Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 3/1 kur. 119-120
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Kutoa Mimba?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Kutoa Mimba
    Amkeni!—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 3/1 kur. 119-120

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Mtu akiwa katika hatari kubwa kwa sababu ya afya mbaya, je! ana haki ya kutoa mimba?

Ingawa hili ni tatizo linalohusu huzuni na wasiwasi mwingi wa kibinadamu, mashauri bora ya Mungu yanaonyesha kwamba mama au mtoto akielekea kuwa hatarini, hiyo haitoi haki ya kuharibu mimba.

Maoni ya wanadamu juu ya ulizo hili yanatofautiana na kupingana. Lakini maoni ya Biblia yanaheshimu uhai. Uhai wa kibinadamu ulianzwa na Mungu akiwa na kusudi. (Mwa. 1:27; Ayubu 33:4; Zab. 100:3-5) Biblia yote yaonyesha kwamba Mungu anaheshimu sana uhai. Alisihi wanadamu kwa upendo wathamini sana maisha zao na kuheshimu maisha za wengine kama kitu kitakatifu. Mtu aliyedharau sheria ya kimungu akaua mwanadamu mwenzake, hata kitoto kichanga kilichokuwa katika tumbo la uzazi, alikuwa na hatia na alipasishwa adhabu.​—Mwa. 9:5, 6; Kut. 21:14, 22-25.

Haiwezi kukanwa kwamba nyakati nyingine mwanamke mwenye mimba huwa katika hatari kubwa. Tatizo la afya, kama vile kukosa sukari na vyakula vya starch, kukazika kwa mishipa ya damu kiasi cha damu kupiga sana isivyo kawaida, au magonjwa mengine yanayohusu mishipa ya moyo, linaweza kufanya madaktari wanyofu waamue kwamba maisha ya mama yamo hatarini. Huenda wakamwambia, ‘Utatoa mimba, au sivyo ufe.’ Au huenda wakapendekeza atoe mimba ielekeapo kuwa mtoto atazaliwa akiwa kipofu au sehemu fulani za mwili zikiwa mbaya, kama inavyokuwa wakati mama apatapo ukambi anapokuwa na mimba. Huenda wengine wakawaza kwamba kutoa mimba nyakati hizo ni kuheshimu uhai. Mtu apaswa kufikiria uhai wa mama na mtoto pia, ingawa kwa vyo vyote hataelekea kuonyesha matatizo hayo si makubwa wala hataonyesha kwamba wanaopendekeza mimba itolewe si wanyofu.

Siku hizi hakuna kitu kama mimba kamilifu, kwa sababu wanadamu wote hawajakamilika. (Rum. 5:12) Hivyo kila mwanamke mwenye mimba anakabiliwa na hatari fulani; jambo la kuhuzunisha ni kwamba wanawake wengine, hata wenye afya, hufa wanapokuwa na mimba na wanapojifungua. (Mwa. 35:16-19) Je! kila mimba itatolewa kwa sababu tu uhai au afya ya mama yaweza kuwa hatarini? Hapana. Ni kweli kwamba nyakati nyingine hatari inakuwa kubwa zaidi kwa sababu mwanamke mwenyewe ni mzee au ana afya mbaya. Hata hivyo, je! wanawake wengi wanaokabiliwa na hatari kubwa ajabu, hawajifungui kwa usalama? Na lazima ikubaliwe kwamba madaktari wanaweza kukosea, hata ikiwa wamepima ugonjwa wakiwa na makusudi mema. Kwa hiyo je! mtu anayekubali maoni ya Mungu juu ya utakatifu wa uhai atakataje maneno kwamba ana haki ya kutoa mimba kwa sababu tu huenda akawa hatarini? Je! uhai wa kitoto kinachokua utamalizwa ati kwa sababu huenda jambo fulani likatokea?a

Vivyo hivyo, kwa kila mama mwenye mimba kunakuwa na uwezekano wa kwamba mtoto atazaliwa na kasoro au akiwa ameharibika sehemu fulani ya mwili. “Karibu mmoja kati ya watoto 14 huzaliwa na kasoro; wengine wanapatwa nazo kwa sababu ya kukosa sukari na starch . . . wengine hawajiwezi kwa kuwa ni vilema na huenda wakaishi siku chache tu.” (New York Times Magazine, Sept. 8, 1974, uk. 100) Je! tutakata maneno kwamba mimba zote zapaswa kutolewa ati kwa sababu hatari yaweza kutokea? Hata kidogo.

Huenda nyakati nyingine kukawa na hatari kubwa sana ya mtoto kuwa na kasoro. Kwa mfano, ndivyo inavyoelekea kuwa wakati mwanamke amepita miaka 40 au ikiwa alitumia dawa fulani zenye nguvu sana au akapatwa na ugonjwa wenye kumharibu wakati mimba ilipokuwa ikianza. Vitoto 10 mpaka 15 kati ya mia moja vinavyozaliwa na mama wanaopatwa na ukambi wakati wa juma kumi na mbili za kwanza za kuchukua mimba vinapatwa na madhara ya ugonjwa huo, nayo yanaonekana katika mwaka wa kwanza wa uhai wa mtoto. (Bila shaka, hiyo yamaanisha pia kwamba 85 mpaka 90 kati ya watoto 100 wa namna hiyo hawapatwi na ugonjwa huo.) Lakini mtu mwenye kuheshimu sana uhai awezeje kusema kwamba ana haki ya kumaliza uhai wa mtoto anayekua kwa sababu tu kuna uwezekano kwamba mtoto atapatwa na madhara?

Kuna mfano wa mwanamke mmoja katika Afrika Kusini unaoonyesha hakuna hakika kwamba hatari hizo zinaweza kutokea. Mwanamke huyo alitungwa sindano ya ugonjwa wa figo bila ya kujua alikuwa na mimba. Kwa sababu hiyo, daktari wake alisema baadaye kwamba mtoto angekuwa mkosa-akili au angekuwa na kasoro mbaya sana ya mwili; akamsihi mama huyo atoe mimba. Mama huyo alipojifunza kwa mashahidi wa Yehova kwamba Biblia yasema uhai uheshimiwe, akakataa kutoa mimba. Alijua kwamba, hata ikiwa mtoto wake alipatwa na madhara, Yehova angeweza kuyaondoa katika Taratibu Mpya inayokuja. (Linganisha Isaya 35:5, 6; Ufunuo 21:4) Matokeo yalikuwa nini? Alizaa kisichana chenye afya. Lakini hata kama binti huyo angalikuwa na madhara na kuhitaji uangalizi zaidi na matibabu, bado mama angalikuwa amefanya haki kwa kuamua kumwacha awe hai, awe na tumaini la kupata uzima wa milele.

Kwa hiyo, mwanamke ambaye amesihiwa atoe mimba ndiyo apone kwa sababu afya au uhai wake au wa mtoto wake umo hatarini, apaswa kukumbuka sana, sana, maoni ya Biblia. Hatari inayoweza kutokea, hata iliyo kubwa sana, haitoi haki ya kujiamulia mambo na kuua kwa makusudi kitoto kilicho katika tumbo la uzazi. Imani halisi na ushujaa utahitajiwa ili kuamua kulingana na maoni ya maandiko, lakini huo ndio utakaokuwa uamuzi ufaao kweli kweli, utakaokubaliwa na Yehova milele.

[Maelezo ya Chini]

a Nyakati nyingine matibabu ya ugonjwa, kama cancer ya shingo huua kijitoto kilichoanza kuumbika ndani ya mimba. Lakini huenda jambo hilo lisiepukike: kuharibu mimba siyo matibabu ya ugonjwa huo wala hakufanywi kwa makusudi. Vivyo hivyo, nyakati nyingine mbegu ya mwanamke iliyotiwa mimba hubaki katika mrija (fallopian tube) unaotumiwa na yai linaposafiri kutoka mfuko wa mayai kuelekea kwenye mji wa mimba, kisha mbegu hiyo huanza kukulia mrijani badala ya kukulia katika mji wa mimba. Mimba hiyo iliyokaa mahali pabaya haiwezi kuwa mtoto katika mrija huo mdogo; baadaye itakwisha na kapasua mrija na kuua kijitoto kilichokuwa kimeanza kuumbika. Kwa kawaida madaktari huponya hali hiyo kwa kuondoa mrija huo kabla haujapasuka, ikiwa wameiona hali hiyo mapema. Mwanamke Mkristo mwenye mimba katika mrija aweza kuamua kama atakubali kupasuliwa. Katika hali za kawaida, bila shaka angekuwa na nia ya kukabili hatari zo zote za mimba ili mtoto wake aweze kuishi. Lakini mimba ikikaa katika mrija anakuwa katika hatari kubwa na hali kijitoto kilichokuwa kimeanza kuumbika hakiwezi kuendelea kuishi na kuzaliwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki