Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 3/15 kur. 23-24
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Hawaoni Ubora wa Hekima Nyakati Zote
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Maskini
    Amkeni!—2013
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 3/15 kur. 23-24

Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Watu Hawaoni Ubora wa Hekima Nyakati Zote

Katika ulimwengu huu, mara nyingi mambo yanakuwa tofauti sana na vile mtu anavyotazamia yawe. Ni kama vile Mfalme Sulemani alivyoona: ‘Huenda mwenye hekima akakosa chakula na mwenye ustadi akakosa upendeleo.’ (Mhu. 9:11) Sababu kubwa inayofanya mambo yawe hivyo ni kwamba wanadamu wanaweza kuamua mambo kwa kutazama sura badala ya kuangalia jinsi mambo yalivyo hasa.

Mfalme Sulemani mwenye hekima alitoa mfano mzuri sana wa jambo hilo, mfano ambao aliuona kuwa “neno kubwa” kwake. Tunasoma hivi: “Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa ni neno kubwa [“ilinistaajabisha sana,” New Berkeley Version]. Palikuwa na mji mdogo [mahali padogo sana], na watu ndani yake walikuwa wachache [kwa hiyo hawakuwa na nguvu nyingi za kupalinda]; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga. Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule; lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.” (Mhu. 9:13-15) Kama isingalikuwa ni kwa sababu ya maskini huyo mwenye hekima, mji ungaliingia mikononi mwa huyo “mfalme mkuu.” Lakini hekima ya maskini huyo ilimshinda mfalme na watu wake wa vita walipokuwa wameuzingira mji. Hata hivyo, badala ya watu kuona kwamba walikuwa na deni ya kusaidiwa na maskini huyo, walimsahau kabisa baada ya hatari kupita.

Sulemani alikata maneno hivi kutokana na tukio hilo: “Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.” (Mhu. 9:16) Naam, mtu anapokuwa hana cheo kikubwa au umashuhuri, mara nyingi maneno yake yanapuzwa. Yanaonekana kuwa yasiyofaa kitu. Nyakati nyingine, maneno ya maskini yanafuatwa kwa sababu wenye kuyafuata hawana jambo jingine la kufanya ila kuyasikiliza, lakini hatari ikiisha pita maskini huyo hapewi heshima yo yote.​—Linganisha 1 Wakorintho 1:26, 27; 2:8-11.

Hata hivyo, hekima ina ubora mwingi nayo haidharauliwi nyakati zote kwa sababu tu imetokana na mtu asiye mashuhuri. Sulemani aliendelea kusema hivi: “Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu. Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.”​—Mhu. 9:17, 18.

Kama vile mwenye hekima alivyoonyesha hapo, ni afadhali sana, tena ni busara zaidi, kuyasikiliza maneno yasemwayo na wenye hekima kwa utaratibu na heshima, hata wawe wana cheo kidogo namna gani, badala ya kusikiliza makelele ya mtawala anayeungwa sana mkono na raia wanaoonyesha kwa mwenendo na matendo yao kwamba ni wapumbavu. Kama ilivyoonyeshwa katika kisa cha maskini mwenye hekima, hekima inaweza kuleta faida nyingi kuliko vifaa vya vita. Lakini, mtenda dhambi mmoja tu au mpumbavu anaweza kuleta matata yasiyoelezeka. Mtu huyo anaweza kuchafua mipango mizuri sana, kuharibu sifa ya mtaa wa watu au kutapanya nguvu na mali kwa sababu ya mawazo yake mabaya ambayo labda anayatamka, au kwa sababu ya matendo yake mabaya. (Linganisha 3 Yohana 9-11.) Hakika hekima inapasa kupendelewa zaidi hata wanadamu wasipowathamini wale walio nayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki