Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 7/1 uku. 312
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • Mahubiri ya Mlimani—Kuzuia Uzinzi na Talaka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Uzinzi
    Amkeni!—2015
  • Heshimu “Kile Ambacho Mungu Ameunganisha”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 7/1 uku. 312

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Mke wangu, ambaye si mtumishi wa Mungu, ampenda mwanamume mwingine. Je! inafaa nimpe talaka kwa sababu inaelekea “amekwisha kuzini naye moyoni mwake,” kama Yesu alivyotaja katika Mathayo 5:28?

Katika Mathayo 5:28 Yesu hakusema kinachoitwa na wengine “uzinzi wa kiroho” ni msingi wa kutoa talaka.

Angalia maneno ya Yesu: “Mlisikia kwamba ilisemwa, ‘Usifanye uzinzi.’ Lakini mimi nawaambia kwamba kila mtu aendeleaye kutazama mwanamke ili kumtamani amekwisha fanya naye uzinzi moyoni mwake.”​—Mt 5:27, 28, NW.

Hapa Kristo alikuwa akieleza kwamba Wayahudi waliosikiliza walipokuwa wakipewa Amri Kumi hawakuielewa amri ya saba kuwa na maana ya kuepuka uzinzi halisi tu. (Kut. 20:14; Kum. 5:18) Alionyesha kwamba uvunjaji huo wa sheria huanzia moyoni mwa mtu. Kama Yakobo alivyoeleza baadaye, tamaa mbaya za moyoni zinaweza kuongoza mtu afanye dhambi, nazo zimeongoza watu mara nyingi. (Yak. 1:14, 15; Mit. 6:25) Zilimwongoza Daudi, akatazama mke wa mwanamume mwingine na kumtamani, kisha akazini naye. (2 Sam. 11:2-4) Kwa hiyo Yesu alihimiza wasikilizaji wake waepuke tamaa yenye dhambi inayoweza kuongoza watu watende dhambi, si kuliepuka tendo lenyewe tu la kufanya dhambi.

Ikiwa mtu fulani, mwanamume au mwanamke anasitawisha tamaa mbaya hiyo (anaendelea kumtazama mwanamke’) Mungu ajua hivyo kwa sababu Yeye “huutazama moyo.” (1 Sam. 16:7; Mit. 24:12; Ebr. 4:13) Mungu ajua kwamba mtu anayetaka sana kufanya uasherati huenda akawa hajapata nafasi ya kutosheleza tamaa yake. Kwa hiyo mtu wa namna hiyo amekwisha kuwa na lawama machoni pa Mungu.

Lakini je! tamaa hiyo tu ya kufanya uzinzi inatoa msingi unaopatana na Maandiko wa kutaliki mwenzi wa mtu na kuwa na uhuru wa kuoa tena? Sivyo. Yesu hakuwapa wanadamu mamlaka ya kuamua mambo wakitegemea tamaa ambazo labda mtu anazo moyoni. Kwa mfano, mtume Yohana aliandika kwamba “kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji.” (1 Yohana 3:15) Lakini, wazee Wakristo katika kundi hawana mamlaka ya kufukuza mtu wakisema ni mwuaji, kwa sababu wanadhani ana chuki ya kadiri fulani moyoni mwake. Hawawezi kama Mungu kusoma mioyo ya watu na kuihukumu kwa usahihi.

Kwa hiyo, Yesu aliposema kwamba sababu ya pekee inayopatana na Maandiko ya kutaliki mtu ni “uasherati” (Kigiriki, porneia, maana yake ufisadi unaohusu viungo vya uzazi), alimaanisha matendo halisi ya uasherati.​—Mt. 19:9.

Ikiwa mke wako ana nia ya kuzungumza nawe, mwaweza kuzungumza jambo hili: Mungu Muumba wetu ajua yaliyo bora kwa wanadamu, na kwa hiyo atuhakikishia kwamba kufanya uasherati hakuleti furaha ya kudumu. Hilo laonyeshwa wazi tunapochunguza kwa uaminifu jinsi uasherati umeharibu maisha za watu wengi ambao wameufanya. Hivyo ni hekima kuondoa upesi tamaa za kufanya uasherati kabla hazijatuongoza kuufanya na kutuletea huzuni. Hata mtu aweza kukosa furaha akifurahia mawazo ya kufanya uasherati.

Kunapokuwa na matatizo katika ndoa, kwa kawaida yako mambo ambayo wenzi wote wawili wanaweza kufanya waimarishe uhusiano wa ndoa na kurudisha upendano uliowafanya waoane. Katika habari hiyo, pengine wewe na mkeo mwaweza kuzungumza pamoja habari zilizomo katika mfululizo wa makala zinazosema “Kufaulu Kutatua Matatizo ya Jamaa” katika Awake! la Aprili 22, 1974.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki