninyi.” (Mt. 28:19, 20, NW) Mkazo mkuu katika kielelezo kilichowekwa na Yesu ulikuwa juu ya kuhubiriwa na kufundishwa kwa habari njema za Ufalme. Maandishi yaonyesha kwamba wanafunzi wake wa wakati huo, na kwa kweli kundi lote la kwanza la Kikristo, walifuata sana kielelezo icho hicho. Hii, pamoja na kutokuwa kwao sehemu ya ulimwengu, ndiyo iliyowaletea chuki na upinzani wa ulimwengu, ikifanya wachukue mti wa mateso.—Yohana 15:19, 20; 17:14-18; Matendo 8:4.
8 Tutapata ufahamu zaidi wa maana ya mambo ya lazima yaliyotangulia ya uanafunzi tuangaliapo namna na sababu gani Yesu mwenyewe aliuweka mfano katika kutimiza mambo ayo hayo ya lazima. Je! yeye alijikana mwenyewe na kuchukua mti wake wa mateso na kufanya hivyo sikuzote? Je! aliipoteza nafsi yake kwa njia fulani?
9. Kama ielezwavyo katika Wafilipi 2:5-8, Yesu alijikanaje kabisa?
9 Ilikuwa kana kwamba mtume Paulo alikuwa na maulizo aya haya akilini alipoandika yafuatayo kwa Wakristo katika Filipi: “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya [mti wa mateso].” (Flp. 2:5-8) Hakuna mtu ambaye angaliweza kujikana mwenyewe kabisa na kwa kiasi hicho. Ikiwa wewe u mali ya Kristo Yesu kama mmoja wa wafuasi wake, lazima uendeleze na kuionyesha nia ii hii.
10. Ni habari gani zaidi juu ya hili zinazotolewa katika Isaya sura ya 53?
10 Maandiko mengine yahakikisha hili na kutoa sababu ya mateso na kifo cha Masihi ili apate kuwa mkombozi wa wanadamu. Kwa mfano, nabii Isaya aliandika hivi juu yake: “Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; . . . [Yehova] ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. Alionewa, lakini alinyenyekea . . . maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; . . . Utakapofanya [mtu mwenyewe] nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, [Masihi] ataona uzao wake [au atapata kuwa na uzao kwa njia hii], ataishi siku nyingi, na mapenzi ya [Yehova] yatafanikiwa mkononi mwake.”—Isa. 53:3-12.
11. Kristo Yesu alipewa zawadi gani kubwa na Yehova mwishowe?
11 Kuangalia kwetu kwa mara nyingine mwendo aliofuata Yesu na kupata hasara kubwa hiyo kusingekamilika bila ya kuangalia matokeo yalikuwa nini mwishowe. Hata kabla ya kuandika yaliyoko juu, Isaya aliongozwa na Mungu aandike mambo aliyokuwa ameyasema Yeye juu ya Masihi anayekuja: “Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.” (Isa. 52:13) Baadaye, Paulo aliendelea kuandika juu ya Masihi kwa Wafilipi Wakristo: “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe . . . na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Flp. 2:9-11) Baada ya kutaja mambo ya lazima ya uanafunzi, Yesu alihakikisha kutukuzwa huku kwa wakati ujao, akisema kwamba “Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” (Mt. 16:27) Paulo alizungumza juu ya “mapenzi yake [Yehova], sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo.” Twaona madaraka hayo (au “usimamizi,” NW) katika jamii ya mashahidi wa Yehova wa Kikristo, njia hiyo ya kufanya mambo, yakiwa yangali yanaendelea baada ya karne kumi na tisa.—Efe. 1:9, 10.
HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA
12. (a) Wengi wanamkubali Yesu kama Mwokozi wao kwa msingi gani? (b) Ni nini uongozi wetu wa pekee ulio salama katika habari hii?
12 Je! wewe u wa Yesu na Baba yake, Yehova? Wewe u mali yao iliyonunuliwa kwa dhabihu ya ukombozi ya Kristo, ukiwa mshiriki wa jamaa ya kibinadamu. (1 Tim. 2:5, 6) Walakini, huenda usikubali hilo. Ni wachache sana wakubalio. Wengi katika Jumuiya ya Wakristo (Kristendomu) wajidaio kuwa washiriki wa mojawapo la makanisa yake wanasema wanamkubali Bwana Yesu kama mkombozi wao. Lakini, wao wanahudhuria kanisani na kutolea kanisa msaada wa fedha na karibu mambo yote yaishia hapo tu. Huenda wakatii kanuni zake za mwenendo mwema, na kunyenyekea mamlaka za kibinadamu na uhusiano wa kibinadamu, lakini hawakujitoa kwa Yehova na Kristo Yesu kwa kuingia katika uhusiano wa wazi nao. Je! wewe umefanya hivyo? Neno la Mungu laonyesha namna hili liwezavyo kufanywa na lipaswavyo kufanywa, hatua kwa hatua.
13. (a) Lazima ujue nini kwanza, nayo hii yapaswa ionyeshweje? (b) Ni hatua gani zaidi lazima Ichukuliwe, nayo hii yaonyeshwaje wazi?
13 Kwanza, imekupasa ujue kwamba kama mshiriki wa jamaa ya kibinadamu umezaliwa asiyekamilika na mwenye dhambi. Umerithi dhambi na mauti. Huwezi kujiokoa mwenyewe na hali hiyo, wala mwanadamu mwingine ye yote hawezi kufanya hivyo. Walakini, kama ilivyokwisha zungumzwa, Neno la Mungu laonyesha kwamba Yeye, Chanzo cha pekee cha uzima, amefanya mpango kwa fadhili kupitia kwa Mwanawe ambao kwao waweza kupatanishwa naye. Kwa kuuitikia ukaribishaji wake waweza kuokolewa na kuingia katika uzima wa milele. Imekupasa ujione kuvutwa uchukue hatua mbili za kwanza, kwa kufahamu hivyo na kuongozwa na dhamiri. Imekupasa ujione kujuta na kuhuzunikia mwendo wako wa zamani kwa unyofu na kweli kwa kufuata njia ya ulimwengu. Ingawa yawezekana huna hatia ya jambo lo lote la uvunjaji wa sheria, wewe ulitoshelezwa na kuishi maisha yako mwenyewe, usiheshimu sana matakwa na kanuni za Mungu. Ikiwa uliongozwa na dini, pengine sasa waona kwamba kwa kweli ulidanganywa na dini ya uongo. Hivyo, zaidi ya hatua ya toba, waona na kukubali pia haja ya kuchukua hatua ya kugeuka. Yaani, ubadili kabisa mwendo wako na kuipa njia ya ulimwengu kisogo. Kama vile Petro alivyowaambia Wayahudi wa siku zake: “Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.” “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.”—Matendo 2:40; 3:19.
14. Baada ya kujifunza maoni ya Mungu juu ya hali ya ulimwengu, imekupasa uoneje?
14 Kwa kweli hatua mbili hizi ni za lazima na za busara kuchukuliwa, zaidi upatapo kuona namna Mungu aionavyo taratibu iliyopo ya mambo, ‘iliyowekwa akiba kwa moto ikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.’ (2 Pet. 3:7) Walakini, kungali kuna hatua ya tatu iliyo ya busara pia nayo yatokezwa na zile nyingine mbili. Dhamiri pia ni ya lazima katika hili. Ulipokuwa katika njia ya mauti, ukiwa mtumwa wa dhambi kwa kutumainia mauti, hukuwa na dhamiri njema kwa Mungu. Lakini sasa, ukiisha kujua na kuthamini Mungu na Mwanawe mpendwa wamefanya iwezekane kujipatanisha nao kwa hasara kubwa namna gani, sasa wajiona kwa njia tofauti sana.—Rum. 6:16; 5:6-8; 1 Yohana 4:9.
15. (a) Ndipo imekupasa ufikie uamuzi gani wa lazima, ukiongoza uchukue hatua gani? (b) Hii yatia ndani uanafunzi gani, pamoja na uhakikisho gani wa kukubaliwa?
15 Juu ya yote, sasa watamani, si baraka ya Mungu tu, bali pia kuingia katika uhusiano wa karibu naye na kuufurahia ukiwa na dhamiri safi. Unaamua kujitoa kwake kwa unyofu na nafsi yote. Hii ndiyo hatua ya wakf. Kwa sala ya moyo kwa Mungu, kupitia kwa Yesu Kristo, wamweleza uamuzi wako, ukimwomba akukubali wewe kulingana na mambo ya lazima ayatakayo kwako. Una uhakikisho wa kwamba atakukubali kwa sababu wamjua ukiuamini ustahili wa dhabihu ya Kristo. Hii yamaanisha kuwa mwanafunzi pia, mfuasi wa nyayo za Yesu Kristo. Unahakikishiwa kwamba yeye pia atakukubali kwa furaha kwa maana yeye ni kama Baba yake. Ukifikiria hili, wapata kujua kwamba jambo jingine latiwa ndani mbali na uamuzi wa ndani wa akili ambao umekwisha ufikia.—Isa. 55:7; Mt. 11:28-30.
16. (a) Yesu alionyeshaje kujitoa kwake afanye mapenzi ya Mungu kwake kama mwanadamu? (b) Hiki ni kielelezo kwako kwa njia gani, ukikumbuka tofauti gani?
16 Petro aliandika hivi: ‘Kristo aliwaachia kielelezo mfuate nyayo zake sana.’ (1 Pet. 2:21) Hatua ya kwanza ionekanayo aliyoichukua Yesu alipojua ulikuwa wakati wa Mungu ufaao, ilikuwa ile ya ubatizo wa maji mikononi mwa Yohana Mbatizaji. Hii ilikuwa mfano wa kujitoa kwake afanye mapenzi ya Mungu kama ilivyokuwa imesemwa kwa unabii juu yake katika Zaburi 40:6-8. (Tazama pia Waebrania 10:5-10.) Yesu hakuwa na dhambi za kutubia. Alikuwa na dhamiri njema kwa Mungu. Lakini kwa habari yako, hatua ya ubatizo ni mfano wa wazi unaoonyeshwa kwa watu wote juu ya wakf wako kufanya mapenzi ya Mungu, na kwa sababu umekuwa mtumwa wa dhambi, ni “ombi linalofanywa kwa Mungu kwa dhamiri njema.” Ingawa ungali asiyekamilika, ‘sasa unatoa viungo vyako kama watumwa kwa haki kwa tumaini la utakatifu.’—1 Pet. 3:21-4:3; Rum. 6:19, NW.
17. Kwa sababu ya 2 Wakorintho 5:14, 15, imekupasa uzioneje hatua zilizokwisha kutajwa?
17 Zikionwa kwa maoni yafaayo, imekupasa ujione inakulazimu kuchukua hatua hizi kwa itikio lenye upendo na shauku kwa mpango wa Mungu wenye upendo na ukaribishaji wa fadhili. Huwekwi chini ya mkazo wala kulazimishwa ufanye hivyo. Badala yake, imekupasa ulione kama pendeleo kubwa.—2 Kor. 5:14, 15.
PENDELEO KUBWA
18. (a) Yesu alionyeshaje kwamba amri yake katika Yohana 13:34 ilikuwa mpya? (b) Kwa sababu gani ni pendeleo kubwa kufuata mwendo ule ule alioufuata Yesu?
18 Hii ndiyo amri ya pili kati ya amri mbili kubwa walizopewa Israeli, kama ilivyosemwa kwa ufupi na Yesu: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” (Mt. 22:39) Lakini Yesu aliwaambia wanafunzi wake hivi: “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” Baadaye jioni iyo hiyo aliongeza hivi: “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.” (Yohana 13:34; 15:13) Yesu alifanya lilo hilo. Alijikana mwenyewe. Yeye hakujaribu kuhifadhi au kuokoa nafsi yake mwenyewe. Alikaribisha wafuasi wake wafanye vivyo hivyo. Kwa sababu gani? Kwa sababu lilikuwa kusudi la Mungu alilolijua tangu zamani kwamba nafasi ingetolewa ya kuuitikia ukaribishaji wake huku uovu ukiruhusiwa uendelee: “Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; ili nipate kumjibu anilaumuye.” (Mit. 27:11) Kama ilivyoonyeshwa kwa habari ya Ayubu, Shetani alikuwa akimlaumu Yehova kwamba hakuna mtu angeendeleza ukamilifu wake kwa Mungu isipokuwa kwa kusudi la kichoyo, isipokuwa akijifaidi kwa kufanya hivyo. (Ayubu 1:9-11; 2:3-5) Yaani, hakuna mtu ambaye angejikana kwa nia kwa sababu ya kumpenda Mungu. Akiifahamu hali hiyo kabisa, Yesu alichukua nafasi kwa nia na furaha afuate mwendo huu. Hata leo hii, wale wanaokuwa wanafunzi wa Yesu kwa nia wanafuata mwendo uo huo. Ni pendeleo tukufu kwetu namna gani kushiriki kweli ingawa kidogo katika kushuhudiwa kwa jina la Yehova! Tunalo pendeleo la kushiriki kutoa jibu hilo kubwa na kamili ambalo Yehova aweza kumrudishia adui yake na mwenye kumlaumu.
19. Ni pendeleo na takwa gani lililowekwa mbele yetu sote wakati huu?
19 Pendeleo la kuchukua “mti wa mateso” ni la wanafunzi wote wa Kikristo kuruhusiwa kwa uovu kukiwa katika kipindi chake cha mwisho, tumaini lao la uzima kukamatana na Ufalme liwe la kimbinguni au la kidunia. Baada ya “dhiki kubwa,” wakf utakuwa unafaa bado, ukiongozwa na upendo ule ule kama sasa, lakini chini ya hali tofauti. Litakuwako takwa la kutolea Yehova uaminifu wa nafsi yote, wala si kuchukua “mti wa mateso.”—Isa. 25:8.
20. (a) Ulizo la uenyeji litaamuliwaje kwa kweli? (b) Kwa habari ya ustahili wa uenyeji wa Mungu, Wakristo wote wa kweli wana maoni gani?
20 Hivyo twaweza kufahamu namna ulizo la uenyeji, lililokwisha hakikishwa, litakavyoamuliwa. Kwa kweli kuamuliwa kwa ulizo kutaonyeshwa baada ya “dhiki kubwa” Shetani na mashetani zake watakapotiwa katika shimo refu lisilopimika nalo litaamuliwa kwa umilele wakati wao na wale wajipangao upande wao watakapoharibiwa milele. Lakini kwa habari ya ustahili wa uenyeji wa Yehova, ushuhuda mwingi umetolewa na wanafunzi wa kweli wa Kikristo, na Kristo Yesu mwenyewe kwamba wanaikubali kwa furaha mamlaka kuu zaidi ya Yehova, na kwamba hata wakipewa nafasi ya kuchagua mwendo wa kujitenga na Mungu wajitegemee wenyewe, wataikataa kabisa.
21. Ni kazi gani yenye kufurahisha na tumaini tukufu vilivyoko mbele yetu?
21 Wakati wa utawala wa Ufalme wa miaka elfu, ushindani juu ya ustahili unaoendelea wa Yehova hautapangwa wala kukubaliwa. Lakini kazi kubwa sana itakayofanywa kipindi hicho, kazi ya kuharibu fujo zote na uharibifu ulioletwa juu ya dunia hii muda wa miaka elfu sita na utawala wa dhambi—huo utakuwa ushindani wenye kufurahisha. Itakapomalizwa, kutafuata nini? Kama vile Paulo alivyoandika: “Hapo ndipo mwisho, [Kristo] atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. . . . ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.” (1 Kor. 15:24-28) Wanadamu wote wakiisha kuunganishwa pamoja, Kristo atamrudishia Baba yake Ufalme, kwa kuukubali uhakika wa kwamba uumbaji wote ni mali ya Yehova kweli. Kwa sababu ya tumaini hilo, twasihiwa tujiunge sasa katika wimbo ule wa kimbinguni: “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”—Ufu. 4:11.
22. Ulizo: Wewe u wa nani laweza na limepaswa lijibiweje?
22 Wewe u wa nani? Umeuitikia ukaribishaji wenye upendo ujitoe kufanya mapenzi ya Mungu kama yaelezwavyo katika Neno lake? Kama sivyo, yaweza kuwa kwamba kuna kuwaza kwa kichoyo au tamaa inayokuzuia? Tukisema ‘kama badala ya Kristo tunaomba: ‘Upatanishwe na Mungu.’ ‘ Na uwe mali yake. Uingie katika uhusiano wa karibu naye na kuufurahia urafiki mwingi naye. Ufurahie shauri la uenyeji wa watu wawili, kwa kumfanya yeye Mungu wako, na kujifanya mwenyewe mmoja wa watu wake waliojitoa.—2 Kor. 5:20, NW; Mik. 4:5; Yohana 15:15; Ufu. 21:3.
—Kutoka The Watchtower, Oct. 1, 1974.