Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 5/15 kur. 222-230
  • Karamu ya Arusi ya Mfalme Katika Kusudi la Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Karamu ya Arusi ya Mfalme Katika Kusudi la Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “WALIOALIKWA KUJA KWENYE KARAMU YA ARUSI”
  • NIA YA “WALIOALIKWA KUJA KWENYE KARAMU YA ARUSI”
  • TAARIFA YA PILI KWA “WALIOALIKWA”
  • Mfalme Awaita Wale Walioalikwa Kwenye Karamu ya Ndoa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kielezi cha Karamu ya Ndoa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kielezi cha Karamu ya Ndoa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kukusanywa kwa Wenye Kuchukua Nafasi Zilizo Wazi Karamuni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 5/15 kur. 222-230

Karamu ya Arusi ya Mfalme Katika Kusudi la Mungu

“Ufalme wa mbingu umekuwa kama mtu, mfalme, aliyefanya karamu ya arusi kwa ajili ya mwanawe. Akawatuma watumwa wake wakawaite wale walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi, lakini hawakutaka kuja.”​—Mt. 22:2, 3, NW,

1. Ni nini kimehubiriwa kwa mataifa kwa miaka 60 sasa, na ni mfano gani wa kweli uonyeshao kama itikio lao litakuwa lenye faida?

ULIMWENGU mzima umo taabani. Hakuna sababu ya kutia shaka kwamba taratibu ya mambo ulio chini yake haimo katika “wakati wa mwisho” uliotabiriwa. Miaka 60 iliyopita “ufalme wa mbinguni,” “ufalme wa Mungu,” umetangazwa katika sehemu zote za dunia kama “tumaini la peke yake” kwa wanadamu wanaotaabika. Lakini inaelekea idadi kubwa zaidi ya wanadamu hawa hawauamini ufumbuzi huu wa kimungu. Watu kwa ujumla hawautaki. Wao ni kama taifa la watu ambao, miaka mia kumi na tisa iliyopita, hawakuutaka “ufalme wa mbinguni,” ulipotolewa kwao. Kukataa kwao toleo hili lifaalo hakukuliletea taifa lao mema. Kulingana na yaliyowapata kama taifa, kugeuka kutoka kwa “ufalme wa mbinguni” leo hakutawafaidi hata kidogo wale wanaopendelea mipango ya kibinadamu badala ya hili “tumaini la peke yake” kwa ulimwengu wetu unaotaabishwa.​—Dan. 12:4; Mt. 3:1, 2; 4:17; Marko 1:14, 15; Luka 6:20.

2. Ni wakati gani, wapi na kwa nani “ufalme wa mbinguni” ulianza kuhubiriwa, nao ulipaswa upewe kwa taifa gani?

2 Zamani, Milki ya Kirumi ilikuwa katika karne yake ya kwanza tu ya utawala juu ya Mashariki ya Kati wakati “ufalme wa mbinguni,” “ufalme wa Mungu,” ulipoanza kutangazwa huko. Mwaka wa 33 wa Wakati wetu wa Kawaida ndio uliokuwa mwaka na nne wa kutangazwa kwake. Ufalme huu ndio uliokuwa habari ya mazungumzo yenye chuki katika mji wa Kiyahudi wa Yerusalemu. Mazungumzo yake yaliingia hata katika hekalu lijulikanalo ulimwenguni katika mji huo mtakatifu. Mazungumzo yalipokuwa yakiendelea, Mtangazaji mkuu wa habari njema za Ufalme aliwaambia hivi wasikilizaji wake wengi, ambao kati yao walikuwako wakuu wa makuhani na wanaume wa madhehebu ya Mafarisayo: “Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.” (Mt. 21:43-46) Kulingana na maneno hayo, ufalme wa Mungu basi ulipaswa uondolewe karibuni kwa taifa lao lipewe taifa lililoanzishwa karibuni ambalo lingezaa matunda yenye kulitambulisha kama linalotawaliwa na ufalme wa Mungu. Maneno ya msemaji yalitokea kweli, kwa maana leo hii taifa lililopendelewa wakati mmoja halina ufalme wa Mungu.

3. Msemaji alianzaje mfano unaohusiana na maneno yake ya unabii?

3 Sababu ya hili kutukia ilikuwa nini? Msemaji wa maneno hayo ya unabii aliendelea kuonyesha kwa kusimulia mwingine wa mifano yake iliyojawa na maana. Mwanamume aliyeusikia aliuandika kwa ajili yetu, naye aanza masimulizi haya sasa kwa kusema hivi: “Akiendelea kujibu Yesu tena akasema nao kwa mifano, akisema hivi: ‘Ufalme wa mbingu umekuwa kama mtu, mfalme, aliyefanya karamu ya arusi kwa ajili ya mwanawe. Akawatuma watumwa wake wakawaite wale walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi, lakini hawakutaka kuja.’”​—Mt. 22:1-3, NW.

4. Ni nini kionyeshacho “mtu, mfalme,” katika mfano wa Yesu alifananisha nani?

4 Anayehusika sana katika mfano huu alikuwa ndiye “mtu, mfalme.” Basi, je! yeye alifananisha nini? Alimfananisha Mungu mwenyewe, kwa maana mfano wote ulianza kwa kusema, “Ufalme wa mbingu umekuwa kama mtu, mfalme,” kwa kuchukua hatua fulani iliyoshinda itikio fulani. Usemi “ufalme wa mbingu” una maana moja na “ufalme wa Mungu,” kwa maana Mungu atawala kama mkuu kupita wote katika mbingu za kiroho zisizoonekana. Kwa mfano, mtawala wa kale wa Babeli alipasishwa jambo lenye kuaibisha kwa kusudi hili lililotajwa: “hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye . . . baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.” (Dan. 4:25, 26) Yesu alikuwa akimtaja Mungu aliposema hivi juu ya Yerusalemu: “Usiape . . . kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.” Yesu aliwafunza wanafunzi wake kusali kwa Mfalme huyu wa kimbinguni, wakisema: “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”​—Mt. 5:34, 35; 6:9, 10.

5. “Mwana” afanyiwaye “karamu ya arusi” na Mfalme wa Kimbinguni ni nani, na ni nini kinachohakikisha hili?

5 Mfalme aliyemo katika mfano wa Yesu asemekana kuwa na mwana. Walakini, Mungu Mfalme wa kimbinguni anao mamia ya mamilioni ya wana wa kiroho, ambao Maandiko yanawaita ‘wana wa Mungu.’ (Ayubu 38:7; Dan. 7:9, 10) Ni yupi kati ya hawa wana wengi anayemaanishwa katika mfano wa Yesu? Ndiye Mwana wa wana katika jamaa ya Mungu ya kimbinguni. Mwana huyu mkuu ndiye anayefanyiwa “karamu ya arusi,” nayo Maandiko Matakatifu yaonyesha kwamba mwana huyu ndiye msemaji wa mfano, Yesu Kristo mwenyewe. Yohana Mbatizaji, aliyembatiza Yesu, alisema hivi kwa habari ya Yesu aliyebatizwa: “Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.” (Yohana 3:28, 29) Katika mfano mwingine, Yesu alijimaanisha mwenyewe, aliposema: “Ndipo ufalme wa mbinguni “utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.”​—Mt. 25:1; 9:15.

6, 7. (a) “Bibi arusi” wa Mwana huyu wa Mfalme wa kimbinguni ni nani? (b) Waefeso 5:23-32 yafananisha uhusiano kati ya Yesu Kristo na kundi lake na nini?

6 Kama ye yote anayetazamia kuwa bwana-arusi, bila shaka Yesu alikuwa mwenye furaha nyingi alipokuwa akimfikiria na kusema juu ya “bibi arusi” huyu ambaye Mfalme, Baba yake wa kimbinguni, angempa. Bila shaka, “bibi arusi” si mtu mmoja, si mwanafunzi mmoja wa Yesu Kristo. Badala yake, ni mtu mwenye watu wengi ndani yake, mwili wake mzima au kundi la wanafunzi waaminifu waliotiwa mafuta. Hili halipaswi lionekane kuwa jambo geni. Katika unabii wa Biblia taifa la kale la Israeli linafananishwa na mke wa Yehova Mungu, kwa maana taifa hilo lilikuwa kana kwamba liliolewa na Yeye kwa kulikubali agano la Torati lililopatanishwa na nabii Musa katika Mlima wa Sinai katika Arabia. (Isa. 54:5; Yer. 3:14; 31:31, 32) Kwa hiyo uhusiano kati ya Mwana wa Mungu na kundi lake lililotiwa mafuta unafananishwa na ule wa mume na mke; kama vile tusomavyo:

7 “Mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.”​—Efe. 5:23, 25, 32.

8. Ni wapi na kwa njia gani arusi ya Mwana wa Mfalme wa kimbinguni na “bibi arusi” wake itakamilishwa?

8 Kukamilishwa kwa ndoa kati ya Mwana wa Mfalme na “bibi arusi” wake wa mfano kutakuwa kwa kuungana kwa Yesu Kristo na kundi lake jaminifu katika mbingu za kiroho kuhusiana na “ufalme wa mbinguni.” Washiriki wa kundi hili lililotiwa mafuta lazima wawe waaminifu kwa Yesu Kristo mpaka kufa kwao, kama bikira aliyeposwa. Kama thawabu kwa uaminifu wao wa ubikira mpaka mwisho wa mwendo wao wa kidunia, watafufuliwa kutoka kwa wafu wakawe “bibi arusi” wake wa kimbinguni milele, ambaye ndilo kundi lake lenye mfano wa Bibi-arusi, katika nyumba ya Baba na Mfalme wa Kimbinguni,​—2 Kor. 11:2, 3.

“WALIOALIKWA KUJA KWENYE KARAMU YA ARUSI”

9. Katika mfano wa Yesu, wale walioalikwa kuja kwenye “karamu ya arusi” walikuwa na uhusiano gani na mfalme, nalo tendo lao la kukubali mwaliko lingeonyesha nini?

9 Kualika kwenye karamu ya arusi ya mwanawe ulikuwa upendeleo mkuu kwa upande wa mfalme. Wale aliowaalika walikuwa watu ambao yeye alikuwa mfalme wao. Walikuwa raia zake. Yeye aliwajua kwa majina. Alijua walikoishi katika milki yake, na kwa hiyo angeweza kuwatuma watumwa wake waliko wakawaarifu karamu ikiwa tayari, karamu ambayo walikuwa wamekwisha alikwa. Tendo la kukubali la watu hawa walioalikwa walipopata taarifa ya utayari wa karamu lingeonyesha heshima ifaayo kwa mfalme wao. Basi, ni nani waliofananishwa na “walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi” katika mfano wa Yesu?

10. Wakati wa mfano, Yehova Mungu alikuwa Mfalme juu ya watu gani, na kupitia kwa mpango gani?

10 Basi, kwa kuwa mfalme amfananisha Yehova Mungu, ni nani waliokuwa watu ambao Yeye alikuwa mfalme wao wakati huo? Ni nani ambao Yesu aliwaambia, “Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake”? Lilikuwa taifa la Kiyahudi. Katika mwaka wa 1513 B.C.E. Yehova Mungu alikuwa amewaingiza katika agano naye kupitia kwa upatanishi wa nabii wake Musa, katika Mlima wa Sinai. Waliingia katika agano hili kwa nia, kushika Torati yake, sheria za msingi ambazo kati yazo zilikuwako Amri Kumi zijulikanazo sana. (Kut. 19:1 mpaka 24:8) Hasa kwa mpango huu wa agano, Yehova akawa Mfalme wa kimbinguni juu ya watu hawa, na hii ilimaanisha kwamba sasa walikuwa “taifa” lililo chini Yake. (Kum. 33:5) Tayari Waisraeli walikuwa wamekwisha imba sifa Zake kama Mfalme wao, baada ya kuwakomboa na kifo katika Bahari ya Shamu, wakiimba kwa sauti: “[Yehova] atatawala milele na milele.”​—Kut. 15:18.

11, 12. (a) Taifa la Israeli lilikuwa limepataje kuwa watu wa Jina la Mungu? (b) Ni kwa njia gani Mungu angeweza kupeleka mwaliko kwao kwa jina lao la taifa?

11 Mfalme huyu wa kimbinguni ana jina​—Yehova​—na, kwa nguvu za kuliingiza taifa la Israeli katika agano la Torati naye kama Mungu wao, wakawa watu wa Jina lake. Waliitwa kwa jina lake. Mpatanishi Musa alisema hivi kwa watu wa agano wa Israeli: “[Yehova] atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya [Yehova], Mungu wako, na kutembea katika njia zake. Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la [Yehova], nao watakuwa na hofu kwako.” (Kum. 28:9, 10) Yehova alisema hivi kwa taifa lake teule, kwa kinywa cha nabii wake Amosi: “Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani.” (Amosi 3:2) Si kwamba tu taifa lilitambuliwa kwa jina Lake, bali Yeye alilijua taifa kwa jina.

12 Aliliambia hivi kwa kinywa cha nabii Isaya: “Lakini sasa, [Yehova] aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.” (Isa. 43:1) Kwa hiyo, ikiwa Yeye alitaka kuwapelekea mwaliko au kuwapa mwaliko wa kudumu, angeweza kufanya hivyo kwa jina la taifa.

13. Mfalme wa kimbinguni alijuaje walikoishi “walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi,” na uhakika huu ulionyeshwa kwa habari ya kuzaliwa kwa nani?

13 Mfalme wa mfano wa Yesu aliyajua makao ya wale aliokuwa amewaalika kwenye karamu ya arusi. Vivyo hivyo Yehova aliyajua makao ya watu wake wateule, watu wale walioalikwa. Alijua walikoishi. Ilikuwa nchi ambayo Yeye alikuwa amewaahidia babu zao Ibrahimu, Isaka na Yakobo, na nchi ambayo Yeye alikuwa amewaleta kwa uaminifu. Hata baada ya uhamisho wao katika nchi ya Babeli, Yehova aliwarudisha kwenye nchi iyo hiyo. Bila ya kuongozwa vibaya, Yehova Mfalme alimtuma Mwanawe Yesu kwenye nchi hiyo. Halikuwa kosa au kwa bahati kwamba Yesu Mzao wa Ibrahimu na wa Mfalme Daudi akazaliwa katika mji wa Bethlehemu katika Jimbo la Uyahudi, katika vuli ya mwaka wa 2 B.C.E, Karne nyingi mapema, Yehova Mfalme alikuwa ametabiri makao ya kuzaliwa huku kwa mwujiza, kwa nabii Wake Mika.​—Mik. 5:2.

14. Mwaliko wa kwanza ulitolewa kwa “walioalikwa” wakati wajumbe wenye kupeleka taarifa walipofika, au taarifa ihusianaje na mwaliko?

14 Kwa utimizo wa mfano wa Yesu, Yehova Mfalme aliyajua makao ya “walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi.” Kwa vyepesi, basi, yeye alijua kwa kuwatuma wajumbe wake wa kupeleka taarifa wakati ambapo karamu ya arusi waliyokuwa wamealikwa ilikuwa tayari na ilipokuwa saa yao ya kuja wakiwa na hamu nyingi ya kula. Mwaliko wa karamu haukutolewa kwanza kwao wakati wajumbe wenye taarifa walipofika nyumbani kwao kuwaambia karamu sasa ilikuwa tayari na imewapasa waje mara moja. Kuwafikia huko lilikuwa jambo la ziada tu, sio mwaliko wa kwanza. Basi, sasa, ni wakati gani na kwa njia gani walikuwa ‘wamealikwa’ au kupewa mwito wa kwanza?

15. (a) Mwaliko wa kuja wenye “karamu ya arusi” ulitolewa mwaka gani, na kwa nani? (b) Wakati huo, mwaliko ulikuwa katika nini, na katika masharti gani?

15 Kwa kweli, hii ilikuwa katika mwaka wa 1513 B.C.E., nayo ilifanywa Mungu Mfalme alipochukua hatua, kwa kuwaingiza watu wa Israeli katika agano la Torati kupitia kwa Musa kama mpatanishi. Mwito wa kwanza au “mwaliko” ulitolewa kwa Waisraeli kama taifa, si kama watu mmoja mmoja, kwa maana taifa wala sio washiriki mmoja mmoja ndilo lingeendelea kuwako mpaka “karamu ya arusi” ya Mfalme iandaliwe. Mwito wa kwanza au “mwaliko” kwa taifa la Israeli ulitiwa ndani katika masharti ya Mungu yaliyoonyesha faida kwa taifa la Israeli ya kuingia katika agano la Torati na Yehova Mungu na kulishika. Wakati alipokuwa akilitoa agano kwa Israeli katika Mlima wa Sinai, Mungu alimwambia Musa aseme hivi: “Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.”​—Kut. 19:1-6.

16. (a) Agano la Torati lilifanywa na taifa la Israeli juu ya msingi gani, na kwa njia gani? (b) Masharti na mwaliko uliokuwamo katika agano hilo yalifikia nani, mpaka wakati gani?

16 Hivyo matumaini ya Ufalme yaliwekwa mbele ya taifa la Israeli, nafasi, kwa kweli mwaliko, wa kuwa “ufalme wa makuhani.” Ufalme huo wa kikuhani ungetenda kama mtumishi wa Mungu kwa faida ya wanadamu wengine wote. Watu wa Israeli waliukubali mwaliko huu wa Mfalme wao wa kimbinguni kwa kuyakubali mashauri Yake na kusema: “Hayo yote aliyoyasema [Yehova] tutayatenda.” Kwa hiyo, Mungu Mfalme alifanya agano la Torati na taifa la Israeli kwa dhabihu zilizotolewa na mpatanishi Musa. (Kut. 19:7, 8; 24:1-12) Si masharti tu ya agano hilo la Torati la Musa yaliyowafikia wazao wa asili wa Waisraeli hao wenye kufanya agano mpaka karne ya kwanza ya Wakati wetu wa Kawaida, bali pia mwaliko wa kuwa “ufalme wa makuhani.” (Rum. 9:4, 5; Matendo 3:25, 26) Kwa sababu wazao hao wa asili wa karne ya kwanza C.E walikuwa taifa ‘lililoalikwa,’ Mungu Mfalme alikuwa akitenda kulingana na masharti ya agano lake kwa kumwinua Yohana Mbatizaji na kumtuma akahubiri hivi kwa taifa la Israeli: “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”​—Mt. 3:1, 2.

17. (a) “Karamu ya arusi” kwa ajili ya mwana wa mfalme inahusianaje na ufalme? (b) Ni kazi gani nyingine itakayofanywa na wale wanaomfanyiza “bibi arusi” wa Baba wa Milele?

17 Hata hivyo, “ufalme wa makuhani” una uhusiano gani na karamu ya arusi ya mfalme kwa ajili ya mwanawe? Kwamba kuna uhusiano kati ya mambo haya mawili Yesu Kristo mwenyewe alifahamu kwa kuuanza mfano wake kwa maneno haya: “Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.” (Mt. 22:1, 2) Kwa kawaida “bibi arusi” ambaye mwana wa mfalme alimwoa angekuwa mkuu na malkia aliyechaguliwa. Kwa hiyo, “bibi arusi” ambaye Mungu Mfalme anamwoza Mwanawe Yesu Kristo ni kundi lake lililotiwa mafuta la wanafunzi waaminifu. Katika mbingu wanafunzi hawa waaminifu waliotiwa mafuta watakuwa zaidi ya “bibi arusi” mmoja kwa Yesu Kristo kama yeye atakayekuwa “Baba wa milele” kwa taifa la wanadamu lililokombolewa. Watakuwa pia warithi wenzi wa Bwana-arusi wa kimbinguni katika Ufalme ambao Mungu Mfalme anampa Mwanawe Yesu Kristo juu ya wanadamu wote.

18. Yesu aliwekaje tumaini la Ufalme mbele ya wanafunzi wake katika Mahubiri yake juu ya Mlima na siku yake ya mwisho ya Kupitwa?

18 Sikuzote Yesu Kristo aliliweka tumaini hili mbele ya wanafunzi wake wa kweli. Katika Mahubiri yake juu ya Mlima, aliwaambia hivi: “Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao. . . . Kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” (Mt. 5:3, 10; 6:32, 33) Na usiku wa sikukuu ya Kupitwa ya mwisho akiwa na mitume wake waaminifu na baada ya Yesu kuandaa Kijio cha Bwana, aliwaambia hivi: “Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.”​—Luka 22:23-30.

19. Ni kwa njia gani Mwana haendelei kuwa wa kifalme bila ya ufalme, nalo kundi la nalo kundi la Bibi-arusi lashirikije pamoja naye?

19 Kwa hiyo kundi la Bibi-arusi la Yesu Kristo litashiriki naye, wao wakiwa warithi wenzake katika ufalme wa kimbinguni naye akiwa kichwa chao kama Bwana-arusi. Yeye atakuwa Mtawala kama Melkizedeki wa kale, aliyekuwa mfalme wa Salemu na vile vile kuhani wa Mungu Aliye Juu Zaidi na kwa hiyo kuhani-mfalme. (Mwa. 14:18-20; Zab. 110:1-4; Ebr. 5:5, 6; 6:20 mpaka 7:28) Yesu Kristo atumikia kama Kuhani Mkuu wa Yehova, na kundi la Bibi-arusi la Kristo ndio makuhani wadogo. Kwa njia hii kundi la kweli la Kikristo linakuwa “ufalme wa makuhani.” Mtume Petro aliliandikia kundi hili akisema hivi: “Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.” (1 Pet. 2:9) Hivyo Yesu Kristo Mwana wa Mungu haendelei kuwa Mwana wa kifalme asiye na ufalme, bali Mungu Mfalme ampa Mwana ufalme wa pekee juu ya wanadamu wote, nayo jamii yake ya Bibi-arusi inaushiriki ufalme huu wa Kimasihi pamoja naye.​—Rum. 8:16, 17.

NIA YA “WALIOALIKWA KUJA KWENYE KARAMU YA ARUSI”

20. (a) Ulizo lilitokea juu ya habari gani ya kizazi hicho kilipoarifiwa kwamba ndicho kitakachoweza kuhudhuria karamu ya arusi? (b) Ni ulizo gani linalotokea juu ya ni wangapi wangeitikia vizuri?

20 Kwa kuingizwa katika agano la Torati la Musa taifa la Israeli lilipewa pendeleo zuri ajabu na “mwaliko.” Kwa habari ya “karamu ya arusi” iliyoandaliwa na Mungu wao, Yehova Mfalme, walikuwa taifa la “walioalikwa.” Lakini zilikuwako hali zilizoshikamanishwa na kuwa kwao “ufalme wa makuhani.” Kwa hiyo ulizo sasa latokea, Nia ya taifa ingekuwa nini likiarifiwa kwamba ndilo lilikuwa kizazi kilichopendelewa na nafasi ya kutenda sasa kulingana na mwaliko wa Mfalme wao na kuingia katika sherehe za arusi? Je! watu wengi wa taifa hilo wangeitikia vizuri kulingana na hesabu na viti vilivyokuwamo katika chumba cha karamu ya arusi? Kulikuwa na nafasi ya wengi, kwa maana mfano waonyesha kwamba mfalme alialika wengi na kwamba vilikuwako viti vingi vilivyotolewa kwa walioalikwa waweze kuegemea meza ya karamu.

21. Ni wakati gani Mfalme wa kimbinguni alipoanza kutuma “watumwa” wake wakawaarifu “walioalikwa” kwamba karamu ilikuwa tayari?

21 Ni wakati gani Mungu Mfalme alipowatuma “watumwa” wake wakawaarifu “walioalikwa” kwamba wakati wa “karamu ya arusi” ulikuwa umefika na kwa hiyo imewapasa waje mara moja, kwa utimizo wa mfano? Hii ilikuwa baada ya ubatizo wa maji wa Yesu na kutiwa mafuta kwake kwa roho takatifu ya Mungu apate kuwa Kristo, yeye aliyetiwa mafuta awe Mfalme wa Kimasihi. Wakati Yesu Kristo aliporudi baada ya siku 40 alizokaa katika jangwa la Uyahudi, Yohana Mbatizaji alielekeza kwake na kuwaambia wasikilizaji, “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Yohana hakumtambua Yesu kama Mwana-kondoo wa mfano tu bali pia alishuhudia kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu. Muda mfupi baada ya hili, Yesu aliyetiwa mafuta alianza kazi yake ya kufundisha pamoja na wengine walioanza kumfuata kama Masihi. Mmoja wa hawa, aliyeitwa Andrea, alimwona ndugu yake Simoni na kumwambia hivi: “Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).” (Yohana 1:26 mpaka 2:2) Hivyo Yesu alianza kuunda kundi la wanafunzi.

22. Kipindi cha kwanza cha taarifa kilikuwa cha muda gani, na ni akina nani walioarifiwa kwanza?

22 Si Yesu Kristo peke yake aliyeuhubiri ufalme wa Mungu wa Kimasihi bali pia aliwatuma wanafunzi wake wa Kiyahudi wakahubiri naye: “Ufalme wa mbInguni umekaribia.” (Mt. 10:1-7; Luka 9:1-6; 10:1-9) Kwa njia hii Mfalme wa kimbinguni, Yehova Mungu, aliwatuma “watumwa” wake waliokuwa chini ya agano la Torati wakatoe taarifa ya kwanza. Hii iliendelea tangu vuli ya mwaka wa 29 C.E. mpaka masika ya 33 C.E., au karibu miaka mitatu na nusu. “Watumwa” hawa walitumwa kwa “walioalikwa” peke yao. Yaani, taifa la Kiyahudi lililokuwa chini ya agano la Torati la Musa lililotoa nafasi ya kuwa “ufalme wa makuhani.” Kwa kuwatambua “walioalikwa,” Yesu aliwaambia hivi wanafunzi wake aliowatuma wakatangaze kwamba wakati ulikuwa umefika: “Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”​—Mt. 10:5, 6; 15:24.

23. Yesu alionyeshaje ulikuwa ndio wakati ufaao wa mwito wa kwanza, lakini mfano wake ulionyeshaje nia ya walioalikwa?

23 Ulikuwa wakati ufaao wa kazi hii ya kwanza ya kutoa taarifa. Yesu aliikumbusha “nyumba ya Israeli” huku kuweka wakati wa mambo kwa kimungu, alipowaambia Wayahudi hivi: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.” (Marko 1:15) Lakini je! kuhubiri katika taifa lote kwa “watumwa” wa Mfalme wa kimbinguni kulilifanya taifa litubu na kuongoka na kumkubali Mwana wa Mfalme kama Masihi wa kifalme? Ilikuwa karibu na mwisho wa mwito wa kwanza wa kutoa taarifa Yesu aliposimulia namna mwito huu wa kwanza ulivyokuwa umepokewa. Katika mfano wake aliendelea kusema hivi: “Lakini hawakutaka.”

24. Kutotaka kwa “walioalikwa” kulikuwa kwa ushupavu kadiri gani, nao mwito wa kwanza ulikoma nini kilipotukia?

24 Ah, ndiyo, taifa halikuongolewa, taifa lote halikumkubali Mwana wa Mfalme Yesu Kristo kama Masihi ambaye kwa ajili yake “karamu ya arusi” ingeandaliwa. Kutotaka kwao kulikuwa kwa ushupavu sana hata wakamshurutisha gavana wa Kirumi Pontio Pilato amwue siku ya Kupitwa ya 33 C.E. Hivyo Yesu alikufa kama “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” (Yohana 1:29, 36) Kifo chake kama dhabihu kamilifu ya kibinadamu kilipaswa kitokeze faida ya milele kwa “walioalikwa” kwenye “karamu ya arusi” iliyo halisi ya Mfalme. Walakini, kifo hiki cha dhabihu kilikomesha kushiriki kwa kipekee na kwa moja kwa moja kwa Yesu Kristo katika kazi ya kutoa taarifa. Kwa njia hii, mwito wa kwanza kwa “walioalikwa” ulikoma.

25. (a) Kwa sababu gani kusudi la Mungu la karamu ya arusi halikushindwa? (b) Kwa sababu gani Mungu bado aliwatambua wale “walioalikwa” kwanza kulingana na agano la Torati?

25 Halafu? Je! matayarisho yote ya “karamu ya arusi kwa ajili ya” mwana wa Mfalme yalikuwa ya bure? Je! sasa yalipaswa kushindwa? Sivyo, si kulingana na kusudi la Mungu Mfalme. Mungu Mwenye Nguvu Zote alimfufua Mwanawe mwaminifu Yesu Kristo kutoka kwa wafu na kumkweza kwenye kiti cha kifalme mkono wa kulia wa Mungu mbinguni. (Matendo 2:32-36; Zab. 110:1, 2; Mt. 22:41-45) Yesu aliyefufuliwa alitoa thamani ya dhabihu yake ya kibinadamu kama Mwana-Kondoo wa Mungu mbele za Mungu, nayo hii ikakomesha agano la Torati la Musa pamoja na dhabihu zake za wanyama walio wadogo kuliko wanadamu. Ijapokuwa agano la Torati lilifutwa likawekwa agano jipya Yesu Kristo akiwa Mpatanishi, Yehova Mungu Mfalme bado aliwatambua kwa rehema “walioalikwa kuja kwenye karamu ya arusi” kulingana na agano la Torati. Alifanya hivi kwa sababu walikuwa ndiyo “nyumba ya Israeli” ya asili na wazao wa asili, wa kimwili wa mzee mwaminifu wa ukoo Ibrahimu, rafiki ya Mungu.​—Dan. 9:24, 27.

TAARIFA YA PILI KWA “WALIOALIKWA”

26. Yesu aliyefufuliwa alionyeshaje taarifa ya pili ilipaswa itolewe kwa walioalikwa wajaze nafasi zote wao peke yao?

26 Yehova Mungu Mfalme alikuwa na sababu ya kughadhibika sana juu ya taifa la “walioalikwa,” lakini akalipa taifa nafasi zaidi ya kuketi katika viti vyote peke yao penye “karamu ya arusi kwa ajili ya mwanawe” iliyokusudiwa. Aliwapelekea taarifa ya pili, lakini ya mwisho. Yesu Kristo alionyesha rehema hiyo ya Mungu iliyoendelezwa muda mrefu kwa walioalikwa, alipowaambia wanafunzi wake hivi muda mfupi tu kabla ya kupaa kwake mbinguni: “Mtapokea nguvu, wakati roho takatifu itakapofika juu yenu ninyi, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu mimi katika Yerusalemu na katika Uyahudi wote na [kwanza baada ya hapo] katika Samaria na kwenye sehemu ya mbali zaidi sana ya dunia.”​—Matendo 1:8, NW.

27. Yesu alionyeshaje ambavyo itikio la walioalikwa lingekuwa kwa taarifa ya pili?

27 Yesu alitabiri itikio lingekuwa nini kwa taarifa hii ya pili kwa upande wa taifa kwa ujumla, akisema: “Tena yeye [mfalme] akatuma watumwa wengine, akisema, ‘Kawaambie wale walioalikwa hivi: “Tazameni! Nimeandaa chakula changu kikuu, ng’ombe zangu na vinono wangu wamechinjwa, nayo mambo yote yako tayari. Njoni kwenye karamu ya arusi.”’ Lakini wao wakaondoka bila kujali, mmoja akaenda kwenye shamba lake mwenyewe, mwingine kwenye biashara yake; lakini wale wengine, wakiwakamata watumwa wake, wakawatenda kijeuri na kuwaua.”​—Mt. 22:4-6, NW.

28. Taarifa ya pili ilianza wakati gani, na ni shtaka gani la Baraza Kuu ya Kiyahudi lionyeshalo kwamba taifa la walioalikwa lilikuwa likiarifiwa?

28 Sehemu hii ya mfano wa Yesu ilianza siku ya Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E., wakati roho takatifu ilipomiminwa juu ya wanafunzi wa Yesu wenye kungojea nao wakaanza kuzihubiri habari njema za ufalme wa Mungu wa Kimasihi katika Yerusalemu kwa Wayahudi na waongofu wasiotahiriwa wa dini ya Kiyahudi. Maandishi yaliyoongozwa kwa roho hayasemi ni mamia mangapi ya maelfu ya waadhimishaji kutoka sehemu nyingi za dunia waliokuwako Yerusalemu. Maelfu ya waadhimishaji walianza kuzisikia habari njema juu ya Yesu Masihi aliyefufuliwa. Kabla ya muda mwingi kupita, Baraza Kuu ya Kiyahudi iliwaambia hivi mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo: “Tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.” (Matendo 5:27, 28) Bila shaka, taifa la “walioalikwa” lilikuwa likipewa taarifa, sasa kwa mara ya pili.

29. Wale walioalikwa waliuitikiaje mwito wa pili wa mfalme, na ni maandishi gani yaonyeshayo mfano wa Yesu ulivyokuwa kweli juu ya jambo hili?

29 Idadi kubwa ya taifa iliuitikiaje ukumbusho wa pili wa Mfalme wa kimbinguni kuja kwenye “karamu ya arusi” iliyokuwa tayari sasa? Kwa kumtukana Mfalme na kumdharau Mwanawe mwenye uwezo wa kuoa, kwa kuonyesha kupendezwa kwingi zaidi kwa kipekee kwa faida zao za vitu vya kimwili kuliko kwenda kwenye karamu ya arusi ya Mwana Wake! Hata waliwaua “watumwa” wake watiifu waziwazi, wahubiri wa Kikristo wa habari njema wa ufalme wa Mungu wa Kimasihi. Yampasa mtu asome kitabu cha Matendo ya Mitume, sura ya tatu mpaka ya tisa tu, ili kupata historia iliyoandikwa ya namna mfano wa Yesu wa unabii ulivyokuwa kweli katika habari hii.

30, 31. (a) Taarifa ya pili ilikoma wakati gani? (b) Katika mfano, mfalme alifanya nini taarifa yake ya pili ilipokataliwa?

30 Basi, taarifa ya pili kwa walioalikwa haikufikia kikomo kwa njia ya vivi hivi tu, ilikuwa lazima ifikie kikomo kulingana na unabii. Ilifanya hivyo mwaka wa 36 C.E., miaka mitatu na nusu baada ya kifo cha kushindania imani cha Yesu Kristo Yerusalemu. Hii ilikuwaje? Mfano wa Yesu ulionyesha ni kwa njia gani. Akiionyesha adhabu ambayo taifa la “walioalikwa” lingeipata kwa kuukataa mwaliko wa Mfalme wao wa kimbinguni kwa kutoaminika, Yesu alisema hivi:

31 “Lakini mfalme akaghadhibika, na kuyapeleka majeshi yake na kuwaangamiza wauaji hao na kuuteketeza mji wao. Kisha akawaambia watumwa wake, ‘Karamu ya arusi i tayari kweli kweli, lakini wale walioalikwa hawakustahili. Kwa hiyo enendeni kwenye njia za kuondokea mjini, na ye yote mtakayemwona mwalikeni kwenye karamu ya arusi.’ Kwa hiyo watumwa hao wakaenda kwenye njia na kuwakusanya pamoja wote waliowaona, waovu na wema pia; nacho chumba cha sherehe za arusi kikajawa na wale wenye kuegemea mezani.”​—Mt. 22:7-10, NW.

32. Maneno yalivyopangwa katika mfano wa Yesu yamaanisha kwamba mfalme alikawiza mipango zaidi ya karamu ya arusi mpaka baada ya kuagiza mji wa “walioalikwa” uharibiwe?

32 Kutokana na yalivyopangwa maneno ya Yesu yaliyo juu anapotoa maelezo ya mfano, haitupasi tuelewe kwamba, kabla mfalme hajaifikiria tena karamu ya arusi, aliyaagiza majeshi yake yakaushambulie mji ambako “walioalikwa” wasio na shukrani waliishi na “kuwaangamiza wauaji hao na kuuteketeza mji wao.” Ama sivyo, ingemaanisha kwamba Mfalme wa kimbinguni, Yehova Mungu, hakuwatuma watumwa wake wakawakusanye watu wake bila ubaguzi kwenye karamu ya arusi mpaka ilipokuwa kuchelewa katika mwaka wa 70 wa Wakati wetu wa Kawaida, kwa maana ni wakati wa kiangazi cha mwaka huo Yerusalemu ulipoangushwa na Warumi wakiwa chini ya Jemadari Tito mwana wa Mfalme Vespasio. Wakati huo, “wauaji” hao waliuawa kweli kweli. Kama inavyoelezwa na Flavio Yosefo, Wayahudi 1,1,00,000 walitoweka katika mazingiwa na uharibifu wa Yerusalemu na 97,000 wakachukuliwa mateka wakawe watumwa.​—Luka 21:20-24; 19:41-44.

[Picha katika ukurasa wa 226]

Katika mfano juu ya mfalme aliyeandaa karama ya arusi, Yesu alionyesha kwamba wengine wanaodhani watakwenda mbinguni hawataweza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki