Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 5/15 kur. 11-16
  • Ahadi ya Mungu Juu ya Serikali Yake ya Ulimwengu Yategemeka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ahadi ya Mungu Juu ya Serikali Yake ya Ulimwengu Yategemeka
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • LIWALI AJAYE WA ULIMWENGU AAHIDIWA
  • KUTEGEMEKA KWA AHADI YA KIMUNGU
  • Yerusalemu—“Jiji la Yule Mfalme Mkubwa”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • “Ufalme wa Bwana Wetu na wa Kristo Wake” Waanza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Kitabu Cha Biblia Namba 10—2 Samueli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Kitabu Cha Biblia Namba 26—Yeremia
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 5/15 kur. 11-16

Ahadi ya Mungu Juu ya Serikali Yake ya Ulimwengu Yategemeka

“[Yehova] asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake; ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi.”​—Yer. 33:20, 21.

1. Ni kwa njia gani Jamaa ya kifalme ya Mfalme Daudi isivyokuwa na ulinganifu?

ULIMWENGU huu haujapata kuona kitu kama hicho! Kitu gani? Nasaba ya wafalme katika jamaa moja ikifuatana kwa miaka 470 na kisha baada ya kukatishwa kwa muda wa miaka 2,520, ikajichukulia tena mamlaka kamili ya kifalme. Jamaa hiyo isiyolinganika ilikuwa ile ya Mfalme Daudi wa Yerusalemu, baba mashuhuri wa Yesu Kristo, aliyezaliwa katika mahali penyewe alipozaliwa Daudi, Bethlehemu.

2. Yeremia alikuwa wapi katika mwaka 608 K.W.K. wakati wa utawala wa mfalme wa mwisho wa nasaba ya kidunia ya Daudi, naye ni nani peke yake angeweza kutumiwa kurudisha tena utawala wa nasaba ya Daudi?

2 Utawala wa Daudi juu ya watu wake ulianza katika mwaka 1077 kabla ya Wakati wa Kawaida wetu. Walakini wakati nabii Yeremia alipoanza kazi yake yenye hatari katika mwaka 647 K.W.K., nasaba ya Daudi ya wafalme wa duniani iliingia kwenye miaka 40 ya mwisho ya utawala katika Yerusalemu. Yeremia aliunga mkono sana ahadi iliyo nzito ya agano la Mungu na Daudi ya ufalme wa milele. Hata hivyo, katika mwaka 608 K.W.K. Yeremia alijipata akiwa katika kizuizi cha kijeshi katika mji mkuu wa kifalme. Aliwekwa kizuizini pale pale katika Ua wa Walinzi ulioshikamanishwa na jumba la kifalme la Mfalme Sedekia, mfalme wa 21 kutawala katika nasaba ya Daudi, tukihesabu kutoka kwa Daudi mwenyewe. Sedekia alipopinduliwa na Wababeli katika mwaka 607 K.W.K., ile miaka 470 ya utawala wenye kuendelea wa nasaba ya Daudi katika Hebroni na Yerusalemu wa kidunia ukakoma. Ni Yesu Kristo tu, mzao aliyetabiriwa wa Daudi, ambaye angeweza kutumiwa na Mungu kuurudisha ufalme wa Daudi katika kutimiza agano la Mungu naye la ufalme usioharibika.

3. Alipokuwa chini ya kizuizi cha kijeshi, Yeremia aliweza kupashana habari na nani nje, nako kupashana huko kwa habari kulianzaje kwa mara ya pili?

3 Alipokuwa kizuizini nabii Yeremia asingeweza kupashana habari na Wababeli ambao wakati huo walikuwa wanauzingira Yerusalemu, walakini aliweza kupashana habari na Mungu wake, kama vile tusomavyo: “Tena, neno la [Yehova] likamjia Yeremia mara ya pili, hapo alipokuwa akali amefungwa katika [ua] wa walinizi, kusema, [Yehova] alitendaye jambo hili, [Yehova] aliumbaye ili alithibitishe; [Yehova] ndilo jina lake; asema hivi, Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.”​—Yer. 33:1-3.

4. Yale ‘mambo makubwa yasiyojulikana’ ambayo sasa yangesemwa yalikuwa mambo gani?

4 Mambo gani? Kwamba mji ulio juu ya kilima, Yerusalemu, ungeteketezwa kabisa na kisha, baada ya kukaa mahame kwa miaka 70, ungejengwa tena. Zaidi ya hayo, ungekaliwa tena na watu wake wenyewe ambao walikuwa wamehamishwa kupitia njia yenye umbali wa maili 1,000 (kilometres 1,600)! Hata ingawa nasaba ya kifalme ya Daudi isingerudishwa tena juu ya kiti cha enzi cha kidunia, bado ingeendelea kwa miaka 639, kufikia mwaka 33 W.K., wakati wa kutokea kwa mrithi wa kudumu wa hicho kiti cha enzi apate kutawala milele. Mrithi huyo alipata kuwa Yesu Kristo!​—Kol. 1:13.

5. Yehova Mungu aliamuru nini kwa habari ya mji huo wa Yerusalemu uliokuwa unazingirwa?

5 Muumba na Mwanzilishi wa dunia peke yake, Mungu anayeongoza mambo ya kidunia, ndiye angeweza kuona kimbele na kuahidi mambo hayo. Ndivyo alivyofanya. Kwa hiyo, yajapokuwapo maoni yasiyo na tumaini ambayo watazamaji huenda wakatoa kwa habari ya matokeo ya mwisho juu ya nyumba ya kifalme ya Daudi, Yehova huyu tu ndiye angeweza kumwongoza Yeremia kwa roho aseme hivi:

“Maana [Yehova], Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga; Wanakuja kupigana na Wakaldayo [wenye kuzingira], lakini ni kuzijaza kwa mizoga ya watu, niliowaua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu. Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli. Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza. Nami nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi; na kukosa juu yangu. Na mji huu [Yerusalemu] utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo [wafungwa], nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo [Yerusalemu].”​—Yer. 33:4-9.

6. Kuponywa kwa Yerusalemu baada ya kumwagwa kwa hasira na ghadhabu ya Yehova juu yake kuwa na matokeo gani juu ya mataifa, na sababu gani?

6 Kupitia kwa Wababeli, au Wakaldayo wenye kushinda ulimwengu, Yehova Mungu alikuwa akimwaga hasira na ghadhabu yake yote juu ya miji ya Ufalme wa Yuda. Nalo lilikuwa jambo la haki, kwa kuwa Wayahudi walikuwa wamekosea amri zake nao walikuwa wamefanya dhambi juu ya agano lililofanywa na babu zao. Kwa hiyo Yerusalemu ulipaswa kuharibiwa na waokokaji wake walipaswa kuhamishwa mpaka Babeli na nchi kuachwa ukiwa pasipo mtu au mnyama. Fadhili zisizostahilika za Yehova peke yake ndizo zingeweza kuleta na ndizo zilileta maponyo na kurudishwa kwenye afya kwa Yerusalemu kuwa mji uliojengwa upya. Kuponywa kwake na Yehova kungekuwa; kusikotazamiwa na kusikofahamika na mataifa yasiyo ya Kiyahudi hata kwamba yangejawa na hofu ya Mungu huyo mwenye kufanya maajabu. Yale ambayo yangetokea kwao yangewafadhaisha mataifa.

7. Ni mambo gani ya maisha ya kawaida ya Waisraeli ambayo yangefanywa upya katika nchi ya Yuda na ya Benyamini na Yerusalemu ambazo wakati mmoja zilikuwa zimeondolewa wakaaji wake?

7 Ijapokuwa Yerusalemu ungeachwa kama magofu mahame kwa miaka 70, Yeremia nabii wa Mungu huyu mwenye kufanya miujiza, hakuwa akizungumza juu ya mambo yasiyowezekana alipotabiri yale ambayo yangesemwa juu yake wakati wa mazingiwa yake:

“[Yehova] asema hivi, Katika mahali hapo ambapo mnasema kwamba ni ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, naam, katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu, zilizo ukiwa, hazina mwanadamu wala mwenyeji wala mnyama, itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao, Mshukuruni [Yehova] wa majeshi, maana [Yehova] ni mwema, [fadhili zisizostahilika] zake ni za milele; na sauti za waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa [Yehova]. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema [Yehova]. . . . Katika miji ya nchi ya vilima, katika miji ya nchi tambarare, katika miji ya [kusini], na katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo karibu na Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mikono yake awahesabuye, asema [Yehova].”​—Yer. 33:10-13.

LIWALI AJAYE WA ULIMWENGU AAHIDIWA

8. Je! kuponywa kwa Yerusalemu katika mwaka 537 K.W.K. kulitokeza kurudishwa tena kwa ufalme wa Daudi, na ni Jambo gani ambalo bado lilikuwa la wakati ujao?

8 Kupona kwa Yerusalemu kulianza katika mwaka 537 K.W.K., lakini wakati huo haukupata kuwa na mfalme wa nasaba ya kifalme ya Daudi. Ulipata tu kuwa na liwali wa jimbo katika nasaba ya uzao wa Daudi. Liwali huyu alikuwa chini ya milki ya Wamedi na Waajemi, walioshinda Mamlaka ya Ulimwengu ya Babeli. Hivyo, basi, namna gani juu ya agano la Yehova alilofanya na Mfalme Daudi la ufalme wa milele katika uzao wa Daudi? Kujapokuwa kushushwa kwa muda kwa nasaba ya kifalme ya Daudi wakati huo, agano la Ufalme lilihakikisha kwamba kipindi chenye utukufu zaidi cha nasaba ya kifalme ya Daudi kilikuwa kingali mbele.

9, 10. Kusudi jambo hilo liwe hivyo, Yehova aliahidi kutokeza nini kutokana na jamaa ya kifalme ya Daudi iliyoshushwa?

9 Sisi leo twaweza kuwa wenye furaha kama nini kwa sababu ya hilo! Sababu gani hivyo? Mti wa jamaa ya Daudi ya kifalme ulikuwa umekatwa, walakini kisiki chake kilikuwa hakijafa. Mungu Mwenye Nguvu Zote angekifanya kitokeze “Chipukizi” ambalo lingekuwa Mrithi wa Kudumu wa ufalme ulioahidiwa. Ebu tusikilize haya:

10 “Tazama, siku zinakuja, asema [Yehova], nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda [ambayo ndiyo ilikuwa nyumba ya Daudi]. Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii. Katika siku zile Yuda [kabila la Daudi] ataokolewa, na Yerusalemu [baada ya kuponywa kwake kulikoahidiwa] utakaa salama; na jina lake atakaloitwa ni hili, [Yehova] ni haki yetu.” Hili ndilo jina lile lile ambalo Mfalme wake wa wakati ujao angeitwa.​—Yer. 33:14-16; linganisha Yeremia 23:4-6.

11. “Chipukizi” lililoahidiwa lilitokezwa katika mtu gani, na, katika mwaka 1914 W.K.. yeye alijionyeshaje kuwa “Chipukizi” la Yehova kweli kweli?

11 Je! ahadi hiyo yenye kuhusiana na serikali ya ulimwengu ilijionyesha kuwa ya kutegemeka? Ndiyo! Ijapokuwa zaidi ya miaka 640 ilipaswa kupita, kisiki cha jamaa ya Daudi isiyo na fimbo, iliyopinduliwa, isiyo na kofia ya kifalme, kilitokeza chipukizi kwa wakati wenyewe wa Yehova. Hii ilikuwa kwa njia ya Yesu, ambaye alikuwa amezaliwa katika mji wa nyumbani kwa Daudi wa Bethlehemu na ambaye alibatizwa na mtangulizi wake, Yohana Mbatizaji, na muda mfupi tu baadaye akatiwa mafuta kwa roho ya Mungu apate kuwa Mrithi wa Kudumu wa agano la Ufalme ambalo lilikuwa limefanywa pamoja na Daudi. (2 Sam. 7:4-17; Eze. 21:21-27) Kweli alipata kuwa ndiye lile “Chipukizi” la Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova, kwa kuwa, baada ya kumalizika kwa “nyakati saba” (miaka 2,520) ya enzi ya mataifa juu ya dunia, katika mwaka 1914 W.K., Yesu Kristo aliyetukuzwa ametumiwa kurudisha tena enzi kuu ya Yehova kuielekea dunia katika kulitimiza agano la Ufalme.​—Dan. 4:13-26; Zek. 6:12, 13.

12. (a) Yesu Kristo alithibitishwaje kuwa ‘‘mwenye haki” akiwa chipukizi? (b) Alipata kuwa ‘‘Bwana” wa nani, nao wokovu uliweza kupatikanaje kwa “Yuda” na “Yerusalemu”?

12 Yehova Mungu alithibitisha kwamba “Chipukizi” hili lilikuwa “lenye haki” alipomfufua Yesu Kristo kutoka kwa kifo cha kufia imani katika siku ya tatu na kumkweza kwenye mkono Wake mwenyewe wa kuume mbinguni. Hivyo Yesu Kristo, ingawa wakati mmoja alikuwa ‘mwana wa Daudi’ wa kidunia, akapata kuwa “Bwana” wa Daudi. (Zab. 110:1-4; Mt. 22:41-45) Wakati alipopaa kwenye mkono wa kuume wa Baba yake wa kimbinguni, alikuwa na thamani ya dhabihu yake kamilifu ya kibinadamu. Hivyo angeweza kuleta wokovu kwa “Yuda,” ambayo mji wake mkuu ulikuwa “Yerusalemu.” Basi, bila shaka, Yesu alifanya ufalme wa nyumba ya Daudi uchipuke kwa mara nyingine!​—Ufu. 22:16.

13. (a) Ni Yerusalemu upi ambao sasa hukaa kwa usalama? (b) Jina ‘Yehova ni Haki Yetu’ linataja juu ya “haki” ya nani. na ni kwa sababu gani jina hilo linahusu kwa kufaa yule ambaye anaitwa “Chipukizi” vilevile?

13 Yesu Kristo anaitwa “Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi.” (Ufu. 5:5) Kwa sababu ya kumkataa na kumwua huyu ‘Simba wa kabila ya Yuda,’ Yerusalemu wa kidunia ‘haukukaa salama,’ bali uliharibiwa katika mwaka 70 W.K. (Mt. 23:37, 38; Luka 21:24) Hata hivyo, Yerusalemu wa juu zaidi, “Yerusalemu wa mbinguni,” unafurahia usalama huo, kwa kuwa watoto wake wa kiroho, wafuasi wa Yesu Kristo watiwa mafuta 144,000, wanakaa katika usalama chini ya uangalizi wa Yehova. (Ebr. 12:22; Gal. 4:26-28) Huu “Yerusalemu wa juu” ndilo tengenezo lile linaloitwa ‘Yehova Ni Haki Yetu.’ Kwa kuwa ni ‘Haki Yetu,’ si, ‘Haki Yangu,’ mtajo huu unahusu watoto wa kiroho 144,000 wa Yerusalemu wa kimbinguni, kwa kuwa Yehova Mungu anawatetea hawa au kuwatangaza kuwa wenye haki kwa sababu ya ubora wa dhabihu ya Kristo. Jina la Yesu Kristo ni “Chipukizi” tena ni ‘Yehova Ni Haki Yetu,’ yeye akiwa ndiye wakili wa wafuasi wake waliotiwa mafuta 144,000.​—Yer. 23:5, 6; tazama pia 1 Wakorintho 1:30, 31; Warumi 3:21, 22.

14. Kwa kuwa Kristo na tengenezo lenye kushirikiana naye wana jina hilo, serikali ya ulimwengu ya Mungu inayokuja ni serikali ya namna gani?

14 Kwa Mfalme aliyetiwa mafuta na tengenezo lake linaloshirikiana naye kuitwa kwa jina hilo walilopewa na Mungu, serikali ya ulimwengu ya Mungu inayokuja kwa hakika itakuwa serikali ya namna gani? Si nyingine ila serikali yenye haki. Lo! namna tunavyoweza kuwa wenye shukrani kwa ajili ya hilo!

KUTEGEMEKA KWA AHADI YA KIMUNGU

15, 16. (a) Kulingana na Yeremia 33:17, 18, Yehova hatashindwa kuwa na watumishi gani rasmi? (b) Ni nani ambao watachukua vyeo hivyo rasmi. Nao, watamtumikia Yehova wakiwa wapi?

15 Vilevile Yehova Mungu atakuwa na ukuhani unaofaa pamoja na Ufalme wake ulioahidiwa. Yeye anatuhakikishia hili kwa kuongezea yote yaliyotangulia kutajwa, akisema: “Maana [Yehova] asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli; wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.”​—Yer. 33:17, 18.

16 Basi, je! ni kitu kwamba tangu kuharibiwa kwa Yerusalemu uliorudishwa upya katika mwaka 70 W.K. hakujakuwa hekalu halisi la Yehova duniani na vilevile hakuna mshiriki anayetambulikana wa kabila la Lawi na wa nyumba ya ndugu ya Musa, Haruni, ili atumikie katika hekalu hilo? Hata kidogo! Kwa kuwa sasa Yehova anaye Kuhani Mkuu wake na makuhani wadogo wale ambao walifananishwa kimbele na makuhani wa Kilawi wa kale katika Israeli, yaani, Yesu Kristo na wafuasi wake waliochaguliwa ambao wametiwa mafuta kwenye ukuhani wa kiroho kwa roho ya Mungu. Mbingu ambazo Mungu anafanya kiti chake cha enzi ndizo Patakatifu Zaidi pa hekalu la kiroho ambapo ukuhani huu unatumikia.​—Ebr. 9:24; 1 Pet. 2:9, 10.

17. Kama vile tusivyoweza kuzuia mchana na usiku usitokee, ndivyo tusivyoweza kumzuia Yehova asifanye nini kwa habari ya ufalme na ukuhani huo?

17 Kwa hiyo, kwa wakati wote ahadi za Mungu zimejionyesha kuwa ni za kutegemeka, na bado zitajionyesha kuwa za kutegemeka kwetu sisi. Sikiliza: “[Yehova] asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake; ndipo agano langu nililofanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika.”​—Yer. 33:20-22.

18. Yehova aliliendeleza agano lake kuhusiana na ukuhani kwa muda mrefu kadiri gani baada ya siku za Yeremia, mpaka kufika kwa nani?

18 Kama jua laweza kuacha kuangaza juu ya dunia yetu na dunia hii kuacha kuzunguka katika mihimili yake ndipo na Yehova angeweza kuvunja maagano yake kuhusu Daudi na Walawi. Mungu Mwenye Nguvu Zote aliongeza “uzao” wa Daudi kwa muda wote wa miaka 600 na zaidi mpaka Mrithi wake wa Kudumu, Yesu Kristo, alipofika. Huyu ndiye aliyefananishwa na kuhani mkuu Haruni na vilevile akawa kuhani juu ya kiti chake cha enzi cha kimbinguni, kama Melkizedeki. (Zab. 110:1-4; Mwa. 14:18-20; Zek. 6:13; Ebr. 6:20–7:3) Kwa njia hiyo Yehova amezuia inayoelekea kuwa misiba juu ya Yerusalemu na hekalu lake akaendeleza maagano yake.

19. Ni matukio gani ya ajabu kwa habari ya dunia yetu ambayo kama yangeweza kukoma, naye Yehova angeweza kuvunja agano lake na Daudi la ufalme wa milele?

19 Kwa mfano, wakati jeshi la Wababeli chini ya amri ya Mfalme Nebukadreza lilipokuwa likiuzingira Yerusalemu mara ya pili, maneno yafuatayo yalitolewa: “Kisha neno la [Yehova] likamjia Yeremia, kusema, Je! hufikiri neno hili walilolisema watu hawa, wakinena, Jamaa zile mbili alizozichagua [Yehova] amezitupilia mbali? Hivyo ndivyo wanavyowadharau watu wangu, ili wasiwe taifa tena mbele yao. [Yehova] asema hivi, Ikiwa agano langu la mchana na usiku halikai imara, ikiwa mimi sikuziamuru kawaida za mbingu na dunia; ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae baadhi ya wazao wake watawale juu ya wazao wa Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.”​—Yer. 33:23-26.

20. Ni jambo gani lililotukia katika siku za Yeremia lililofanya ionekane kama kwamba Yehova asingeweza tena kuwa na ufalme ukitawala juu ya dunia au kuwa na ibada yake ikiendeshwa duniani?

20 Katika mwaka uliofuata unabii huo, Yerusalemu uliingiwa na kuharibiwa. Waokokaji wa Kiyahudi walichukuliwa mateka na wengi wao wakahamishwa mbali sana mpaka Babeli. Ilielekea kama kwamba Yehova alikuwa amekataa kwa hakika “jamaa zile mbili” ambazo alikuwa amezichagua pindi moja. Hali ilionekana isiyo na tumaini kwa jamaa ya wazao wa kifalme wa Daudi na jamaa ya makuhani waliokuwa wazao wa Haruni, kuhani mkuu wa kwanza wa Israeli. Tofauti na ambavyo Muumba wa mbingu na dunia alivyokuwa amesema, ilionekana kama kwamba Yehova alikuwa amevunja maagano yake kwa habari ya jamaa ya kifalme na jamaa ya kikuhani. Lilikuwa suala la kama kungekuwa ufalme wa Yehova wakati mwingine au kurudishwa upya kwa ibada yake ya kweli duniani!

21. Yehova alijionyeshaje kuwa mwaminifu kwa habari ya kuweka maagano, kwa faida ya Waisraeli waliohamishwa?

21 Walakini, tangu ule msiba wa taifa zima, mchana na usiku na kawaida za mbingu na dunia hazijaacha kufanya kazi. Kwa hiyo Muumba ambaye hajavunja maagano yake kuhusiana na vitu hivyo visivyo na uhai vya ulimwengu asingeweza kutazamiwa kwa haki avunje maagano yake yaliyofanywa na viumbe vyake vyenye akili kuhusiana na ufalme wake na ibada yake safi. Wala hajafanya hivyo? Aliwahurumia wazao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Baada ya miaka 70 ya uhamisho walikusanywa na kurudishwa tena kwenye makao yao waliyopewa na Mungu.

22. Mungu alitimizaje agano lake kwa watu hawa waliorudishwa kwa habari ya “Chipukizi la haki,” nalo hili lathibitisha nini kuhusiana na ahadi ya Mungu?

22 “Chipukizi la haki,” Yesu Kristo, alikuja kwa watu hawa waliorudishwa tena karne 19 zilizopita. Kifo chake cha kufia imani katika mwaka 33 W.K. hakikuharibu agano la Mungu, kwa kuwa Mungu alimtukuza mbinguni. Huko, yeye asema hivi, “Ni hai hata milele na milele.” (Ufu. 1:18) Yeye ameokoka mpaka kuwekwa kwake na Yehova kama Mfalme katika serikali ya ulimwengu iliyoahidiwa. Ahadi ya Mungu ya jambo hilo imekuwa yenye kutegemeka!

[Picha katika ukurasa wa 15]

Kama ambavyo kwa hakika jua linakucha kila siku ndivyo na Mungu atakavyoweka ahadi yake

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki