Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 3/1 kur. 3-7
  • “Tini” Zinazofurahisha Hata Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Tini” Zinazofurahisha Hata Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • VIKAPU VIWILI VYA TINI
  • “TINI MBOVU”
  • Kila Mtu Ataketi Chini ya Mtini Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Matunda—Mazuri na Mabaya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Atumia Mtini Kufundisha Kuhusu Imani
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Una “Moyo wa Kumjua” Yehova?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 3/1 kur. 3-7

“Tini” Zinazofurahisha Hata Mungu

“[Yehova], Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema.”​—Yer. 24:5.

1. Mtini ulikujaje kwenye mambo ambayo tumeona maishani mwetu?

MTINI ulikuwako katika bustani ya kwanza iliyopata kupandwa katika dunia yetu. Wazazi wetu wa kwanza wa kibinadamu ndio waliokuwa wa kwanza kula tunda hili tamu, tini. Je! mtini uliruhusiwa ukue nje ya bustani hiyo ya kwanza? Ndiyo, na kwa sababu hiyo twaweza kufurahi. Hivyo sisi leo vilevile twaweza kuwa na furaha ya kula kichala hiki chenye utamu. Likiwa jambo lisilo la kawaida kabisa, mavazi ya kwanza ambayo wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Hawa, walivaa kwa muda mfupi ili kufunika viuno vyao yalikuwa yametengezwa kutokana na majani ya tini, yaliyoshonwa pamoja. Hii ilikuwa kabla tu ya kufukuzwa ndani ya Paradiso yao ya Furaha kwa ajili ya kumwasi Mpanzi na wenyeji wa bustani hiyo ya Edeni.​—Mwa. 2:8; 3:1-7.

2. Katika mfano wake, Yothamu aliutumiaje mtini ukiwa na maana yenye furaha kwetu?

2 Katika mfano uliosemwa muda mrefu baadaye na Yothamu mwana wa Mwamuzi Gideoni aliufanya mtini uzungumze. Uliuliza hivi: “Je! niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti?” (Amu. 9:11) Katika mfano wa Yothamu mtini ulikataa kuacha sifa zake nzuri. Kwa kweli leo, mtini ungali una uzuri na utamu wake uliorithiwa. Katika hili ungali unatimiza kusudi la Mungu lenye fadhili.

3. Yothamu alitumia mtini kufanaisha nini, walakini Yesu Kristo aliutumia kufananisha nini, na katika mfano gani?

3 Yothamu alitumia mtini kumfananisha mtu mmoja, Mwisraeli mwaminifu ambaye angekataa kuwekwa kuwa kiongozi wa serikali iliyowekwa kwa kura ya kidemokrasi ya uchaguzi wa taifa zima. Muda mrefu sana baadaye, Yesu Kristo alitumia mtini kufananisha taifa la Israeli. Katika mfano mmoja, yeye alisema hivi:

“Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! la, usipozaa, ndipo uukate.”​—Luka 13:6-9.

4. Baada ya miaka mitatu na nusu ya utumishi wa wakili wake duniani, ni katika njia gani Mpanzi hakupata matunda yo yote Juu ya mtini wa mfano?

4 Yesu alitoa mfano huo muda fulani baada ya Wayahudi kusherehekea siku-kuu ya vibanda (Sukothi) ya wakati wa vuli katika mwaka 32 W.K., hivyo, miaka mitatu baada ya kuanza kwake utumishi wa waziwazi katika nchi ya Israeli. Sasa alikuwa katika mwaka wa nne wa kazi yake ya kiinjilisti. Kwa hiyo kwa muda unaopungua miezi sita taifa la Israeli lingemkataa na kufanya auwawe juu ya mti nje ya kuta za Yerusalemu. Kama matokeo ya kazi ya miaka mitatu u nusu kati ya Waisraeli, alikuwa na wanafunzi mia chache tu wakiwa mazao ya kazi yake ngumu. Baba yake wa kimbinguni, Yehova Mungu, alikuwa amepanda mti huo wa mfano wa Israeli. Kwa haki, baada ya miaka mitatu u nusu ya kutunzwa na kuangaliwa kipekee na Mwanawe aliyekuwa wakili wake duniani, alitazamia matunda. Walakini, kwa njia ya kufananisha, hakupata yo yote kwa namna ya wafuasi wa Mwanawe, aliye Masihi. Kama vile yule “mtunzaji wa shamba la mizabibu” wa ule mfano, Mwana wake aliendelea ‘kupalilia’ kuzunguka mtini wa mfano mpaka katikati ya mwaka nne wa utumishi wake. Walakini ilikuwa bure tu.

5, 6. (a) Kwa kutumia mtini wa halisi, Yesu alionyeshaje kwamba mtini wa mfano ungekatwa? (b) Mtini huo wa mfano ulikatwa wakati gani, kama inavyoonyeshwa na mambo gani yaliyotukia?

5 Karibu sana na katikati ya mwaka huu wa nne Yesu alionyesha kwamba “mtini” wa taifa zima usiozaa matunda ungekatwa. Siku ya Jumatatu, Nisani 10, mwaka 33 W.K., alipokuwa akielekea Yerusalemu Yesu alifika kwenye mtini. Ujapokuwa ulikuwa na majani, haukuzaa matunda yo yote. Kwa sababu hiyo Yesu “Na asubuhi walipokuwa wakipita, wali Ni jambo gani lililotukia? Twasoma hivi: leo hata milele mtu asile matunda kwako, aliulaani mtini huo, akisema hivi: “Tangu uona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.”​—Marko 11:12-21.

6 Basi, sasa, je! Yesu alikuwa akionyesha chuki juu ya mti usio na akili? Sivyo, walakini alikuwa akitumia mtini huo usiozaa kama mfano. Mtini huo ulifananisha taifa la Israeli ambalo kwalo Yehova alikuwa amemtuma Mwana wake akusanye matunda kwa namna ya watu wenye kumwunga mkono Masihi au Kristo wa kweli. Wakati, chini ya uongozi wa kuhani mkuu walo na viongozi wengine wa kidini walipomkataa Yesu kuwa wakili wa ufalme wa Mungu, mia chache za watu mmoja mmoja waliomkubali zilikuwa kama kwamba si kitu. Kama vile mti unaopasishwa ushuru unaoharibu mchanga, mtini huo wa mfano ulistahili kukatwa, kwa kuwa ulilaaniwa na Mungu. (Linganisha Kumbukumbu la Torati 28:15-68.) Siku 51 baada ya Yesu kuuawa kama kwamba alikuwa Masihi wa uongo, “mtini” wa Kiisraeli ulikatwa, kwa kuwa wakati huo Mungu alitokeza taifa jipya, Israeli wa Kikristo, Israeli wa kiroho, ili lizae matunda. (Mt. 21:43; 1 Pet. 2:9; Gal. 6:16; Yak. 1:1) “Mtini” uliokatwa uliwekwa kwa ajili ya moto kwenye uharibifu wa Yerusalemu katika mwaka 70 W.K.

VIKAPU VIWILI VYA TINI

7. Katika mwaka 617 K.W.K., Yehova aliutajaje mtini wa mfano katika njozi aliyompa Yeremia?

7 Yerusalemu ulipata kuharibiwa mara nyingine, na Wababeli chini ya Nebukadreza huko nyuma katika mwaka 607 K.W.K. Hata hivyo, miaka 10 kabla ya msiba huo wa taifa zima, au katika mwaka 617 K.W.K., Mungu alitumia mtini kufananisha taifa la Kiyahudi. Huu ulikuwa wakati alipompa nabii wake Yeremia njozi ya kuogopesha sana, ambayo juu yake Yeremia atuambia yanayofuata:

“[Yehova] akanionyesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la [Yehova]; baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia [au, Yehoyakini], mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi wa wafua chuma, kutoka Yerusalemu, na kuwaleta Babeli. Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama tini zilizotangulia kuiva; na kikapu cha pili kilikuwa na tini mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa zilikuwa mbovu sana.”​—Yer. 24:1, 2.

8. Yehova alielezaje yaliyomaanishwa na kikapu cha tini nzuri?

8 Alipoulizwa aliyoona katika njozi, Yeremia alisimulia kwa usahihi aliyoona. (Yer. 24:3) Walakini tini hizo zilifananisha nini? Kwani, si Waisraeli ambao walikusudiwa kuhamishwa mpaka Babeli? Kwa habari ya hili, twasoma hivi:

“[Yehova], Mungu wa Israeli, asema hivi, kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda, wala sitawang’oa. Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni [Yehova]; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.”​—Yer. 24:5-7.

9. “Tini” hizo zilitokana na mti gani wa mfano, nazo zilitia nani ndani yake?

9 “Tini” hizo za mfano zilitokana na mti wa mfano. Kutokana na “mti” gani? Kutokana na taifa la Israeli, ambalo Yehoyakini mwana wa Yehoyakimu alikuwa mfalme wake kwa miezi mitatu na siku 10 tu. (2 Nya. 36:9, 10; Mt. 1:11, 12) Kati ya wale ambao mfalme wa Babeli alipeleka uhamishoni wakati huo alikuwa Danieli, wenzi wake watatu Waebrania Hanania, Mishaeli na Azaria, na Ezekieli. (Dan. 1:11-17; Eze. 1:1-3) Hivyo, huko nyuma katika wakati wa Yeremia, Yehova alitumia mtini kufananisha taifa la watu wake wateule. Kufikia wakati huo wa kuhamishwa, Yeremia alikuwa ametabiri kwa miaka 30.

10. Yehova alitimizaje kusudi lake lililotangazwa kwa habari ya zile “tini nzuri,” na zilimwonyeshaje “utamu”?

10 Kwa aliyosema Yehova kuhusiana na njozi ya tini zile nzuri alionyesha nyakati zenye nafuu. Alisema juu ya mambo mazuri ambayo angefanyia mabaki waaminifu wa watu wake wa agano, Hii ingekuwa wakati wa mwisho wa “miaka sabini” aliyotabiri miaka minane tu iliyotangulia (Yer. 25:11, 12) Yehova ndiye Mungu wa kweli, na maandishi ya historia yanaonyesha jambo hilo, katika mwaka 537 K.W.K., alitimiza kusudi lake lililotangazwa. Alimtumia Mwajemi Koreshi Mkuu kuipindua Babeli katika mwaka 539 K.W.K., kisha akamchochea arudishe “tini nzuri” za mfano kwenye nchi ambamo mtini wa mfano ambao kutoka kwao zilitoka ulikuwa umepandwa kwa mara ya kwanza. Huko walijenga upya Yerusalemu na kujenga hekalu jipya kwa ajili ya ibada ya Yehova. Kwa kufanya yote haya, walionyesha “utamu” kama ule wa tini nzuri sana kwa Mungu wao, Mpanzi wa taifa lao lililo kama mti.

11, 12. (a) “Tini nzuri” za leo zinaitwa kwa jina la nani’ (b) Babeli ya kisiasa ya nyakati za kale ilikuwa nini, na Babeli Mkuu ni nani?

11 Je! jambo hili lina maana yo yote kwa siku zetu? Ndiyo, katika karne yetu wenyewe ya 20 utimizo wa mwisho wa unabii wa Yehova kupitia kwa Yeremia umetimia tena kwa kadiri kubwa zaidi. Hii maana yake ni kwamba kungali pamoja nasi Wakristo ambao wanafanana na zile “tini nzuri.” Mungu wa Yeremia amewaangalia hawa vilevile ‘kwa njia nzuri.’ Yeye amewakomboa kutoka kwa Babeli Mkuu. Si ndio wa kwanza kuitwa kwa jina la Mungu mwenyewe. Huko nyuma katika wakati wa Yeremia “tini nzuri” za mfano zilikuwa Waisraeli walioitwa kwa jina la Mungu wake. Hata jina la nabii huyu, Yeremia, lilitia ndani jina hilo la kimungu, kwa kuwa linamaanisha “Yehova Hufungua (tumbo la uzazi).” Katika siku za Yeremia, Babeli ilipata kuwa mamlaka ya ulimwengu yenye kutawala kama tengenezo la kisiasa. Ilikuwa yenye nguvu kwa muda unaozidi miaka 90 na kwa hiyo ikaendeleza dini ya uongo ambayo chanzo chake ni Babeli ya siku za Nimrodi. Sehemu hii ya kidini inawekwa wazi katika kitabu cha mwisho cha Biblia kinachozungumza juu ya Babeli Mkuu na inaifanya kuwa mtumishi wa kike wa kufanya ngono na mamlaka za kisiasa. Kama vile Babeli ya kale ilivyofananisha milki, ndivyo Babeli Mkuu anavyofananisha milki, milki ya ulimwengu ya dini ya uongo.

12 Babeli ya kale ya kisiasa ilianguka na mwishowe ikatoweka isiwepo tena, walakini Babeli Mkuu wa kidini aliendelea kuwapo. Kwa hiyo angali ndiye milki ya ulimwengu ya dini ya uongo.​—Ufu. 14:8; 17:1-8.

13. Ni amri gani inayopewa watu wa Mungu kwa habari ya Babeli Mkuu, naye alipata ‘kulewa’ namna gani kwa damu ya mashahidi?

13 Hata hivyo, je! Babeli Mkuu ataanguka vilevile katika uharibifu? Ndiyo, kitabu cha mwisho cha Biblia kimetabiri hivyo. Hivyo, katika Ufunuo 18:4, 5, amri ifuatayo inatolewa kwa watu wa Mungu waliopelekwa uhamishoni, kundi la Kikristo: “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Katika kutaja sehemu ya dhambi zake, Ufunuo 17:6 unafananisha milki hii ya kidini iliyo ya kikahaba kuwa ‘imelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.’ Alipata kuwa na hatia ya kumwaga damu ya watu wa Yehova waliojiweka wakf wakati wa Vita ya Kwanza ya Ulimwengu (ya mwaka 1914-1918) na kwa kuchukua wengi utumwani kwa kusudi la kusimamisha kuhubiri kwao ufalme wa Mungu.

14. Kwa kutii amri ya Mungu, “tini nzuri” za mfano zimepata matokeo gani, nao ni nani waliojiunga katika shamba lao la kiroho?

14 Watumwa hao wenye kuonewa wa Babeli Mkuu walikuwa kama “tini nzuri” za ile njozi ya Yeremia. Baada ya kumalizika kwa Vita ya Kwanza ya Ulimwengu, Yehova alivunja uwezo wa Babeli Mkuu na, katika mwaka 1919, aliwafungulia njia watende kwa kutii amri yake: “Tokeni kwake, enyi watu wangu.” Waisraeli wa kiroho ambao walitii kwa kuacha kuwa wenzi kwa njia yo yote na Babeli Mkuu (kutia ndani Jumuiya ya Wakristo) walirudishwa kwenye kibali ya Yehova wakapewa kazi katika utumishi wake wa Ufalme. Mara moja waliongoza kuhubiriwa kwa ulimwenguni pote kwa ‘habari njema hizi za ufalme,’ kama ambavyo Yesu alitabiri katika Mathayo 24:14 na Marko 13:10. Mpaka siku hii Yehova hajaliona kuwa jambo zuri kuwaacha wang’olewe kutoka katika shamba lao la paradiso ya kiroho ambalo katika hilo amewaleta. Tofauti yake, zaidi ya watu 2,000,000 ambao si Waisraeli wa kiroho wamekuitikia kuhubiriwa kwa Ufalme wakachagua kushirikiana na watu wa Yehova waliorudishwa katika shamba lao la kiroho. Hivyo wamechukua makao ya kuishi chini ya mtini wa mfano wenye uzuri na utamu wake katika zaidi ya nchi 200.

“TINI MBOVU”

15, 16. (a) Ni nani waliohesabiwa kati ya “tini nzuri” za mfano katika wakati wa Yeremia? (b) Mfalme Sedekia alijionyesha kuwa “tini” ya namna gani, naye Yehova alitabiri nini juu ya zile “tini mbovu”?

15 Kati ya wale ambao walihesabiwa kuwa jamii ya “tini nzuri” za siku za Yeremia alikuwa Mfalme Yehoyakini (au, Yekonia) wa Yuda. Yesu Kristo alikuwa mzao mlelewa wa Mfalme Yehoyakini kupitia kwa mzao wake mwenye kujulikana Zerubabeli, ambaye alikuwa kama “tini nzuri.” (1 Nya. 3:17-19; Mt. 1:12; Luka 3:23-27) Katika mwaka 617 K.W.K., Baada ya Mfalme Yehoyakini kukubali kushindwa kwa Yerusalemu na mfalme wa Babeli, Nebukadreza alimfanya Sedekia, amu (ndugu ya baba) wa Yehoyakini, mfalme mpya wa Yuda, chini ya kiapo mbele za Yehova kuwa kibaraka mshikamanifu wa Babeli. Walakini Mfalme Sedekia aligeuka kuwa “tini mbovu,” kama ilivyokuwa. Kwa hiyo yule Mungu ambaye kwa yeye alikuwa ameapa, Yehova, alimfananisha na tini isiyolika, akisema hivi:

16 “Na habari za tini zile mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana; hakika, asema [Yehova], ndivyo nitakavyomtoa Sedekia, mfalme wa Yuda, na wakuu wake, na mabaki ya Yerusalemu, waliosalia katika nchi hii [baada ya kupelekwa uhamishoni kwa Yehoyakini], na hao wanaokaa katika nchi ya Misri [ambako Wayahudi walikimbilia katika kuwaogopa Wababeli]. Naam, nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote & dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana, katika mahali pote nitakapowafukuza. Nami nitatuma upanga, na njaa, na tauni, kati yao, hata watakapopotelea mbali katika nchi niliyowapa, wao na baba zao.”​—Yer. 24:8-10.

17. Sedekia alijionyesha kuwa “tini mbovu” namna gani, nayo matokeo yakawa nini?

17 Bila shaka Yehova hakupata furaha yo yote katika zile “tini mbovu” za mfano, ambazo aliazimia kuzileta kwenye mwisho wenye msiba, chini ya suto na chuki ya mataifa yote. Lo! namna Mfalme Sedekia alivyojionyesha kuwa mbaya! Alivunja kiapo chake akaiasi Babeli na, chini ya mkazo kutoka kwa wakuu wake, alimweka Yeremia kizuizini kana kwamba alikuwa hatari kwa taifa zima. Licha ya “upanga” wa watekaji nyara wa Babeli na tauni kati ya Wayahudi waliozingirwa, njaa yenye kuumiza sana ndiyo iliyovunja upinzani wa walinzi wa Yerusalemu baada ya mazingawa ya muda wa miezi 18. Mfalme mwenye kushinda aliamuru kuuawa kwa wakuu wa serikali wenye kujulikana, wa kisiasa na wa kikuhani. Mtekwa Sedekia aliona wana wake mwenyewe wakiuawa, kisha akapofushwa na kuburutwa kifungoni Babeli, ambako alifia katika aibu.

18. Kwa sababu ya mfano huo wenye kuonya, sasa inatupasa tufanye nini kusudi tuokoke “dhiki kubwa” inayokuja?

18 Je! sisi leo tunatetemeshwa na yaliyopata hizo “tini mbovu” za mfano? Ebu na ziwe mifano ya kutuonya sisi ili tusiige mwendo wao wa kutenda. Iwapo Waisraeli wa kiroho wa leo hawataishi kulingana na agano jipya, iwapo hawatategemeza enzi kuu ya Yehova ya ulimwenguni pote, iwapo hawataunga mkono ufalme wa Kimasihi wa Mwanawe Yesu Kristo, watapatwa na mambo kama yale yaliyopata zile “tini mbovu” za kale, katika “dhiki kubwa” inayokuja. (Mt. 24:21, 22) Kisha, vilevile, idadi ya watu wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo, wanaojifanya kuwa Waisraeli wa kiroho, watafikia mwisho wao wenye msiba kama vile “tini mbovu.” Kweli kweli, sasa inatupasa tuwe kama Yeremia na mwandishi wake Baruki na rafiki zake wachache wenye kujitoa, watu walio waaminifu kwa Yehova ambao waliokoka uharibifu wa Yerusalemu.​—1 Kor. 10:11.

[Picha katika ukurasa wa 6]

Jumuiya wa Wakristo, kama vile “tini mbovu,” inaelekeana na mwisho ule ule wenye msiba kama vile Yerusalemu wa kale

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki