Taabu ya Yakobo na Agano Jipya la Mungu
“Nami nitafanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.”—Yer. 31:31, NW.
1, 2. (a) Yakobo na Raheli walikuwa na sehemu gani kwa habari ya taifa la Israeli? (b) Taabu isiyolinganika ilitabiriwa kumpataje Yakobo?
YAKOBO na Raheli walikuwa wapenzi. Yakobo aliyekuja kujulikana kama Israeli, alikuwa baba wa taifa la Israeli lenye makabila 12. Raheli, akiwa mke wake aliyependelewa, akaja kuwa mama wa kabila la Benyamini. Kabila la Yuda lilitokana na Lea mke wa Yakobo aliyependwa kidogo. Kwa hiyo jina Yakobo likaja kuwa mfano wa taifa lote, na Raheli akafananisha wakili mama mwenye kuheshimiwa wa taifa hilo. Taabu isiyo na kifani kufikia wakati huo ilitabiriwa kumpata Yakobo, naye Raheli angepatwa na matokeo yake yenye kuhuzunisha. Kwa kutarajia taabu hiyo itokee katika siku zake, nabii Yeremia, aliyeishi katika Anathothi katika eneo la Benyamini, aliongozwa na Mungu kusema hivi:
2 “Ole! maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo [katika wakati uliotangulia]; maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”—Yer. 30:7.
3. (a) Raheli alitabiriwa akilia pasipo kufarijiwa kwa ajili ya hali gani? (b) “Wakati wa taabu” ulimpata Yakobo wakati gani?
3 Ambayo huu “wakati wa taabu yake Yakobo” usiolingana na wakati wo wote uliopita ungemaanisha kwa Raheli wa mfano yalitabiriwa katika Yeremia 31:15 katika maneno haya: “Sauti imesikiwa Rama [mji mmoja katika eneo la Benyamini], kilio na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako.” Hii ilimaanisha, si kwamba walikuwa wameuawa, bali kwamba walikuwa wametekwa na kuchukuliwa kutoka kwa nchi yao mpaka kwenye nchi ya adui kama wahamishwa. Aha, ndiyo! Baada ya miezi 18 ya mazingiwa yenye kutaabisha na watekaji wa Babeli, Yerusalemu, ambao ulikuwa katika mpaka wa kaskazini kati ya maeneo ya Yuda na Benyamini, ulikuwa umeharibiwa, hekalu lake limeharibiwa, mfalme, wakuu na makuhani wametekwa, na hesabu kubwa ya waokokaji kuhamishwa katika Babeli. Kufikia katikati ya mwezi wa saba (Tishri) wa mwaka 607 K.W.K., nchi yote ya Ufalme wa Yuda ilikuwa imeachwa na Wayahudi wachache waliobaki na iliachwa ukiwa pasipo mtu na mnyama wa kufuga. Hali hii ya mahame, ya ukiwa wa nchi iliamriwa na Mungu iendelee kwa miaka 70.
4. Yakobo ‘angeokolewa’ wakati gani kutokana na taabu iliyotabiriwa?
4 Huo ulikuwa “wakati wa taabu” kama nini kwa Yakobo! Yeye hakuokolewa kutokana nayo, hakuiepuka, na isingekuwa mpaka baada ya hiyo miaka 70 ya kufanywa ukiwa kabisa kwa nchi hiyo kwamba Mungu angetimiza maneno yenye kufariji aliyoongeza: “Lakini ataokolewa nayo.” (Yer. 30:7) Wokovu huu ungekujaje?
5. Yehova alisema nini kwa kumfariji Raheli, naye alitimizaje ahadi yake?
5 Yehova alizungumza juu ya jambo hilo kwa urefu wakati, baada ya kutabiri kufiwa kwa Raheli na wana wake, alipoongeza maneno haya: “[Yehova] asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; maana kazi yako itapata thawabu, nao [wana wako] watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo [Yehova].” (Yer. 31:16) “Nchi ya adui” ilikuwa Babeli. (Mik. 7:8-10) Kwa hiyo mamlaka ya Babeli juu ya “watoto” wa Raheli ingeondolewa. Kama uhakikisho wa jambo hilo kwa Raheli aliyefiwa, Mungu aliendelea kusema hivi: “Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho [wakati wako ujao, NW]— asema [Yehova]; na watoto wako watarejea hata mpaka kwao wenyewe.” (Yer. 31:17) Kwa mshangao wa mataifa yenye uadui yasiyoamini, kurejea huku kwenye eneo lao wenyewe, kutia na Rama, kulitokea kuanzia mwaka 537 K.W.K. na kuendelea. (Neh. 7:30; 11:31-33) Baada ya “jeraha” hilo la taifa zima lenye kutaabisha katika mwaka 607 K.W.K., lo! Yehova alitokeza ‘kurudishiwa afya’ kimwujiza kama nini!
6. Kwa habari ya kuponya “jeraha” zake, Yehova angegeuzaje Sayuni, au Yerusalemu, usiwe kama mwanamke aliyefukuzwa ambaye hakuna mwanamume amtakaye?
6 Kwa habari ya jambo hilo yeye alisema hivi: “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema [Yehova]; kwa sababu wamekuita, [mwanamke] mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. [Yehova] asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji [Sayuni, au, Yerusalemu] utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao.”—Yer. 30:17-19.
7. Ni jambo gani juu ya ule usemi wa Yehova linaloonyesha kama wakati wa “jeraha” Yehova angelivunja agano la Torati, lakini Wayahudi walikuwa wamelitendaje agano hilo?
7 Yehova ni “Mungu wa furaha,” naye anataka wale walio na uhusiano naye kwa njia ya agano wawe wenye furaha pia. Yeye mwenyewe hucheka! Ahadi yake ya kuchangamka kwa wakati ujao kwa watu wa Kiyahudi waliohamishwa ilithibithisha kwamba yeye hakuwa amevunja agano la Torati ambalo lilipatanishwa na Musa kati Yake na taifa la Israeli. Lakini loo! jinsi Waisraeli walivyokuwa wamevunja mapatano ya agano hilo! “Tena,” Yehova akawaambia, “walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu [kusini mwa hekalu la Yerusalemu], ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto [kama dhabihu za kibinadamu] kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda [Ufalme wa Yuda].”—Yer. 32:35.
8. Kwa hiyo ni baada ya kupatwa na jambo gani lenye kuwastahili Waisraeli wangekuwa watu wa Yehova?
8 Kwa sababu hizo Waisraeli walistahili kupata taabu kama tufani yenye kusonga mbele kuja juu ya Ufalme wa Yuda na mji wake mkuu, Yerusalemu. Walakini, baada ya kutabiri hayo, Yehova mwenye huruma aliendelea kusema hivi: “Wakati huo [wa kurudishwa kwa Israeli], asema [Yehova], nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu.”—Yer. 30:23 hadi 31:1.
9, 10. Ili Waisraeli waliokusanywa tena waendelee milele katika uhusiano wenye furaha pamoja naye, Yehova angeweka nini ndani ya mioyo yao, na kwa matokeo gani?
9 Ijapokuwa historia yao ya wakati uliopita isiyopendeza, Mungu angewashughulikia kwa kulingana na ambavyo wangejionyesha kuwa sasa. Angewatakia hali njema na kuweka mbele yao nafasi ya kuendelea kuwa katika uhusiano wenye furaha pamoja naye kwa wakati usiojulikana. Kwa habari ya jambo hilo, yeye alisema hivi:
10 “Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu, na uchungu wangu, na ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; nami nitawapa moyo mmoja, na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao; nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu moyoni mwao, ili wasiniache. Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa [nafsi] yangu yote.”—Yer. 32:37-43; pia 31:27-30.
AGANO BORA ZAIDI
11, 12. (a) Baada ya mwanzo huo mpya unaofaa Yerusalemu ulidumu kwa muda gani, na sababu gani Yehova asingelaumiwa? (b) Je! kuharibiwa kwa Yerusalemu kufutilia mbali agano la Torati, naye Yehova alionyesha nini kwa kuwarudisha watu wake kwenye nchi yao?
11 Kukiwa na mwanzo mpya mzuri sana kama huo, inakuwaje kwamba Yerusalemu uliojengwa upya ulidumu miaka 606 zaidi tu, au kufikia kiangazi cha mwaka 70 W.K.? Hakika, kwa sababu ya namna Yehova katika maneno yaliyotangulia alivyokuwa amefanya agano kutegemeza watu wake, lawama isingeweza kuwekwa upande wake. Agano jipya lisingehitaji kufanywa kwa ajili ya makosa yo yote upande wake. Hata hivyo kupitia kwa Yeremia yeye alitangaza kwamba angefanya agano jipya lililo bora zaidi. Pamoja na hayo, Israeli wa mwili angekuwa wa kwanza kufaidika kutokana nalo.
12 Katika mwaka 1513 K.W.K. Yehova alikuwa amefanya agano la Torati pamoja na Israeli kupitia kwa Musa kama mpatanishi. Hiyo ilikuwa miaka 906 kabla ya Yehova kutumia Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kuharibu Yerusalemu na hekalu lake. Walakini jambo hilo halikutangua au kufuta agano lake la Torati na Israeli. Kwa hiyo Yehova hakuhitaji agano jingine la namna nyingine kusudi aponye hali yenye jeraha ya Wayahudi kwa kuwaokoa kutoka nchi ya adui ya Babeli na kuwarudisha kwenye nchi yao waliyopewa na Mungu. Hata hivyo, kwa kufanya jambo hilo yeye alijionyesha kwa mara nyingine kuwa Mungu wao naye aliwahakikishia kwamba walikuwa watu wake bado na kwamba Sayuni, au Yerusalemu, haukuwa tena kama ‘mwanamke aliyetupwa’ ambaye hakuna mtu aliyekuwa akimtaka.
13, 14. (a) Wale Waisraeli waliookoka upanga wa wawatekaji walikujaje kuwa katika hali ya “jangwa,” nao walikuwa wakitafuta pumziko wapi? (b) Kwa upendo Yehova alipenda Israeli kwa kadiri gani, na kwa hiyo ni kwa sifa gani ya kibinafsi angewavuta kwake mwenyewe?
13 Yehova alikusudia kuonyesha watu wake wa agano wonyesho mkubwa sana wa fadhili zake zisizostahilika. Hiyo ndiyo sababu hakuuacha upanga wa watekaji wao uwaue kabisa. Kungekuwako waokokaji. Hawa wangekuona kuishi katika uhamisho katika nchi ya adui kuwa kama kutandaza hema katika jangwa ambalo katika hilo hawakupata pumziko la kweli, kwa kuwa halikuwa nchi ya kwao, siyo nchi yao waliyopewa na Mungu. Kwa kumgeukia kwa kutubu katika hali hii ya “jangwa,” wangepata kibali machoni pake, kwa sababu yeye hakuwa amevunja agano lake nao. Matokeo hayo ya furaha aliyatabiri hivi:
14 “Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha [katika nchi yake ya Palestina]. [Yehova] alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli, mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria [hapo mbeleni ulikaliwa na Ufalme wa Kaskazini wa Israeli]; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake. Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu [kabila lenye kuongoza la Ufalme wa Kaskazini wa Israeli], Inukeni, tukaende Sayuni [Yerusalemu], kwa [Yehova], Mungu wetu.”—Yer. 31:2-9.
15, 16. (a) Kulingana na unabii huo ambao umetajwa sasa hivi, makabila yote 12 yangerudisha upya ibada ya Yehova wapi? (b) Baadaye angefanya nini pamoja na nyumba ya Israeli, na kukiwa na matokeo gani kwa watu wake?
15 Aha, ndiyo, makabila yote ya kusini na ya kaskazini ya Israeli yangekusanywa tena na kuungana katika kumwabudu Yehova katika Sayuni! Hilo lilimaanisha kwamba, kwa sababu ya upendo wa Mungu wa kudumu milele, Yakobo (makabila yote 12 ya Israeli) angeokolewa na “wakati wa taabu” ambao ulimalizika kwake kwa kufanywa ukiwa kwa Yerusalemu na Yuda katika mwaka 607 K.W.K. (Yer. 30:7) Hata hivyo, kabla ya “taabu” hiyo kutokea, fadhili za Yehova zisizostahilika zilimsukuma atabiri jambo la ajabu mno kuliko kukusanywa tu kwa watu wake waliohamishwa:
16 “Angalia, siku zinakuja, asema [Yehova], nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema [Yehova]; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue [Yehova]; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema [Yehova]; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”—Yer. 31:31-34.
MPATANISHI MPYA AHITAJIWA
17. Sababu gani bado sisi leo twapaswa kupendezwa na agano Jipya, na ni muda mrefu namna gani uliopita ambapo agano la Torati lilikuwa tayari limekwisha chakaa na kukaribia kutoweka?
17 Je! sisi leo tunapendezwa na agano hilo jipya? Twapaswa kupendezwa, kwa kuwa lingali linatenda kazi. Lakini limekuwa likitenda kazi kwa nani mpaka wakati huu? Mamilioni ya Wayahudi kuzunguka dunia yote hawadai kuwa linatenda kazi kwao. Wao wanaamini kwamba wangali chini ya agano lililofanywa na baba zao kwenye Mlima Sinai. Hiyo ilikuwa zaidi ya miaka 3,490 iliyopita! Ahadi ya Yehova ya agano jipya ilifanywa kupitia kwa Yeremia zaidi ya miaka 2,580 iliyopita. Ikiwa Wayahudi hao wanasema kweli, sababu gani Mungu amechukua muda mrefu hivyo kulitendesha kazi agano jipya lilioahidiwa? Ala, zaidi ya miaka 1,900 iliyopita agano la Torati la Kiyahudi lilikuwa tayari limekwisha chakaa na kwa wazi lilikuwa limekaribia kutoweka na kufungulia njia agano hilo jipya. Je! lilifanya hivyo?
18. (a) Ahadi ya Mungu ya agano ambalo lilikuwa “jipya” ilionyesha nini kwa habari ya agano la Torati na ilionyesha kuwa lilikaribia kufanya nini? (b) Taifa la Israeli lilipelekewaje orodha ya Torati?
18 Juu ya jambo hilo mwanafunzi wa wa Kiyahudi aliyekuwa akiketi miguuni pa mwalimu Farisayo mwenye kujulikana sana, Gamalieli, katika Yerusalemu, aliandika hivi: “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.” (Ebr. 8:13; 2 Kor. 3:14) Wakati mwandikaji huyo wa Kiyahudi alipoandika maneno hayo kwa Waebrania waliofanywa Wakristo katika Yerusalemu, ilikuwa wapata mwaka 61 W.K. Katika barua ya mapema zaidi kwa makundi ya Kikristo katika jimbo la Kirumi la Galatia, yeye aliandika hivi: “Torati ni nini basi? Iliingizwa [kwa agano la Ibrahimu juu ya Uzao ule] kwa sababu ya makosa [ya wanadamu], hata aje huyo mzao [wa Ibrahimu] aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa [mpatanishi].”—Gal. 3:19.
19. Kwa sababu agano la Torati lilimhitaji Musa mpatanishi, jambo hilo linatoa sababu gani kwa habari ya agano jipya, ambalo vilevile limefanywa kati ya Mungu na wanadamu?
19 Mpatanishi huyo asiyetajwa jina alikuwa Musa. Basi ikiwa kufanywa kwa agano la kale la Torati kulimhitaji yeye kama mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu wasiokamilika, wenye dhambi, hakika kufanywa kwa agano jipya kati ya Mungu na wanadamu kungehitaji mpatanishi, ingawa yeye hatajwi katika Yeremia 31:31-34. Kufikia wakati wa Yeremia, Musa alikuwa amekufa kwa muda mrefu. Kwa sababu yeye alikuwa ametenda kama mpatanishi, Torati ya agano la kale iliitwa “Torati ya Musa.”—Matendo 15:5.
20, 21. (a) Katika kulitabiri agano jipya, Mungu alionyeshaje ubora walo juu ya agano lililotangulia? (b) Mungu angewafanya Waisraeli kuwa nini kiwapo wangelifuata agano hilo kwa uaminifu?
20 Kwa sababu ya agano jipya kuwa agano bora zaidi, lilihitaji kuwa na mpatanishi aliye bora zaidi ya Musa. Ebu tuone namna Mtoaji wa kimbinguni wa agano jipya alivyoonyesha ubora walo juu ya agano lile la kwanza. Yeye anazungumza juu yalo kuwa “si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao.” (Yer. 31:32) Alifikiria kufanya jambo kuu kutokana nao kupitia kwa agano alilofanya na Waisraeli baada ya kuwaleta kutoka Misri. Hivyo, aliwaambia hivi:
21 “Ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, [itakuwaje?] hapo ndipo mtakapokuwa [mali ya pekee] kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.”—Kut. 19:5, 6.
22. (a) Huo “ufalme wa makuhani” ungekuwa serikali ya namna gani na yenye kufaa kwa nani? (b) Hilo “taifa takatifu” lingekuwa ‘mali ya pekee’ kwa nani, na katika uhusiano wa namna gani pamoja naye?
22 Bila shaka maneno “ufalme wa makuhani” yanaonyesha serikali inayofaa kabisa mahitaji ya wanadamu wote. Makuhani wayo wanamwakilisha na kumtumikia Mungu aliye Mwokozi wa wanadamu. “Ufalme wa makuhani” huo wenyewe ni “taifa,” kikundi cha kitaifa kilicho safi kutosha kuitwa “takatifu,” kinachofaa kutumiwa na Mungu. Kati ya mataifa yote juu ya dunia Mungu alikichagua. Kilikusudiwa kiwe ‘mali ya pekee’ ya Mungu, kama vile tu mke ni mali ya pekee ya mume wake. Kwa kweli, Mungu aliwafananisha Waisraeli wa kale waliokombolewa na mke aliye taifa zima kwa kusema kwamba ‘alikuwa mume kwao.’ Walakini mahali pa kumpa utii kama vile mke kwa kulishika agano lake takatifu, alipuza matakwa ya pekee ya uhusiano huu wenye pendeleo. (Yer. 3:1-3, 20) Alistahili kutalikiwa!
23. Je! agano la Torati ya Musa lilifanya kazi, naye Mungu alifanya nini juu ya serikali inayofaa iliyokusudiwa wanadamu?
23 Kutokana na historia ya baadaye ya watu hao wa agano wa Yehova Mungu, twafahamu kwamba mambo hayakupata nafuu ya kudumu kwao. Kwa hiyo uhakika wa kwamba agano la Torati lililopatanishwa na Musa halikufanya kazi hauwezi kupingwa. Lo! namna tunavyoweza kuwa wenye furaha kwa sababu hiyo kwamba Mungu hakuacha kufanya mipango kwa ajili ya huo “ufalme wa makuhani” wenye kutamaniwa! Akiitazamia serikali hiyo yenye kufaa, yeye aliweka agano bora zaidi mahali pa lile la kale.
[Picha katika ukurasa wa 8, 9]
Raheli akililia wana wake