Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 1/15 kur. 8-9
  • Kielezi cha Karamu ya Ndoa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kielezi cha Karamu ya Ndoa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kielezi cha Karamu ya Ndoa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mfalme Awaita Wale Walioalikwa Kwenye Karamu ya Ndoa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kukusanywa kwa Wenye Kuchukua Nafasi Zilizo Wazi Karamuni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Karamu ya Arusi ya Mfalme Katika Kusudi la Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 1/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Kielezi cha Karamu ya Ndoa

KWA njia ya vielezi viwili, Yesu amefichua waandishi na wakuu wa makuhani, nao wataka kumuua. Lakini Yesu angali mbali kumaliza mambo nao. Yeye aendelea kuwaambia kielezi kingine zaidi, akisema:

“Ufalme wa mbingu umekuwa kama mtu, mfalme, aliyefanya karamu ya ndoa kwa ajili ya mwana wake. Naye akatuma watumwa wake wakaite wale walioalikwa kwenye karamu ya ndoa, lakini wao hawakuwa na nia ya kuja.”

Yehova Mungu ndiye Mfalme ambaye atayarisha karamu ya ndoa kwa ajili ya Mwana wake, Yesu Kristo. Hatimaye, bibi-arusi wake wa wafuasi wapakwa-mafuta 144,000 ataungamana naye mbinguni. Raia za Mfalme ndio watu wa Israeli, ambao, walipoingizwa ndani ya agano la Sheria katika 1513 K.W.K., walipokea fursa ya kuwa “ufalme wa makuhani.” Hivyo, katika pindi hiyo, wao hapo awali walipelekewa mwaliko waje kwenye karamu ya ndoa.

Hata hivyo, wito wa kwanza kwa wale walioalikwa haukupelekwa mpaka vuli ya 29 W.K., wakati Yesu na wanafunzi wake (watumwa wa mfaIme) walipoanza kazi yao ya kuhubiri Ufalme. Lakini Waisraeli wa asili waliopokea wito huu uliotolewa na watumwa hao kuanzia 29 W.K. hadi 33 W.K. hawakuwa na nia ya kuja. Kwa hiyo Mungu alilipa fursa nyingine taifa hilo la waalikwa, kama vile Yesu aelezavyo:

“Tena akatuma watumwa wengine, akisema, ‘Ambieni wale walioalikwa: “Tazameni! Mimi nimetayarisha mlo wangu mkuu, ng’ombe ndume wangu na wanyama waliononeshwa wamechinjwa, na mambo yote yako tayari. Njoni kwenye karamu ya ndoa.’”” Wito huu wa pili na wa mwisho kwa wale walioalikwa ulianza Pentekoste 33 W.K., wakati roho takatifu ilipomiminwa juu ya wafuasi wa Yesu. Wito huu uliendelea mpaka 36 W.K.

Hata hivyo, walio wengi wa Waisraeli hao walikataa wito huo pia kwa madharau. “Bila kujali wakaenda zao,” Yesu aeleza, “mmoja kwenye shamba lake mwenyewe, mwingine kwenye shughuli yake ya kibiashara; lakini wale wengine, wakiwashika watumwa wake, waliwatenda kwa ufidhuli na kuwaua.” “Lakini,” Yesu aendelea, “mfalme akawa na hasira kuu, naye akapeleka majeshi yake na kuharibu wauaji hao na kuchoma jiji lao.” Hilo lilitukia katika 70 W.K., Yerusalemu ulipotandazwa kwa kuharibiwa kabisa na Waroma, na wauaji hao wakauawa.

Halafu Yesu aeleza lililotukia wakati hayo yalipokuwa yangali hayajakamilika: “Ndipo [mfalme] akasema kwa watumwa wake, ‘Karamu ya ndoa iko tayari kweli kweli, lakini wale walioalikwa hawakustahiki. Kwa hiyo endeni kwenye barabara zinazoongoza nje ya jiji, na mtu yeyote mmpataye mwalikeni kwenye karamu ya ndoa.’” Watumwa wakafanya hivyo, na “chumba cha sherehe za arusi kikajawa na wale wenye kuegemea kwenye meza.”

Kazi hii ya kukusanya wageni kutoka kwenye barabara zilizo nje ya jiji la walioalikwa ilianza katika 36 W.K. Ofisa Mwitalia wa kijeshi na jamaa yake walikuwa ndio wa kwanza kukusanywa wakiwa watu wasiotahiriwa wasio Wayahudi. Mkusanyo wa hawa wasio Wayahudi, wote wakiwa ni wenye kuchukua nafasi za wale ambao hapo awali waliukataa wito, umeendelea ukaingia katika karne hii ya 20.

Chumba cha sherehe za arusi chajaa wakati wa karne ya 20. Yesu asimulia ni jambo gani latukia wakati huo, akisema: “Mfalme alipokuja ndani ili akague wageni alitupa jicho akaona mtu mmoja asiyevikwa vazi la ndoa. Kwa hiyo yeye akasema kwake, ‘Jamaa, wewe uliingiaje humu bila kuwa na vazi la ndoa?’ Akaduwaa. Halafu mfalme akasema kwa watumishi wake, ‘Mfungeni mkono na mguu mmtupe nje ndani ya giza lililo nje. Huko ndiko kutakakokuwa kulia kwake machozi na kusaga meno yake.’”

Mtu huyo asiye na vazi la ndoa ni picha ya Wakristo wa mwigizo tu wa Jumuiya ya Wakristo. Mungu hajapata kamwe kuwatambua wao kuwa wenye kitambulisho kifaacho cha kuwa Waisraeli wa kiroho. Mungu hakuwapaka mafuta kamwe kwa roho takatifu wawe warithi wa UfaIme. Kwa hiyo wao hutupwa ndani ya giza nje ambamo watapatwa na uharibifu.

Yesu amalizia kielezi chake kwa kusema: “Kwa maana kuna wengi walioalikwa, lakini wachache waliochaguliwa.” Ndiyo, kuna wengi walioalikwa kutoka taifa la Israeli wawe washirika wa bibi-arusi wa Kristo, lakini ni Waisraeli wachache tu wa asili waliochaguliwa. Walio wengi wa wale wageni 144,000 ambao hupokea thawabu ya kimbingu huthibitika kuwa ni watu wasio Waisraeli. Mathayo 22:1-14; Kutoka 19:1-6; Ufunuo 14:1-3, NW.

◆ Wale walioalikwa kwenye karamu ya ndoa hapo awali ni nani, nao wapelekevya mwaliko huo wakati gani?

◆ Wito wapelekwa lini mara ya kwanza kwa wale walioalikwa, na ni nani watumwa wenye kutumiwa kuutoa?

◆ Wito wa pili wapelekwa lini, na ni nani ambao waalikwa baadaye?

◆ Yule mtu asiye na vazi la arusi ni picha ya nani?

◆ Ni nani wale wengi walioitwa, na wale wachache waliochaguliwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki