Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 7/1 uku. 23
  • Sababu Gani Uuzuie Ulimi Wako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Gani Uuzuie Ulimi Wako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Kutumia Hekima Tunapozungumza
    Amkeni!—2010
  • Kwa Sababu Gani Yakupasa Uzuie Ulimi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Kuuongoza Ulimi Kama Farasi Anavyoongozwa kwa Hatamu
    Amkeni!—2004
  • Onyesha Upendo na Heshima kwa Kuzuia Ulimi Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 7/1 uku. 23

Sababu Gani Uuzuie Ulimi Wako?

Je! wewe wamjua mtu ambaye husema-sema sana? Mithali 10:19 hutoa sababu ya kujilinda na jambo hilo. Inasema: “Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.

Yakobo ndugu mzazi mmoja na Yesu alithibitisha kwamba kuna uhitaji wa kujilinda tusikwaze wengine kwa ulimi, kwa sababu kushindwa kuuzuia kwaweza kufanya ibada ya mtu kuwa ya bure. (Yak. 1:26) Hakuna ye yote kati yetu anayeweza kuuzuia ulimi kwa ukamili, walakini bila shaka tunaweza kufanya maendeleo.​—Yak. 3:2-8.

Hiyo haituhitaji tukae kimya, pasipo kushiriki kamwe mazungumzo. Walakini sababu gani usifanye jaribio hili? Fikiria maelekeo yako kwa muda fulani. Uone kama, katika mazungumzo ya kikundi, unajisikia kusukumwa useme zaidi katika kila habari inayozungumzwa. Katika mazungumzo ya habari mbalimbali juu ya maisha je! yanamalizika ukiwa kila wakati umezungumza zaidi kuliko wengine katika kikundi? Ikiwa ndivyo, huenda kutafakari juu ya Mithali 10:19 kukakulinda.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki