Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 3/1 uku. 24
  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • “Katika Msafara wa Ushindi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kufukiza Uvumba—Je, Kunahitajiwa Katika Ibada ya Kweli?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Kueneza Manukato ya Maarifa juu ya Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 3/1 uku. 24

Maswali Kutoka Kwa Wasomaji

● Mtume Paulo alikuwa na maana gani katika 2 Wakorintho 2:15, 16 alipojitaja mwenyewe na wenzake kuwa “harufu”?

Mtume Paulo aliandika hivi: “Sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima.”​—⁠2 Kor. 2:15, 16.

Tunaweza kuyafahamu maneno hayo vizuri zaidi tukifikiria mambo yaliyotukia wakati wa maandamano ya ushindi ya Warumi. Wakati jeshi lenye ushindi liliporudi na kupita katika mji wa Rumi kwa kuandamana, ubani ulichomwa (ukafukizwa) juu ya madhabahu za mahekalu na kueneza harufu nzuri hewani. Manukato ya ubani huo yalikuwa na maana mbalimbali kwa watu mbalimbali. Harufu hiyo ilikuwa nzuri kwa askari walioshinda vitani, ikawa na maana ya kwamba wangepata vyeo vyenye heshima, madaraka makubwa zaidi na mali. Lakini kwa mateka wasiosamehewa waliokusanywa pamoja waandamane katika barabara, ubani huo wenye kuchomwa uliwakumbusha kwamba wangeuawa baada ya maandamano. Vivyo hivyo, ujumbe uliohubiriwa na mtume Paulo pamoja na wenzake ulikuwa kama harufu yenye kuwapendeza walioukubali lakini ukawa harufu mbaya sana kwa walioukataa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki