Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 10/15 kur. 5-8
  • ‘Amani kwa Watu Aliowakubali’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Amani kwa Watu Aliowakubali’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUFA KWAKE NI KWA MAANA ZAIDI
  • ‘WATU ALIOWAKUBALI’
  • UTOAJI WA KRISMASI WATOFAUTIANA NA UTAOJI WA KIKRISTO
  • Kwa nini watu fulani hawasherehekei Krismasi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Krismasi—Je, Kweli Ni ya Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Yesu Alizaliwa Wakati Gani?
    Amkeni!—2008
  • Je! Yesu Alizaliwa Wakati wa Theluji?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 10/15 kur. 5-8

‘Amani kwa Watu Aliowakubali’

Kuzaliwa kwa Yesu lilikuwa tukio kubwa, walakini, ulikuwa mwanzo tu!

KATIKA mwaka 2  K.W.K., kama tarehe 1 Oktoba hivi, mwanamume mmoja pamoja na mke wake walikuwa wamesafiri kwenda Bethlehemu ili kujiandikisha kwa kutii amri iliyotolewa na Kaisari Agosto. Mwanamke huyo alikuwa amekaribia kuzaa mtoto. “Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”​—⁠Luka 2:6, 7.

Mambo mengi kuhusu kuzaliwa huku yalikuwa mambo yasiyo ya kawaida, vile-vile na tangazo lililofanywa la kuzaliwa huko lilikuwa lisilo la kawaida: “Na katika nchi ile ile kulikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa [Yehova] akawatokea ghafula, utukufu wa [Yehova] ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.”​—⁠Luka 2:8-11.

Hii ilikuwa habari kuu! Wayahudi walikuwa wakitazamia kuja kwa Masihi. Je! wachungaji hao wangeamini kweli kweli kwamba kitoto hicho kilichozaliwa ndicho yeye? Malaika aliendelea kusema hivi: “Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.” Kwa ghafula, jeshi la malaika likatokea, likimsifu Mungu na kutangaza: “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu [aliowakubali].” Upesi wachungaji wakaenda Bethlehemu​—⁠walifahamu kwamba huo ndio uliokuwa mji wa Daudi, ambamo Masihi angezaliwa. Walipata kitoto hicho katika hori ya kulia ng’ombe​—⁠ishara waliyopewa na malaika. Hivyo wakawa mashahidi waliojionea kwa macho yao utimizo wa unabii uliohusu kuzaliwa kwa kibinadamu kwa Masihi. Wakiwa na furaha nyingi sana, wachungaji hao walirudi kwenye makundi yao, wakimtukuza na kumsifu Mungu.​—⁠Luka 2:12-20, maneno ya pambizoni; Mik. 5:2; Mt. 2:4-6.

Kuzaliwa huku ndiko mataifa mengi husherehekea wakati wa Desemba 25. Kwamba hii si tarehe sahihi inaonyeshwa na maneno haya kutoka katika kitabu cha kueleza Biblia Clarke’s Commentary kuhusu Luka 2:8:

“Ilikuwa desturi kati ya Wayahudi kupeleka kondoo wao nyikani, wakati wa Sikukuu ya Kupitwa, na kuwaleta nyumbani wakati wa kunya mvua ya kwanza: Wakati walipokuwa nje, waliwaangalia usiku na mchana. Kwa kuwa Sikukuu ya Kupitwa ilitukia wakati wa masika, nayo mvua ya kwanza ilianza mapema katika mwezi wa Marchesvan, ambao ni sehemu ya Oktoba na Novemba yetu, twaona kwamba kondoo waliwekwa nje wakati wote wa kiangazi.”

Hakuna makundi ambayo yangekuwa nje usiku wakati wa Desemba, kwa hiyo kitabu hicho cha Clarke’s Commentary kinamalizia hivi:

“Kwa sababu hii siku hii ya kuzaliwa katika Desemba yapasa iachwe.”

Tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu yaweza kuwekewa mipaka hata zaidi ya wakati ambao wachungaji walikuwa nje pamoja na makundi yao wakati wa usiku. Yesu alianza utumishi wake alipokuwa na umri wa miaka 30; nao uliendelea kwa miaka mitatu na nusu, alipouawa juu ya mti wa mateso akiwa na umri wa miaka 331⁄2.a Nusu hiyo ya mwaka inamaanisha kwamba kuzaliwa kwake kulipaswa kuwe miezi sita kabla ya Sikukuu ya Kupitwa fulani, au vuli, yapata Oktoba 1. Hata hivyo, uhakika wa kwamba siku yenyewe ya kuzaliwa kwa Yesu haionyeshwi unaonyesha kwamba Wakristo hawakutazamiwa waisherehekee. Kuzaliwa kwake kulikuwa mwanzo tu.

KUFA KWAKE NI KWA MAANA ZAIDI

“Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake.” (Mhu. 7:8) Bila shaka hiyo ilikuwa kweli kwa habari ya maisha ya Yesu hapa duniani. Yesu mwenyewe aliona kwamba tukio la maana zaidi lilikuwa kukumbuka kifo chake, si kuzaliwa kwake. Kifo chake kilionyesha mwisho wenye kufaulu wa kusudi la Yehova katika kumtuma Yesu duniani. Kwa kifo cha Yesu ukombozi wa wanadamu wote wanaoweza kukombolewa ulitolewa. Kwa kifo chake Yesu aliendeleza ukamilifu wake chini ya majaribu makali zaidi akamthibitisha Shetani kuwa mwongo. Kwa kifo chake alipata ufalme ambao utamaliza uovu na kuleta amani yenye kuendelea. Nia yake ya kukubali kutoka mbinguni, kuja hapa duniani kufa kama dhabihu, na kisha kutukuzwa kwake katika uweza wa Ufalme kunaonyeshwa katika Wafilipi 2:5-11:

“Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, ilipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya [mti wa mateso]. kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, kamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

Yesu Kristo anakuwa Mfalme wa Amani anayetajwa katika Isaya 9:6, na kama Mfalme wa Yehova wa haki ataleta hali zenye amani za Zaburi 72:6, 7: “Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa kama manyunyu yainyweshayo nchi. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.” Kwa kufaa, basi, malaika aliyetangaza kuzaliwa kwake kwa wachungaji alimtaja yeye kuwa ndiye atakayeleta ‘amani kwa watu aliowakubali.’ Kutokana na yote haya tunaweza kuona kwamba kifo chake ndicho kilicho cha maana zaidi. Kuzaliwa kwake kulikuwa lazima kama utangulizi wa kifo chake, walakini kifo chake ndicho kilichotimiza mambo mengi zaidi na ndicho kinachostahili kukumbukwa. Kwa hiyo, tarehe ya kuzaliwa kwake hata haikuandikwa, walakini tarehe ya kifo chake inajulikana na aliamuru ikumbukwe.​—⁠Luka 22:7, 19, 20.

‘WATU ALIOWAKUBALI’

Yehova amekataza kuchanganya ibada yake na ile ya miungu ya mashetani. “Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao. Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwazo.” (Kut. 23:32, 33; 1 Sam. 5:1-4) Katazo hili linarudiwa kwa Wakristo: “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi: Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?”​—⁠2 Kor. 6:14, 15.

Makala iliyotangulia ilionyesha vyanzo visivyo vya Kikristo vya Krismasi. Msingi wake ni kuabudiwa kwa jua na watu wengi wa kale. Hata kazi ya ukombozi na upatanisho iliyotimizwa na kifo cha Yesu inaigwa. Kristo aliyefufuliwa anapatanisha Mungu na wanadamu wenye dhambi. Kitabu cha Hislop kiitwacho The Two Babylons kinazungumza juu ya hili pamoja na busu ya kawaida chini ya kifabakazi:

“Msomaji na angalie zoea ambalo lingali likifuatwa katika sehemu ya kusini katika usiku wa Krismasi, la kupigana busu chini ya tawi la kifabakazi. Tawi hilo la kifabakazi katika ushirikina wa Kidruidi [ukuhani wa Waingereza wa kale], kama tulivyokwisha kuona, lilitolewa Babeli, lilikuwa mfano wa Masihi, ‘Mwanamume tawi.’ Kifabakazi hicho kilionwa kuwa tawi la kimungu​—⁠tawi lililotoka mbinguni, na kukua katika mti uliotoka duniani [ardhini]. Hivyo kwa kupandikiza tawi hilo la kimbinguni katika mti wa kidunia, mbingu na nchi, zilizokuwa zimetenganishwa na dhambi, ziliunganishwa pamoja, hivyo hilo [tawi] la kifabakazi lilikuja kuwa mfano wa kupatanisha kwa Kimungu kwa mwanadamu, ile busu ikiwa mfano unaojulikana sana wa kusamehe na kupatanisha.”​—⁠kur. 98, 99.

Wanaume na wanawake wanaokubaliwa na Yehova na hivyo kufurahia amani iliyoahidiwa watajiepusha kabisa na sherehe za kipagani, ijapokuwa zinaonyeshwa kuwa kuheshimu kuzaliwa kwa Yesu. Na zaidi ya hayo, ujinga mkubwa wa kuifanya Krismasi kuwa ya kibiashara unavunja kabisa roho ya Yesu.

UTOAJI WA KRISMASI WATOFAUTIANA NA UTAOJI WA KIKRISTO

Hali ya kufanya Krismasi kuwa ya kibiashara inasikitikiwa sana sana, walakini wengine wanabisha kwamba hilo linasawazishwa na uhakika wa kwamba utoaji mwingi unafanywa wakati huo. Hiyo inafanya sikukuu hiyo kuwa ya Kikristo, kwa kuwa Yesu alikazia jambo hili la kutoa. Ndivyo wanavyobisha. Hata hivyo, katika visa vingi inakuwa ni jambo la kubadilishana zawadi, kunakuwa kutazamia zawadi kutoka kwa mtu ambaye amepelekewa zawadi. Mtu aliyepewa zawadi asipompelekea zawadi yule aliyempelekea anaondolewa katika orodha ya watakaopelekewa zawadi za Krismasi katika mwaka ujao. Huu ni mwendo ulio kinyume na ule uliopendekezwa na Yesu. Alionyesha roho inayofaa katika maneno haya:

“Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”​—⁠Luka 14:12-14.

Roho iyo hiyo inaonyeshwa katika shauri la Mithali 19:17: “Amhurumiaye maskini humkopesha [Yehova]; naye atamlipa kwa tendo lake jema.” Andiko hili pamoja na lile ambalo limetangulia kutajwa yanaonyesha kwamba Yehova ndiye anayetoa malipo. Huenda yule unayempa akataka kukupa vilevile. Hakuna kosa lo lote katika jambo hilo, walakini jambo lenyewe ni hili: kusudi lako katika kutoa si kupata zawadi kama malipo. Kutoa kwako kwaweza kumsukuma anayepewa atake kukupa vilevile, kama alivyoonyesha Yesu: “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” Hata hivyo, wewe unatoa kwa sababu unapata furaha katika kutoa: “Kuna furaha nyingi zaidi katika kutoa kuliko zilivyo katika kupokea.”​—⁠Luka 6:38; Matendo 20:35, NW.

Jizoeze kutoa katika wakati wote mwakani. Kufanya hivyo kunasaidia wengine. Kunakupa furaha. Kunampendeza Yesu zaidi kuliko kutenga sikukuu ya kilimwengu katika jina lake kwa ajili ya kupelekeana zawadi. Tena kunakubaliwa na Yehova, ambaye ndiye atakayemlipa mtoaji mwenye furaha na amani chini ya ufalme wa Mungu kupitia kwa Kristo.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa ushuhuda wa Kimaandiko wa huduma ya miaka mitatu na nusu. angalia Aid to Bible Understanding, uku. 921.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki