Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 7/15 uku. 320
  • Nilipata Uhuru Gerezani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nilipata Uhuru Gerezani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • Utoro Wangu Kuelekea Kweli
    Amkeni!—1994
  • Kushinda Vipingamizi kwa Kuweka Miradi
    Amkeni!—2001
  • Simba Angurumaye awa Kondoo Mpole
    Amkeni!—1999
  • “Mmebadili Maoni Yangu Juu ya Mashahidi wa Yehova”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 7/15 uku. 320

Nilipata Uhuru Gerezani

NAONA ni muda mrefu sana umepita tangu nilipotiwa gerezani Canada, baada ya kufyatuliwa na afisa wa polisi wa kaskazini ya Ontario risasi ya kiasi cha 30.30.

Lakini, kwanza nilipelekwa hospitalini nikakatwe mkono wangu wa kuume uliovunjwa. Ndipo niliposhtakiwa mahakmani kwamba nilijaribu kuua kwa kujitia katika pigano la kutumia bunduki nikiwa nimelewa, likahatirisha maisha yangu mwenyewe, ya mwenzangu na polisi aliyehusika. Kwa hiyo nililazimika kuishi nikiwa nimefungwa katika gereza lenye kuta za rangi ya kijivu.

Ili nisikae bila kufanya lo lote, nilijaribu kuwa na elimu nzuri zaidi. Nilipokuwa nikijifunza habari za viumbe na mazingira yavyo nilijua kwamba jamii yetu ya leo inaelekea kumalizika kabisa.

Hilo lilinikumbusha jambo jingine la namna hiyo. Miaka kadha kabla ya hapo shahidi mmoja wa Yehova mwenye subira nyingi alinitembelea akatumia kitabu kidogo kinachohusu Biblia kuzungumza nami kirafiki juu ya Maandiko, aliponikuta nyumbani. Alikuwa amenionyesha katika Biblia kwamba kizazi hiki ndicho kitakachoona jamii yenye kuharibu dunia ikiondolewa kisha taratibu mpya ya mambo ianzwe hapa ikiwa chini ya utawala wa Yehova Mungu, kwa kutumia Mwanawe, Yesu Kristo, kama mkuu wa serikali hiyo.

Muda mfupi baada ya hapo nilianza kuzungumza kwa bidii na mfungwa mwenzangu, jina lake Bill, aliyekuwa katika mwaka wake wa kwanza wa kifungo cha miaka kumi na miwili, nasi tuliendelea kuzungumza na kuacha-acha nyakati nyingine kwa muda wa miezi miwili. Mazungumzo yalikolea tulipopata gazeti Mnara wa mlinzi na kamusi ya Biblia.

Ndipo nilipojua kwamba tusingefaulu bila kupata msaada zaidi. Nilifikiria mwanamume yule wa kaskazini ya Ontario nikamwandikia atusaidie na kutuletea vitabu. Vitabu kadha vilipelekwa lakini vilizuiwa visitufikie. Lakini, afisi ya tawi ya Watch Tower Society ilipashwa habari nao wakaagiza wajumbe wa kundi la Mashahidi wa Yehova la sehemu tuliyokuwa watufikie.

Kwanza hatukukubaliwa tuwe na chumba kingine cha kujifunzia. Kwa hiyo mimi nilifunzwa peke yangu, naye Bill alifunzwa peke yake, katika eneo la wageni, huku watu wakivuta sana sigareti hata zikatutoa machozi. Baada ya muda mfupi watu wote gerezani walijua lililokuwa likitendeka. Kwa hiyo, jina la Yehova lilitangazwa zaidi kuliko tulivyotazamia. Mwishowe, tulipewa chumba kingine tukaagizwa tusiendeshe mafunzo zaidi katika eneo la wageni.

Novemba mwaka 1973 nilipewa ruhusa ya kuondoka gerezani kwa muda, nayo ilikuwa ndefu kuniwezesha nihudhurie hotuba ya ubatizo katika nyumba ya Shahidi na kuzamishwa katika kidimbwi kilichokuwa nje. Maji na hali ya hewa yalikuwa baridi, lakini nilichangamka moyoni kwa kushirikiana na ndugu. Masika yaliyofuata Bill pia alionyesha alijiweka wakf kwa Yehova.

Mimi nimepewa kifungo cha nje na sasa ninatangazia watu ufalme wa Mungu mlango kwa mlango, karibu na kuta za gereza za rangi ya kijivu, nilikokaa siku nyingi.

Kwa sababu ya jitihada za Bill, na za mtu mwingine sasa, aitwaye Phillip, kazi ya Ufalme yaendelea upande mwingine wa kuta, ijapokuwa vipingamizi vinatokezwa na wajumbe wa dini kubwa-kubwa na wafuasi wao. Waalimu, walinzi na wafungwa pia wamepewa ushuhuda, kadiri nafasi ilivyopatikana. Kama vile watu wengi wasivyoitikia huko nje, ndivyo wengi wasivyoitikia upande wa ndani wa kuta za gereza.

Lakini kazi inaendelea, na huenda mtu mmoja au wawili zaidi wakapata nafasi ya kuitikia na kujifunza kweli ya Mungu, kwa fadhili zisizostahilika na subira ya Yehova.

Siwezi kueleza kwa maneno mambo mengi ambayo Yehova alinifanyia na yale anayofanyia ndugu zangu wa kiroho gerezani. Tunajitahidi tuitikie upendo wa Mungu kwa njia ya pekee tuwezayo, yaani, kujitahidi kwa utii tuwape wengine ujumbe huu wa uzima.

Huenda vipingamizi vinavyokupata maishani vikaelekea kutoshindika dunia yote ipatwapo na huzuni nyingi. Jipe moyo na uache Mashahidi wa Yehova wakusaidie, kama walivyonisaidia mimi, uone katika Neno Takatifu la Mungu kwamba unaweza kuwa na tumaini imara, kama vile wengine wengi wamekuwa nalo.​—Imetolewa na mtu fulani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki