Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 12/1 kur. 20-21
  • Mahubiri ya Mlimani—“Upatane Kwanza Na Ndugu Yako”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahubiri ya Mlimani—“Upatane Kwanza Na Ndugu Yako”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Habari Zinazolingana
  • Jambo la Kufanya Unapoudhi Wengine
    Amkeni!—1996
  • Dhabihu Zilizompendeza Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Tunapaswa Kuwatendea Wengine Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 12/1 kur. 20-21

Mahubiri ya Mlimani​—⁠“Upatane Kwanza Na Ndugu Yako”

BAADA ya kuwaonya wasikilizaji wake juu ya hasara iletwayo na hasira iliyoendelezwa, Yesu alielekeza fikira zao katika kuondoa vyanzo vya hasira. Yeye alisema: “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.”​—⁠Mt. 5:23, 24.

Katika habari hii “sadaka” ilimaanisha dhabihu yo yote ambayo mtu angetoa kwenye hekalu la Yehova. Dhabihu za wanyama zilikuwa zenye maana zaidi, ziliamriwa na Mungu kama sehemu ya ibada ya kweli. Walakini kwa mtu ambaye angekumbuka ‘ya kuwa ndugu yake ana neno juu yake,’ kulikuwako jambo lenye maana hata zaidi. “Iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako,” kasema Yesu. “Upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.”

Pengine jambo hili halikuwa gumu kama linavyoonekana, kwa sababu pindi za kawaida za kuleta dhabihu za namna hiyo zilikuwa wakati wa sikukuu tatu za kila mwaka; Sikukuu ya Kupitwa, Pentekoste na ya Vibanda. (Kum. 16:16, 17) Yaelekea ndugu aliyeudhika alikuwa kati ya wasafiri waliokusanyika Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu hizo.

Hapa huenda mtu akakumbuka takwa la torati ya Musa kuhusiana na sadaka za hatia. Katika visa vya wivi, upotezaji au udanganyifu uliohusu mali, sheria ya Mungu ilimtaka mtu aliye na hatia lakini mwenye kutubu arudishe yote pamoja na sehemu ya 20 kwa mia ya kuongezea kabla ya kutoa sadaka yake. (Law. 6:1-7) Hata hivyo, maelezo ya Yesu hayakuhusu sadaka za hatia peke yake pamoja na makosa fulani fulani. Kulingana ,na maneno ya Mwana wa Mungu, kutolewa kwa sadaka yo yote kulipaswa kuahirishwa ikiwa mtu alikumbuka kwamba kwa haki ndugu yake alikuwa na neno juu yake​—⁠jambo ambalo dhamiri yake ilimwambia kwamba amemfanyia au alikosa kumfanyia ndugu yake, au pengine aliona kutokana na maoni ya ndugu yake kumwelekea kwamba alikuwa ameudhika. Katika hali ya namna hiyo, sadaka ilipaswa kuachwa ingali hai “mbele ya madhabahu,” yaani, madhabahu ya sadaka za kuteketezwa katika ua wa hekalu wa makuhani.

Kwa maoni ya Mungu uhusiano wa mtu na mwenzake ni sehemu ya maana ya ibada ya kweli. Dhabihu za wanyama, hata ziwe “elfu za kondoo waume,” zilikuwa bure tu kwa Mungu ikiwa wenye kuzitoa hawakuwatendea wanadamu wenzao ifaavyo. (Mik. 6:6-8) “Kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona,” aandika mtume Yohana, “hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.”​—⁠1 Yohana 4:20.

Na zaidi Yesu aliwasihi wasikilizaji wake waepuke kukawia kurekebisha makosa, akisema: “Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani.”​—⁠Mt. 5:25a.

‘Akiwa na mshtaki njiani kuelekea mahakmani’ mkosaji alipaswa kujitahidi sana kurekebisha kosa nje ya mahakma. Ikiwa mkosaji angekubali kosa lake, aonyeshe huzuni na kuonyesha nia ya kufanya malipo, inaelekea mshitaki angemwonyesha huruma, pengine hata kufanya mapatano ambayo mkosaji angefikiliza bila shida nyingi.

Akitoa sababu inayofaa ya kurekebisha mambo upesi namna hiyo, Yesu alisema hivi: “Yule mshitaki asije akakupeleka kwa [hakimu], na [hakimu] akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.”​—⁠Mt. 5:25b.

Mara tu kesi ifikapo mahakmani, ikiwa mshtakiwa angeonekana na hatia na asiweze kulipa deni yake, huenda hakimu angempeleka kwa “askari.” Halafu, naye askari huyu, angemtupa mtu huyu mwenye hatia gerezani. Kwa muda gani?

“Amin, nakuambia,” akasema Yesu, “Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.” (Mt. 5:26) Kulingana na Kigiriki cha Mathayo, kifungo kingeendelea mpaka malipo ya kodrantes ya mwisho, au “quadrans,” sarafu (fedha) yenye thamani ya sehemu moja kwa sitini na nne ya malipo ya kawaida ya siku nzima kwa vibarua wakulima. Kama mtu asingekuja alipe deni ya mfungwa huyu, muda wake wa kukaa gerezani pengine ungeendelea kwa kipindi kirefu.

Ibada inayokubalika lazima itie ndani kutendea wanadamu wengine ifaavyo. Mtume Paulo anawashauri waamini wenzake hivi: “Toeni [uamuzi huu], mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.” (Rum. 14:13) Kitu cha kukwaza cha namna hiyo kikitokea, Mkristo apaswa kukumbuka maneno ya Yesu “patana na mshitaki wako upesi.” (Mt. 5:25) “Maana nataka fadhili,” asema Yehova, “wala si sadaka.”​—⁠Hos. 6:6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki