Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 7/15 kur. 23-24
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
  • N’nini Kinachozuia Amani ya Ulimwengu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Kitabu cha Ufunuo Kinamaanisha Nini kwa Maadui wa Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Mamilioni Wanajitayarisha kwa Uzima Usiokatizwa Hapa Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 7/15 kur. 23-24

Maswali kutoka kwa Wasomaji

● Ufunuo 19:19-21 husema kwamba katika vita ya Mungu inayokuja, yule mnyama wa mfano pamoja na nabii wa uongo watatupwa kwenye ziwa la moto, lakini “wale waliosalia” watauawa kwa upanga. Ni nani “wale waliosalia,” na ni jambo gani litakalowapata?

Baada ya maelezo juu ya “Mwana-Kondoo” pamoja na malaika zake watakaopiga vita juu ya adui za Mungu, Ufunuo 19:19-21 husema hivi: “Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”

Kusoma fungu hili la maneno haraka-haraka kwaweza kudokeza kwamba kuna tofauti ya msingi kati ya matokeo juu ya yule mnyama na nabii wa uongo na yale ya “wale waliosalia.” Walakini, maneno yanayozunguka fungu hili la maneno pamoja na sehemu nyingine za Ufunuo huonyesha kwamba “wale waliosalia” ni adui za Mungu za kibinadamu wanaokatiliwa mbali katika vita ya Mungu inayokuja.

Ufunuo 19:11-21, unaoitwa na The New Bible Commentary “Hukumu ya kimasihi ya Armagedoni,” huanza kwa kumwonyesha Mwana-Kondoo, Yesu Kristo, akimpanda farasi mweupe. Akiwa pamoja na majeshi yake ya kimbinguni yeye anapanda kwenda kufikiliza hasira kuu ya Mungu juu ya mataifa. (Mist. 11-16) Akitazamia mauaji yanayokuja, malaika mmoja anawaita ndege wala-nyama waje wale nyama ya wale watakaouawa.​—Mist. 17, 18.

Kisha, katika fungu hilo la maneno tunalolisoma hapo juu, Yohana aliiona vita yenyewe. Kwanza hatua inachukuliwa juu ya yule mnyama wa mfano (anayefahamika kuwa anafananisha taratibu ya kisiasa ya duniani pote ya Shetani) na nabii wa uongo (anayewakilisha Mamlaka ya Saba ya Ulimwengu).a (Ufu. 13:1, 2) Njozi hiyo inaonyesha waziwazi kwamba mpaka kufikia wakati wa kuharibiwa kwao vyombo hivi vitakuwa bado vinatenda, vikipigana na Mungu. Je! vitatokea tena, kama vile ilivyofanya hapo mapema ile sanamu ya mfano ya yule mnyama? (Ufu. 17:8-11) Hakuna nafasi ya hilo. “Wakatupwa . . . katika lile ziwa la moto na kiberiti.” Humo ndimo Shetani atakamoharibiwa pia. Hilo “ziwa la moto” hufananisha kuangamizwa kabisa kabisa.​—Ufu. 19:19, 20; 20:10, 14; 21:8.

Kisha Ufunuo 19:21 wasema kwamba “wale waliosalia waliuawa” kwa upanga mrefu na kuachwa waliwe na ndege. Je! “wale waliosalia” ni watu wasiohusika, wasiounga mkono upande wo wote katika vita hii?

Ufunuo unajibu kwa wazi, Hapana. Angalia kwamba hapo nyuma katika Ufunuo 19:18 wakati Malaika anapowaalika ndege karamuni, alitaja waziwazi ni nyama ya watu wa namna gani itakayoliwa: wafalme, majemadari, watu hodari, wawapandao farasi, “watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.” Vilevile katika mstari wa 19 wafalme na majeshi yao wanashirikishwa na mnyama katika kupigana na Mwana-Kondoo. Kwa hiyo, “wale wanaosalia” ni wapinzani wa Mwana wa Yehova. Ni wale waliojitoa kumwunga mkono yule mnyama, waheshimiwa na akina yahe.

Ufunuo 14:9-11 huwataja waungaji mkono hao wa huyo mnyama, wale wanaokubali kwa akili zao jitihada zake au wanaomwunga mkono: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.”​—Ufu. 14:9-11.

Kuhubiri kunakofanywa duniani pote na Mashahidi wa Yehova husaidia kuwatenganisha wale wanaochagua kumwunga Mungu mkono na wale wanaomwabudu huyo mnyama. Kupita kwa wakati tu ndiko kutakakoonyesha ni jambo gani zaidi litakaloweza kutokea kabla ya mwisho kuwafanya watu wachukue msimamo wa waziwazi katika upande mmoja au mwingine. Kwa vyo vyote, ukisema juu ya kuharibiwa kunakokaribia kwa yule mnyama na yule nabii wa uongo, Ufunuo 19 huwataja waziwazi wale ‘wanaopokea ile chapa ya yule mnyama.’

Lakini namna gani juu ya uhakika wa kwamba Ufunuo 19:20, 21 husema kwamba yule mnyama na yule nabii wa uongo wanatupwa katika lile ziwa la moto na kiberiti hali “wale waliosalia” wanauawa kwa upanga na kuachiwa ndege?

Inastahili kuangaliwa kwamba kuuawa kwa “wale waliosalia” (wale waliojitoa kumwunga mkono huyo mnyama) ni wonyesho wa “ghadhabu ya hasira ya Mungu.” (Ufu. 19:15) Ufunuo 13:8 husema hivi juu ya wale wanaomwabudu huyo mnyama: “Kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Na kwa msingi Ufunuo hutumia usemi uo huo juu ya wale wanaomwabudu huyo mnyama kama vile Ufunuo 20:10 hufanya kuhusu Shetani, yule mnyama na nabii wa uongo, yaani: “Watateswa mchana na usiku hata milele na milele.” Hivyo, inaonyesha kwamba kuuawa, kuachwa pasipo kuzikwa na kuliwa na ndege kunaonyesha kukataliwa kabisa na Mungu kwa “wale waliosalia.” Badala ya kuzikwa kana kwamba walistahili kufufuliwa, maiti zao zinaachwa juu ya nchi. Ndege wala-nyama watazila. Hivyo, Ufunuo 19:21 haufananishi zikiteketezwa. (Linganisha Ezekieli 39:17-19.) Juu ya hili kitabu The Tyndale New Testament Commentary kinasema hivi: “Mfano wa uharibifu unamaliziwa kwa usemi wa kwamba ndege walishiba kwa nyama za waliouawa, wazo la kawaida la msiba wa mwisho.”

Kwa hiyo, Ufunuo 19:21 unaonyesha hukumu ya Mungu juu ya adui zake wa kibinadamu waungaji mkono waliojitoa wa yule mnyama watakaoangamizwa katika “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” inayokuja,—Ufu. 16:14.

[Maelezo ya Chini]

a Kitabu “Babylon the Great Has Fallen!”​—God’s Kingdom Rules! kur. 506, 511, 561, 562, 628.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki