Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 10/15 kur. 20-21
  • Maadhimisho ya Kukombolewa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maadhimisho ya Kukombolewa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Chakula cha Kutusaidia Sisi Tukumbuke
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Kumkumbuka Yehova na Mwana Wake
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Kuadhimisha Kifo cha Mwanamume Mkuu Zaidi Aliyepata Kuwa Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Nisani 14—Siku ya Kukumbukwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 10/15 kur. 20-21

Neno la Mungu Li Hai

Maadhimisho ya Kukombolewa

LO! KULIKUWA kukombolewa kwa ajabu namna gani! Taifa la Israeli lilikuwa utumwani Misri, naye Farao alikataa kuwaacha waende wakiwa huru. Kwa hiyo Yehova akawaagiza Waisraeli waue mwana-kondoo na kunyunyiza damu yake juu ya vizingiti vya milango ya nyumba zao, kama unavyoweza kuona. Usiku huo huo malaika wa Yehova alipita juu ya nyumba zenye damu katika vizingiti vya milango lakini akawaua wana wazaliwa wa kwanza katika nyumba za Wamisri wote. Ndipo Farao alipowaacha Waisraeli waende wakiwa huru.

Je! kukombolewa huko kwa Waisraeli kulikuwa kamili kweli? Basi, wazaliwa wao wa kwanza walikuwa hai; wao walikombolewa kutoka utumwani Misri na mwishowe wakaingizwa ndani ya “nchi imiminikayo maziwa na asali.” (Kut. 13:5) Lakini bado watu hao walipatwa na magonjwa; walizeeka na kufa. Hawakukombolewa kutokana na dhambi na matokeo yake, kifo.

Baadaye, Yesu Kristo alionekana duniani. Siku moja Yohana, aliyekuwa amembatiza Yesu, alielekeza kidole kwake na kusema: “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29) Kama vile damu ya mwana-kondoo wa Kupitwa ilivyomaanisha kukombolewa kwa mzaliwa wa kwanza wa Kiisraeli, ndivyo damu ya Kristo iliyomwagwa chini iwezavyo kukomboa watu. Inaweza kutoa ukombozi bora zaidi, ulio kamili. Wale wanaozoea kuiamini dhabihu ya Kristo wataondolewa dhambi zao. (Yohana 3:16, 36) Wataweza kuishi milele bila kuzeeka wakati wo wote, bila kuwa wagonjwa wala kufa.​—Ufu. 21:4.

Yesu alianzisha chakula cha pekee kuadhimisha ukombozi huu mkubwa, na hasa kwa sababu unawahusu wale watakaofufuliwa wawe warithi pamoja naye wa ufalme wa kimbinguni. Jioni iliyotangulia kutundikwa kwake mtini, Yesu aliwapa mikononi mitume wake waaminifu mkate na kusema: “Chukueni, leni. Huu unamaanisha mwili wangu.” Halafu akawapa kikombe cha divai na kusema: “Nyweni kutoka kwacho, ninyi nyote; kwa maana hii inamaanisha ‘damu ya agano’ yangu, ambayo itamwagwa chini kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.” Vilevile, Yesu akasema: “Endeleeni kufanya hili katika ukumbusho wa mimi.”​—Mt. 26:26-28; Luka 22:19, 20, NW.

Kwa hiyo huu ulipasa uwe mwadhimisho wa kila mwaka katika kushika ukumbusho wa kifo cha Yesu. Wakati wa pindi hii ya pekee yale yanayomaanishwa na kifo cha Kristo, si kwa warithi wa Ufalme peke yao bali kwa wanadamu wote wenye kuamini, yanarudiwa kutajwa na kukaziwa sana juu ya akili na moyo. Mashahidi wa Yehova wanakukaribisha ujiunge nao katika mwadhimisho wa ukumbusho huu mwaka ujao, Aprili 8. Uhudhurie kwenye Jumba la Ufalme lililo karibu zaidi na wewe. Ukawaulize Mashahidi wa Yehova wa kwenu wakati barabara wa kufanya hivyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki