Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 12/15 kur. 572-573
  • Aleksanda Mkuu na Mifano ya Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aleksanda Mkuu na Mifano ya Biblia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • Ugiriki—Ile Serikali Kubwa ya Tano ya Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Milki ya Wamedi na Waajemi Katika Unabii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Ni Nani Atakayeutawala Ulimwengu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 12/15 kur. 572-573

Aleksanda Mkuu na Mifano ya Biblia

BIBLIA inatumia mifano mingi sana, hasa ya unabii. Mifano hiyo inasaidia wasomaji na wasikilizaji kufahamu mambo upesi. Tena, mifano iliyo wazi inaweza kukumbukwa sana kuliko mambo mengi yanayotajwa bila mifano. Faida nyingine ya mifano ni kwamba, habari nyingi zinaweza kuonyeshwa wazi kwa njia nyepesi.

Mfano mmoja ni kitabu cha Danieli, nacho kimejawa na mifano mingi sana. Kwa mfano, Mamlaka ya Ulimwengu ya Ugiriki inafananishwa na beberu (mbuzi dume) na chui mwenye vichwa vinne na mabawa. Tukichunguza sana mifano hiyo tunaona kwamba inafaa sana. Tena tunashangaa kuona jinsi unabii wa Biblia umetimizwa kwa njia ya ajabu.

Mamlaka ya Ulimwengu ya Ugiriki inafananishwa na mbuzi na kusemekana hivi: “Tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. Naye akamwendea huyo kondoo mume [mwenye kufananisha Milki ya Wamedi na Waajemi, kama inavyoonekana wazi katika Danieli 8:20] mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake. Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ikavunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.”​—Dan. 8:5-8.

Ukilinganishwa na Milki ya Wamedi na Waajemi, Ugiriki ulikuwa upande wa magharibi. Kwa hiyo beberu huyo, ambaye ni Milki ya Ugiriki, alitoka magharibi kuelekea mashariki. Milki ya Ugiriki ilipanuka upesi kama umeme, kama kwamba ilikuwa ‘haigusi nchi.’ Baada ya karibu miaka saba tu ya kupiga vita, Aleksanda Mkuu aliweza kupanua utawala wake ukafika katika Asia Ndogo, Misri, Shamu, Milki kubwa sana ya Wamedi na Waajemi na hata sehemu fulani za Bara Hindi. Si ajabu basi kwamba Milki ya Ugiriki inafananishwa na chui mwenye mabawa katika Maandiko. (Dan. 7:6) “Kondoo, mume,” ambaye ni Milki hodari ya Wamedi na Waajemi, alikuwa hoi akilinganishwa na mbuzi aliyefananisha Ugiriki.

“Pembe ile kubwa” au “mashuhuri” ni Aleksanda Mkuu. Yeye ndiye kiongozi aliyewezesha majeshi yake kushinda maeneo mengi sana. Muda mfupi baada ya kufa kwake akiwa na umri wa miaka 33, “pembe” nne au watawala wanne walitawala sehemu fulani za maeneo makubwa yaliyokuwa yakitawalwa na Aleksanda.

Karibu miaka 22 baada ya “pembe ile kubwa,” yaani, Aleksanda, ‘kuvunjika’ kwa kufa, majemadari wake wanne walitawala. Seleucus Nicator alitawala Mesopotamia na Shamu. Cassander alitawala Makedonia na Ugiriki. Ptolemy Lagus alitawala Misri na Palestina. Lysimachus alitawala Thrace na Asia Ndogo. Hivyo ndivyo milki hodari iliyokuwa imejengwa na Aleksanda Mkuu ilivyokuwa kama chui mwenye vichwa vinne, kama inavyoelezwa katika Danieli 7:6: “Kisha nikatazama, na kumbe! mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Hakika unabii wa Danieli ulitimizwa kwa njia ya ajabu sana kuhusu Milki ya Ugiriki, lakini hasa kumhusu Aleksanda Mkuu. Jambo hilo limekubaliwa muda mrefu. Yosefo, mwanahistoria Myahudi wa karne ya kwanza, anasema kwamba Aleksanda alifika Yerusalemu akaonyeshwa unabii wa Danieli. Yosefo anaandika yafuatayo juu ya maoni ya mshindi huyo: “Wakati alipoonyeshwa kitabu cha Danieli, ambamo alikuwa amesema kwamba mmoja wa Wagiriki angeharibu milki ya Waajemi, aliamini kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa ametajwa.” Ingawa watu wengi leo wanatia shaka wakisema jambo hilo halikutukia, ni hakika kwamba Aleksanda Mkuu alionekana kuwa ametimiza unabii, kwa maana Yosefo anayataja mapokeo hayo.

Hakika Biblia inasema kweli kabisa juu ya matukio yaliyotukia katika Milki ya Ugiriki, yakifananishwa na matendo ya mbuzi (beberu) na chui mwenye mabawa manne. Huo ni mmoja tu wa mifano mingi inayoonyesha jinsi Maandiko yanavyotumia mifano. Tunaweza kufaidika sana na kupata nguvu katika imani yetu kwa kuchunguza mifano hiyo ya unabii. Ikiwa ungependa kusaidiwa, Mashahidi wa Yehova walio katika eneo lako watafurahi kukusaidia ujifunze Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki